.
EXCLUSIVE: usiku wa kuamkia jana, Wezi wameruka ukuta  na kuingia kwenye nyumba anayomiliki mwimbaji DIAMOND Sinza na  kufanikiwa kumuibia vitu kibao vikiwemo vifaa vya gari.
wakati wanaiba, DIAMOND hakushtukia chochote, baadae usiku ndio jirani yake akamuamsha akamwambia jamaa wamemuibia na kusepa.
vifaa vya gari alivyoibiwa thamani yake ni milioni 1.9! na  ndani ya gari kulikua kuna nguo alizozitumia kushoot video yake mpya  ambayo bado hajamaliza kuishoot na aliakiwa kuwa na nguo hizo hizo kwa  ajili ya muendelezo wa SCENES.
kwenye gari pia kulikua na pete, saa 2, 1 ya rolex aliyonunua  SOUTH AFRICA, cheni ya gold, viatu,mikanda na headphones za DR DRE  ambavyo vyote wezi wamevibeba na mpaka sasa hajafaham ni watu gani  waliohusika.
mlinzi alikuepo lakini walimteka na kumpiga, DIAMOND kuamka anakuta wamemfunga na gunia na damu kibao.


No comments:
Post a Comment