TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, September 8, 2014

TAARIFA RASMI KUTOKA JESHI LA MAGEREZA KUHUSU TAARIFA ZA UZUSHI ZINAZOZAGAA KUWA BABU SEYA NA MAWAE WAMEACHIWA HURU

Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).

Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.

Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014.

No comments:

Post a Comment