TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, September 11, 2014

WAZIRI MAGUFULI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA BENKI YA DUNIA OFISINI KWAKE LEO PAMOJA NA KUKAGUA BARABARA ZA KUPUNGUZA MSONGAMANO (BRT)

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akizungumza na Mkurugenzi Mkuu kutoka Benki ya Dunia Bi. Sri Mulyani Indrawati watatu kutoka kushoto pamoja na ujumbe alioambatana nao kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia Wadau hao wa Maendeleo.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akitoa zawadi kumkabidhi Mkurugenzi Mkuu kutoka Benki ya Dunia Sri Mulyani Indrawati kushoto kwake mara baada ya kufanya mazungumzo kuhusu miradi mbalimbali ya Barabara
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akimshukuru Mkurugenzi Mkuu kutoka Benki ya Dunia Sri Mulyani Indrawati mara baada ya kufanya mazungumzo na Waziri Ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi akizungumza katika mkutano wa Uwasilishaji wa Mada ya Mradi wa Ujenzi wa Barabara za kupunguza msongamano (BRT) jijini Dar es Salaam leo
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli aliyesimama akizungumza kwenye Mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu kutoka Benki ya Dunia Sri Mulyani Indrawati.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakwanza kushoto akiangalia mandhari ya Barabara za Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT)
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakwanza kulia akiwa na Mkurugenzi Mkuu kutoka Benki ya Dunia  Sri Mulyani Indrawati wapili kulia, Mheshimiwa Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI pamoja na wajumbe mbalimbali kutoka Benki ya Dunia wakifatilia kwa makini utolewaji wa taarifa za Mradi wa Ujenzi wa Barabara za mabasi yaendayo haraka(BRT)
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akiwasilisha mada katika mkutano huo.

Dkt. John Magufuli, Waziri wa Ujenzi akizungumza na Wananchi kuhusu mradi wa Ujenzi wa Barabara za mwendokasi Ubungo Dar es Salaam

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale wakwanza kushoto akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Barabara za Mwendokasi Ubungo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment