TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, September 9, 2014

TASAF NA WADAU WA MAENDELEO WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM.

 Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na wadau wa Maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi wameanza Mkutano wa kupitia mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini,PSSN unaoratibiwa na Mfuko huo nchini. 

Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango huo unaowahusisha wataalamu mbalimbali kutoka Taasisi za Fedha na mashirika ya misaada ya kimataifa utawawezesha pia wataalamu hao kutembelea maeneo kadhaa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini  katika mikoa y Dodoma, Lindi na Zanzibar.

Akitoa tathmini ya utekelezaji wa Mpango  wa kunusuru kaya maskini Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema tayari kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 13 kimetumika katika kutoka ruzuku kwa walengwa wa Mpango huo na kuwa katika maeneo ambako ruzuku hiyo imetolewa kumekuwa na mafanikio makubwa ya uboreshaji wa maisha ya kwalengwa wa  mpango huo.

Kwa Upande wao wadau wa Maendeleo kutoka BENKI YA DUNIA , UNICEF,ILO, UNPF,na  DFID,,wameonyesha kuridhishwa kwao na namna TASAF inavyotekeleza Mpango wa kunusuru kaya maskini na kuonyesha kuwa kazi hiyo itakamilimka kwa mafanikio makubwa .

 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga akiongoza Mkutano wa wadau wa maendeleo na maafisa wa TASAF juu ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru Kaya maskini nchini ,PSSN ulioanza leo Jijini DSM.
 Baadhi ya wadau wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa kutathmini  utekelezaji wa shughuli za Mpango wa kunusuru Kaya Maskini, unaoratibiwa na TASAF.
 Baadhi ya wadau wa maendeleo  na watendaji wa TASAF wakiwa katika mkutano wa kutathimini utekelezaji wa mpango wa Kunusuru kaya maskini PSSN.
Baadhi ya wadau wa maendeleo wakiongozwa na mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, aliyevaa tai  walipotembelea chumba cha kurekodi takwimu za walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini  ambacho kimefungwa zaidi ya kompyuta 100.

No comments:

Post a Comment