TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 25, 2016

Breaking News.... Tanzia: Mwanamuziki Mkongwe Kassim Mapili afariki dunia

Nimepokea kwa Masikitiko Makubwa Taarifa za Kifo cha Mzee wetu Mzee Mapili (Pichani kulia) baada ya kuonekana hajatoka Chumbani kwake kwa Muda Mrefu.... Ndipo mlango ukavunjwa nyumbani kwake Tabata Matumbi jijini Dar es salaam na kukuta Mzee wetu hatunaye tena... 

Mzee atakumbukwa kwa Kibao cha "Napenda Nipate Lau Nafasi" na "Rangi Ya Chungwa" na vingine nyingi...Pia alikuwa kiongozi wa kwanza wa Tanzania Dance Music Association ama Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA). 

Mara ya mwisho hadharani Marehemu Mzee Kassim Mapili alionekana akiongoza wanamuziki katika mazishi ya mwanahabari nguli wa burudani Marehemu Fred Mosha katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, ambako pamoja na kushirki mazishi aliimba kwa hisia beti kadhaa za kumuenzi marehemu Fred.

Taarifa zaidi za msiba huu mzito  zitawajia kadri zitavyopatikana.
Kwa mawasiliano zaidi kwa wasanii wa Tanzania piga namba 0744150000 
 Nawaomba wanamuziki wote Tujitoe 
kwa wingi kumpa heshima Mzee wetu Kassim Mapili....!! 

Imetolewa na Addo November
 Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania..!!

No comments:

Post a Comment