TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 25, 2016

MUHIMBILI YAENDESHA ZOEZI LA KUCHANGIA DAMU JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Praxeda Ogweyo akifungua zoezi la utoaji damu linaloendelea leo katika viwanja vya Karume mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Zoezi hilo linaendea hadi kesho.
Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Praxeda Ogweyo akiongoza zoezi la utoaji damu leo katika viwanja vya Karume mkabala na Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Muuguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Nemganga Kizega akipima afya ya Mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, Merry Kapande aliyefika leo kuchangia damu katika viwanja vya karume mkabala na ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Tambaza wakichangia damu leo katika zoezi linaloendelea leo jijini Dar es Salaam.
Dk Patrick Shao ni mmoja wa wafanyakazi wa Muhimbili ambaye alifika katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Tambaza na Jangwani wakisubiri kutoa damu leo katika viwanja wa Karume mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

……………………………………………………………
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo emeendesha zoeti la kuchangia damu katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam ambako watu wamejitokeza kwa wingi kutoa damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.

Zoezi hilo limeanza leo asubuhi na litaendelea hadi kesho. Wanafunzi wa Jangwani Sekondari na Tambaza ni kati ya makundi yaliojitokeza kutoa damu.

Pia watu mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kutoa damu akiwamu Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk Praxeda Ugweyo, madaktairi wa muhimbili na kijana Joseph Starford Mgoha aliyetembea kwa mguu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli kutokana na utendaji wake uliotukuka.

Katika zoezi hilo Dk Ogweyo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchagia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu.

Pia, amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na amewaondoa shaka Watanzania kwamba utoaji wa damu hauna madhara yoyote kwa kuwa kabla ya mtu kutoa damu anaandaliwa kitaalamu ili kufanikisha kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment