TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 24, 2016

ziara ya Tume ya Mipango katika Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO).

Bw. Omar Jumanne Bakari (wa tatu kulia) Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO) akitoa maelezo kwa timu ya wataalam kutoka Tume ya Mipango ikiongozwa na Bibi. Florence Mwanri Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kuhusu ufanisi wa mashine ya kutengenezea sabuni katika kiwanda kidogo cha sabuni ambazo soko lake linapatikana jijini Dar es Saalam na mikoa ya jirani.
Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Obedi Sylvester Musiba Mkurugenzi wa kampuni, (wa kwanza kushoto), kuhusu bidhaa wanazotengeneza kutokana na mimea na matunda. Wengine ni Bw. Omar Jumanne Bakari, Mkurugenzi Mkuu SIDO (wa pili kushoto), Bw. Omary Abdallah, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Mipango na Ufuatiliaji (wa tatu kushoto), pamoja na maofisa kutoka Tume ya Mipango.
Viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa Bw. Abdallah Kayumbi (wa kwanza kulia) kuhusu uzalishaji wa vifaa vinavyotumika kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia upepo (wind Turbines).
Viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango na SIDO wakiangalia mashine ya kuzalisha nyuzi kwa ajili ya kutengeneza nguo inavyofanya kazi katika kiwanda cha Fruitful Goshen, Matengenezo Textile.
Bibi. Florence Mwanri, Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango, alipata pia fursa ya kutembelea kiwanda cha TEMSO Engineering kinachozalisha vifaa mbalimbali vya ujenzi kama vile mashine za kufyatulia matofali na matoroli (wheelbarrows

No comments:

Post a Comment