
Nahodha wa timu ya Jambo Leo Mwishehe akimkabidhi zawadi ya majarida ya Jambo mgeni rasmi Mh. Gaudensia Kabaka
Waziri
wa Kazi na Ajira mara baada ya kuzindua rasmi mashindano ya kombe la
NSSF kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe jijini Dar es salaam leo
asubuhi.
Katika mchezo wa soka auliokutanisha timu za Jambo Leo
na TBC timu ya Jambo Leo ambao ndiyo mabingwa watetezi wa kombe hilo
wameibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya TBC hivyo kuanza vyema
utetezi wa kubaki na kombe hilo.

Wachezaji wa TBC na Jambo Leo wakichuana vikali katika mchezo huo kwenye viwanja vya
TCC Sigara Chang'ombe.

Timu zikisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo.

Kwa
upande wa Netboli timu za IPP na Mwananchi Communication zikichuana
vikali hata hivyo IPP wamekuwa washindi baada ya kuikandamiza timu ya
Mwananchi magoli 16-12 na kuibuka na ushindi.

Kikosi cha timu ya TBC kikiwa katika picha ya pamoja.
Kikosi cha timu ya Jambo Leo kikiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment