Mkurugenzi
Mkuu Mwandamizi wa shirika la Millenium Challenge Account Tanzania
Dar es Salaam(MCA-T Dsm) Bw. Bernard Mchomvu akimkabidhi zawadi ya
Khanga yenye nembo ya shirika hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia
Stella Manyanya walipoonana ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said
Thabit Mwambungu (kulia) jana kujadili miradi ya barabara
inayodhaminiwa na shirika la Millenium Challenge Cooperation (MCC)
kupitia Tanzania Millenium Challenge Account (MCA-T Dsm). (Pichana
Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
Shirika hilo linafadhili ujenzi wa
barabara kuu za lami zinazojengwa Mkoani Rukwa zenye jumla ya Km. 224
kwa miradi ya Tunduma-Ikana, Ikana-Laela, na Laela-Sumbawanga. Kwa
mujibu wa Bwana Mchomvu miradi hiyo yote pamoja na changamoto zote
kuzingatiwa itakuwa imekamilika ifikapo mwezi June 2013 na barabara
zote zitakuwa zimekabidhiwa kabla ya mwezi wa nane 2013.
Kwa upande wa Ruvuma shirika hilo
linafadhili ujenzi wa barabara itokayo mjini Songea kuelekea Wilaya ya
Mbinga ambapo ujenzi huo unaendelea na unategemewa kukamilika mwakani.
Hata hivo Mkurugenzi huyo
aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano wanaoutoa
kuwaeleimisha wananchi wao juu ya umuhimu wa miradi hiyo na ulinzi wa
vifaa vya ujenzi kwani umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza wizi wa
vifaa vya ujenzi vilivyokuwa vinafanywa na baadhi ya wananchi na
wafanyakazi wasiokuwa waaminifu.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Injinia Stella Manyanya allishukuru shirika hilo kwa jitihada zao
za kuchangia maendeleo nchini. Aliwashukuru pia kwa hatua za hivi
karibuni walizochukua kujenga daraja la Laela ambalo ni kiunganishi
muhimu kwa wananchi wa eneo hilo katika shughuli zao za kila siku
hususani kuwaunganisha na kituo cha afya cha Laela.
Picha
ya pamoja kati Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu, Injinia
Stella Manyanya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa
Ruvuma Tarimo na wawakilishi wa Jumuiya ya Millenium Challenge
Cooperation (MCC) Bw. Carl Fickenscher Mkurugenzi Mkazi nchini
(kushoto) na Bw. Bernard Mchomvu Mkurugenzi Mkuu Mwandamizi wa shirika
la Millenium Challenge Account Tanzania Dar es Salaam(MCA-T Dsm).
No comments:
Post a Comment