Mkurugenzi
wa Shughuli za Bunge Bw. John Joel (kushoto) akijadili jambo na
Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Teknologia ya Mawasiliano Bw. Didas
Wambura mara tu kabla ya makabidhiano rasmi ya jengo la nymba
atakayokuwa anatumia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
iliyoko eneo la Uzunguni nje kidogo ya mji wa Dodoma leo.
Muonekano
wa nyumba hiyo kwa mbele. Jengo hili ambalo litakuwa makazi ya Spika
yeyote atakayeliongoza Bunge la Tanzania lilianza kujengwa Disemba 2009
na limegharimu takriban sh. 1.5 bilioni. Hapakuwahi kuwa na nyumba
rasmi ya Spika wa Bunge Dodoma
Mshauri Mwelekezi (consultant) wa Pacha Building Construction Company
( ambayo ndiyo imejenga jengo hilo) Bw. Shaban Mwatawala (kulia)
akitoa maelezo ya ujumla kabla ya kuwapitisha viongozi wa Ofisi ya
Bunge katika jengo hili. Kulia kwake ni Mhandisi wa Miradi wa Pacha Bw.
Johanes Maganga, Mkurugenzi wa Mipango na Teknolojia ya Mawasiliano wa
Bunge Bw. Siegfied Kuwite, na Mkurugenzi wa Sgighuli za Bunge Bw. John
Joel.
Bw. Siegfried Kuwite akitia saini makabidhiano hayo kwa niaba ya Katibu wa Bunge ambaye ndiye Mshitiri (client) wa jengo.
Bwana Mwatawala akimkabidhi Msanifu
Majengo M. F. M Msangi (kulia) anyewakilisha Wakala wa Majengo ya
Serikali. Wakala wa Majengo Tanzania ndiye Meneja wa Mradi huu.
Picha zote na Prosper Minja-Bunge
No comments:
Post a Comment