TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, October 16, 2014

KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE ILIVYOFANA KIBAMBA HOSPITALI JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Tanzania Wushu Kung-fu, Kawina Hadji Konde(kushoto), akifafanua jambo wakati wa Kuazimisha Siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyofanyika Katika Viwanja vya Kibamba Hospitali Juzi(Picha Zote kwa Hissani ya Mideta)
Kikosi cha Timu ya Veterani kutoka Kwembe, katika picha ya Pamoja
 Mchezaji wa zamani wa Yanga, Vicent Peter akitoa Maelekezo wakati wa Mapumziko wakati timu ya Mshikamano ilipocheza na Timu ya Kibamba Veterani,
 Baadhi ya Timuzikipanga mstari kuashiria ufunguzi wa Tamasha hilo la Mwalimu Nyerere
 Baadhi ya Wachezaji waliofika kwenye Michuano ya Tamasha hilo, wakilalamika kwa Mratibu wa Tamasha hilo ,Victor Victor, kuhusiana na muda kuwa mchache wakati wa Mchezo ndani ya Uwanja, Muda ulipungunzwa kutokana na Timu shiriki kujitokeza kwa Wingi.
 
 

  Makamu wa Rais wa Tanzania Wushu Kung-fu, Kawina Hadji Konde, akikagua timu Kuazimisha Siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyofanyika Katika Viwanja vya Kibamba Hospitali Juzi
 Kikumndi cha Ngoma cha Jembe Culture Group, kutoka kabila la Wagogo, wakitumbuiza wakati wa Sherehe hizo.
 Baadhi ya wakazi wa Kibamba na Vitongoji vyake wakifuatilia kwa makini BURUDANI.
 Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa, Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Kalist Lyimo( MNEC), akipunga mikono kwa wakazi wa Kibamba na Maeneo ya Jirani muda mfupi baada ya kuwasili Ukumbini.
 Kikundi cha Selonyota kutoka Mbwewe,  wakifanya vitu vyao wakati wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyofanyika Kibamba Hospitali.
 Kundi la Wanunguli kutoka Mbwewe na ngoma ya Kizigua, wakionyesha vitu vyao
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Luguruni, Said Ally, akisalimiana na moja ya Viongozi wa Timu, wakati wa Tamasha hilo kwenye Viwanja vya Kibamba Hospitali.
 Mchezaaji wa Zamani wa Yanga, Edibili Jonas Lunyamila, akizozana na Mratibu wa Tamasha hilo Bwana, Victor, kuhusiana na kile kilichodaiwa kuchezesha muda wa dakika 15 kwa kila mchezo kitendo ambacho timu nyingi zililalamika.
 Baadhi ya Mashabiki wakifuatilia kwa makini michuano hiyo
 Mchezaji wa Zamani wa Yanga na Timu ya Taifa, Edibili Lunyamila, akitoa maelekezo kwa wachzaji wa Timu ya Mshikamano waliofika kwenye Tamasha hilo la Kumbu kumbu ya Mwalimu Nyerere. iliyofanyika kwenye uwanja wa Kibamba Hospitali.

  Mchezaji wa Zamani wa Yanga na Timu ya Taifa, Edibili Lunyamila, akitoa maelekezo kwa wachzaji wa Timu ya Mshikamano waliofika kwenye Tamasha hilo la Kumbu kumbu ya Mwalimu Nyerere. iliyofanyika kwenye uwanja wa Kibamba Hospitali.
 Mmoja wa wachezaji wa mchezo wa Tanzania Wushu Kung-fuu, akionyesha jinsi mcezo huo unavyofanyika.
  Makamu wa Rais wa Tanzania Wushu Kung-fu, Kawina Hadji Konde akikagua timu
  Makamu wa Rais wa Tanzania Wushu Kung-fu, Kawina Hadji Konde akifungua michezo hiyo kwa kupiga penalt kwa niaba ya mgeni Rasmi





==================================================================

Na: 
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa, Kalist Lyimo, alisema kuwa Michezo kwa Vijana ni changamoto kwa ajili ya kujenga ushirikiano na umoja katika kufanikisha masuala mbali mbali.

aidha alisema hayo wakati alipokuwa mgeni Rasmi kwenye Tamasha la kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyofanyika wakati wa Maadhimisho kwenye Viwanja vya Kibamba CCM jijini Dar es Salaam.
aidha katika hafla hiyo baadhi ya timu kutoka maeneo mbali mbali yanayoizunguka Kibamba na maeneo ya jirani walishiriki kwenye michezo hiyo ikiwa ni pamoja na Mchezo wa Mpir wa Pete(Netball), Ngonjera, Shahiri, Sarakasi, mpira wa Miguu na mchezo wa Wushu Kung-fuu.

michezo mingine iliyotumbuizwa katika hafla hiyo ni pamoja na michezo ya Sanaa kutoka kwa wasanii wa ngoma za asili kutoka Mbwewe, Wanunguli wa kabila la kizigua, pamoja na makabila ya Wagogo ambao walitumbiza na kukonga nyoyo za mashabiki wa ngoma za asili.

hafla hiyo ilianza majira ya asubuhi na kumalizika jioni wakati Timu ya Kibamba Veterani ilipoibuka mshindi wa Tamasha hilo na kukabidhiwa Kikombe na Mgeni Rasmi baada ya kuwafunga wenzao wa Kwembe kwa jumla ya mabao 2-0.

No comments:

Post a Comment