Naibu Waziri
wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles
Kitwanga (katikati) akitoa maelekezo kwa wataalamu wa shirika la Tanesco
katika kituo cha Chalinze ya jinsi ya kuboresha hali ya umeme katika
mji wa Chalinze
……………………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Pwani
Ili kuhakikisha wananchi
wananufaika na nishati ya umeme na kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi,
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeagiza Shirika la Umeme
Nchini (Tanesco) kufanya kazi kwa weledi na ufanisi lengo likiwa ni
kuwaunganishia wateja wake umeme ndani ya siku moja mara baada ya
kukamilika kwa taratibu za malipo.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Charles Kitwanga alipokutana na mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantum Mahiza, watendaji wa Tanesco katika ziara yake ya kutembelea miradi ya umeme inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya pili.
Waziri Kitwanga alisema kuwa ili kuendana na kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi, shirika la Tanesco linatakiwa litoe huduma kwa ubora wa hali ya juu, wa kuridhisha na kwa wakati.
“ Inabidi ifikie mahali iwapo mteja atalipia umeme kabla ya saa nne asubuhi na ambaye haitaji nguzo, basi aunganishiwe umeme ndani ya siku hiyo hiyo, na hili linawezekana.” Alisema Kitwanga.
Kitwanga aliendelea kusema kuwa kwa wateja wanaohitaji huduma ya nguzo za umeme, shirika linatakiwa liwe limewaunganishia umeme kwa kipindi cha siku tatu.
Waziri Kitwanga aliongeza kuwa shirika la Tanesco linatakiwa kuondoa mfumo wa wateja kulipa madeni yao kwa foleni badala yake, walipe kwa kufuata mfumo wa kielektroniki ili kurahisisha ulipaji wake na wananchi kupata huduma kwa wakati.
Aidha, Kitwanga aliongeza kuwa ili kuondokana na adha ya kukatika kwa umeme mara kwa mara kutokana na sababu za matengenezo ya miundombinu ya umeme, shirika la Tanesco linatakiwa kubuni mifumo mbadala ya kuwezesha huduma ya umeme kuendelea kupatikana wakati matengenezo yakiendelea pasipo kukwamisha shughuli za uchumi.
“ Inatakiwa ifike umeme uwe ni kama oksijeni katika mwili wa binadamu, mwili wa binadamu ukikosa oksijeni kwa muda mfupi unapoteza uhai, tukielewa umuhimu wa umeme kwa mantiki hii, zitatumika mbinu mbadala za kuzuia kukatika umeme wakati wa matengenezo hivyo kupelekea uchumi wa nchi kukua kwa kasi.” Alisisitiza Kitwanga.
Kitwanga aliendelea kusema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imejipanga kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inachangia katika kutimiza lengo la Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025 ya kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025 nchi ya Tanzania inaondoka kwenye kundi la nchi masikini duniani na kuwa nchi ya kipato cha kati.
Alisema kuwa katika nchi nyingi zilizopiga hatua kubwa katika ukuaji wa uchumi wake, nishati ya umeme imechangia kwa kiasi kikubwa mno na kusisitiza kuwa Wizara ya Nishati na Madini imejizatiti kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakua kupitia mchango wa sekta ya nishati.
Wakati huo huo akielezea hali ya umeme katika mkoa wa Pwani, Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Mahende Mugaya alisema kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu Shirika la Tanesco lilifanikiwa kuwaunganishia umeme wateja 10, 100 katika mkoa wa Pwani na kufikisha asilimia 21.3 lengo likiwa ni kufikisha asilimia 30 ifikapo mwaka 2015.
Mhandisi Mahende aliongeza kuwa kwa sasa shirika la Tanesco linaendelea na zoezi la ukarabati wa miundombinu ya umeme iliyochakaa na kuongeza kuwa ifikapo Februari mwakani tatizo la kukatika umeme mara kwa mara litakuwa limekwisha kabisa.
Akielezea changamoto Shirika la Tanesco linalokumbana nazo katika shughuli zake katika mkoa huo, Mhandisi Mahende alitaja kuwa ni pamoja uchakavu wa miundombinu ya umeme na kusisitiza kuwa ukarabati bado unaendelea katika maeneo yaliyoathirika.
Mhandisi Mahende aliendelea kusema kuwa changamoto nyingine ni pamoja na madeni sugu kwa wateja na kuongeza kuwa hadi sasa Shirika linadai shilingi bilioni 16 wateja mbalimbali na kusisitiza kuwa Tanesco imepanga mikakati mipya ya ukusanyaji wa madeni hayo.
Alibainisha changamoto nyingine kuwa ni pamoja na wizi wa umeme, na madai ya fidia katika utekelezaji wa mradi wa umeme wa awamu ya kwanza uliokuwa unafadhiliwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) na kuongeza kuwa wananchi walidai fidia iliyokuwa kubwa kuliko gharama za mradi.

No comments:
Post a Comment