Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt
Rajabu Rutengwe akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake hawapo
pichani wakati akielezea mkoa kufanyakuzindua kampeni ya chanjo ya
magonjwa ya surua na Rubella kuzinduliwa leo nchini ambapo mikoa 16
inshiriki na katavi ikiwemo,katika mkoa wa Katavi zinafanyika
Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo.
………………………………………………………………
Na Kibada Kibada-Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt
Rajabu Rutengwe amesema Mkoa wa Katavi kupitia mpango wa Taifa wa
chanjo na wadau mbalimbali utaendesha kampeni shirikishi ya
chanjo dhidi ya Surua Rubella, matone ya vitamin A, utoaji wa dawa za
minyoo na kinga dhidi ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele.
Akizungumza katika mkutano wa
Waandishi wa Habari Dkt Rajabu Rutengwe ameeleza kuwa katika kampeni
hiyo chanjo ya surua-rubella itatolewa kwa watoto wote wenye umri kati
ya miezi tisa hadi miaka mitano.
Matone ya Vitamini A’yatatolewa
kwa watoto wenye umri kati ya miezi sita na miaka mitano, dawa dhidi ya
minyoo itatolewa kwa watoto wenye umri kati ya mwaka mmoja na miaka
mitano, kinga tiba dhidi ya matende, mabusha au ngiri maji na usubi kwa
wenye umri wa miaka mitano na kuendelea.
Mkuu wa Mkoa alisema Kampeni ya
Chanjo ya surua inaendeshwa ikiwa ni muendelezo wa utaratibu wa kufanya
kampeni kila baada ya miaka mitatu, utaratibu huu unaotokana na ukweli
kwamba baadhi ya watoto hukosa chanjo ya surua katika utaratibu wa
kawaida ,pia watoto 15 kati ya 100 wanaopewa chanjo ya surua
hawajijengei kinga ya mwili ya dhidi ya surua, hali hii husababisha
kutokea milipuko ya surua.
Amesema Wizara ya Afya na
ustawi wa Jamii kupitia Mpango wa Chanjo imekuwa ikifanya ufuatiliaji wa
ugonjwa wa surua,kila mtu anayejitokeza na dalili za surua sampuli
huchukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara,sampuli huchukuliwa kwa
ajili ya uchunguzi wa kimaabara, Sampuli nyingi zilizochukuliwa
zilithibitika kuwa ni ugonjwa wa Rubelle .
Akaongeza kuwa ugonjwa wa
Rubella una dalili zinazofanana na surua ingawa husababishwa na vimelea
tofauti, njia za kuthibiti magonjwa haya mawili zinafanana ,kwa
kuzingatia haya shirika la Afya ulimwenguni (WHO) liliamua kuunganisha
chanjo ya surua na Rubella ili kuongeza ufanisi wa rasilimali na pia ni
mkakati wa kidini kutokomeza surua na Rubella kwa pamoja ifikapo mwaka
2020.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Dkt Yahaya Husein anaeleza kuwa lengo kuu la kufanya
kampeni hii ni kudumisha upungufu wa magonjwa ulemavu na vifo
vinavyotokana na surua na Rubella,pamoja na kutoa matone yaVitamini A’na
dawa ya kukinga ugonjwa minyoo tumbo,usubi,mabusha na matende,ngirimaji
ili kutibu maradhi na kuimarisha afya.
Naye Katibu Tawala mkoa wa
Katavi Mhandisi Emmanuel Kalobelo ameleza kuwa katika kampeni hiyo Mkoa
wa Katavi umelenga kutoa chanjo ya surua –Rubella kwa watoto wapato
392,174,walengwa wa matone ya vitamin A’watoto 107,609,walengwa,wa kinga
tiba dhidi ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ni watu
451,683,na walengwa wa dawa dhidi minyoo ni 95,652.
Huduma hizi zitatolewa katika
vituo maalum ambavyo vitahusisha vituo vya kutolea huduma za Afya ,Shule
za Msingi,Sekondari na maeneo mengine yaliyopangwa.
No comments:
Post a Comment