Meneja
wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo, akimpa maelezo ya ujenzi wa
nyumba za gharama nafuu Mkuu wa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Bi Susan
Omari alipotembelea mradi huo ulioko eneo la Isikizya Wilayani Uyui
jana. (Picha kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa
Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)
Mwonekanao wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Isikizya Mkoani Tabora.
Meneja
wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akiendelea kutoa maelezo ya mradi
kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Bi Susan Omari
Nyumba
38 zilizojengwa karibu kabisa na Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui eneo la
Isikizya. Nyumba zingine 12 zimejengwa upande wa pili wa barabara eneo
la Isikizya.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Chilambo
Msimamizi
wa mradi wa NHC isikizya Bw. Tokimu Mondo akitoa maelezo ya utekelezaji
wa mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu eneo la Isikizya jana.
Sehemu ya nyumba zilizojengwa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu eneo la Isikizya Wilayani Uyui zinavyoonekana.
Meneja
wa Mkoa wa Tabora Bw. Chilambo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Bi. Susan Omari yanayohusu viwanja vya
Shirika vilivyoko eneo la Itetemia Manispaa ya Tabora.
Meneja
wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akielezea hatua mbalimbali
zilifikiwa na Mkoa huo za kutengeneza nyumba za Shirika. Hili ni
mojawapo ya jengo la Hoteli ya Golden Eagle baada ya kufanyiwa
matengenezo.
Sehemu ya mtaa wa Jamhuri/Shule wenye nyumba zilizofanyiwa matengenezo makubwa na NHC Mkoa wa Tabora
Mojawapo wa jengo lililofanyiwa matengenezo na NHC Mkoa wa Tabora linavyoonekana kwa sasa
Sehemu
ya Maafisa Vijana wakisikiliza mada iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari (hayuko pichani)
alipoelezea mpango wa NHC wa kugawa mashine kwa ajili ya kusaidia vijana
kwenye Halmashauri zote za Wilaya hapa nchini. Jumla ya mashine 656
zimeshambazwa kwa ajili hiyo.
Washiriki wa semina iliyotolewa na NHC wakisikiliza mada kwa makini
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari
akitoa mada juu ya mpango wa NHC wa kusaidia vijana mashine za
kufyatulia matofali katika Halmashauri zote za Wilayanchini.
No comments:
Post a Comment