TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, January 19, 2016
WENGI WAJITOKEZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA
Monday, January 18, 2016
Maoni: 0
Mwili ukiwasili katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa
aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman kabla ya mazishi yake.
Mwili wa
aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman uwasili katika makaburi ya Kisutu leo.
Mwili wa
aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman ukihifadhiwa katika nyumba yake ya milele.
Read more »
TANZIA: GEORGE SEBO MWENYEKITI WA CCM DMV HATUNAE TENA
Monday, January 18, 2016
Maoni: 0
Aliyekuwa Mwenyekiti tawi la CCM DMV Bwn. George Sebo enzi za uhai wake
George Sebo mwenyekiti wa CCM DMV amefariki Dunia muda si mrefu Katika hospitali ya Prince George taarifa zaidi zinakuijia hivi punde
DC AWATAKA MADIWANI WASHIRIKIANE KUMALIZA MIGOGORO
Monday, January 18, 2016
Maoni: 0
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Lucas Mweri akizungumza juzi kwenye baraza la madiwani wa wilaya hiyo (katikati) ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jackson Sipitieck na Makamu Mwenyekiti Albert Msole.
Diwani wa Kata ya Ruvu Remit Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Alamayani Ranga akisoma taarifa kwenye baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo juzi juu ya uboreshaji wa huduma za jamii
Na Woinde Shizza,Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewataka madiwani wa kata 18 za wilaya hiyo kushirikiana na maofisa watendaji wa vijiji vyao kuhakikisha migogoro inakwisha.
Kambona aliyasema hayo juzi wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo na kuagiza mipaka ya vijiji na vitongoji vya miji midogo ya Orkesumet na Mirerani izingatiwe kwa kupimwa.
Alisema kila diwani akishirikiana na maofisa watendaji wa vijiji wataweza kumaliza migogoro hiyo na maeneo ya kilimo na mifugo yabainishwe na kuhakikisha suala la mifugo kuzagaa likomeshwe ikiwemo punda na ng’ombe.
“Mifugo inazagaa ovyo na kuharibu mazao, lidhibitini hilo kwa kutumia kanuni ndogo zetu, kwani mifugo inaachiwa sana na ukitembelea sehemu nyingine unakuta punda wanaingia hadi kwenye madarasa ya shule,” alisema Kambona.
Pia, Kambona amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Lucas Mweri kuwapangia wakuu wa idara, vitengo na watumishi wengine wawe walezi wa kata mbalimbali ili wawe wanazitembelea na kutoa ushauri.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Jackson Sipitieck alisema hivi sasa madiwani na watumishi kwa pamoja wanatakiwa kujipanga kikamilifu ili kuhakikisha wananchi wa kata za eneo hilo wanapatiwa maendeleo.
“Tujipange kikamilifu kwa pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wetu wanapata huduma stahiki, kwani sisi tulichaguliwa kwa ajili ya kutumikia jamii ya Simanjiro ili wapate maendeleo kwenye sekta mbalimbali,” alisema Sipitieck.
Read more »
WAZIRI MKUU, MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKUTANO WA SADC GABORONE
Monday, January 18, 2016
Maoni: 0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Botswana, Bw. Tshenolo Mabeo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama uliopo Gaborone Januari 17, 2016. Majaliwa amemwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa SADC.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mtendaji wa SADC,Dkt, Srergomena Tax mjini Gaborone ambako Mheshimiwa Majaliwa anamwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa SADC Januari 17, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MHE:BONNAH KALUWA AZINDUA KAMPENI YA MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA JIMBO LA SEGEREA.
Monday, January 18, 2016
Maoni: 0
Mwanamitido wa Kimataifa, Flaviana Matata akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ya Mazingira Bora kwa Elimu Bora yenye lengo la kufanikisha maendeleo ya elimu katika Jimbo la Segerea kwa kusaidia kununua madawati, kuchimba matundu ya vyoo, kuchimba visima vya maji na kujenga vyumba maalum vya watoto wa kike, chini ya uratibu wa Mfuko wa Udhamini wa Elimu wa Bonnah (BETF), jijini Dar es Salaam jana. Wengine pichani ni mwandaaji wa kampeni hiyo ambaye ni Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa na Mratibu wa Elimu Josephat Peter.
Mbunge wa jimbo la Segerea,Mhe: Bonnah M.Kaluwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ya Mazingira Bora kwa Elimu Bora yenye lengo la kufanikisha maendeleo ya elimu katika Jimbo la Segerea kwa kusaidia kununua madawati, kuchimba matundu ya vyoo.
Mkutano ukiendelea.
Read more »
MBUNGE WA JIMBO LA LINDI AENDELEA KUTIMIZA AHADI ZAKE JIMBONI KWAKE
Monday, January 18, 2016
Maoni: 0
Mh. Hassani Selemani Kaunje ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Lindi kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) leo hii ameweza kutekeleza ahadi yake aliyowaahidi kikundi cha wanawake wachuuzi wa samaki cha Mitwero ya kuwapatia msaada wa Majokofu mawili (2) ya kutunzia Samaki.
Akikabidhi majokofu hayo leo hii Mh. Mbunge amewataka wachuuzi hao kutunza vitu hivyo kwani ni vyagharama na vitadumu kwa muda mrefu endapo wataviweka katika mazingira mazuri. Nao wanakikundi hicho cha akinamama wachuuzi wa samaki wameweza kupongeza hatua hiyo, wamemsifia kuwa ni mtu wa kutimiza ahadi kwani ametimiza kile alicho ahidi.
Mh. Mbunge amekuwa mstari wa mbele kutekeleza ahadi zake kwa kipindi hiki kifupi tangu alipochaguliwa na wananchi wa jimbo la Lindi mjini kwani hivi karibuni aliweza kutoa msaada wa Matanki ya kutunzia maji katika kata ya Kineng’ene.
JAMES KATORO AWASHUKURU WAKAZI WA KATA YA KAYENZE MANISPAA YA ILEMELA KWA MAAMUZI YAO.
Monday, January 18, 2016
Maoni: 0
Wazee wakimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Katoro alichaguliwa kuwa diwani wa Kata hiyo katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25,2015 kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.
Tukio hili limejiri jana katika Mkutano wa hadhara wa CCM kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa kumchagua Katoro kuwa diwani wa Kata hiyo.
Wazee wakimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Mchungaji Elias Lutalamamila (wa pili kulia) kwa niaba ya viongozi wa dini akimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Diwani wa Kata ya Kayenze Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza James Katoro (CCM) akihutubia katika mkutano wa kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa kumchagua kuwa diwani wao. Aliahidi kushughulikia kero mbalimbali zilizo katika Kata hiyo ambazo ni pamoja na kero ya maji, ujenzi wa zahanati na vituo vya afya, miundombinu pamoja na ujenzi wa shule za msingi na Sekondari.
Salum Abdallah Said ambae ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kayenze akizungumza katika mkutano wa chama hicho wa kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa ushindi waliokipa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25,20515.
Kulia ni Jeremiah Mtoni ambae ni Katibu wa CCM Kata ya Kayenze akizungumza katika mkutano wa chama hicho wa kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa ushindi waliokipa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25,20515.
Elias Makaranga (mwenye kinasa sauti) ambae alikuwa Meneja Kampeni wa Diwani Katoro katika uchaguzi uliopita akizungumza jambo katika mkutano wa kuwashukuru wananchi uliofanyika jana.
www.shaabanmpalule.blogspot.com
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment