TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 19, 2016

WIZARA YA NISAHATI NA MADINI YATOA UFAFANUZI MRADI WA UMEME WA KINYEREZI II (CHANDIMU). UMENG'OA SANA KUCHA ZA MIGUU KWENYE MCHEZO HUU SISI WA USWAZI ALICHOSEMA LOWASSA KUHUSU VIONGOZI WA SERIKALI WALIOMTEMBELEA SUMAYE HOSPITALINI RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR LEO Joto Kali Jijini Dar es Salaam Laibua Mambo Mazito.. MHE. KASSIM MAJALIWA AWATAKA WADAU WA SEKTA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO KUSHIRIKIANA NA WAKEZAJI KUTOKA NCHINI JAPAN MHE. KAIRUKI AAGIZA TATHMINI YA MAFUNZO YANAYOTOLEWA KWA WATUMISHI WA UMMA IFANYIKE NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA BALOZI WA SYRIA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA JESHI LA ZIMAMOT WAZIRI MAHIGA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MWAKILISHI MPYA WA UNICEF NCHINI MKE WA MAKAMU WA RAIS MSTAAFU, MAMA ASHA BILAL AHITIMU STASHAHADA YA UZAMILI KATIKA MENEJIMENTI YA KIMATAIFA MISA YA KUMBUKUMBU YA MPENDWA MAMA YETU LETICIA NYERERE KUFANYIKA JUMAMOSI ST EDWARD, BALTIMORE Kichupa cha leo Victoria Kimani Ft Khuli Chana – All The Way Mzee Majuto akielezea kwanini ameamua kusupport vijana kwenye muziki. Maalimu Seif sasa amwangukia Papa Francis uchaguzi Z'bar. Magufuli ampa zawadi ya kiwanja Samatta. Karume pasua kichwa CCM. Lukuvi atoa siku 18 ghorofa livunjwe D’salaam MISA YA KUMUOMBEA MAREHEMU FELICIAN FERDNAND MINDE. Nape aitaka Chadema imtimue Lowassa ZOEZI LA KUWASAKA WAHAMIAJI HARAMU LAPAMBA MOTO MKOANI MBEYA MAOMBI YA KUMUOMBEA RAIS MAGUFULI, WASAIDIZI WAKE PAMOJA NA TAIFA YAFANA JIJINI MWANZA. KITWANGA APOKELEWA KWA SHANGWE USAGARA, AMALIZA ZIARA YAKE MISUNGWI, WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUMTEUA KUWA WAZIRI

















k5
k6
k7

k9
k8

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka wadau wa Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kushirikiana na wakezaji kutoka nchini Japan katika kuendeleza miradi mbalimbali ya ujenzi, usafirishaji na mawasiliano nchini.
Akizungumza jijini Dar es salaam katika mkutano uliowakutanisha wadau wa sekta hiyo kutoka nchini Japan na Tanzania, Waziri Mkuu Majaliwa amesema ushirikiano huo utaleta tija kwa taifa kwani wadau wa Sekta hiyo wataweza kujifunza masuala mengi kutoka kwa wataalam hao.
“China na Japan ni moja ya nchi zenye Wakandarasi wengi na wazoefu katika sekta ya ujenzi, kushirikiana nao kutaongeza ushindani na kupelekea kupata fursa ya uwekezaji ndani na nje ya nchi, amesema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyataka Makampuni yote yenye miradi ya ujenzi nchini kufanya kazi vizuri na kumaliza kwa wakati katika kipindi hiki ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Amesema fursa ipo kwa Kampuni kutoka Nje ya nchi kufanya kazi na Kampuni za ndani kwa lengo la kupata Zabuni ndani na nje ya nchi, mara zinapotangazwa.
“Kutokana na uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi, hatuna budi Makandarasi wetu kuungana na kufanya kazi kwa ushirikiano na wenzenu kutoka nje ili kupata maendeleo katika Sekta hii”, alisisitiza Waziri Mkuu.
Naye, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kwa niaba ya Waziri, Prof. Makame Mbarawa amewaomba Wawekezaji, Wakandarasi na wadau wa Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutumia fursa hiyo, kuungana na kutengeneza kampuni za ubia baina ya nchi hizo mbili ili kuweza kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
“Tumieni fursa hii kupata elimu na uzoefu na hata kuunganisha Makampuni kwani wenzetu wa Japan wana uzoefu mkubwa na maendeleo katika Sekta hii, ukilinganisha na sisi”, alisema Naibu Waziri.
Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa kupitia mkutano huo Wakandarasi nchini wataweza kujifunza njia za kisasa ambazo zitasaidia katika kuboresha Sekta ya Miundombinu na Mawasiliano.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Miundombinu kutoka Wizara ya Ardhi, Miundombinu, Usafirishaji na Utalii wa Japan, Bwana Takatoshi Nishiwaki, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kukubali kushirikiana katika kuendesha mkutano huo na wadau wa sekta ya ujenzi wenye lengo la kubadilishana ujuzi na teknolojia kuhusu Miundombinu bora.
Mkutano huo wa siku moja umewashirikisha Wawekezaji, Wakandarasi na na Wafanyabiashara kutoka nchini Japan na Tanzania walio katika Sekta ya Miundombinu na Mawasiliano.
 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (hawapo pichani), katika ukumbi wa Chuo cha Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa tatu kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na washiriki wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ulifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Wa tatu kutoka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Injinia Pius Nyambacha na wa poli kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utalawa na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Lilian Mapfa.

(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).




Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, amemwangukia Papa Francis kwa kumwandikia barua, akimuomba kutumia ushawishi wake na Tanzania kumaliza mzozo wa kisiasa kisiwani humo kabla hali haijawa mbaya.

Kwa mujibu wa barua yake ya Novemba 25, mwaka jana ambayo gazeti hili imefanikiwa kuona nakala yake, Maalim Seif alimwomba Papa kutumia ushawishi alionao kwa serikali ya Tanzania ili kuhakikisha haki inatendeka na kuepusha vurugu zinazoweza kutokea.

“Ni wiki tatu sasa tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu na hali hii imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli za kuichumi kutokana na wananchi wengi kuwa na hofu kuhusu mustakabali wa hali hii….watu wanashindwa kujua nini kitatokea maana wana hofu kwamba hali hii inaweza kuharibu umoja wa kitaifa kwa watu kuishi kwa upendo bila kujali dini wala kabila,” ilisema barua hiyo.


Barua hiyo ya Maalim Seif ilisema, Zanzibar ina mchanganyiko wa Waislamu na Wakristo, hivyo hakuna mgawanyiko kwa misingi ya udini lakini hatua ya wananchi kukosa haki yao ya kidemokrasia kupitia sanduku la kura baada ya miaka 20 ya chaguzi visiwani humo kunaweza kusababisha vijana ambao hawafurahishwi na mwenendo huo kutumia njia mbaya kutafuta haki yao.

“Badala ya kuchukua hatua za pamoja kuzuia uovu huu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo chama chake kilishinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita, imekuwa ikisaidia serikali ya Zanzibar kwa kutumia askari na majeshi yake kutishia watu wa upinzani,” ilisema.

“Wakati mmishenari wa kikristu alipomuomba Sultan wa Zanzibar mwaka 1840 kibali cha kujenga asasi ya kusaidia jamii kwenye eneo lake, Sultani yule ambaye alikuwa Muislamu alimtambua kama mtumishi wa Mungu aliyekuwa na lengo la kuendeleza neno la Mungu” ilisema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Papa.

Iliongeza kuwa, Zanzibar ilipopata Uhuru wake mwaka 1963, kwa kiwango kikubwa watu wake waliishi kwa amani na ushirikiano baina ya watu wa madhehebu yote ya Katoliki, Anglikana, Sunni, Shia na Hindu na hakukuwahi kuwa na mgogoro wala hofu ya watu hao kuhitilafiana kwa misingi ya tofauti ya dini.

Ilisema Chama cha Wananchi CUF kimekuwa kikishinda chaguzi zote tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, lakini haijawahi kupewa ushindi wake hata muhula mmoja.
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, imetoa zawadi ya kiwanja kwa Mbwana Samatta kutokana na mshambuliaji huyo wa TP Mazembe na Taifa Stars kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, jana alimkabidhi Samatta hati ya kiwanja hicho kilicho Kigamboni jijini Dar es Salaam.

“Hii ndiyo hati yenyewe. Ila ukiwa tayari karibu ofisini kwangu ili nikukabidhi hati na vijana wakakuonyeshe kiwanja. Kitakuwa ni kiwanja katika sehemu nzuri kabisa, si zile sehemu watu wamefanya eneo liwe skwata,” alisema Lukuvi.

Mbali na kiwanja, Lukuvi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kumuaga Samatta kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alitoa zawadi ya fedha taslimu kwa straika huyo matata ambazo hata hivyo, hazikuelezwa ni kiasi gani.

“Nimekupa hizi, huu mzigo ni wako kwa niaba ya serikali. Wewe mwenyewe ukiamua kuzionyesha, basi fanya hivyo,” alisema.

Baadaye Samatta alimkabidhi jezi yake TP Mazembe Lukuvi ambaye alisema ataiwasilisha kwa Waziri Mkuu ambaye alimuwakilisha katika hafla hiyo.

Baadaye Samatta pia alitoa jezi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ambaye amekuwa karibu yake kwa kipindi kirefu kabla hajaenda Nigeria alikoshinda tuzo ya Mwanasoka Bora na baada ya kurejea.

Nyota huyo wa zamani wa African Lyon na Simba, ametwaa tuzo ya Mwasoka Bora wa Afrika Anayecheza barani baada ya kuiwezesha TP Mazembe kutwaa taji la tano la Klabu Bingwa Afrika mwaka jana huku akiibuka Mfungaji Bora wa michuano hiyo.
Sakata la kutaka Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, avuliwe uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai amekuwa akishirikiana na wapinzani, sasa linaelekea kukipasua kichwa chama hicho kikongwe nchini.

Hoja ya kumvua uanachama wa CCM Dk. Karume ilitolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Sadif Khamis Juma, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Maisara mwishoni mwa wiki.

Akizungumza na Nipashe jana visiwani humu, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema hoja ya kutaka kumjadili na kumfukuza uanachama Dk. Karume, bado haijawiva.

Vuai alisema kuwa CCM ina taratibu zake katika kuwajadili wanachama wake wanaokwenda kinyume na miiko na maadili ya chama hicho kabla ya kufikia hatua ya kutoa maamuzi.

Alisema Chama hakiwezi kujadili mwanachama wake kabla ya kupokea malalamiko kutoka katika tawi la mwanachama ama jumuiya na mhusika kupewa nafasi ya kujitetea.

Aliongeza kuwa CCM inafanya kazi kwa kufuata Katiba na taratibu za Chama na haiwezi kumjadili mtu kwa pupa au jazba.

“Kama wahusika wataleta malalamiko yao, lazima wathibitishe tuhuma zao na mhusika apewe nafasi ya kujitetea kupitia vikao vya Chama,” alisisitiza Vuai.

Aidha, alisema kuwa malalamiko ya mwanachama kuvunja miiko na maadili, yanatakiwa kujadiliwa katika vikao vya Chama na si mkutano wa hadhara.

“Suala hilo bado halijaiva na huwezi kumjadili mwanachama kabla ya kupokea malalamiko rasmi na mhusika kupewa nafasi ya kujitetea,” aliongeza Vuai.

Hata hivyo, akihojiwa na Nipashe mjini hapa jana kuhusu shutuma zilizotolewa na UVCCM dhidi yake, Rais mstaafu Dk. Karume alikataa kuzungumza chochote.

“Sadallah (jina la mwandishi wetu), unataka nini kuhusu jambo hilo? Waulizeni wenyewe waliosema,” alijibu kwa kifupi Dk. Karume.

Wakati hayo yakitokea, Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, kimekanusha kuwa hakina ushirikiano na Dk. Karume wa kuihujumu CCM Zanzibar.

Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, alisema chama chake kimekuwa kikimpa heshima kubwa Dk. Karume kama kiongozi mstaafu na mtu aliyefanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Wazanzibari kupitia maridhiano yaliyozaa Serikali ya Umoja wa Kitaifa mwaka 2009.

“Tunamheshimu Karume kama kiongozi aliyeongoza nchi na mtu aliyefanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Wazanzibari yeye na Maalim Seif Sharif Hamad,” alisema Shehe.

Alisema CUF haihitaji msaada wa kisiasa kutoka chama chochote kutokana na nguvu zake za kisiasa kujitosheleza kufikia malengo ya kuleta mabadiliko ya utawala visiwani Zanzibar.

Alisema bahati mbaya baadhi ya watu hawapendi kuona Wazanzibari wakiwa kitu kimoja baada ya maridhiano kufanikiwa kuimarisha hali ya amani na mshikamano kwa wananchi wake.

Alisema kimsingi CCM imeshindwa kusimamia misingi na malengo ya Mapinduzi na kupoteza nguvu za kisiasa na kuanza kufikiria kufukuza wanachama wake kama ilivyotokea kwa Waziri wa zamani, Mansoor Yussuf Himid na mwanasiasa mkongwe visiwani humu, Hassan Nassor Moyo.

Hata hivyo, alitahadharisha kuwa kama CCM watamfukuza Dk. Karume, basi huo ndiyo utakuwa mwisho wao wa kisiasa duniani kwa sababu kitendo hicho ni sawa na binadamu kumkata miguu.

Wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Maisara, Mwenyekiti wa UVCCM, Sadif Khamis Juma, alisema wakati umefika kwa Dk. Karume kufukuzwa katika Chama kwa madai kwamba anashirikiana na wapinzani kuizorotesha CCM.

Alidai kuwa kwa muda mrefu Dk. Karume amekuwa na ajenda za kuwasadia wapinzani kisiasa badala ya chama chake, kitendo alichokieleza kuwa ni kwenda kinyume na miiko na maadili ya chama hicho.
By Raymond Kaminyoge, Mwananchi
Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametoa siku 18 kwa uongozi wa Manispaa ya Ilala kuvunja jengo la ghorofa 16 lililopo katika Mtaa wa Indira Gandhi kabla halijaleta maafa.

Akizungumza jana katika jengo hilo, Lukuvi alisema anashangaa hadi sasa kazi ya kuvunja jengo hilo haijaanza licha ya manispaa kuelekezwa kulivunja.

Uamuzi wa Serikali kulivunja ulikuja baada kuporomoka kwa jengo katika mtaa huo lililosababisha vifo vya watu 37 na wengine 18 kujeruhiwa mwaka 2013.

“Ni aibu, manispaa mnataka jengo hilo liporomoke na kuua watu tena! Tutachekwa kwa uzembe kama ikitokea tena ajali,” alisema.

Lukuvi alisema kuanzia Februari Mosi uvunjaji wa jengo hilo unatakiwa kuanza vinginevyo wahusika wajiandae kuchukuliwa hatua.

“Nataka nikipita hapa siku yoyote kuanzia mwezi ujao nikute mkandarasi anabomoa jengo hili vinginevyo hatutaelewana,” alisema.

“Hili ni eneo hatarishi hata tuliosimama hapa hatari yoyote inaweza kutukuta lakini Manispaa ya Ilala haioni kwamba hapa kuna tatizo,” alisema.

Waziri alisema uvunjaji wa jengo hilo utakapoanza, wananchi wanaoishi jirani watatakiwa kuhama kwa muda kwa tahadhari.

“Mkuu wa Wilaya ya Ilala, wakianza kuvunja jengo hilo tafadhali waondoeni wakazi wote kwa sababu eneo hili litakuwa hatarishi,” alisema.

Jengo hilo linamilikiwa kwa pamoja kati ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Ali Raza Investment.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngulumi alisema kilichochelewesha ni makandarasi walioshinda zabuni hiyo kujitoa katika hatua za mwisho wakitoa sababu mbalimbali.

Alisema hivi sasa amepatikana mkandarasi Patty Interplan ambaye yuko katika hatua za mwisho za kupewa kazi hiyo.

“Tutaanza kazi kama ulivyoelekeza,” alisema Mngulumi.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, alisema atatoa ushirikiano kwa manispaa hiyo ili kuhakikisha jengo hilo linabomolewa.



Mwananchi
Dar es Salaam. CCM imemjibu mwanasheria Mkuu wa Chadema ikisema ili chama hicho kikuu cha upinzani kionekane kinapambana na ufisadi kwa vitendo, kinatakiwa kumuunga mkono Rais John Magufuli na kumvua uanachama Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho tawala, Nape Nnauye alisema Chadema iliachana na ajenda ya kupambana na ufisadi baada ya kumpokea Lowassa Julai mwaka jana baada ya jina lake kukatwa katika mchakato wa CCM kusaka mgombea wake wa urais.

“Sisi hatukumpitisha (Lowassa) awe mgombea wetu wa urais kwa sababu hiyo (ya ufisadi) na ndiyo maana yeye mwenyewe aliamua kuondoka na kwenda Chadema,” alisema Nape.

“Hata katika kampeni za uchaguzi mkuu, Chadema hawakuzungumzia ajenda ya ufisadi, ni kama Lowassa aliifunika tu.”

Alikuwa akimjibu Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ambaye katika mahojiano maalum na Mwananchi juzi, alisema ufisadi ni ajenda ya kudumu ya chama hicho kwa kuwa Rais Magufuli hataweza kuufumua wote katika kipindi cha miaka mitano.

Huku akichelea kueleza kiundani sababu za CCM kutomfukuza Lowassa kwa tuhuma za ufisadi mpaka alipoamua kujiondoa na kujiunga na Chadema, alisema kauli ya Lissu inalenga kuwahadaa Watanzania.

“Kauli ya Lissu ni ya kushangaza sana. Sisi tunajua jinsi ambavyo Chadema na washirika wake walivyojitenga na ajenda ya ufisadi. Kama kweli wanaupinga, basi wamuunge mkono Rais Magufuli ambaye kwa sasa anapambana na ufisadi kwa kasi,” alisema mbunge huyo wa Mchinga.

“Wakati mwingine kila jambo hufanyika kwa wakati wake. Suala la kupinga ufisadi CCM lilianza siku nyingi tangu enzi za kujivua gamba. Tumeendelea nalo mpaka watu wakajiondoa wenyewe,” alisema Nape.

Alisema hoja ya kupinga ufisadi ndani ya CCM ilikibeba chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kikapata ushindi mnono, huku Chadema iliyokuwa ikilia na ufisadi ikishindwa.

“CCM tulieleza sababu za kutompitisha Lowassa kugombea urais na hilo lilikuwa wazi,” alisema.

Katika ufafanuzi wake wa juzi, Lissu alisema ili apambane na ufisadi, Rais Magufuli anapaswa kuacha tabia za CCM na kumtaka mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) amtangaze mshindi halali wa Uchaguzi Mkuu ambao Chadema wanaamini Maalim Seif Sharif Hamad alishinda.

Pia Lissu alimtaka Rais ataje majina ya waliokwepa kodi ili kama watajitokeza kuwania uongozi, wadhibitiwe kwa kuwa Katiba imezungumza kwa maneno makali dhidi ya vitendo hivyo viovu.

Aidha, aliponda uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo anayetajwa kuhusiska katika sakata la uchotwaji wa Sh3060 bilioni kutoka akaunti ya Tetega Escrow.

Miaka 39 ya CCM

Akizungumzia maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM, Nnauye alisema uzinduzi utafanyika Januari 31, visiwani Zanzibar na mgeni rasmi atakuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.

Alisema kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa Februari 6, mjini Singida na yataongozwa na mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete ambaye aliiongoza Serikali ya Awamu ya Nne.

“Viongozi wa kitaifa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu watakaohudhuria maadhimisho haya watapangiwa shughuli za ujenzi wa chama na taifa katika wilaya zote za mkoa wa Singida, siku tatu kabla ya kilele cha maadhimisho,” alisema.

Alisema mikoa yote nchini inapaswa kuandaa shughuli hiyo wiki moja kabla ya maadhimisho, na kwamba lengo ni kufanya shughuli za ujenzi wa chama hicho katika maeneo yao.

“Tutakachokifanya wiki hiyo ni kupokea wanachama wapya, kufanya mikutano ya kuwashukuru wananchi kwa kuiamini CCM na kuichagua iendelee kuongoza, kuhamasisha wananchi kufanya kazi ili kujiletea maendeleo,” alisema.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya Ndugu Asumsyo Achacha akizungumza ofisni kwekwe juu ya zoezi linaloendelea la kuwasaka wahamiaji haramu mkoani humo. 

Na jamiimojablogu,Mbeya

Zoezi la kuwasaka wahamiaji haramu na wageni wanaofanya kazi bila kibali limeendelea kufanikiwa mkoani Mbeya ambapo jumla ya wageni 20 wamekamatwa mkoani humo kutokana na makosa mbalimbali likiwemo la kuingia nchini kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwakwe Afisa uhamiaji Mkoa wa mbeya Ndugu Asumsyo Achacha amesema hatua hiyo imefanyika ikiwa ni kutekeleza majukumu yao ya kila siku sanjali na kutekeleza agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Charles Kitwanga alilotoa hivi karibuni.

Aidha amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria mpya ya kuratibu ajira za wageni ,Sherii Na.1 ya mwaka 2015 ambayo inawataka wageni wote walioajiliwa hapa nchini kuwa na vibali vya kazi na hati za ukaazi nchini.

Afisa uhamiaji huyo amewataja raia hao waliokamatwa katika msako huo ni pamoja wakenya watatu (3)wamalawi 14 pamoja na wakongo watatu (3).

Aidha amesema kuwa mwaka 2015 jumla ya wahamiaji haramu 478 kutoka mataifa mbalimbali walikamatwa na kuchukuliwa hatua mbalimbali ikiwemo kufikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa nchini.

Amesema mbali na changamoto zilizojitokeza ikiwemo upungufu wa vitendea kazi ,fedha pamoja na rasilimali bado shughuli za uhamiaji mkoani humo ziliendelea kufanyika kama kawaida na kwa ufanisi mkubwa.

Pia Afisa Uhamiaji huyo amebainisha kuwa zoezi hilo ni endelevu hivyo ofisi yake itahakikisha kila mtu aliyevunja sheria anakamatwa hivyo ametoa wito kwa waajiri kuacha tabia ya kuwapa ajira wafanyakazi wa kigeni wasio na vibali vya kazi na ukaazi kwani msako huo utaendelea katika viwanda ,migodi mashuleni na mahotelini.

Mwisho.


No comments:

Post a Comment