TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 9, 2011

WEZI WALICHOMFANYIA DIAMOND!



.
EXCLUSIVE: usiku wa kuamkia jana, Wezi wameruka ukuta na kuingia kwenye nyumba anayomiliki mwimbaji DIAMOND Sinza na kufanikiwa kumuibia vitu kibao vikiwemo vifaa vya gari.
wakati wanaiba, DIAMOND hakushtukia chochote, baadae usiku ndio jirani yake akamuamsha akamwambia jamaa wamemuibia na kusepa.
vifaa vya gari alivyoibiwa thamani yake ni milioni 1.9! na ndani ya gari kulikua kuna nguo alizozitumia kushoot video yake mpya ambayo bado hajamaliza kuishoot na aliakiwa kuwa na nguo hizo hizo kwa ajili ya muendelezo wa SCENES.
kwenye gari pia kulikua na pete, saa 2, 1 ya rolex aliyonunua SOUTH AFRICA, cheni ya gold, viatu,mikanda na headphones za DR DRE ambavyo vyote wezi wamevibeba na mpaka sasa hajafaham ni watu gani waliohusika.
mlinzi alikuepo lakini walimteka na kumpiga, DIAMOND kuamka anakuta wamemfunga na gunia na damu kibao.

MASTAA WAANGUA VILIO KUTOKANA NA MSANII WA ZE COMEDY VENGU HALI YAKE KUENDENDELEA KUWA TETE



Na Joseph Shaluwa
WINGU zito limetanda kwa mastaa nchini wakionesha majonzi makubwa juu ya afya ya staa mwenye uzani wa juu Bongo, Joseph Shamba a.k.a Vengu (pichani) ambaye hali ya afya yake ni tete, kalamu ya Risasi Mchanganyiko inaandika kwa simanzi.

Vengu ambaye ni mchekeshaji wa Kundi la Orijino Komedi linalorusha michezo yake kupitia Kituo cha Runinga cha TBC1 cha jijini Dar es Salaam, kwa muda mrefu sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiendelea na matibabu huku ugonjwa unaomsumbua ukiwa siri.

Habari ambazo zimepatikana mpaka sasa, zinaeleza kwamba Vengu anasumbuliwa na maradhi ya kichwa bila kufafanua zaidi aina ya tatizo alilonalo kichwani.

Kwa nyakati tofauti, mastaa wameonesha vilio vyao juu ya staa mwenzao huyo kwa kile walichoeleza kuwa wanafichwa maradhi yanayomsumbua, lakini pia hawapati taarifa rasmi kutoka kwa watu wa karibu na msanii huyo ili nao waweze kuonesha undugu wao kama familia moja katika fani.

Mastaa waliopata fursa ya kuzungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, juzi Jumatatu na kutoa maoni yao ni Vincent Kigosi ‘Ray’, Ruth Suka ‘Mainda’, Maimartha Jesse, Aunt Ezekiel, Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Ambwene Yesaya ‘AY’ na Jacqueline Wolper.
Ray, Mainda, Aunt na Wolper ni wasanii wa filamu, Maimartha ni mtangazaji, AY ni mwanamuziki wa Bongo Fleva wakati Sugu ni Mbunge wa Mbeya Mjini huku akiendeleza harakati zake katika muziki wa kizazi kipya.

RAY
“Kaka kwenye hili suala (la Vengu) fedha si tatizo, tatizo ni usiri wa kinachomsumbua ndugu yetu. Hata sisi wasanii wenzake tukiuliza, hatupewi ushirikiano mzuri.

“Kwa mfano ni juzi tu, nilimpigia Masanja (Emmanuel Mgaya) na kumuuliza kuhusu tatizo la Vengu, hakusema chochote zaidi ya kuniambia anaumwa tu. Ugonjwa unafichwa. Jambo lingine ni utaratibu wa kumuona, sisi wasanii nadhani tungepewa kipaumbele kwenda kumuona mwenzetu, maana ICU (Chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum) hawaruhusu watu kuingia hovyo.

“Hata hivyo, siamini kama Komedi wameshindwa kumsaidia kama anahitaji usaidizi. Unajua Vengu anafanya kazi TBC1, televisheni ambayo ipo chini ya serikali, nini kinashindikina?” alisema na kuongeza:
“Huu ni wakati wa wasanii wote nchini kushikamana. Kwa kufanya hivyo tutaonesha umoja wetu.”

AY
“Najua kwamba jamaa anaumwa, lakini sijapata details (maelezo) zaidi ya kusikia anaumwa kichwa. Inauma sana kwa kweli, unajua Vengu ni msanii mwenzetu na katika kipindi kama hiki anahitaji sana faraja yetu.

“Kiukweli bado sijaenda kumuona, lakini nitajipanga nikamuone. Kama kutakuwa na harambee ya kumsaidia, nipo tayari muda wowote kutoa kile nitakachojaliwa.”

MAIMARTHA
“Maradhi hayana hodi. Leo kwa Vengu kesho kwa mwingine. Mastaa tuoneshe mshikamano katika kumsaidia mwenzetu. Nilipata bahati ya kwenda kumuona Muhimbili siku kama sita zilizopita, hali yake ni mbaya...
“...maskini! Haongei...hajitambui. Tunapaswa kuchangishana tumsaidie. Sisi ndiyo ndugu zake. Nashukuru sana kwa kutukumbusha na ninawaomba mastaa wenzangu tumkumbuke jamani.”

SUGU
“Kiukweli sijapata nafasi ya kwenda kumuona, majukumu yamenibana sana, lakini najipanga niende. Kwa mara ya kwanza nilisoma taarifa za kuugua kwake kwenye gazeti, tena nilimuona Mhe. Rais (Dk. Jakaya Kikwete) naamini atakuwa amemsaidia.

“Unajua rais ndiyo kila kitu katika nchi, kwa hiyo kama alikwenda kumuona, nina imani ikiwa Vengu anahitaji msaada wowote, basi ni lazima atakuwa amepatiwa. Juzi tu, nimesoma kwenye gazeti, serikali imewapeleka watoto kama 20 hivi India kwa matibabu, naamini kwa Vengu ambaye ni msanii na ana mchango kwa taifa ni rahisi zaidi.

“Sema kuna tatizo la taarifa. Washkaji zake (Orijino Komedi) hawajajipanga vizuri kuhusu kutoa taarifa. Ukiachana na hao, kuna vyama vya wasanii, nadhani walipaswa kutoa maelekezo vizuri kwa wasanii badala ya kuona na kusikia kutoka kwenye vyombo vya habari.”

MAINDA
“Nilisoma kwenye gazeti, lakini kiukweli inaumiza sana. Kuna umuhimu wa Kundi la Orijino Komedi kutoa taarifa rasmi kwa wasanii, maana tupo gizani. Mimi nilisikia juujuu kuwa anaumwa, lakini nilipoona kwenye gazeti ndiyo nikashtuka. Sikujua kama yupo serious (amezidiwa) vile. Namuombea kwa Mungu ampe afya.”

WOLPER
“Ndiyo kwanza nasikia habari hizi kutoka kwako, nipo busy namuuguza mama yangu ambaye ni mgonjwa sana. Enhee... amelazwa wapi ili nikitoka hapa nikamuone?”
Risasi Mchanganyiko lilimtajia wodi na hospitali aliyolazwa ili akamtembelee kama alivyosema mwenyewe kwamba hana taarifa zozote!

AUNT
“Sikuwa najua chochote kuhusu Vengu, nilisoma tu gazetini. Kinachoonekana ni kwamba, haya mambo yanapelekwa kimyakimya sana. Sisi kama wasanii wenzake tuna haki ya kupata taarifa ya moja kwa moja juu ya afya ya mwenzetu lakini pia tuna wajibu wa kumsaidia.

“Wasanii hatuna umoja wa kweli, nashauri tuitane, tuketi na kujadiliana namna ya kumsaidia. Ni kweli Kibongobongo wasanii hatuna uwezo kivile wa kumsaidia kifedha, lakini kwa sababu tuna wadau wapenda burudani wanaweza kutupa support kama sisi tukianza. Wasanii tuamke, tushikamane tumsaidie mwenzetu.”

KALAMU YA RISASI
Hakuna jambo gumu linaloshindikana kwa Mungu, Vengu kwa sasa ni mgonjwa lakini kwa maombi yetu Watanzania, siku moja ataamka na kuendelea kutoa burudani kwa jamii. Tunamuombea kwa Mungu apone haraka– MHARIRI.

DIAMOND AMWAGA WEMA SEPETU


Musa Mateja na Imelda Mtema
“Washikaji, nimewaita hapa nifunguke mbele yenu kuwa nimemmwaga rasmi yule demu (Wema) kwa sababu hapatani na mama yangu (Sandra Sammy).

ALINILAZIMISHA NITENGANE  NA MAMA
“Kwanza Wema amekuwa akinilazimisha nitengane na mama yangu, yaani nimrudishe kule Tandale tulipokuwa tukiishi mwanzo , halafu mimi na yeye tuishi Sinza (Madukani), jambo ambalo sipo tayari kulifanya.
“Mimi na mama tumetoka mbali, hakuna kama yeye, alikuwa akishinda njaa ili mimi nisome, alinilea kwa shida sana, hata siwezi kuelezea kwani nikikumbuka huwa natokwa machozi, kwa hiyo siwezi kumtelekeza kwa sababu ya Wema.
“Hata katika muziki, nakumbuka nilishamuibia pete yake ya dhahabu nikaenda kuiuza ili nirekodi muziki na alinivumilia.
NI WAKATI WA MAMA ‘KUINJOI’
“Piga ua, huu ni wakati wa mama yangu kula na ‘kuinjoi’ matunda ya mwanaye, mapenzi hayawezi kusababisha nimtende vibaya. Natamka rasmi huyu demu nimemmwaga bwana.”
SWALI LA MWANDISHI WA IJUMAA
“Mlianza mapenzi muda mrefu na ni wiki mbili tu zimepita tangu ulipomvisha pete ya uchumba, je, hukujua kwamba mambo kama haya yangetokea?
DIAMOND AKAJIBU
“Sikuligundua hilo mapema na pia si unajua mambo ya ujana tena? Ukweli ni kwamba tukio hili limenikumbusha kuwa ujana ni jalala linalotupwa kila aina ya takataka.”
UPANDE WA WEMA
Baada ya Diamond kumwaga unga na ishu hiyo kuwa gumzo jijini Dar usiku kucha, kama ilivyo desturi ya gazeti hili namba moja kwa habari za mastaa nchini, asubuhi na mapema (Jumatano), mapaparazi wake wa kuheshimika walimsaka Wema ili kupata mzani wa habari hiyo.
NDANI YA HOTELI YA LAMADA
Kutokana na uzito wa habari yenyewe, Ijumaa lilisaga lami hadi Hoteli ya Lamada Ilala, chumba namba 35 flati ya Mikumi ambapo Wema alikuwa kambini kwa ajili ya kurekodi filamu.
HALI ILIKUWA HIVI
Baada ya kubisha hodi, ‘mkaribisha wageni’ alikuwa  Elizabeth Michael ‘Lulu’, alifungua mlango ambapo Wema alishuhudiwa akinyanyuka na kwenda kuosha uso, aliporejea na kuwaona ‘polisi’ wa Ijumaa wakifunga ‘makamera’ yao alipaza sauti na kufuatiwa na kilio: “Maweee! Nimeachwa? Nyiii….nyiiiii.”
Lulu: Nyamaza Wema usikie kilichowaleta.
Ijumaa: Mambo vipi Wema?
Wema: Hata salamu yenu sitaki, niambieni nimeachwa?
Ijumaa: Poa, ili mgonjwa apone lazima achomwe sindano inayouma au ameze vidonge vichungu. Iko hivi Wema; jana pale Lion Hotel, Sinza,  Diamond alitangaza rasmi kukutema kwa sababu eti umekuwa ukimlazimisha kumtenga mama yake ili muishi peke yenu, yeye hayupo tayari kufanya hivyo, je, hili unalizungumziaje?
Wema: (kilio) siko tayari kuzungumza chochote.
Ijumaa: Tafadhali waambie mashabiki wako umeipokeaji taarifa hii?
Wema: Amenidhalilisha, nitaweka wapi uso wangu? Anyway, niacheni nitawatafuta baadaye niongee.
Lulu: Dada Wema, funguka tu kile unachokijua, itakusaidia watu wajue ukweli.
Wema: No, please. Waondoke tu nitawatafuta baadaye.
UTABIRI
Ili kuthibitisha kuwa kile kinachoandikwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers kina uhakika asilimia zote, wakati hayo yanatokea, tayari gazeti tumbo moja na hili, Risasi Mchanganyiko toleo namba 844 la Jumatano wiki hii lililokuwa na kichwa cha habari: WEMA, DIAMOND HAKUNA NDOA, lilitabiri na kuweka vigezo kuwa Wema na Diamond hawatadumu.
Aidha, Gazeti la Risasi Jumamosi iliyopita, ukurasa wa 16 kulikuwa na habari yenye kichwa; ETI WEMA, MAMA MKWE WAKE HAWAIVI.
Diamond alionesha kutokubaliana na madai hayo, lakini yaliyotokea yameweka wazi.
WADAU WANASEMAJE?
Kwa mujibu wa wadau walioinyaka habari hiyo walilieleza Ijumaa kuwa haijawahi kutokea Wema akamwagwa na midume kwani yeye ndiye huwa anawamwaga.
“Ama kweli mtenda akitendewa…safari hii kaachwa yeye!” alisema mmoja wa wadau hao.
ANATAMANI DUNIA IRUDI NYUMA
Uchunguzi wa Ijumaa ulibaini kuwa usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii, Wema hakupata usingizi kwa kuwa alishanusa dalili za tukio hilo.
“Ukweli Wema hakulala kabisa, alikuwa akijigeuza mara kwa mara na kutaja jina la Diamond huku akilia, alipoulizwa kulikoni alijibu: “Natamani dunia irudi nyuma ili lile tukio la kuvishwa pete ya uchumba pale New Maisha Club wiki mbili zilizopita lifutike,” alisema mmoja wa wasanii aliyekuwa naye kambini hapo.

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AONGOZA WATANZANIA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA


Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam mchana huu hapa akisalimiana na Rais wa Namibia Mhshimiwa Hifikepunye Pohamba. FULLSHANGWE inakumuvuzishia moja kwa moja matukio ya maadhimisho hayo kutoka kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ili kukujuza mambo mbalimbali yaliyojiri katika sherehe hizo.
Rais Jakaya Kikwete akielekea Jukwaa kuu mara baada ya kukagua gwaride katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru huku akiwa ameongoza na na Mkuu wa Majeshi nchini Jenerari Davis Mwamunyange.
Rais Jakaya Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kikosi hiki ni cha Jeshi la Wananchi wanawake
Rais Jakaya Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kikosi hiki ni cha Jeshi la Wananchi wanaume.
Rais jakaya Kikwete akipokea heshima wakati mizinga ikipigwa na jeshi la wananchi kwa heshima ya Rais.
Hiki ni kikosi cha Jeshi la wananchi wanamaji kikiwa tayari kutoa heshima kwa amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tamnzania Dk. Jakaya Kikwete.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akipungia mkono wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya kuongoza sherehe za miaka 50 ya Tanzania.
Msafara wa Rais Dk Jakaya Kikwete ukiwasili kwenye uwanja wa Uhuru tayari kwa kuongoza watanzania katika sherehe za miaka 50 ya Tanzania.
Walinzi wa rais walikuwa kivutio katika sherehe.wakati msafara wa Rais Dk. Jakaya Kikwete ukiwasili katika uwanja wa Uhuru leo.(Picha Zote na Shaaban Mpalule).

WATANZANIA WATAKIWA KUWA MAKINI NA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA.

Na Lydia Churi- MAELEZO
Bagamoyo –PWANI.
WATANZANIA wametakiwa kutowapa nafasi watu wanaopotosha mchakato wa kupata Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali washiriki mchakato huo kwa amani na utulivu.
Akizungumza na Vijana wa Chama cha Mapinduzi wa wilaya ya Bagamoyo leo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel  Nchimbi  amesema kuwa Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya  Kikwete ana nia njema ya kuhakikisha kuwa watanzania wanapata katiba mpya baada ya kutimiza miaka 50 ya uhuru wa nchi yao.
Amesema taarifa zinazotolewa na serikali juu ya kuanza kwa mchakato wa katiba mpya ni za dhati na serikali ina nia njema katika hili hivyo wananchi hawana budi kuwapuuza wale wanaopotosha taarifa hizo.
Waziri  Nchimbi  amesema hayo wakati wa  uzinduzi wa  Mnara wa kumbukumbu ya mkutano wa kwanza wa TANU kitaifa uliofanywa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika mwaka 1954.
 Amewaasa  vijana kuwa Mnara huo usibaki kuwa kumbukumbu tu bali  wayafanyie  kazi yote yaliyofanywa na waliowatangulia.
Amewataka vijana kudumisha amani na utulivu uliopo nchini kwa faida ya vizazi vijavyo na kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara kwa kutathmini kazi zilizofanywa na waanzilishi ili waweze kuwarithisha watoto wao baadaye.
Naye Katibu mkuu wa UVCCM Taifa, Martin Shigella akizungumza wakati wa uzinduzi huo amewataka  vijana wa CCM kuwa na moyo wa kujitolea ili waweze kuliletea taifa  maendeleo.

Tuesday, December 6, 2011

KILIMANJARO STARS USO KWA USO NA UGANDA YATINGA NUSU FAINALI KWA KUINYUKA MALAWI 1-0

Timu ya Soka ya Kilimanjaro Stars, muda huu imefanikiwa kutinga hatua ya Fainali ya Michuano ya Tusker Challenge Cup kwenye Uwanja wa Taifa baada ya Nurdin Bakari kuifungia timu yetu ya Tanzania goli katika dakika ya 36 ya mchezo kipindi cha kwanza kwa shuti kali , lilikwenda moja kwa moja na kumshinda mlinda mlango wa Timu ya Malawi.

kwa ujumla mchezo ulikuwa mkali na wa kusisimua, zaidi niipongeze timu ya Kilimanjaro Stars kwa kuonyesha kandanda safi ambalo watanzania wengi hawakutarajia kupata ushindi kama huo, pamoja na ushindi huo pia pongezi nyingi ni kwa mlinda mlango wa Kilimanjaro Juma kaseja kutokana na kuonyesha umahiri mkubwa katika kulinda lango.

pamoja na mabadiliko ya hapa na pale lakini hadi mwisho KILIMANJARO STARS 1-0  MALAWI, ambapo sasa kwenye Nusu Fainali timu ya Rwanda itakutana na Timu ya Sudan, wakati Kilimanjaro Stars wenyeji watakutana na Timu ya Uganda.

SHEREHE ZA MAHAFALI YA CHUO CHA ARDHI DAR ES SALAAM

Mhitimu wa Shahada katika  Survey  & Geographic Infomation Systeam-Chuo Kikuu Ardhi-Dar es Salaam, Elius Chundu, katika pozi
Mhitimu wa Shahada katika  Survey  & Geographic Infomation Systeam- Elius Chundu, akiwa na wadogo zake, muda mfupi baada ya kumalizika hafla hiyo katika chuo cha Ardhi Dar es Salaam
Mhitimu wa Shahada katika  Survey  & Geographic Infomation Systeam- Elius Chundu, akiwa na wana familia
Mhitimu wa Shahada katika  Survey  & Geographic Infomation Systeam- Elius Chundu, akivishwa shada ya maua na Rafiki yake
 Mgeni Rasmi akiendelea kutangaza wahitimu wa Mahafali ya Chuo Kikuu Ardhi Dar es Salaam
Mhitimu wa Shahada katika  Survey  & Geographic Infomation Systeam- Elius Chundu,akimlisha keki mke wake, wakati wa sherehe baada ya mahafali hayo
Mhitimu wa Shahada katika  Survey  & Geographic Infomation Systeam- Elius Chundu, akiwa na rafiki yake wakati wa kupata menyu
Mhitimu wa Shahada katika  Survey  & Geographic Infomation Systeam- Elius Chundu, akigonganisha glass na ndugu zake
Mhitimu wa Shahada katika  Survey  & Geographic Infomation Systeam- Elius Chundu akipokea ua
Mhitimu wa Shahada katika  Survey  & Geographic Infomation Systeam- Elius Chunduakiwa na ndugu zake
Mhitimu wa Shahada katika  Survey  & Geographic Infomation Systeam- Elius Chundu akipokea zawadi ya ua kutoka kwa mke wake (Picha Zote na Shaaban Mpalule).

MAHAFALI YA 46 YA CHUO CHA BIASHARA CBE DAR ES SALAAM

 Baadhi ya wahitimu wa chuo cha biashara CBE Dar es Salaam 2011
 Baadhi ya wahitimu wa chuo cha biashara CBE Dar es Salaam 2011
 Baadhi ya wahitimu wa chuo cha biashara CBE Dar es Salaam 2011
 Baadhi ya wahitimu wa chuo cha biashara CBE Dar es Salaam 2011
Mhitimu wa Stashahada ya Uongozi katika Biashara, Paul Mkoga - (wa kwanza kushoto) akiwa katika pozi wakati wa mahafali Katika chuo cha Uongozi wa Biashara (CBE)-Dar es Salaam 2011-
Mhitimu wa Stashahada ya Uongozi katika Biashara, Paul Mkoga - (wa kwanza kushoto) akiwa katika pozi wakati wa mahafali Katika chuo cha Uongozi wa Biashara (CBE)-Dar es Salaam 2011-
Mkurugenzi wa Mwana Milambo Bend, Amoni Mkoga(kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mhitimu wa Stashahada ya Uongozi katika Biashara, Paul Mkoga - (kulia) wakati wa mahafali Katika chuo cha Uongozi wa Biashara (CBE)-Dar es Salaam 2011-kati kati ni Dada yao Mkubwa Lucy Mkoga na Rafiki yake
Dada wa Mhitimu wa Stashahada ya Uongozi katika Biashara, Paul Mkoga -Lucy Mkoga (kushoto), akikabidhi zawadi ,wakati wa mahafali Katika chuo cha Uongozi wa Biashara (CBE)-Dar es Salaam 2011-
Mhitimu wa Stashahada ya Uongozi katika Biashara, Paul Mkoga - (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha na baadhi ya wanafamilia wakati wa sherehe  iliyofanyika Dar es Salaam 2011-
Mhitimu wa Stashahada ya Uongozi katika Biashara, Paul Mkoga - akiwa katika pozi  Katika chuo cha Uongozi wa Biashara (CBE)-Dar es Salaam 2011-
Mhitimu wa Stashahada ya Uongozi katika Biashara, Paul Mkoga - (wa pili kulia) akiwa katika na kaka yake Amon Mkoga(wa kwanza kulia) Dada yake Lucy Mkoga (wa Pilia Kushoto na rafiki yao, wakati wa mahafali Katika chuo cha Uongozi wa Biashara (CBE)-Dar es Salaam 2011
Bendi ya jeshi ambayo ilitumbuiza katika mahafali ya chuo cha Uongozi na Biashara CBE 2011(Picha Zote na Shaaban Mpalule)

Tuesday, November 29, 2011

RAIS WA AWAMU YA TATU NDG, WILIAM BENJAMINI MKAPA, ALIPOTEMBELEA MAHAFALI YA PILI YA CHUO KIKUU DODOMA

mhitimu wa shahada ya kwanza ya Uhusiano wa kimataifa katika chuo kikuu cha Dodoma, Balu Lada(kulia), akipeana mkono na mmoja wa walimu wake muda mfupi baada ya kumaliza mahafari ya pili ya chuohicho juziiiii, mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa rais mstaafu wa awamu ya Tatu ndg. Benjamini Wiliam Mkapa.

Mhitimu wa Shahada ya Uongozi katika biashara-Chuo Kikuu cha Dodoma, James Mande(nyuma)akiwa na wazazi wake  pamoja na wadogo zake Veronica Mande, Muda mfupi baada ya mahafali ya pili ya chuo hicho. kati ni rafiki wa James mande
Mhitimu wa Shahada ya Uongozi katika biashara-Chuo Kikuu cha Dodoma, James Mande(kushoto)akipokea zawadi ya Shada la Maua kutoka kwa mdogo wake Veronica Mande, Muda mfupi baada ya mahafali ya pili ya chuo hicho. kati ni rafiki wa James mande
 Baadhi ya Wahitimu wa mahafali ya pili ya Chuo Kikuu Cha Dodoma, wakipiga picha na ndugu zao muda mfupi baada ya hafla hiyo chuoni hapo mjini Dodoma
 Mhitimu wa Mahafali ya pili ya chuo Kikuu dodoma, akipokelewa na ndugu zake
 Mhitimu wa mahafali ya pili ya chuo kikuu dodoma 2011- akipozi katika picha
 Wahitimu wa mahafali ya Pili ya Chuo Kikuu Dodoma, wakiondoka kwenye Hafla ya Mahafali ya Chuo Kikuu hicho cha Dodoma 2011
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamini Wiliam Mkapa,(kati) akiondoka kwenye hafla ya Mahafali ya Pili ya chuo kikuu cha Dodoma. ambapo alikuwa Mgeni Rasmi.
 
Mgeni Rasmi wa mahafali ya Pili ya chuo kikuu cha Dodoma, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mh. Benjamini Wilium Mkapa, akiondoka kwenye hafla ya mahafali hayo mjini Dodoma
 Bendi ya Kikosi cha Jeshi, kikiongoza Mgeni Rasmi, Rais wa awamu ya Tatu kuondoka kwenye hafla ya mahafali ya pili ya chuo kikuu dodoma 2011.(Picha Zote na Shaaban Mpalule)

Tuesday, November 22, 2011

LAKAIRO MWANZA YADHAMINI MISS UTALII VYUO VIKUU KANDA YA KATI 2011-2012


 Hoteli ya kitalii ya Lakairo Hotel ya jijini Mwanza,imejitokeza kudhamini shindano la Miss Utalii Vyuo Vikuu - Kanda ya kati,lililopangwa kufanyika Dodoma siku ya uhuru tarehe 9-12-2011. 

Akithibitisha udhamini huo, mkurugenzi wa hoteli hiyo inayomilkiwa na Mheshimiwa Lameck Okambo Airo mbunge wa wa jimbo la Rorya,Daniel Airo alisema kuwa hoteli hiyo inatoa jumla ya shilingi lakitano (500,000/=) kwa ajili ya kuchangia zawadi za washindi wa shindano hilo,linaloshirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mikoa ya kanda ya kati,ikiwemo mikoa ya Dodoma,Singida na Tabora. Daniel alisema kuwa wameamua kudhamini shindano hilo kwa kutambua umuhimu na mchango wake katika kukuza sekta ya utalii nchini,aliongeza kuwa ushiriki wa wanafunzi wa vyuo vikuu katika shindano hilo ni fulsa nyingine ya pekee ya kukuza utalii wa ndani ,kwani iwapo wasomi hao wakihamasika na suala zima la utalii hususani utalii wa ndani basi ni rahisi jamii kuiga na kufuata mfano wa wasomi hao,ambao pia ndio viongozi watarajiwa katika nyanja mbalimbali nchini baada ya kuhitimu masomo yao.

Wadhamini wengine waliojitokeza kudhamini shindano hilo ni Duka la mavazi na vipodozi la Happy Fashion wanaotoa zawadi yenye thamani ya shilingi laki tatu (300,000/),Master Pub , NAM Hotel,Becko Qulity Centre wanatoa zawadi yenye thamani ya laki tatu kwa mshindi wa vipaji,New Soft Saloon,CF Communication & Stationary, Club 84 na Royal Village Hotel,PAPA MSOFE.

Washindi wa 1-5 na wa taji la vipaji watawakilisha Vyuo vikuu kanda ya kati katika fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2011/12 zilizopangwa kufanyika mwezi February 2012, ambapo washindi wa taifa watawakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia ya Miss Tourism World,Miss United Nations,Miss Tourism United Nations,Miss Heritage World,Miss Globe International,Miss Tourism University World na United World International Pageant