TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, December 22, 2013

IRINGA SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI WAFANYABISHARA WATAKAO PANDISHA BEI YA VYAKULA MSIMU HUU WA SIKUKUU YA KRISMAS NA MWAKA MPYA



RC Iringa Dr Christine  Ishengoma
Mkuu wa mkoa  wa  Iringa  Dr Christine  Ishengoma ametuma  salama  kali za  Krismas na Mwaka  mpya kwa   wafanyabiashara  watakaopandisha bei  ya  vyakula msimu  huu wa sikukuu kuwa watachukulia hatua  kali.
 
Huku  akiwataka wakurugenzi  wa Halmashauri  zote za wilaya ,wakuu wa wilaya ,maofisa  biashara  wa  wilaya  na mkoa huo  kuanza  kuzunguka mitaani  kuchunguza  bei ya  bidhaa na  kuwataka kuchukua hatua kwa  wote  wanaliopandisha  bei kiholela. 
Akizungumza na  wanahabari jana  ofisini  kwake  ,mkuu  huyo wa mkoa alisema  kuwa imekuwa ni kawaida kwa baadhi  ya  wafanyabiashara  kutumia  sikukuu mbali mbali  kujipatia fedha  kwa kuwanyonya wananchi jambo ambalo katika mkoa huo halitavumiliwa kamwe.
Alisema  kuwa  lengo  la  serikali  ya  mkoa kuwabana  wafanyabiashara ni kutaka  kuona  wananchi  wanasherekea  sikukuu  hizo   na kununua vyakula na vitu  mbali mbali  vya sikukuu kulingana na bejeti  waliyoitenga  kwa  sikukuu  hizo.
” Serikali  ya  mkoa haitakubali  kuona  wananchi  wakiibiwa kwa kuuziwa vyakula kwa bei   kubwa za  sikukuu….tumejipanga  kuchukua hatua  kali na tunaomba  wananchi pia  kutoa ushirikiano “
Hata  hivyo mkuu  huyo wa mkoa alivipongeza  vyomba vya  habari  mkoani Iringa kwa mchango  mkubwa  wa kuhamasisha maendeleo   na kutaka  kuonyesha  ushirikiano katika wakati  huu wa sikukuu kwa  kufanya  uchunguzi  wa  wafanyabiashara  wanaopandisha  bei.
Katika hatu  nyingine  mkuu  huyo wa mkoa aliwataka  wakulima  kutumia mvua  zinazoendelea  kunyesha  kwa  kupanda  mazao mbali mbali yakiwemo  yale yanayohimili ukame kwa maeneo  yeye  changamoto  ya  mvua.
Pia  aliwataka  maofisi  kilimo na  mabwana shamba  kuachana na mpango  wa kuvaa suti na  kushinda maofisini wakati  huu wa msimu wa kilimo badala ya kwenda  kuwaelimisha  wakulima .
Dr  Ishengoma  aliwataka  wakulima  kuendelea  kutumia mbolea  ya Minjingu ambayo  alidai hata  yeye  amekuwa akiitumia na ni miongoni mwa mbolea  bora nchini na kuwataka  kuepuka maneno ya kukatisha tamaa yanayoendelea  kutolewa na  watu juu ya mbolea  hiyo.
Wakati  huo huo  serikali  ya  mkoa  wa Iringa imepiga marufuku  wazazi kuwaruhusu watoto  wao kwenda  kushiriki madisco toto  ambayo alidai ni hatari  na ni  vema  wazazi na walezi wa watoto mkoani Iringa  kuwa makini na kuachana na tabia ya  kuwaacha  watoto  wao peke  yao wakati  huu wa sikukuu.

MH. LOWASSA ASHIRIKI TAMASHA LA WAENDESHA BODABODA JIJINI DAR

 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwahutubia Vijana waliojiajiri kwa kazi ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.Mh. Lowassa alikuwa ni Mgeni Rasmi katika hafla hiyo iliyofana sana.
 Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza machache kwenye Tamasha hilo kabla ya Kumkaribisha Mgeni Rasmi kwenye Tamasha hilo,Mh. Edward Lowassa (kulia).Katikati ni Kamanda wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R. Mpinga.
Kamanda wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R. Mpinga akizungumza akitoa hotuba yake mbele ya Vijana waliojiajiri kwa kazi ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala,Michael Roewe akisoma Risala yao mbele ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea Risala ya Chama cha Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam,Kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala,Michael Roewe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi Zawadi kwa Afisa wa Benki ya FNB kwa kutoa Mchambo mkubwa kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi Zawadi kwa Afisa wa Mfuko wa PSPF kwa kutoa Mchambo mkubwa kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea Zawadi Kutoka kwa Mwenyekiti wa Muda wa Shirikisho la Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam,Said Magamba.
Salamu kwa waendesha Bodaboda.
Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya wanaounda kundi la KIBEGA,wakitoa Burudani mbele ya Waendesha Bodaboda hao.

Sehemu ya Waendesha Bodaboda hao wakifatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi.
Msanii Linex akifanya yake Viwanjani hapo mapema leo.
Mgeni Rasmi katika Tamasha la Waendesha Bodaboda Mkowa wa Dar es Salaam,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka viwanjani hapo huku Vijana Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam wakimsindikiza kwa shangwe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwaaga Vijana wa Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati alipokuwa akiondoka viwanjani hapo huku shangwe zikitawala viwanjani hapo.
Vijana wa Bodaboda wakilisukuma gari la Mh. Lowassa ikiwa ni sehemu ya Furaha waliokuwa nayo.

ALEX MSAMA:SOLOMON MAHLANGU KUTOKA AFRIKA KUSINI KUTUA LEO


1Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Krismas Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam wakati alipoelezea maandalizi ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika siku ya sikukuu ya Krismas kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam likishirikisha waimbaji wa injili kutoka mataifa mbalimbali na wa hapa nchini wakiongozwa na mwaimbaji wa kimataifa kutoka nchini Afrka Kusini Solomon Mahlangu anayetarajiwa kuwasili kesho nchini akitokea Afrika Kusini. 2Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Krismas Bw. Alex Msama akisisitiza jambo katika mkutano huo 3Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Krismas Bw. Alex Msama akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo.

MBEYA CITY KUINGIA MZIGONI RASMI BAADA YA KRISMASI, MWAMBUSI AACHIA MKWARA MZITO NGWE YA PILI!!

1239581_432061306914560_864943343_n1
KLABU ya Mbeya City inatarajia kuanza kambi yake rasmi baada ya sikukuu ya krismasi kuongeza makali yao kuelekea mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kushika kasi mnamo januari 25 mwakani.
Akizungumza leo hii, kocha mkuu wa klabu hiyo, Juma Mwambusi  amesema kwasasa wanaendelea na mazoezi ya kawaida ambapo vijana wake wanatokea kwao, lakini baada ya sikukuu wataingia kambini rasmi.
“Tunafahamu kuwa timu nyingi zinachukua tahadhari kubwa zaidi kwa ajili yetu. Hii ni changamoto kubwa kwetu na ndio maana mikakati yetu ni kuwa na kambi bora kuandaa vijana wetu kwa ajili ya kuwa na kasi zaidi mzunguko wa pili”. Alisema Mwambusi.
Mwambusi aliongeza kuwa wachezaji wake wapo katika hali nzuri na kilichobaki ni kuanza programu ya mazoezi rasmi.
Kocha huyo aliyejizolea umaarufu baada ya kumaliza mzunguko wa kwanza bila kufungwa mechi yoyote alisisitiza kuwa ana kikosi bora na ndio maana hakufanya usajili katika dirisha dogo la usajili.
“Ninao vijana wengi wenye kiwango cha juu, ni maamuzi yangu kumtumia yupi na kumuacha yupi. Tutafanya vizuri kutokana na ubora wetu”. Aliongeza Mwambusi.
Aidha Mwambusi amewaomba mashabiki wao Tanzania nzima kuendelea kuwa na ushirikiano mkubwa kama mzunguko wa kwanza.
“Mashabiki ni mchezaji wa kumi na mbili. Nawashukuru sana kwa kuendelea kutuunga mkono, lakini nawaomba waendelee kuwa nasisi katika harakati zetu. Hatuna cha kuwalipa zaidi ya kuucheza mpira wenyewe kwa kiwango cha juu”. Alisema Mwambusi.
Mbeya City FC  ilimaliza mzunguko wa kwanza katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 27 sawa na Azam fc waliopo nafasi ya pili kwa pointi sawa na klabu hiyo, lakini wana wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Vinara wa ligi hiyo ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo, klabu ya Dar Young Africans wenye pointi 28, huku watani zao wa jadi, Simba Sc wapo nafasi ya nne kwa pointi zao 24.

UFUNGUZI WA MATEMBEZI YA UVCCM ZANZIBAR

A4085 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamis,alipowasili katika  uwanja wa  Mpira Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika ufunguzi wa matembezi Umoja  wa  Vijana wa CCM Zanzibar katika kuadhimisha miaka 5o ya Mapinduzi.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
A4087 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu  wa UVCCM Zanzibar  Shaka Hamdu Shaka,alipowasili katika  uwanja wa  Mpira Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika ufunguzi wa matembezi Umoja  wa  Vijana wa CCM Zanzibar katika kuadhimisha miaka 5o ya Mapinduzi.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.] 
A4374 
Vijana wa UVCCM wakiwa wamebeba Pich za Viongozi wa Chama katika Matembezi ya Madhimisho ya miaka 5o ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(hayupo pichani)kuanzia  Micheweni kuelekea Wete Mkoa wa Kasakazini Pemba. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.] 
A4134 
Vijana wasoma Utenzi Saumu Mohammed,na Rehema Juma,wakiwaburudisha wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliohudhuria katika ufunguzi wa Matembezi ya Umoja wa Vijana UVCCM Zanzibar ya kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi,ambapo  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,atafungua matembezi hayo yatakayoanza   Micheweni ,Mkoa wa Kaskazini Pemba, [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.] 
A4253 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,alipokuwa akizungumza na Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar na Wanachama wa CCM Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo,pamoja na kuyafungua Matembezi ya Umoja huo ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, katika uwanja wa Mpira Micheweni kwa Shaamemata, (kushoto) Naibu Katibu Mkuu  wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai, [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
A4127 (1) 
Vijana wa Chama cha Mapinduzi,UVCCM wa Mikoa na Wilaya wakiwa katika uwanja wa Mpira wa Micheweni kwa Shaamemata,Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakisubiri ufunguzi wa matembezi ya umoja huo ya kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi,na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

MANJI AMKINGIA KIFUA KASEJA, ASEMA SIMBA KUMTUNGUA MATATU SIO KIGEZO CHA KUSHUSHA THAMANI YAKE!!


KASEJA32 
Juma Kaseja `Tanzania One` amekingiwa kifua na bosi wake ,Yussuf Manji baada ya kufungwa mabao matatu jana kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji amemkingia kifua mlinda mlango wao mpya, Juma Kaseja baada ya kufungwa mabao matatu jana akiwa langoni katika mchezo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya watani zao wa jadi, Simba Sc ambao Mnayama alishinda 3-1.
Mbao ya Simba sc katika mechi ya jana yalifungwa na Amis Tambwe aliyepiga mawili na kiungo Juma Awadh Issa, wakati la Yanga lilifungwa na Emmanuel Okwi.
Akizungumza leo na waandishi wa habari, Manji amasema hawakumsajili Kaseja kwa ajili ya kuifunga Simba SC, bali malengo yao ni kupata msaada wake katika michuano mikubwa ya soka barani Afrika.
Baada ya Yanga kufungwa jana, huku Kaseja akiwa langoni, katibu mkuu wa baraza la wazee la klabu hiyo, Mzee Ibrahim Akilimali, iliulaumu uongozi kwa kusema kuwa  usajili wa kipa huyo ni makosa na hauna baraka zao.
Manji amejibu mapigo na kueleza kuwa umri unazidi kumtupa mkono mzee Akilimali  kwani ameshindwa kukumbuka kuwa , huyo Ivo mwenyewe aliondoka Yanga akiwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita na uongozi wa wakati huo kwa tuhuma za kufungisha kwenye mechi dhidi ya  Simba SC.
Pia Manji alihoji wakati Simba ikisawazisha mabao yote matatu  katika mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania bara oktoba 20 dhidi ya Simba sc , Kaseja alikuwa langoni?.
Mwenyekiti huyo alisema  si jambo zuri kulaumiana pale yanapotokea makosa, bali ni kuwa na mshikamano kwa ajili ya maendeleo ya Yanga.
“Tunaheshimu uwezo wa Kaseja, thamani yake ni kubwa. Hakuna kipa yeyote nchini aliyedaka mechi nyingi za kimataifa kama kipa huyu. Kamwe hatuwezi kumshusha thamini yake na uwezo wake kwa kufungwa mabao matatu kwenye mechi ya jana ambayo ilikuwa sawa na bonanza tu”. Alisema Manji.
Manji alisema mechi ya jana walicheza kumfurahisha mdhamini wao, TBL, lakini haikuwa na maana yoyote na matokeo ya kufungwa wala hayajawaingia akilini.
Hata hivyo Manji amewapongeza Simba SC kwa kucheza soka safi, hivyo walistahili ushindi katika mchezo wa jana.
 Kuelekea ngwe ya lala salama ya ligi kuu na michuano ya Kimataifa , Manji alisema wataboresha timu pamoja na benchi la ufundi  kwa tafsiri ya kuwaondoa makocha wao Ernie Brandts na wasaidizi wake, Mzawa Fredy Felix Minziro na Mkenya, Mkenya Razack Ssiwa 
“Timu itaenda tena Ulaya kuweka kambini kama walivyofanya waka jana. Naamini tutajivua vizuri na kuwa makali zaidi kutetea ubingwa wetu na kufanya vizuri michuano ya kimataifa”. Alisema Manji.
Ili kuongeza makali, Yanga imesajili wachezaji watatu katika dirisha dogo la usajili ambao ni mlinda mlango, Juma Kaseja, kiungo Hassan Dilunga na mshambuliaji mahiri raia wa Uganda, Emmanuel Anord Okwi.
Wachezaji hao walitumika jana, lakini hawakufua dafu mbele ya kikosi cha Simba Sc kilichoonekana kuwa bora zaidi Yanga.

KASEBA KIDUME- AMCHAKAZA ALIBABA KWA K,O RAUNDI YA NNE

Bondia Japhert Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Alibaba Ramadhani wakati wa kugombania ubingwa wa Taifa uliofanyika Manzese Dar es salaam Kaseba alishinda kwa KO ya raundi ya nne ya mpambano huo Picha na superdboxingcoach.blogspot.com

Kanda kabongo akimhudumia Japhert Kaseba

Bondia Omari Nampekecha ‘Peche Boy’ kushoto akipambana na hasani Kiware wakati wa mpambano huo nampekecha alishinda kwa pointi

Kaseba akiwa na familia yake pamoja na mashabiki baada ya kushinda mchezo wake


Bondia Pendo Njau kushoto akiwa na bondia Llulu Kayage wakati wa mpambano huo

mashabiki wakiangalia mpambano

Wapiganaji wa mpambano wa Kick Boxing kareem kutch kushoto akipambana na Hassani Juma ‘Tata Boy’ wakati wa mpambano huo kutch alishinda kwa pointi.

Wapiganaji wa mpambano wa Kick Boxing kareem kutch kushoto akipambana na Hassani Juma ‘Tata Boy’ wakati wa mpambano huo kutch alishinda kwa pointi.

RONALDO AVUNJA REKODI YA KUFUMANIA NYAVU REAL MADRID, APIGA MOJA KATIKA USHINDI WA 3-2 DHIDI YA VALENCIA !!

Cristiano Ronaldo ameifungia bao Real Madrid jana usiku na kuvunja rekodi ya mmoja wa washambuliaji waliopo katika orodha ya kufunga mabao mengi zaidi enzi zao wakisakata soka.
Mshambuliaji huyo raia wa Ureno amefunga mabao 164 katika michezo 151 na kuvunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Mexico, Hugo Sanchez aliyefunga mabao 164 katika mechi 207.
Ronaldo ameingia katika orodha ya wafungaji wanne wa juu waliowahi kufunga mabao mengi katika historia ya Real, lakini amebakiwa na rekodi tatu kuzivunja, yaani ya Santillana mwenye magoli 186,  Alfredo Di Stefano magoli  216 na Raul aliyetia kambani magoli 228. 
Real Madrid waliwafunga Valencia mabao 3-2 jana, shukurani zimwendee Ronaldo kwa kichwa chake mahiri dakika ya 40  kufuatia mpira mzuri wa adhabu uliochongwa na Agel Di Maria alimbadili Gareth Bale katika mchezo huo.
Madrid walipata bao la tatu na la ushindi kupitia kwa kinda wao mwenye miaka 20 Jese Rodriguez katika dakika ya 84.
Bao la kwanza lilifungwa na Angel Di Maria katika dakika ya 28 kufuatia kuwazidi ujanja mabeki wa Valencia.
 Mabao ya Valencia yalifungwa na Pablo Piatti dakika ya 34 na Jérémy Mathieu dakika ya 62.
Kikosi cha Valencia jana: Guita, Pereira, Ruiz, Mathieu, Romeu, Feghouli, Bernat, Parejo (Banega, 84), Cartabia, Piatti (Guardado, 80), Jonas.
Kikosi cha Real Madrid: Lopez, Arbeloa (Carvajal, 80), Ramos, Nacho, Marcelo, Alonso, Modric, Di Maria (Illarramendi, 87), Isco (Jese, 73), Ronaldo, Benzema.
Record: Cristaino Ronaldo's goal against Valencia saw him become the joint fourth top scorer in Real's history 
Rekodi: Bao la Cristiano Ronaldo jana usiku dhidi ya  Valencia limemfanya aungane na wafungaji wanne waliowahi kufunga mabao mengi katika historia ya Real Madrid
Jumping for joy: Ronaldo scored Madrid's second goal of the evening during the 3-2 win over Valencia 
Akiruka kwa furaha: Ronaldo aliifungia bao la pili Real Madrid katika ushindi wa mabao 3-2 jana usiku
Team effort: Ronaldo is congratulated by his team-mates after his goal gave Madrid a half-time lead 
Jitihada ya timu: Ronaldo akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao la pili lililowafanya waende mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1
Ahead: Angel di Maria celebrates with left back Marcelo after opening the scoring for Real Madrid against Valencia 
Kifua mbele: Angel di Maria  na beki wa kushoto Marcelo  wakishangilia bao la Margentina huyo
Leveller: Valencia's Pablo Piatti (centre) celebrates with his team-mates after equalising at the MestallaAmesawazisha: Mchezaji wa Valencia,  Pablo Piatti (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kusawazisha bao
Game on: Valencia French defender Jeremy Mathieu clenches his fist after scoring on the hour mark 
Kipute kinaendelea: Beki wa Valencia, Mfaransa , Jeremy Mathieu akishangilia baada ya kusawazisha bao la pili dakika ya 62
Winner: Striker Jese (left) celebrates with team-mate Luka Modric after clinching the victory for Madrid 
Mshindi: Mshambuliaji  Jese (kushoto) akishangilia  na mchezaji mwenzake Luka Modric baada ya kuifungia Madrid bao la ushindi
So close: Real Madrid defender Sergio Ramos puts his hands on his head after missing a good chance to score 
Aaaah! nimekosaje?: Beki wa Real Madrid,  Sergio Ramos akishika kichwa chake baada ya kupoteza nafasi ya wazi  kufunga  bao
Challenge: Real Madrid midfielder Xabi Alonso gets the better of Valencia winger Pablo PiattiChangamoto: Kiungo wa Real Madrid ,  Xabi Alonso akimtoka winga wa Valencia  Pablo Piatti katika mchezo wa jana usiku