TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, December 23, 2013

HAFRA FUPI YA SHIRIKISHO LA NGUMI ZA RIDHAA TANZANIA KWA AJILI YA KUHAMASISHA MCHEZO WA NGUMI KWA VIJANA TANZANIA

 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa wa ngumi za Ridhaa pamoja na wadau wengine wa mchezo huo katika Picha ya pamoja, wakati wa hafra hiyo
 Aliyesimama kushoto ni mkurugenzi wa Afrika Mashariki kupitia kinywaji cha Battery Bwana Tony Misokia akiwa anaongea na wananchi walioshiriki katika Hafra hiyo.
 
 Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF) Bwana. Lukelo  Anderson akiwa sambamba na Afisa habari wa Ngumi za ridhaa Tanzania  Bwana Salum Viduka wakati wa Hafla hiyo.
 Hawa ni Baadhi ya wachezaji wa  Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF)
 Wa kwanza kulia ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ngumi za ridhaa Tanzania bwana Nassari Mafuru
 Kutoka kushoto aliyevaa shati jeupe ni Bwana Anthon Mwang’onda ambaye ni mjumbe wa mashindano na vifaa wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF) akiwa na Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Bwana Hassan Mzonge
Shirikisho la ngumi za ridhaa Tanzania  limefanya hafla fupi iliyojumuisha wachezaji wa ndondi , makocha wadau na Vyombo vya habari kwaajili ya kuendeleza  mshikamano wa kuweza kuwainua vijana ambao bado
hawajaweza kupata ajira  kujiunga na shilikisho la ngumi za ridhaa Tanzania
Shilikisho hilo ambalo limeanzisha mashindano ambayo yanatambulika kwa jina la  PSPF  Boxing Award sambamba na wadhamini wa mashindano hayo waliandaa hafla hiyo  iliyofanyika katika eneo la   (CnG) ambapo waliweza kudhamini kwa kuandaa chakula cha usiku kwaajili ya kuendelea kuweka mahusiano baina ya washiriki wote wanao shiriki katika kuendeleza mchezo wa ngumi Tanzania
Akizungumzia lengo la kuweka hafla  hiyo Afisa habari wa shirikisho la ngumi Tanzania Bw.Salum Kuhowa Viduka amesema “Tunawaomba wanajamii kuweza kutupa ushirikiano kwa muda wote ambao mashindano haya  huwasili katika miji,wilaya, manispaa, nk kuweza kujitokeza kwa wingi ili kuona jinsi fursa kwa vijana zinavyo patikana kupitia mchezo wa ngumi za Ridhaa”
Mwisho Makamu Rais  Bw.Lukelo Andason aliweza kufunga hafla hiyo kwa kuwapongeza watu wote walio weza kufika na kujumuika pamoja ili kuendeleza kujenga umoja wa ngumi Tanzania.

WATOTO YATIMA KITUO CHA NEW LIFE ORPHANS HOME CHA KIGOGO JIJINI DAR ES SALAAM-WAPATIWA MSAADA WA VYAKULA MBALIMBALI KUTOKA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA( TCAA)

01 (3)  
Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila  akiwakabidhi  msaada wa madaftari Rahma Seif na Yusra Yahaya  ambao ni watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Vyakula mbalimbali vilitolewa ikiwemo mchele na Maharage02 (1)  
Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila  (kushoto) akiwa na wafanyakazi wenza katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika kituo  cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Baada ya kuwa kabidhi msaada wa vyakula mbalimbali yakiwemo mafuta ya kupikia , mchele na sukari.03 (2) 
 Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila  akiwakabidhi  msaada wa mafuta ya kula Mohamed Achume ambaye ni miongoni mwa  watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Vyakula mbalimbali vilitolewa ikiwemo mchele na Maharage.04 
Mohamed Achume anayelelewa katika kituo cha kule yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam akikabidhiwa  msaada  wa gunia la mchele na  Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila (kushoto) ikiwa ni sehemu ya vyakula mbalimbali vilivyotolewa na mamlaka hiyo kwa ajiri ya watoto hao kusherehekea sikukuu ya krismasi.

DKT. SHEIN ASHIRIKI UZINDUZI SEKONDARI CHASASA NA UTAANI A. PEMBA LEO


TA1A4690  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,(katikati) alipokuwa kaitoa maelekezo kwa Mwalimu wa Somo la Phyisics Abrahmani Mussa,alipotembelea darasa hilo baada ya kufungua Skuli hiyo ya Sekondari ya Wanawake Utaani A,katika  Shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Mwalimu Mkuu Mwanakombo Nassor Ahmed,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A4711  
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Utaani B,Maulid Abdi Aweis,akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,(kulia) walipotembelea Makataba ya Skuli hiyo leo, baada ya kuifungua Skuli ya Sekondari ya Wanawake Utaani A,katika  Shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A4725  
Baadhi ya Wanafunzi wa wakiwa katika Maktaba ya Skuli ya Sekondari Utaani B,ambapo hufika kujipatia huduma kuangalia vitabu mbali mbali,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A4757 Wanafunzi wa Skuli ya UtaaniA,Wanawake   wakiwa katika sherehe za ufunguzi wa Skuli yao ya Sekondari,Mkoa wa Kaskazini Pemba,iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A4765  
Baadhi ya walimu na Viongozi katika Wilaya ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakiwa  katika sherehe za ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Utaani A,na Chasasa,zilizofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A4811  
Wasomaji wa utenzi Asha Ali Omar,na Asha Ali Mbarouk,wakitoa burudani yao wakati wa sherehe za ufunguzi wa Skuli
ya Sekondari Utaani A,na Chasasa, Wilaya ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba,zilizofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A4818 
Risala ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Chasasa , Utaani A,Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba ,ikisomwa na Mwalimu Mkuu Msaidizi Zaina Omar Othman,leo baada kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

CHELSEA, ASERNAL -HAKUNA MBABE LIVERPOOL- YAZIDI KUSHIKA KASI KILELENI

LIGI kuu soka nchini England (EPL) imeendelea usiku huu kwa mechi moja  kubwa kupigwa  baina ya washika bunduki wa London, klabu ya Asernal dhidi ya Chelsea.
Kipute hicho kimepigwa katika dimba la Emirates na kushuhudia timu hizo zikitoka suluhu pacha ya bila kufungana (0-0).
Mchezo wa leo ulikuwa muhimu kupata ushindi kwa kocha Aserne Wenger,  kwani amekutana zaidi ya mara 10 na Mourinho wote wakiwa makocha na kushindwa kupata matokeo ya ushindi.
Asernal walicheza vizuri na kufika mara kadhaa katika eneo la hatari la Chelsea, lakini walishindwa kutikisha nyavu za wapinzani wao.
Ulikuwa usiku mzuri kwa Mourinho, kikosi chake kilicheza vizuri sana na kuonesha uimara, lakini mipango yake ilikataa.
Pia mechi hii ilikuwa muhimu kwa Asernal kwani walitakiwa kushinda ili kurejea kileleni mwa msimamo wa EPL baada ya Liverpool kushinda wikiendi na kushikilia usukani kwa kujikusanyia pointi 36.
Kwa matokeo ya suluhu, Asernal wanabakia nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 36 sawa na Liverpool, lakini wanazidiwa kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Sasa Majogoo wa jiji wanaojivunia ubora wa Luis Suarez  wanaendelea kukaa kileleni mwa ligi kuu soka nchini England na wengine wakiisoma namba.
Getting heated: Arsenal and Chelsea players come together during an ill tempered game at the Emirates  
Shughuli inaanza: Wachezaji wa Arsenal na Chelsea wamekutana usiku huu katika mchezo mgumu dimba la Emirates
Nafasi ya tatu inakaliwa na Manchester City wenye pointi 35, huku Chelsea wakibakia katika nafasi yao ya nne kwa pointi 34, sawa na Everton waliopo katika nafasi ya tano, lakini tofauti ni mabao ya kufunga na kufungwa.
Mabingwa watetezi, Manchester United wapo nafasi ya nane na pointi zao 28 na juu yake yupo Tottenham Hospurs mwenye pointi 30.
Kikosi cha Arsenal usiku huu: Szczesny 6, Sagna 7, Mertesacker 7, Vermaelen 7, Gibbs 7, Ramsey 6, Arteta 7, Walcott 6, Ozil 6, Rosicky 6, Giroud 6.
Wachezaji wa akiba: Podolski, Monreal, Cazorla, Flamini, Fabianski, Bendtner, Jenkinson.
Kikosi cha Chelsea: Cech 6, Ivanovic 7, Cahill 7, Terry 7, Azpilicueta 7, Mikel 6, Lampard 7, Ramires 6, Willian 6, Hazard 7, Torres 6.
Wachezaji wa akiba: Cole, Luiz, Mata, Oscar, Schurrle, Schwarzer, Eto’o.
 kwenye mpiral:  Mikel na  Arteta wakichuana kwenye mpira
High jump: Fernando Torres jumps for the ball in the Chelsea penalty area 
Amaruka juu: Fernando Torres akiruka juu kupiga kichwa mpira kwenye eneo la penati la Chelsea
Getting the cross in: Gary Cahill vies with Arsenal striker Olivier Giroud 
Akipiga krosi: Gary Cahill akipambana na mshambuliaji wa Arsenal  Olivier Giroud
Hitting the woodwork: Frank Lampard sees his effort hit the crossbar and bounce to safety 
Ikigonga besela: Frank Lampard akiangalia mpira uliopiga na kugonga mwamba

MWANAUME HACHAGUA KAZI NDIVYO ILIVYO ILIMRADI WATOTO WANAPATA MKATE WA KILA SIKU !!!.

 
Mkazi wa Manispaa ya Morogoro akiwa amejitwisha lundo la kiroba chenye chupa tupu za maji kichwani mara baada ya kuzikusanya katika mitaani mbalimba wakati akielekea kwa wanunuzi wa bidhaa hiyo eneo la makutano ya Old Dar es Salaam na DDC mkoani Morogoro.PHOTO/MTANDA BLOGMfanyakazi wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro akiwa amebeba toroli lenye uchafu huku akiwa hajavaa soksi ngumu za mikononi mara baada ya wafanyakazi wenzake kutoa takangumu katika mitaro inayozunguka stendi kuu ya daladala yaendayo nje ya Manispaa hiyo lengo likiwa kuyawezesha maji kupita bila vikwazo mkoani Morogoro.

WABUNGE WAANZISHA MKAKATI MPYA WA KUMNG'OA WAZIRI MKUU MIZENGO KAYANDA PINDA KISA UTENDAJI MBOVU WA KIONGOZI HUYO KATIKA SERIKALI YA RAIS JK.


DODOMA/DAR ES SALAAM. 
BAADHI ya wabunge wameanzisha mkakati wa kumwondoa madarakani, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kile wanachodai kuwa hawaridhishwi na utendaji wake serikalini.
Hiyo ni dalili kwamba kung’oka kwa mawaziri wanne kutokana na matokeo ya ripoti ya utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili hakujamnusuru Pinda, kwani baadhi ya wabunge wanaendelea na msimamo kwamba naye ajiuzulu kwa kushindwa kuwasimamia wenzake.
Mawaziri waliong’oka baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wao kutokana na ripoti iliyowasilishwa na Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ni Mawaziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo na Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.
Hatua hiyo ya Rais Kikwete inatafsiriwa na wengi kama njia ya kuwapoza wabunge na kumwokoa Pinda ambaye ikiwa atang’oka itamaanisha kuundwa upya kwa Baraza la Mawaziri.
Habari ambazo zimelifikia gazeti hili jana zinasema wabunge 26 wametia saini fomu maalumu ya kutaka Bunge litumie mamlaka yake ya kikatiba kumng’oa Pinda kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.
Kwa mujibu wa Ibara ya 53 A(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu, endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo.
Kwa mujibu wa Ibara hiyo, hoja ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu inapaswa kuungwa mkono na wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote.
Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali alisema hili jana kuwa ukusanyaji saini za wabunge aliouanzisha Ijumaa jioni unakwenda vizuri.
“Kung’oka kwa mawaziri wale wanne inatosha kuthibitisha kuwa Pinda amepoteza uhalali wa kuwa Waziri Mkuu kutokana na kushindwa kuwasimamia walio chini yake,” alisema Machali.
“Rais tunaweza kumuacha, lakini Pinda ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za Serikali. Kama wapo mawaziri wameboronga ni wazi na yeye anaingia moja kwa moja katika hilo kapu,” alisema na kuongeza:
“Kama kweli tunataka taifa lisonge mbele kutoka hapa tulipo ni lazima tumuondoe Pinda…….. amekuwa mpole mno, mzito kufanya uamuzi na analea matatizo.”
Hata hivyo, alisema wabunge waliosaini fomu hiyo, wote wanatoka kambi ya upinzani na kusema wabunge wengi wa CCM aliowafuata kuwaomba watie saini wanaogopa au wanasita kufanya hivyo. MWANANCHI

MAPOKEZI YA MHE ZITTO ZUBERI KABWE HIVI PUNDE KIGOMA

            Zitto Kabwe akiwa katika gari la wazi mara baada ya kutua  kigoma
                        asubuhii ambapo amepata mapokezi ya kishindo

                     wafuasi wa Zitto kabwe wakiwa katika maandamano..
 











BASI LA ALLYS YAUA ABIRIA SABA JANA USIKU BUHONGWA-MWANZA.


Basi la kampuni ya Allys Sport Bus linalosafirisha abiria kutoka Dar es Salaam na Mwanza likiwa limeacha njia na kupinduka baada ya kutokea ajali inayodaiwa kusababishwa na basi la Shabiby lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kwenda Dar es Salaam na kusababisha mabasi matatu kuacha njia katika eneo la Mkundi Makunganya barabaraba kuu Dodoma-Morogoro ambapo katika ajali hizo zaidi ya abiria 40 walijeruhiwa mkoani Morogoro. PICHA MAKTBA/MTANDA BLOG.  WATU saba wamekufa papo hapo na wengine wengi kujeruhiwa baada ya basi la Allys linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam hadi Mwanza kugongana uso kwa uso na daladala katika eneo la Buhongwa mkoani Mwanza.

Sunday, December 22, 2013

KAMISHNA WA SHERIA NA UENDESHAJI WA MAGEREZA AFANYA ZIARA YA KIKAZI MAGEREZA MKOA WA MANYARA

image (7)
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Magereza toka Magereza mbalimbali ya Mkoani Manyara mapema leo (jana) Desemba 21, 2013 alipowasili katika Ofisi za Magereza Mkoa wa Manyara tayari kwa ziara ya Kikazi ya siku mbili.image (8) Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) akiongea na baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wa Mkoani Manyara(hawapo pichani) leo (jana) Desemba 21, 2013. Watatu toka kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Bether Minde.image (9)  
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza toka Vituo mbalimbali vya Magereza Mkoa wa Manyara wakimsikiliza Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(hayupo pichani) wakati Baraza Maalum la Askari lililofanyika katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza, Mkoani Manyara leo (jana)  Desemba 21, 2013.image (10) 
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Bether Minde akiwa ameongozana na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) wakati wa kutembelea baadhi ya maeneo mbalimbali ya Gereza la Mahabusu la Babati
(picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Sahel Traing Co.Ltd YAKABIHI MZANI KWA AJILI YA MABONDIA!!




Mkurugenzi wa Sahel Traing Co.Ltd, Ally hazam kushoto akimkabidhi mzani wa kupimia uzito mabondia kwa Yassin Abdalla ‘Ostadhi’ mzani huo wenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nane umetolewa na kampuni hiyo kutekeleza ahadi yao ya kusaidia mchezo wa masumbwi nchini picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

 MAZANI WA KIMATAIFA WA KUPIMIA MABONDIA AMBAPO UNA UWEZO WA KUPIMA UZITO,UREFU, NA KUTAMBUA UJAZO WA MAFUTA YAKO MWILINI YAPO KIASI GANI NA UNAITAJI  UWE NA UZANI KIASI GANI KULINGANA NA UREFU WAKO
 
Mkurugenzi wa Sahel Traing Co.Ltd, Ally hazam kushoto akimkabidhi mzani wa kupimia uzito mabondia kwa Yassin Abdalla ‘Ostadhi’ mzani huo wenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nane umetolewa na kampuni hiyo kutekeleza ahadi yao ya kusaidia mchezo wa masumbwi nchini picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya  Sahel Traing Co.Ltd kupitia kwa mkurugenzi wake Ally Hazam  wametoa mzani wa kupimia mabondia kwa kiwango cha ali ya juu kwa ajili ya kuondoa ubabaishaji wa upimaji uzito kwa mabondia
akizungumza wakati wa kukabidhi mzani huo wenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nane  Hazam amesema wameamua kutoa mzani wakitegemea ngumi ndio mchezo pekee ambao unaweza kuretea sifa taifa kwa haraka sana
mchezo ambao unapendwa na watu wengi duniani sema hapa kwetu bado atuja usapoti sana na sisi tume onesha mfano ila tuta enderea kusapoti mchezo wa masumbwi nchini kari tuwezavyo
nae Yassini Abdalla ‘Ostadhi’ aliye pokea mzani huo ambao utakuwa ukitumika kwa mabondia kupima uzito ususani mapambano ya kimataifa ame shukulu kampuni hiyo kwa kutoa mzani na ni ahai ambayo walikuwa nayo mda mrefu rakini leo ‘jana’ ndio wameitekeleza 
siku zote dunia nzima cha kwanza kabla mabondia awajapanda ulingoni kwanza wanapima uzito afya ndio mpambano una endelea bila uzani akuna ngumi mana mnaweza kupiganisha mabondia wenye uzani tofauti kitu ambacho akikubaliki dunia nzima
hivyo sina budi kuishukuru kampuni ya Sahel Trading Co. Ltd kwa kunipatia uzani huu

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


a225Diwani-Athumani1
WILAYA YA MOMBA – MAUAJI.

·         KUFUATIA TUKIO LA MAUAJI LILITOKEA MNAMO TAREHE 19.12.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA TAZARA -TUNDUMA   KATA NA TARAFA YA TUNDUMA   WILAYA YA  MOMBA  MKOA WA MBEYA. AMBAPO MTOTO KALIBU S/O KIMWELU, MIAKA 6, MNYAMWANGA,  MKAZI WA MTAA WA TAZARA TUNDUMA ALIUAWA KWA KUCHINJWA SHINGONI KWA KUTUMIA  KISU   NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. AIDHA WATU HAO WALIMNYONGA SISTA D/O NYILENDA, MIAKA 17, MNYIHA, MFANYAKAZI WA NDANI [HOUSE GIRL] KWA KUTUMIA WAYA WA TELEVISHENI ULIOKUWEPO SEBULENI. MBINU NI KUWAVAMIA WAHANGA WAKIWA NDANI NYUMBANI KISHA KUWAUA KINYAMA. MIILI YA MAREHEMU WOTE ILIKUTWA SEBULENI. WAKATI WA TUKIO BABA WA MTOTO AITWAE ESTON S/O KIMWELU,MIAKA 55, MNYAMWANGA,  DIWANI WA KATA YA  MKANGAMO – CCM,  MKAZI WA TAZARA  ALIKUWA  SHAMBANI KIJIJI CHA KIPAKA NA MAMA WA MTOTO AITWAE  TUMAINI D/O YOHANA, MIAKA 29, MNDALI, KATIBU MUHTASI  HALMASHAURI YA  MJI MDOGO WA TUNDUMA ALIKUWA KAZINI.  KATIKA TUKIO HILO WATU HAO PIA WALIIBA MABEGI MAKUBWA MAWILI YENYE NGUO MBALIMBALI YALIYOKUWA KATIKA CHUMBA WANACHOLALA WATOTO. 

·         KATIKA TUKIO HILO MMOJA WA WATILIWA MASHAKA WALIOKUWA WAMESHIKIWA NA JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANO NA UCHUNGUZI ZAIDI AMBAYE NI NDUGU WA MAREHEMU ENOCK S/O SIMWELU, MIAKA 23, MNYAMWANGA, MKULIMA AMEKIRI KUHUSIKA NA TUKIO HILO AKISHIRIKIANA NA GABRIEL S/O KIMWELU, MIAKA 19, MNYAMWANGA, MKULIMA.  WOTE NI WATOTO WA MKE MKUBWA, WAKAZI WA MAJENGO MAPYA TUNDUMA  NA PATRICK S/O MSIGWA, MIAKA 18, MKINGA, MKULIMA MKAZI WA MAJENGO MAPYA TUNDUMA NI MAJIRANI NA RAFIKI WA WATOTO HAO.

·         AIDHA AMESEMA KUWA CHANZO CHA KUHUSIKA NA MAUAJI HAYO NI KUTOKANA NA BABA YAO KUWATELEKEZA NA KUANDIKA MALI ZAKE ZOTE KWA JINA LA MAREHEMU KALIBU S/O KIMWELU KUWA MRITHI WA MALI HIZO.
        KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUZINGATIA SUALA LA MALEZI BORA KWA WATOTO NA VIJANA WAO ILI WAKUE KATIKA MAADILI MEMA NA KUJIEPUSHA NA MATUKIO YA UHALIFU. 
{B.N.MASAKI — ACP )KAIMU: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

MATOKEO MAZURI YA UFAULU SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA YALIVYOIVUTIA BENKI YA WANANCHI MUFINDI


 
 Mkurugenzi  wa shule  ya kimataifa  ya  Southern Highlands Mafinga  Bi Mary  Mungai akimkabidhi  cheti mmoja kati ya  wahitimu wa mahafali ya 13  shule  hapo ,kulia  kwake ni kaimu meneja  wa Benk ya wananchi Mufindi (Mucoba) Bw Ben Mahenge 
Walimu na  wafanyakazi wa shule ya Southern Highlands Mafinga  wakiwa katika  picha ya pamoja na mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Bi Mary Mungai kushoto wa kwanza .
……………………………………………………….
Na Francis Godwin
MAENDELEO mazuri  ya ufaulu  wa  wanafunzi  wa shule  ya kimataifa  ya Southern Highlands Mafinga mkoani Iringa iliyoisukuma benk  ya wananchi Mufindi (MUCOBA) kujitokeza kuunga mkono jitihada za  elimu  katika shule  hiyo .
Ifahamike   kuwa  suala la motisha  kwa  walimu na  wanafunzi  wanaofanya  vema  katika masomo  yao  na walimu  wanaofundisha wanafunzi  hao  ni  moja na hamasa  kubwa  kwa  kuwawezesha  kufanya  vizuri  katika maendeleo  ya  elimu nchini.
 Yamekuwepo  malalamiko  mbali  mbali  kutoka kwa  wadau  wa  elimu nchini  ambao  wamekuwa  wakilalamikia maendeleo mabaya  ya  elimu nchini hasa kutokana na mazingira duni  ya  kufundishia malalamiko ambayo  serikali  kupitia  wizara ya  elimu na mafunzo  ya ufundi  imeendelea  kuyafanyia kazi
Huku  wale  waliokuwa  wakibeza  shule  za kata   hivi  sasa  kuanza kuzipongeza shule  hizo  kutokana na baadhi ya  shule  hizo  kufanya  vizuri  kuliko shule  za awali  ambazo  walikuwa wakizisifia  na hapa ndipo tunaungana na  wahenga  waliosema kupanga ni  kuchagua .
Pia  miaka  ya  hivi  karibuni  zimezuka   shule  nyingi  za sekondari  na msingi za  watu  binafsi ambazo baadhi  ya  shule  hizo  zimeendelea kufanya vizuri na  kutoa  changamoto  kubwa kwa  shule  za  serikali na baadhi  ya shule  zilizoanzishwa na watu binafsi zikionekana  kuendelea  kushuka zaidi  na  wazazi  hata  kuamua  kuhamisha   watoto  wao.
Shule ya Southern Highlands Mafinga imeonekana kuivutia zaidi  benki hiyo ya MUCOBA  kutokana na rekodi  yake nzuri  ya kufaulisha vizuri wanafunzi wote darasa la saba tangu ilipoanzishwa mwaka 1997.
Kiwango  cha  elimu  kinachotolewa katika  shule  ya kimataifa ya Southern Highlands Mafinga kinaisukuma benk ya  wananchi  wilaya ya  Mufindi (MUCOBA)   kuahidi  kutoa  kiasi  cha  Tsh milioni 2.5  kwa  ajili ya  kuwafuingulia  akaunti  katika benk hiyo  wanafunzi  waliofanya  vema  matokeo ya  mtihani  huo  mwaka  huu.
Bw Ben Mahenge  anasema  kuwa  moja kati ya  sababu  iliyopelekea  benki  yake kujitokeza  kuunga  mkono  jitihada za  shule  hiyo  ni  kutokana na ufaulu  mzuri  wa  mitihani  ya Taifa  ya  darasa  la  saba  ambayo shule  hiyo  imeendelea  kuongoza na  hivyo  kutoa  heshima kwa  wilaya  ya  Mufindi na Tanzania  kwa  ujumla.
Kwani  anasema  kuwa  mbali ya  benk hiyo  kuendelea  kutoa  mikopo mbali mbali  ila imekuwa  karibu  zaidi na  shule  hiyo ya  Southern Highlands Mafinga  ambapo  mkurugenzi  wake Bi Mary A. Mungai  ni mmoja kati ya  wateja  wakubwa  wa  benk  hiyo  kutokana na
wazazi  wote  wanaosomesha  watoto  katika  shule hiyo  kulipia ada kupitia  benk  hiyo hivyo  kiasi  hicho cha fedha  kilichotolewa na  MUCOBA ni  kutambua mchango  wa  shule  hiyo katika  uendelezaji  wa  benk hiyo. 
” Kati ya  wateja  wakubwa  wa  benk  ya  MUCOBA ni  pamoja na  shule ya  Southern Highlands Mafinga na  wazazi ambao  wanasomesha  watoto hapo kutokana na   wazazi wa watoto  wanaosomesha  hapo  hulipa ada  kupitia  benk  yetu …..hivyo  kwa  ajili ya  kumpongeza  mkurugenzi  wa  shule hiyo kwa kuzidi  kuiunga mkono  benk  yetu  bado tunazidi  kuwahamasisha  wananchi  wa  wilaya ya  Mufindi na nje ya  mkoa  wa  Iringa kujiunga nasi”
Mahenge  anasema  kuwa  benk hiyo  imeendelea  kutoa  mikopo  mbali mbali  kwa  wateja  wake  ikiwemo mikopo ya  ujenzi  wa  nyumba  bora , ujasiliamali na mikopo  ya kuendeshea  biashara .
Hata  hivyo  Mahenge  anasema  kuwa  wanafunzi  watakaonufaika na msaada  huo  ni  yule  aliyefanya   vizuri katika matokeo  ya mtihami  wa  Taifa  wa darasa la  saba pamoja na mwanafunzi Aida  Mhagama  ambae  aliibuka  mshindi  wa  jumla katika masomo  mbali mbali  na  kupongezwa  wakati  wa  mahafali  ya  darasa  la  saba ya  shule  hiyo .
Anasema  fedha  hizo  zitaingizwa katika akaunti   zao baada ya  kufunguliwa na  benk hiyo  kwa  lengo la kusaidia  kuwasomesha  elimu  ya  sekondari pindi watakaojiunga na  elimu  hiyo ya  sekondari mapema  mwakani .
Mkurugenzi mtendaji wa shule  hiyo Bi Mary Mungai ambae amepata   kuwa afisa  elimu shule za msingi anasema  kuwa shule  imekuwa  ikifundisha kwa kiingereze, yaani english medium school, imefaulisha tena mwaka  huu 2013 wahitimu wote wa darasa la saba na kuiwezesha kuwa katika asilimia mbili (2%) ya juu ya shule zote zenye kufaulisha vizuri kitaifa, na katika 10 bora kati ya shule 449 za mkoani Iringa.
“…Tunawapa hongera wahitimu hao na kuwatakia maendeleo mazuri kokote waendako. ….pia tunawapongeza wazazi/walezi, tunawatakia kila la heri kuwaendeleza watoto wao kufuatia msingi huu ulio bora waliopata kutoka Southern Highlands School.
Anasema pia uongozi  wa shule  hiyo hautaacha  kuwapongeza walimu, kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya kila siku kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyo ya kiwango cha juu.
“ Sisi  tunapokea watoto  kutoka pande zote za nchi  na watakaotaka  watoto wao wajiunge na Southern Highlands School, nafasi zipo kwa wanafunzi wa chekechea, darasa la 1, 2, 3, na 5 kwa wanafunzi wote na darasa la 4 na la 6 kwa wanaotoka shule za English Medium
Anasema  kuwa  toka  shule  hiyo  ilipoanzishwa mwaka 1994 kama Day Care na Pre-school na mwaka 1997 kuanza shule ya msingi imekuwa ikifanya  vizuri na hakuna mtoto aliyepata  kufeli .
“Shule  yetu mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza wa darasa la Saba na wanafunzi walikuwa 17, wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza”
Anasema katika  matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani ya Somo la Kiingereza.
“   Tulimshukuru Mungu na tunaendelea kumshukuru Yeye. Kwa kuwezesha watoto wetu wa Southern Highlands School, kufaulu vizuri, kwa kishindo” alisema Bi Mungai
Hata  hivyo  anasema kila mwaka wanafunzi wote  wamekuwa wakifaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na wote kuchaguliwa na kuendelea na masomo ya Sekondari.
“mwaka  huu tena  wanafunzi wote wa darasa la saba 47 waliomaliza mwaka huu 2013, wamefaulu na kuchaguliwa kuendelea na sekondari”
Mwenyekiti  wa bodi ya shule  hiyo Bw Omary Mahinya anasema kuwa katika moja ya vielelezo kuwa shule  hiyo ni bora nchini ni wazazi kutoka mikoa karibu yote ya Tanzania kupeleka  watoto wao hapo .