TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, March 23, 2014

UZINDUZI WA ALBUM YA MUNGU NI MWAMINIFU WAFANA EAGT TEMEKE

RIDHIWANI ASHUHUDIA SHULE ILIVYOBAKI HOI BAADA YA KUEZULIWA PAA NA KIMBUNGA KATIKA KIJIJI CHA KIKWAZU, JIMBONI CHALINZE, AAHIDI KUSAIDIA KUIBORESHA TENA

 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Kikwete  akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji cha Kikwazu, Mussa Yahaya kuhusu shule ya msingi Kikwazu iliezuliwa paa na kimbunga  mwanzoni mwa mwaka huu na kubakisha darasa moja tu linalotumika.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR ATEMBELEA SHAMBA LA WAZIRI MKUU DODOMA

Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanachuo wa Chuo cha Nyuki cha Tabora waliotembelea shamba lake lililopo Zuzu, Dodoma kujifunza ufugaji bora wa nyuki  Machi 22, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PG4A3916Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd kukagua zao la zabibu  katika shamba lake  lililopo Zuzu , Dodoma Machi 22, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PG4A3921Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa maelezo kuhusu  zao la migomba kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd ambaye alitembelea shamba lake lililopo Zuzu mjini Dodoma Machi 22, 2014. Wapli kulia ni Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka na kulia ni Majasiliamali wa Dar es salaam, Alphonce Buhatwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MTALII ALIYEKWAMA KILELE CHA MAWENZI MLIMA KILIMANJARO AOKOLEWA

Bi.Jeanne Traska kutoka Ujerumani na Muongoza Wageni Athumani Juma wakiwa katika Lango la Marangu pamoja na vifaa mbalimbali walivyokwama navyo katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro mara baada ya kuokolewa.
……………………………………………………..
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kikosi cha Uokoaji katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro kimefanikiwa kumuokoa mtalii Bi. Jeanne Traska (32) kutoka Ujerumani pamoja na muongoza wageni Athuman Juma ambao jana walikwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro. Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kufika eneo la kilele cha Mawenzi na kwa kutumia mbinu za uokoaji za kisasa kabisa kiliweza kuwanasua majira ya kumi na moja jioni.
Licha ya hali mbaya ya hewa iliyotokana na mawingu mazito katika eneo hilo, Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kukabiliana na hali hiyo na kuweza kuwanasua na kisha kuwapeleka katika kituo cha Horombo majira ya saa mbili usiku ambapo walichukuliwa na gari kupitia njia maalum ya uokoaji na kufika katika Lango Kuu la Marangu saa nne na nusu usiku.
Hali ya hewa ilisababisha helikopta maalum iliyoletwa kwa ajili ya zoezi la uokoaji kushindwa kufanya kazi kwa kuwa mawingu mazito hayakuwezesha marubani kuliona eneo la kilele kwa urahisi.
Hivi sasa mtalii huyo pamoja na muongoza wageni wake bado wapo chini ya uangalizi wa hifadhi kwa kushirikiana na Kampuni ya Nordic Tours iliyomleta mgeni huyo.
Aidha, kwa kuwa ni tukio lisilo la kawaida, uongozi wa hifadhi unaendelea kuchunguza sababu zilizowafanya kuchepuka njia na kuelekea kilele cha Mawenzi badala ya Kibo. Kwa kawaida Kilele cha Mawenzi huwa hakitumiwi na watalii isipokuwa kwa kujaza fomu maalum inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa hiyari yake kupanda kilele hicho.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
23.03.2014

MUME AKUSUDIA KUMTOA ROHO MKEWE HUKO MBEZI BEACH DAR

SOKA LINA MAAJABU YAKE, INAWEZEKANA MAN UNITED KUWANYUKA BAYAYER NA KUTINGA NUSU FAINALI UEFA!!

Wakati uso wasaa ya dunia unaenda kasi sana, huku nao wana sayansi wakiumiza kichwa kuhusu ndege ya Malaysia iliyopotea, nayo Brazili ikiwa na maombolezo ya nahodha wake  aliyewaisaidia kutwaa kombe la dunia pale Sweeden  1950 , wakati huo huo sherehe ya mzee Arsene wenger kutimiza mechi 1000 zikishereheshwa kwa kipgo kibaya cha goli 6-0 kutoka kwa Chalsea, bado uso wa saa wa dunia ukasema kwa nini Manchester United wakiwa mabingwa wa EPL wasistahili kukutana na bingwa mwingine wa Bundesliga ,Bayern Munchen.  The Bavarians.
 Luis Figo,  nguli wa zamanI wa Barcelona , Real Madrid na Ureno huenda ameingia kwenye orodha ya watu ambao pengine wanachukiwa na mashabiki wa Man u, hiii ni kutokana na Droo ya robo fainali ambayo Figo alikuwa balozi wake .
Bayern-Munich-Champions-League-Winners-2013-HD-WallpaperKweli Man United ataweza kuwatafuna wanaume hawa?
Katika droo hiyo,  klabu ya Manchester United imepangwa kucheza na bingwa mtetezi  wa kombe hilo Buyern Munich, huku wenzao Chelsea wakipangwa dhidi ya Paris saint Germain ya nchini ufarasa.
Lakini tukio lililoshika hisia za watu wengi, na kuchafua mapumziko ya mwisho ya wiki kwa mashabiki ni hili la  Mancheste united.
 Mashabiki  wengi kama sio wote, wakurugenzi, hata jopo la ufundi la Man United, na hata wachambuzi na waandishi mbali mbali wa habari za michezo wasingetamani  Mashetani wekundu  kwa hali waliyo nayo  kukutana na  Bayern ya Pep Guardiola. 
article-2585919-1C6E2CCB00000578-572_634x461
Wamevurugwa: Wayne Rooney na  Manchester United watautafuna mfupa wa Bayern Munich?
Si  kwamba timu hizi ndio zinakutana kwa mara ya kwanza, la hasha..! kwa mujibu wa vyanzo vya habari,   timu hizi zimekutana takribani mara 9.
 Manchester United imefanikiwa kushinda mara 2, kutoka sare mara  4 na kufungwa mara 3,  huku tukio linalokumbukwa na watu wengi na linalowapa matumaini si mashabiki hata wachezaji wa sasa wa Man United na viongozi wao, ni hili la mwaka 1999 katika fainali hizo ambapo Manchester ikiwa chini ya koch Sir Alex Ferguson ilishinda na kutwaa taji hilo.

WANANCHI KATAVI WAASWA KUTUNZA MAZINGIRA

Kaimu Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Nsimbo Enock Msengi akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi kuhusu hali ya upatikanaji wa maji kwenye halmashauri hiyo wakati wakiwa kwenye moja ya kisima kinachotumika kusukuma maji kupeleka kwenye tanki la maji kasha kusambazwa katika maeneo mengine kijijini hapo
???????????????????????????????Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi,  Kanali Ngemela Lubinga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhiwa lita 90,000 za maji na litaweza kuhudumia wakazi wapatao 2000 katika kijiji hicho cha Isinde siku ya kilele cha wiki ya maji .viongozi wa mkoa huo.
Na Kibada Kibada Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe amewahimiza wananchi  wa Mkoa huo kutunza  mazingira  na kutoharibu vyanzo vya maji kwani kutofanya hivyo kunaleta madhara makubwa katika maisha ya kila siku.
 Akiongea na wananchi wa Mkoa wa Katavi wakati wa maadhimisho ya siku ya kilele cha maji Mkoa yaliyofanyika kwenye kijiji cha Isinde kata ya Mtapenda,  Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lubinga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu amesema wananchi wanatakiwa kutunza mazingira na  kuhifadhi vyanzo vya maji ili  viweze kuwa endelevu.
 Katika hotuba yake  hiyo iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya huyo,  imeeleza changamoto hizo  za uharibifu wa mazingirazi zinazoukabili  Mkoa wa Katavi kuwa ni uhamiaji holela wa wananchi kutoka mikoa ya Kigoma, Mwanza,Tabora,Simiyu na Shinyanga ambapo humami a na  kuchangia kwa kiasi kikubwa uharibifu  kwenye vyanzo vya maji na mazingira
Aidha amewahimiza kuchangia mifuko ya maji ili kutunza na kuendeleza miradi ya maji waliyojengewa na serikali ili iweze kuwanufaisha wananchi wa Mkoa huo kwa kuwaondolea matatizo ya upungufu wa maji uliokuwa ukiwakabili.
Katika hatua nyingine amewahimiza kuchangia mifuko ya maji ili fedha inayopatikana isaidie kuendeleza ukarabati unaoweza kijitokeza iwapo kutakuwa na uharibifu wowote kwenye mradi wa maji kwa kuwa miradi ya maji ni mali yao.
Awali Kaimu  Mhandisi wa Maji  Halmashauri ya Nsimbo Enock Msengi  katika taarifa yake ya ujenzi wa tanki  la maji alieleza kuwa zaidi ya shilingi milioni 200 zimetumika katika  ujenzi wa  tanki la maji lenye uwezo wa  kuchukua ujazo wa  lita  90,000 (90m).
 Msengi ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuwaondolea kero ya maji iliyokuwa ikiwakabili  wananchi wa Kijiji cha Isinde  kwa muda mrefu.
Naye Mhandisi wa Maji Mkoa wa Katavi,  Elieda Mwakasungura katika Taarifa yake ya Mkoa wa kuhusu maji alieleza kuwa wananchi wanaopata maji  safi na salama katika mkoan huo ni asilimia 48 hali ambayo inaonesha bado lipo tatizo la upatikaji wa maji safi na salama katika mkoa huo.
Miradi mingine inaendelea kutekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Mpanda katika kijiji cha Ikola,Ngomalusambo na Karema,miradi mingine inatekelezwa katika Halmashauri ya Nsimbo.

JE WANA SIMBA WANASEMAJE KUHUSU TIMU YAO?

Utawaweza Coastal Union leo?: Kocha wa Simba, Dravko Logarusic yupo katika wakati mgumu kuipatia mafanikio klabu hiyo msimu huu
…………………………………………………………………………
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC wakati wa maandalizi ya mchezo dhidi  Coastal Union ya jijini Tanga.
Wakiwa tayari wameshashuka dimbani mara 21 na kujikusanyia pointi 36 katika nafasi ya nne,  Simba chini ya kocha mkuu, Mcroatia, Dravko Logarusic katika mazingira magumu zaidi ya kupata matokeo ya ushindi.
Simba SC kama vile wameshajitoa katika mbio za ubingwa na kuwaachia Yanga, Azam na Mbeya city. 
Loga amekuwa na wakati mgumu tangu aanze kukinoa kikosi cha Simba mwanzoni mwa mzunguko wa pili akirithi mikoba ya Abdallah Kibadeni.
Kocha huyo anayesifika kudhibiti nidhamu kwa wachezaji, amekifanya kikosi cha Simba kuwa cha `tia maji tia maji.

Hii ndiyo Taswira ya Vituo vya Mabasi vilivyojengwa upya kutokana naujenzi unaoendelea jijini Dar

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wameendelea kupata taabu ya usafiri ususani wakati wa asubuhi na wakati wa jioni kwa kuwa mida hiyo ndiyo watu wengi wanakuwa wanatoka makazini.

pamoja ha hali hiyo pia wakazi wengi wanalazimika kulipa gharama za juu kwa kuwa usafiri unakuwa ni tatizo ambapo wenye vyombo wengi wa usafiri ubadili njia zao za halali na kwenda barabara wasizopangiwa kwa lengo la kujipatia kipato kubwa kwa maana wanapandisha gharama kutoka bei yake na uongeza zaidi ya mara tatu mpaka nne.
hali ambayo uwalazimu wakazi wengi wa jiji kutembea kwa miguu ili kuepusha gharama zisizokuwa za lazima kwao kwa kuwa hata hali ya maisha kwa wakazi wengi wa mjini imemeendelea kuwa ya hali ya juu kutokana na kukua kwa kasi ongezeko la miundo mbinu.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au piga simu 0713869133. 

MBEYA CITY: HAKUNA DHAMBI KUBWA KAMA KUKATA TAMAA, KWA UZURI GANI, MAFANIKIO GANI UNAJIHANGAISHA NA VIDUKU?

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
HAKUNA dhambi kubwa kama kukata tamaa katika maisha. Inafahamika kuwa kuna changamoto nyingi zinazoweza kumkabili mtu na mwisho wa siku akajiona hawezi kufanikiwa tena.Kumbe njia sahihi ni kukubali changamoto iliyopo mbele yako na kutafuta njia ya kukabiliana nayo.Mafanikio si jambo la siku moja, zipo njia za kupita ili kufanikisha malengo yako.
Msimu huu wa 2013/2014  wa ligi kuu soka Tanzania bara kumekuwepo na ushindani mkubwa kuwania ubingwa.Nafasi za juu kuna timu moja mpya kabisa ambayo ni Mbeya City. Msimu wa mwaka juzi, Simba sc klabu walikuwa wanachuana vikali na Azam fc kuwania ubingwa, huku Yanga akiwa nyuma yao akijikongoja.
Mwisho wa msimu, Simba waliibuka vidume baada ya kutwaa ndoo na kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambako walijitahidi kucheza kwa nguvu zote, lakini walitolewa.
Msimu wa mwaka jana, Simba naye akaa pembeni na kuwapisha Azam fc wakichuano  vikali kuwania ubingwa. Mwisho wa siku, Yanga wakaibuka wanaume na kuiwakilisha Tanzania mwaka huu ligi ya mabingwa barani Afrika.Yanga hawajaweza kusonga mbele baada ya kukutana na kigongo cha Al Ahly ya Misri katika safari yao.
Japokuwa walitolewa kwa mikwaju ya penati 4-3 machi 9 mwaka huu nchini Misri, Yanga walipambana sana na kuonesha kukomaa zaidi.Kwa mara nyingine msimu huu  kigogo wa soka la Tanzania, Simba sc hazungumzwi katika mbio za ubingwa.
Watu wanawazungumzia Mbeya City, Yanga na Azam fc waliopo nafasi za juu.Ukiangalia katika misimu mitatu iliyopita, utagundua Yanga na Simba wamekuwa wakibadilika badilika, mara wana makali ya kutosha mara wanalowa.
Azam fc wanaonekana misimu yote ni washindani na ndio maana wamejaribu kutwaa ubingwa kwa misimu yote tangu wapande ligi kuu 2008/2009.Wamekuwa wakiishia nafasi ya pili mara kwa mara. Hii inatoa picha kuwa Azam fc wanaanzia pale wanapoishia.
Katika maisha ya kawaida, kama mwaka huu umepata alama B, basi mwaka ujao unatakiwa kuanzia B kuelekea alama A.Kama utapata alama C na mwaka jana ulipata B, basi ujue hauna mipango mizuri ya kuendeleza mafanikio yako.

MPUNGUZENI GHARAMA YA KUCHIMBA VISIMA – WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameitaka Wizara ya Maji itafute njia mbadala zitazosaidia kupunguza gharama za kuchimba visima ili wananchi waweze kupata maji safi na salama.
“Wizara ya Maji angalieni uwezekano wa kupunguza gharama za uchimbaji wa visima ili wananchi waweze kumudu kuchimba visima na wapate uhakika wa maji safi na salama,” alisema.
 
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Machi 23, 2014), wakati akifunga Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
 
“Hivi sasa nimeambiwa gharama ya kuchimba kisima mita moja ni sh. 150,000/. Je kama mtu anataka kuchimba kisima chenye urefu wa mita 180 au 200 itakuwaje? Ni dhahiri kuwa watu hawataweza kumudu hizo gharama. Angalieni namna ya kuzipunguza,” alisisitiza.
Habari zaidi soma hapa.

www.missdemokrasia.blogspot.com

RIDHIWANI KIKWETE APIGA KAMPENI KATIKA KATA YA FUKAYOSE JIMBONI CHALINZE

MICHEPUKO YA MAGARI, BAJAJI NA BODA BODA KATIKA BARABARA MPYA NA ZA ZAMANI ZIMEKUWA CHANZO CHA AJALI JIJINI DAR.

Katika jiji la Dar es Salaam, Ujenzi wa Barabara Unaendelea ambao kwa asilimia 80 unaelekea kukamilika tena kwa kiwango kizuri kwa mkandarasi kwa kuwa upande wa Serikali sina hakika kama baada ya Muda Gani watavunja na kujenga Ingine, Tanzania ususani serikali inayoongozwa na watu wetu wenyewe imeendeleakuwa na tabia ya kufanya mabadiliko ya rasilimali bila kufuata utaratibu wa matwaka ya watu wanaoishi ndani yake.

Katika Kipindi hiki cha Utawala wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kikwete na Safu ya Mawaziri wake wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuondoa suala la usumbufu wa Barabara kwa kujenga Barabara nyingi nchini Tanzania kwa kiwango kizuri cha ubora wa Barabara Duniani, kitu ambacho kilikuwa tatizo kwenye miaka ya nyumba ususani hata wakati wa utawalawa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,  Utawala wa Mwinyi na Mkapa.

Pamoja na kwamba Barabara hizi zimejengwa ajili yetu wenyewe, lakini barabara hizi hizi zimekuwa tatizo kwetu maana hata ajali zingine pia zinatokea kwa kuwa tunashindwa kuzitumia ipasavyo barabara hizi,  zaidi ikiwa kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri kama vile Pikipiki, Baiskeli na Magari.
Wajenzi wa Barabara hizi bila shaka Magufuli na watu wake(Wakandarasi) wanatambua jinsi taratibu za wapitaji wa vyombo vya usafiri wanavyopaswa kupita wakati zitakapokuwa tayari zimeamuliwa kutumika,
kwa sasa watumiaji wengi wa barabara ususani hizi mpya wanashindwa kuelewa jinsi itakavyokuwa zinatumika kwa kuwa kuna baddhi ya ya maeneo ambayo imeyalazimu magari kupita moja tu kwa maana hakuna eneo la kupishana gari na gari yaani iwe kwenda nyumba wala kupita gari ingine ili uwe mbele, kwa maana hiyo aliye wa mbele hatazidi kuwa mbele na wa nyuma kwa nyuma.
sasa swali  liliko ndani ya vichwa vya watu wengi ni jinsi gani itakavyokuwa wakati itakapokuwa inaharibika gari ya mbele wakiwa safari moja, kwa maana hakutakuwa na njia mbadala ya gari ingine kupita kupisha hilo,  kingine ni jinsi barabara hizo zinavyotakiwa kutumiwa na madereva walioiva katika kazi ya Udereva, maana badala ya njia kutengenezwa zimenyooka, barabara hizi za KIKWETE zimepinda pinda si kwa uharibifu bali kwa maboresho ya kiufundi zaidi ususani  ni fahari kwa Dereva Bora amabaye ni hodari kwa kazi ya kuongoza gari wakati wote wa Safari yake Barabarani.
kinacho nishangaza mimi ni kwa jnsi gani Magufuli ameshindwa kuitumia fulsa hii kuhakikisha anaweka Madaraja ususani maeneo ya Maungio zinapotumika Taa, na badala yake ingewekwa Madaraja kamailivyo kwa nchi zingine Duniani, kwa kuwa gharama iliyotumika na muda uliotumika, na Uongozi uliotumika kufanya haya hauta kuja tena kutokea nna kufanya haya katika kizazi hiki hakika.

Kazi kubwa sasa imebaki ni kwa wazazi wa watoto wa mijini zaidi wale wa maeneo hayo zilipojengwa hizo barabara kuwajengea misingi imara watoto ya kutokatiza hovyo barabarani kwa kuwa ivi sasa ongezeko la kugongwa litakuwa kubwa ukilinganisha na barabara za zamani ambazo kati ya barabara na barabara kuliachwa mwanya wa mtu kupumzika na kusubiri kuvuka upande wa pili.
Nikupongeze tu Magufuli na Wafuasi wako wote kwa Ujasiri wako, ambao umefanikisha kwa kiwango hicho kufikia hatua zilizopo za kukamilisha ujenzi wa barabara zetu za Tanzania ususani hizi za ndani ya majiji na Zinazoingia Mijini, maana umepambana bila woga, na Umefanya kwa ajili ya Watu na si kwa ajili yako bali kwa ajili ya Taifa na Kizazi kijacho.
Pia Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Mrisho, kwa kuweka mkazo usimamiaji wa Maendeleo ususani Barabara
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu, mchimati@gmail.com 
   Hii ajali imetokea maeneo ya Manzese  Hawa wanachepuka hata hawajielewi  Mbele kidogo hapa mchepuko tutafika? 

WANAFUNZI WASHAURIWA KUJENGA MAHUSIANO YA URAFIKI NA WENZAO!!

Mtembeza wageni wa Kanisa la Mkunazini akiwafahamisha kitu wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii kutoka Dar es salam walipokuwa wakitembelea Kanisa hilo.DSC_0572Wanafunzi wakipata maelezo kwa Mtembeza wageni juu sehemu walipokuwa wakihifadhiwa watumwa Kanisani hapo.DSC_0602Hapa wanafunzi wakijichagulia katika moja ya maduka ya vinyago na nguo za Kiswahili yaliopo Ngome kongwe Mjini Unguja.DSC_0612Wanafunzi wakionyeshana Spices.DSC_0630Mtembeza wageni wa Kidishi Multi Spices Farm Bwana. Mur- tala Rashid akiwaonyesha mmoja wa mmea wa Spice na kuwafahamisha matumizi yake, mmea huo unaotambuliwa kwa jina la mchaichai katika chamba hilo.
…………………………………………………………………………………………….
Na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.
VYUO mbalimbali nchini, vimeshauriwa kujenga mahusiano ya kirafiki kati yao ili kubadilishana uzoefu katika kufanya kazi zao.
Ushauri huo umetolewa na mkuu wa msafara wa wanafunzi 70 kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii Dar es Salaam, Dawson Kyungai, wakati wakiwa katika ziara kuwatembelea viongozi wenzao wa Chuo cha Elimu Zanzibar (Zanzibar Education College).
Kyungai ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa ujasiri wao wa kutafuta njia za kujenga mahusiano na vyuo mbalimbali nchini.
Naye Mkuu wa Zanzibar Education College Ussi Said Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari katika Kanisa la Mkunazini walikotembelea, alisema suala la urafiki wa vyuo linawasaidia walimu na wanafunzi kubadilishana mawazo na kujifunza kwa ufanisi zaidi.
Wanafunzi hao 70 wako katika ziara ya siku tatu kuwatembelea wenzao wa Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu pamoja na kuzuru sehemu mbalimbali za kihistoria za Zanzibar.
Kwa upande wao, wanafunzi na walimu wa Zanzibar Education College, wanatarajia kufanya ziara kama hiyo Mkoani Dodoma mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.

MAR 23 JE! NDANI YA MOYO WAKO UNAWAZA NINI KUHUSU WAKATI NA MAISHA YAKO KILA SIKU, NA BAADA YA KUFA NI WAPI UNATARAJIA KWENDA ?

Na: Kanisa la Kristo Tanzania
===========================

Miaka ya ivi karibuni maeneo ya kando kando mwa barabara nyingi za Dar es Salaam, zilikuwa zinatoa uvundo wa harufu mbaya kutokana na wakazi wa maeneo hayo kufanya Mitaro ya barabarani kuwa sehemu sahihi kwao kutupa taka, baada ya ujenzi wa Barabara kuanza inaonekana sasa wakazi wengi wa maeneo mwa barabara hawatakuwa na maeneo ya kutupa taka Ovyo, kama inavyoonekana kwenye picha baadhi ya Taka zikiwa katikati ya njia kuu ya Magari yaendayo kwa Kasi, ambayo ndiyo kwanza inaanza kukamilika baadhi ya maeneo mengine, je hali hii itaachwa hivi mpaka lini? na je hao wanaoweka taka hizo ni watu wa Taifa hili? au je ni Kondoo aliyepotea kama  vinavyosema vitabu vitakatif kwamba anahitaji kuokolewa? kinachonishangaza hapa ni jinsi gani wahusika wa maeneo hayo ambao ni wa ngazi za chini wasichukue hatua za mapemaili kukomesha kabisa Taiba hiyo, barabara hizi ambazo kwa mtazamo wangu si tu kwamba tunamshukuru na kumsifu Magufuli na Kikwete katika mwongo huu wa Utawala, kwa kuzijenga, kitakachobaki si chao maana hata wao wataondoka na kupita, Tanzania itaendelea kuwapo hata pasipi wewe na huyo, maana nchi ni mali ya Mungu naye ametupa tuikalie Vizazi na vizazi, je Unataka kuwa na Choyo ya Kuawaachia watu na jamaa wa vizazi vyako kitu chema? maana kamamtu jambo ndogo namna hiyo linaanza kuonekana hivyi je itakapokuwa kwa makubwa itakuwaje? maendeleo ya nchi yanapopatikana si kwa ajili yako, bali kwa ajili ya watu wa nchi waikaayo, je ni kwa nini wewe unapokuwa umepata fulsa ya kuwa mwakilishi katika kufanya ,kusimamia,na kupanga mipango yoyote ya maeneleo ya jamii, watu, na Nchi kwa ajili ya watu wako, unabadili nia baada ya kuwa wamekupa ridhaa hiyo, na kufanya upendavyo wewe kwa cheo chako, kwa faifa ya wewe na wana wako na wa jamaa zako, kwa uharibifu wa mali nyingi ambazo zingeweza kutoshereza sehemu na watu wengine kwa kuwa wewe umesimama kwa ajilia yao? na wewe unayefanya hivyo kwa kile kidogo wadhani kile kikubwa utabadilika  na kutenda vingine kwa ajili ya watu wengine? Utajili na Mali ulizonazo kaa fikilia tu, na kisha angalia jamii iliyopo maisha yao, unadhani wewe ndiye ungeambiwa sasa utaishi kama huyo jamaa pale, ungehesabu siku ngapi? kwa nini umeshindwa kuwa mwaminifu kwa ajili ya watu wako? kwa nini unasema uongo, unadanganya wakati wa kuzungumzia masuala ya maendeleo ya jamii? je unafikiri kuwa kwenye Uongo kuna Maendeleo ya Kweli? Mnakimbia kuchukua na kuomba nafasi za Uongozi si kwa kuwa mioyo yenu ndani yake kuna dhamira ya kweli, kumbuka hakuna dhambi ndogo na kubwa, dhambi ni dhambi na inakutafuna bila wewe kujua,wewe unayechochea kwa maneno ya Uwongo Hukumu yako ipo, na wewe unayedhulumu nafsi za watu hukumu yako ipo, jambo hili ni kweli, kati ya asilimia 70 za utekelezwaji wa ahadi za wewe uliyesema azikutimiwa zaidi ya asilimia 30 tu ukweli ndani yako.
continue @. www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com

TAZAMA JAMAA WALIPO ZIMIKIWA NA COASTER WAKATI WA FOLENI UBUNGO DARAJANI

Konda wa Daladala linalosafirisha Abiria kati ya Mwenge njia ya Ubungo Kimara, pamoja na abiria wa gari hilo, majira ya saa nne asubuhi,wakishirikiana kusuka ili liweze kuwaka, kitendo kinachosababisha foleni wakati mwingine katikati ya majiji kwa uzembe wa madereva kushindwa kutumia vyombo vyao vya usafiri, na hivyo kuwa chanzo cha ajal za barabarani.

BAADHI YA WIZARA, IDARA NA TAASISI ZA SERIKALI ZAPEWA VIFAA VYA TEKNOLOJIA, HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA)

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo mafupi juu ya Mpango wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa baadhi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 2Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum akimkabidhi laptop Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa baadhi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 3 - 1Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani) 
wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa baadhi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 3Mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo nchini Bw. Richard Martin akitoa maelezo mafupi kwa Wageni waalikwa (hawapo pichani)wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa baadhi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 6Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) akikata utepe kuonesha baadhi ya vifaa vya TEHAMA vilivyokabidhiwa kwa baadhi Wizara, Idara na Taasisi za Serikali leo katika Ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 5Baadhi ya vifaa vya TEHAMA vilivyokabidhiwa kwa baadhi Wizara, Idara na Taasisi za Serikali leo katika Ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.PICHA ZA KUKABIDHI VIFAA 4
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongonzi mbalimbali wa Serikali pamoja na mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo nchini Bw. Richard Martini (kulia kwake) baada ya kumaliza hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa baadhi ya  Wizara, Idara na Taasisi za Serikali iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha.

 (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).