TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, July 17, 2014

MOTO WA MWANANYAMALA NA ROHO ZA UKATILI WA MIOYO YA WATANZANIA


Hii Ilikuwa Kama Picha ya Kivietinamu, maana tukio lenyewe ilikuwa kama jambo la kawaida kuona moshi wa Moto, ukianza Mdogo mdogo, Kamera Yetu inayoangaza pande zote yenyewe kazi yake ilikuwa ni kuhakikisha inakusanya vipande vipande (Crips) za Matukio isipikuwa Mkanda huu meneja aliyeandaa Vipande hivi naona hakutarajia kama kutatokea madhara makubwa kama ilivyo sasa, Pengine kwa mtazamo wake baada ya kuangalia Mikanda ya Wenzetu wa huko Majuu, Maana Movie za wenzetu kama unavyojua  tena, Wakiamua kutumia Magari basi Wanayateketeza kwa moto ili mradi tu Sinema hiyo Ikamilike, Tren na hata NDEGE.
Sasa mimi najiuliza kweli inakuwaje Moto Mkubwa kama huo unatokea wakati Vyombo husika vipo tena Mwananyamala Siyo Eneo ambalo utasema hakuna vitendea kazi, Vyombo husika vipo na Vimewekeza kwenye ardhi ya Mwananyamala, Watu walikuwapo wengi sana wa kuweza kuleta Amani kwa Kuchukua hatua Mapema, Kila Mtu siku hizi hakosi kuwa na Simu Mkononi, Sasa nikuulize wewe unayesoma muda huu hii habari, hiyo simu yako Mkononi unajua Matumizi yake? au ya kwako kazi yake ni kuwasiliana na huyo Mkeo/Mmeo/Boyfred/mchumba/biashara gani?Wizi tu; au kwa kuwa siku hizi kuna hata simu za Shilingi 1500? ndiyo maana hata wewe unayo, maana Simu ZENU hizo kuwaka zinawaka ila kubonyezeka hazibonyezeki.
Umbea tu unakusumbua, kuwa mwandishi wa habari basi utafute habari na utuletee matukio unayodhani kwamba unapenda yaendelee kutokea, unapata faida gani unaposhuhudia Uharibifu Mkubwa tena wa hatari kubwa ususani kwa Watoto wasiojua jinsi ya kujikwamua, au ndiyo ukomavu sasa wa Watanzania katika Maandalizi ya Uvunjifu wa Amani wa Makusudi unaoutafuta kwa Visingizio Visivyoturidhisha?
Tafakari@Kuhusu Mwananyala.

Tuesday, July 15, 2014

MADUKA YANAUNGUA MUDA HUU MWANANYAMALA JIJINI DAR

Zaidi ya nyumba 3 za Biashara zilizopo karibu na Hospitali ya Mwananyamala  jijini Dar es Salaam zinateketea kwa moto ambao bado unaendelea kuwaka kwa kasi na kutishia nyumba zingine zilzopo jirani. Zimamoto wamefika eneo la tukio na kuanza kuzima moto. Endelea kufuatilia kwa taarifa 

Habari na picha zaidi endelea kutufuatilia 

Sunday, June 29, 2014

TMAA YAOKOA BILIONI 15 ZA MADINI, YAPONGEZWA

                                          Na Saidi Mkabakuli
Afisa Habari wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA), Mhandisi Yesambi Shiwa (Kulia) akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa TMAA kwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu (Kushoto) wakati alipotembelea kwenye Banda la TMAA wakati wa Maadhimisho ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Mashine ya kisasa ya kupimia ubora wa sampuli za madini ikioneshwa kwenye Banda la TMAA wakati wa Maadhimisho ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu (Kushoto) akizungumza na watumishi wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) alipowatembelea kwenye Banda lao. Wanaomsikiliza ni Afisa Habari, Mhandisi Yesambi Shiwa (Kulia) na Afisa Utumishi, Bibi Fatma Chondo (Katikati).

Makaa ya mawe yakioneshwa kwenye Banda la TMAA wakati wa Maadhimisho ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya sampuli za madini yapatikanayo nchini yakioneshwa kwenye Banda la TMAA wakati wa Maadhimisho ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu (Kushoto) akihimiza kufanya kazi kwa uzalendo kwa watumishi wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) alipowatembelea kwenye Banda lao.
=======================================================================
Serikali imeupongeza Wakala wa ukaguzi wa madini nchini (TMAA) kwa kufanikiwa kuokoa kiasi kikubwa cha madini yaliyokuwa yakitoroshwa kinyemela katika viwanja vya ndege nchini hivyo kuokoa zaidi ya bilioni 15 zilizolipwa kama mrahaba tangu ilipoanzisha ukaguzi maalum kwa wasafiri waendao nje ya nchi.
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Hab Mkwizu alipokuwa akikagua utendaji kazi wa Wakala katika maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Bw. Mkwizu alisema kuwa kwa muda mrefu sasa wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakiitia hasara Serikali kwa kukwepa ulipaji wa kodi wa madini yaendayo nje ya Tanzania kinyume na utaratibu uliowekwa.
“Hongereni sana kwa kuweza kuokoa kiasi kikubwa cha madini yaliyokuwa yakisafirishwa bila kufuata taratibu zetu za usafirishaji wa madini yaendayo nje ya Tanzania,” alisema Bw. Mkwizu.
Naibu Katibu Mkuu Mkwizu aliwasihi viongozi na watumishi wa Wakala kuongeza uchapaji kazi na uzalendo ili kuweza kukomesha kabisa tabia ya wafanyabiashara hao wasio waaminifu.
Akikaribishwa kwenye banda la Wakala kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na Afisa Habari wa Wakala hiyo, Mhandisi Yisambi Shiwa, Bw. Mkwizu alijulishwa kuwa moja kati ya mafanikio yaliyofikiwa na Wakala mara baada ya ukaguzi wa ziada kwa wasafiri waendao nje ya Tanzania, ni pamoja na kubainika mamia ya wafanyabiashara wa madini ambao wamekuwa wakitorosha kinyemela madini ya thamani kubwa ya fedha bila kufuata taratibu.
“Katika kuboresha utendaji kazi wa Wakala, tulitambulisha mpangokazi mpya wa ukaguzi wa ziada katika viwanja vyetu vya ndege vikubwa vya Dar es Salaam, Kilimanjaro na kile cha Mwanza lengo ni kubaini wafanyabiashara wasio waaminifu na ndipo tulipobaini wizi huu,” alisema Mhandisi Shiwa.
Akizungumzia thamani ya madini hayo, Mhandisi Shiwa alisema kuwa kufuatia ukaguzi huu, mpaka sasa Wakala imeweza kuokoa madini yenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 15.
“Ukaguzi huu umesaidia kuokoa kiasi kikubwa cha madini yenye thamani ya shilingi bilioni 15.3 hadi kufikia mwaka na hivyo kuiongezea serikali yetu mapato ambayo yalikuwa yatoroshwe na wafanyabiashara hao wasio waaminifu,” aliongeza.
Kwa mujibu wa Mhandisi Shiwa, kiasi hiki cha fedha ni sehemu ya mrahaba wa kisheria unaostahili kuchangiwa na wafanyabiashara hao kwa umiliki wao wa madini hayo kabla ya kusafirisha nje ya nchi.
Mhandisi Shiwa aliongeza kuwa katika kuendelea kudhibiti tabia hizi, Wakala kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali imekuwa ikishikilia na kutaifisha madini yanayotiliwa shaka ama kumilikiwa isivyo halali yanayopatikana katika viwanja hivyo.
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania ni Wakala wa Serikali ulioanzishwa tarehe 2 Novemba, 2009 chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura ya 245. Tamko la Waziri la kuanzisha Wakala lilichapishwa kwenye Gazeti la Serikali Namba 362 la tarehe 6 Novemba, 2009.
Lengo la Wakala ni kuhakikisha kwamba, Serikali inapata mapato stahiki kutoka kwenye shughuli za uzalishaji na biashara ya madini nchini kupitia usimamizi na ukaguzi makini wa shughuli za uchimbaji, na kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji thabiti wa mazingira katika maeneo ya migodi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Mheshimiwa Stephen Masato Wasira (Mb) Akiwasilisha Bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013

Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) pamoja na Naibu wake, Bw. Maduka Kessy wakifuatilia kwa umakini uwasilishaji wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 na Mpango na Maendeleo wa Taifa 2014/15.

Wageni wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Mheshimiwa Stephen Masato Wasira (Mb) ambao ni baadhi ya viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakifuatilia kwa umakini uwasilishaji wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 na Mpango na Maendeleo wa Taifa 2014/15.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Mheshimiwa Stephen Masato Wasira (Mb) Akiwasilisha Bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 na Mpango na Maendeleo wa Taifa 2014/15.

Tuesday, April 29, 2014

WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU WATAKIWAKUFANYA KAZI KWA MALENGO ILI KUBORESHA MAISHA YAO CHUNYA


Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro akifungua  semina iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa wakulima wa zao la Tumbaku katika Ukumbi wa Sapanjo unaomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya Chunya

Mwakilishi wa Meneja wa NMB Kanda Sumka Mbuba amesema Benki ya NMB ina mkakati wa kuwa karibu na wakulima wa mazao mbalimbali na kuendesha semina mbalimbali zitakazowasaidia wakulima kujikwamua kiuchumi.

Meneja wa NMB wilaya Chunya Musa Mumba alisema Benki yake ipo tayari kutoa mikopo kwa wakulima wa zao la Tumbaku na kuwataka kuwa waaminifu katika kurejesha mikopo kwa wakati ili iweze kusaidia wakulima wengine.

Baadhi ya wwezeshaji tika NMB wakimsikiliza mgeni rasmi


Wakulima wa zao la Tumbaku wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi




Picha ya pamoja


Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro amewataka wakulima wa zao la Tumbaku kufanya kazi kwa malengo ili kuboresha maisha yao na Watanzania ili kupata matokeo makubwa sasa(BRN).
Ameyasema hayo alipokuwa anafungua semina iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa wakulima wa zao la Tumbaku katika Ukumbi wa Sapanjo unaomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ili kuleta tija kwa wakulima ambao wamekuwa na maisha duni.
Kinawiro ameitaka Benki ya NMB kutoa mikopo nafuu kwa wakulima wa Tumbaku na kukopesha Pembejeo kwa gharama nafuu ili vyama viweze kujikwamua kiuchumi kwa ajili ya kupata majawabu sahihi na Serikali inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Benki hiyo.
Aidha amewataka viongozi wa vyama vya Ushirika na Benki kufanya kazi kwa uadilifu na kuacha kukwepa kutorosha Tumbaku na kupeleka mikoa mingine na nchi jirani kwa nia ya kukwepa madeni wanayodaiwa pia kufanya hivyo kunakosesha serikali mapato yake yanayotokana na ushuru.
Pia amewataka wakulima wa zao la Tumbaku kuweka pesa benki na kuhakikisha wanapanda miti ili kutunza mazingira na kupata nishati mbadala ili kuhifadhi mazingira ya Wilaya ya Chunya.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Chunya alitumia fursa hiyo kuiomba Benki ya NMB kusaidia mazao mengine kama ufuta ambayo yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa pato la wilaya hiyo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Meneja wa Kanda Sumka Mbuba amesema Benki ya NMB ina mkakati wa kuwa karibu na wakulima wa mazao mbalimbali na kuendesha semina mbalimbali zitakazowasaidia wakulima kujikwamua kiuchumi kama siku za hivi karibuni walifanya semina ka hii kwa wakulima wa zao la Kahawa ilyojumuisha wilaya za Mbeya,Mbozi,Rungwe,Ileje na Mbeya.
Meneja wa NMB wilaya Chunya Musa Mumba alisema Benki yake ipo tayari kutoa mikopo kwa wakulima wa zao la Tumbaku na kuwataka kuwa waaminifu katika kurejesha mikopo kwa wakati ili iweze kusaidia wakulima wengine.

Na Mbeya yetu 
Chunya

BASI LA AM LAMGONGA MWENDESHA BAISKELI ENEO LA MAJENGO ARUSHA


Mwendesha Baiskeri akiwa ameumia vibaya Mguuni baada ya kugongwa na Basi hilo
Picha na Arusha yetu Blog