Huku ulimwengu
ukiadhimisha miaka 70 tangu ndege za kijeshi za Marekani ilipodondosha
bomu la kinyuklia juu ya Nagasaki tazama picha za janga hilo.
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, November 11, 2015
JESHI LA POLISI LAANZA KUTOA ELIMU KWA ABIRIA NA MADEREVA ILI KUKABILIANA NA AJALI KATIKA KIPINDI CHA MWISHO WA MWAKA
Mkurugenzi wa habari Ikulu afungasha virago
World Bank Group: Evaluation Officer, Washington DC
JOB OPPORTUNITY
The Independent Evaluation Group (IEG) is the organizational unit in the World Bank Group (WBG) providing evaluation and feedback on the development effectiveness of Bank Group activities in client countries.
They are currently recruiting 3 Evaluation Officers (GF) VIEW HERE under two streams i.e.:
- Human Development: social protection, health and nutrition, and/or education. (1 position)
- Sustainable Development: sustainable development, including Infrastructure (water, transport), environment, agriculture. (2 positions) Under the direction of the Unit Manager, the Evaluation Officer will contribute directly to IEG evaluations. This work will include conducting project-level validations and evaluations (at least 50% of the annual work program will be dedicated to this), contributing to larger thematic, sectoral and corporate evaluations, overseeing contributions from consultants, contributing to budget and team oversight, and commenting on the work of others.
SERIKALI IMEOMBWA KUINGILIA KATI SAKATA LA FAMILIA YA JUMA ISANGU, ARUMERU
![]()
Mkazi wa eneo la Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha, Juma Isangu akiwa na mkewe Janet Tinai pamoja na mwanao, Issa Juma (katikati) wakiangalia nyaraka mbalimbali nje ya nyumba yao mara baada ya kufukuzwa na kisha kuvunjiwa nyumba yao wilayani humo na kampuni ya Majembe Auction Mart kwa amri ya mahakama.
![]()
Mkazi wa eneo la Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha, Janet Tinai akilalamika mbele ya waandishi wa habari akiwa na baadhi ya vyombo vyake mara baada ya kuhamishwa kwa amri ya mahakama na kampuni ya Majembe Auction Mart. |
NIKO TAYARI KUKAMATWA, MAALIM SEIF
By Hassan Ali, Mwananchi, Mwananchi Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema yuko tayari kukamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka, kama kitendo chake cha kujitangazia ushindi ni kosa.
JASIRI WA WANASHERIA WASAIDIA KUPUNGUZA VITENDO VYA UKATILI WA JINSIA SOKO LA TABATA MUSLIM JIJINI DAR ES SALAAM Posted:
Katibu wa soko la Tabata Muslim lililopo Manispaa ya Ilala, John Nombo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG), kutoa mafunzo ya kupinga ukatili huo katika masoko sita ya Manispaa hiyo. Kulia ni Mwezeshaji wa Sheria wa Soko hilo, Aisha Juma na Saada Ngunde.
Tuesday, November 10, 2015
BODI YA MIKOPO YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOENEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO KWA 2015/2016
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuutaarifu umma kuwa kuna taarifa zinazosambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa Bodi haitatoa mikopo kwa waombaji wapya kwa mwaka wa masomo 2015/2016. Taarifa hizo si za kweli na hivyo Bodi inauomba umma kuzipuuza.
KAMPUNI YA TTCL YAWASAIDIA WATOTO VIFAA VYA MASOMO KITUO CHA AWALI LUKEMA VINGUNGUTI
RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI DKT. KIJO-BISIMBA NA KUKAGUA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akimjulia hali Mkurugenzi wa Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu Dkt. Helen Kijo-Bisimba aliyelazwa katika
Hospitali ya Agha Khan mara baada ya kupata ajali mbaya ya gari katika Barabara
ya Ali Hassan Mwinyi jana.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli katikati akitoka kufanya ukaguzi wa
kushtukiza katika Taasisi ya Mifupa MOI kujionea halihalisi ya utoaji huduma
kwa wagonjwa katika taasisi hiyo.
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATANGAZA MFUMUKO WA BEI WA MWEZI OKTOBA, 2015
Na Veronica Kazimoto
09/11/2015
Dar es Salaam.
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 mwezi Septemba mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo amesema kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei kumesababishwa na kupanda kwa bei za bidhaa na huduma zingine za kijamii ikiwemo chakula na nishati.
“Kupanda kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba, 2015 kumechangiwa na ongezeko la bei za vyakula kama vile Mchele ambao umeongezeka bei kwa asilimia 0.8, unga wa muhogo umeongezeka hadi asilimia 0.7, nyama kwa asilimia 0.8, samaki kwa asilimia 5.5, ndizi za kupika asilimia 0.7 na choroko kwa asilimia 0.9”, amesema Kwesigabo.
Bidhaa zisizokuwa za vyakula kama vile vitambaa kwa ajili ya nguo za kike zimepanda kwa asilimia 1.6, viatu vya kiume asilimia 1.1, mkaa asilimia 1.4 na gharama za kupata ushauri kwa daktari pia zimepanda hadi kufikia asilimia 1.4.
Kwa upande Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.1 ambao ni ongezeko sawa na mwezi Septemba, 2015. Fahirisi za bei pia zimeongezeka kutoka 159.04 hadi kufikia 159.17 kwa mwezi Oktoba, 2015.
“Fahirisi za bei za vyakula vya nyumbani na migahawani iliongezeka kidogo hadi kufikia asilimia 10.0 kutoka asilimia 9.4 kwa mwezi Septemba, 2015 ambapo bidhaa zisizokuwa za vyakula zimepungua kidogo kutoka asilimia 1.9 hadi asilimia 1.7 kwa mwezi Oktoba, 2015,” amefafanua Kwesigabo.
Kwesigabo amesema kuwa Mfumuko wa Bei ambao haujumuishi vyakula na nishati kwa mwezi Oktoba, 2015 umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 2.1 kutoka asilimia 2.2 kwa mwezi Septemba, 2015.
Mwisho.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Kuhusu Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 ambao umepanda hadi kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 kwa mwezi Septemba, 2015.
Monday, October 26, 2015
Sunday, October 25, 2015
TUMEPIGA KURA, NA SASA TUPOKEE MATOKEO KWA AMANI NA UTULIVU, KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI.
JUMAPILI ya Oktoba 25, 2015, Tanzania imefanya Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge pamoja na kumpata Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uchaguzi ni nini? Zipo tafsiri mbalimbali lakini mojawapo na iliyo wazi ni kwamba, Uchaguzi ni njia ya kidemokrasia inayotumiwa na watu katika kuchagua viongozi wa kuwaongoza kwa kipindi fulani kwa mujibu wa Katiba au utaratibu waliojiwekea wenyewe.
Huu ni Uchaguzi Mkuu wa Tano kufanyika tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza tena mwaka 1992, lakini ni wa 11 tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoungana mwaka 1964.
Uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa na umuhimu wa kipekee kwa sababu kadha wa kadha, mojawapo ikiwa umri wa miaka 23 tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza.
Huu ni umri mkubwa, na kwa hakika vijana wengi waliojitokeza kujiandikisha safari hii ni wenye umri wa kati ya miaka 18-35, ikimaanisha kwamba wengi wao walizaliwa kuanzia mwaka 1992. Hawa wanatengeneza asilimia 57 ya wapigakura wote.
Umuhimu mwingine ni kwamba, kulinganisha na uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, safari hii demokrasia imekua na kupanuka kiasi cha kushuhudia wapigakura 22.75 milioni, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini tangu tupate Uhuru.
Kwa upande mwingine, hamasa imeongezeka, upinzani umeimarika zaidi na uhuru wa habari umepanuka ukiwamo ukuaji wa sekta ya habari na mawasiliano, hususan mitandao ya kijamii.
Haya yote yanatokea kutokana na kuwapo kwa amani na utulivu, sifa ambazo zimeendelea kuitambulisha vyema Tanzania hata katika jumuiya za kimataifa.
Uchaguzi Mkuu ni gharama kubwa kifedha, rasilimali watu na muda, na kama mambo yatakwenda mrama maana yake nchi itakuwa imeingia hasara kwa kupoteza fedha, lakini pia itaingia kwenye machafuko ambayo yatatowesha amani iliyodumu kwa miaka mingi.
Madhara ya machafuko au vita – kama tulivyoshuhudia kwa majirani zetu Rwanda na Kenya ni vifo, ulemavu wa kudumu, kutengana na familia, ukimbizi na kuvurugika kwa uchumi, jamii na siasa kwa ujumla. Kwa miaka yote tangu Uhuru, licha ya uchanga na umaskini kama taifa, Watanzania hatujazoea maisha ya vurugu na machafuko na ndiyo maana tuna wajibu wa kuhakikisha uchaguzi huu unapita salama.
Wajibu wa kulinda amani ya nchi yetu ni wa kila Mtanzania bila kujali rangi, dini, kabila ama nafasi yake katika jamii. Tunaposema hivyo tunamaanisha kwamba, vyombo vya dola vinapaswa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha Watanzania wanapiga kura kwa amani kuchagua viongozi wao kwa utaratibu waliojiwekea.
Kimsingi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ndio wasimamizi wa chaguzi zote, hivyo wana dhamana kubwa kuhakikisha kila aliyejiandikisha na kujitokeza siku hiyo anatumia haki yake ya kikatiba kupiga kura bila kubughudhiwa.
Ili kuondoa utata huo, NEC pia inapaswa kuhakikisha kunakuwa na uwazi kuanzia hatua ya kupiga kura mpaka wakati wa kutangaza matokeo, ambayo pia yanatakiwa kutolewa kwa wakati ili kuondoa mashaka miongoni mwa wagombea na wananchi kwa ujumla.
Wanasiasa, hususan wagombea ama wapambe wao, wanapaswa kutoa kauli za kuhamasisha amani na utulivu kwa siku hizi chache zilizosalia kuelekea uchaguzi mkuu, siku ya uchaguzi na baada ya kutangazwa kwa matokeo.
Subscribe to:
Posts (Atom)










