TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, August 7, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA SAYANSI KWA NCHI ZA AFRIKA NA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA, JIJINI ARUSHA

Makamu wa Rais Dkt. Bilal katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo, baada ya ufunguzi.Picha na OMR
Kongamano hilo la siku tatu limefanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Jijini Arusha jana Agosti 5, 2014, na kushirikisha mabingwa mbalimbali wa tafiti ndani ya Afrika na nchi za ukanda wa Jangwa la Sahara.

Kongamano hilo ambalo limedhaminiwa na Shirika la misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) linalenga kukuza tafiti za kisayansi na kutanua maendeleo ya tafiti hizo ili yasaidie wananchi wa nchi za ukanda huu hasa vijana ambao wanaelezwa kuwa na idadi kubwa kulinganisha na wazee na akina mama.

Katika Hotuba ya mgeni rasmi Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alisema kuwa, dhana ya umuhimu katika uwekezaji na utanuaji wa sayansi katika Afrika, inahitaji kutazama kundi la vijana na kulihamasisha kushiriki katika masomo ya sayansi ili kuharakisha maendeleo kwa Bara la Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chuo cha Nelson Mandela cha jijini Arusha wakati alipowasili kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Nelson Mandela, Bernard Mussa, aliyetafiti kuhusu kuongeza joto katika Majiko kwa kutumia mwanga wa jua, wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa mradi wa Masai Stove’s & Solar, Kisioki Moitiko aliyetafiti kuhusu mzunguko wau meme wa Jua kutumika katika nyumba za kabila la kimasai (Maboma) wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Hassna Founoune, kutoka Taasisi ya Tafiti ya Kilimo ya Senegal, wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo katika Screen na Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela, Prof. Bulton Mwamila, wakati wakiangalia mjadala uliokuwa ukiendelea kupitia ‘Video Conference’ kati ya Marekani na Tanzania, kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara.

Kanisa la Pugu Chanika SDA lapata milioni 5 kutoka IPTL/PAP kuendeleza ujenzi

 KANISA la Waadventista wa Sabato la Pugu Chanika lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam sasa linaweza kuendeleza mradi wake wa ujenzi na upanuzi wa kanisa baada ya kupata msaada wa fedha wa shilingi milioni 5 kutoka kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL). Msaada huo uliotolewa wakati wa ibada Jumamosi, umefufua jitihada la kanisa za kutanua na kumalizia ukumbi wa kanisa uliopo sasa pamoja na kumalizia ujenzi wa majengo mengine.

Mwakilishi kutoka IPTL ambayo ni kampuni tanzu ya Pan African Power Solutions Tanzania (PAP), Bw. Joseph Makandege, ambaye ni Katibu na Mwanasheria Mkuu wa kampuni hiyo, amesema msaada huo ni sehemu ya jitihada za kampuni yake kuunga mkono miradi mbali mbali yenye manufaa makubwa kwa kijamii.

“Baada ya kupokea maombi toka katika kanisa hilo ya kututaka kusaidia mradi huo wa ujenzi, Bodi ya wakurugenzi ya IPTL/PAP ikiongozwa na Mwenyekiti Mtendaji Bw. Harbinder Singh Sethi mara moja ilipitisha kiasi cha shilingi milioni 5 kwa kuwa inaamini kuwa taasisi za kidini zinasaidia kulijenga taifa lenye watu wanaomuogopa Mungu na hivyo kuifanya nchi iwe na mazingira mazuri ya kufanya biashara ambayo inasaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi.

“Tunaamini kuwa katika makanisa, familia zilizotengana zinaunganishwa, waliuokosa matumaini wanapewa matumaini, na maisha ya watu yanabadilika. Inampendeza Mungu kusikia sauti za nyimbo zinazomtukuza, ujumbe madhubuti kutoka kwa wachungaji, ushuhuda wa kazi zitokanazo na Mungu, na sauti nzuri za watoto zisema Amina.

“Kampuni yetu isingeweza kukataa ombi hilo la kusaidia kanisa katika mradi ambao utatukuza kazi ya Mungu na maisha ya walio wengi katika jamii yetu yatabadilishwa kwa ujumla,” alisema Makandege. Aliliasa kanisa kutumia fedha hizo vizuri ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Naye, Mchungaji wa Kanisa hilo, Gallus Gido aliishukuru IPTL/PAP kwa mchango wao ambao alisema umewagusa watu wengi na utalisaidia kanisa kuweza kuwahudumia waumini wengi wanaomtukuza na kumuomba Mungu.

"Katika kitabu cha Matendo 10:1-4, kulikuwa na mtu aliyekuwa akitoa misaada/sadaka kwa jamii yake. Siku moja Mungu alimtokea na kumwambia kwamba sala na sadaka zake zimefika mbinguni. Nataka kuwaambia IPTL/PAP kwamba mchango wao wa kuendelea kusaidia taasisi mbalimbali ya kidini na jamii kwa ujumla, utawafungulia milango mbinguni kwa ajili ya baraka zaidi," alisema.

Mchungaji aliongeza kuwa mchango wa IPTL/PAP unadhihirisha upendo wa kampuni hiyo kwa Mungu na watu, na kuhaidi kuwa atafanyakazi kwa ukaribu na kamati ya ujenzi kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika vizuri kwa lengo lililokusudiwa.

HUDUMA MPYA YA BWERERE YAZINDULIWA KUTOKA TTCL

 Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL,Bwa.Peter Ngota akionesha kipeperushi chenye taarifa mbalimbali kuhusiana na huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina la Bwerere,Kwa waandishi wa habari,huduma hiyo imezinduliwa leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar. 
 Baadhi ya Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa huduma mpya ya TTCL iliyojulikana kwa jina la Bwerere ,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar. 
Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL, Bwa.Peter Ngota akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uzinduzi wa huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina la Bwerere,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar.
=======  ======= =======
Bwa.Peter alisema kuwa siku ya leo ,TTCL inazindua rasmi promosheni inayolenga kuwapa wananchi huduma bora na za bei nafuu. Promotion hii inajulikana kwa jina la  BWERERE   yaani pata huduma nyingi zaidi kwa bei nafuu zaidi.

''Promosheni hii inatoa fursa kwa wateja wa majumbani na maofisini ambao wanatumia  huduma ya malipo ya kabla(pre-paid) kufurahia gharama ya viwango vya chini kabisa vya kupiga simu TTCL kwenda kwenda mitandao mingine yote ikiwa ni pamoja na TTCL yenyewe,

Vilevile Promosheni hii inatoa fursa maalumu kwa watumiaji wa vifurushi vya intaneti(DATA)  kwa njia ya Broadband mtandao wa Nyaya na Mkongo waTTCL kitaalamu Fixed lines kuweza kupata intaneti bila kikomo''.Alisema Bwa.Peter Ngota.

IPTL/PAP kuendeleza ujenzi kuendeleza ujenzi wa kanisa la Pugu Chanika SDA

 KANISA la Waadventista wa Sabato la Pugu Chanika lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam sasa linaweza kuendeleza mradi wake wa ujenzi na upanuzi wa kanisa baada ya kupata msaada wa fedha wa shilingi milioni 5 kutoka kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL). Msaada huo uliotolewa wakati wa ibada Jumamosi, umefufua jitihada la kanisa za kutanua na kumalizia ukumbi wa kanisa uliopo sasa pamoja na kumalizia ujenzi wa majengo mengine.

Mwakilishi kutoka IPTL ambayo ni kampuni tanzu ya Pan African Power Solutions Tanzania (PAP), Bw. Joseph Makandege, ambaye ni Katibu na Mwanasheria Mkuu wa kampuni hiyo, amesema msaada huo ni sehemu ya jitihada za kampuni yake kuunga mkono miradi mbali mbali yenye manufaa makubwa kwa kijamii.

“Baada ya kupokea maombi toka katika kanisa hilo ya kututaka kusaidia mradi huo wa ujenzi, Bodi ya wakurugenzi ya IPTL/PAP ikiongozwa na Mwenyekiti Mtendaji Bw. Harbinder Singh Sethi mara moja ilipitisha kiasi cha shilingi milioni 5 kwa kuwa inaamini kuwa taasisi za kidini zinasaidia kulijenga taifa lenye watu wanaomuogopa Mungu na hivyo kuifanya nchi iwe na mazingira mazuri ya kufanya biashara ambayo inasaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi.

“Tunaamini kuwa katika makanisa, familia zilizotengana zinaunganishwa, waliuokosa matumaini wanapewa matumaini, na maisha ya watu yanabadilika. Inampendeza Mungu kusikia sauti za nyimbo zinazomtukuza, ujumbe madhubuti kutoka kwa wachungaji, ushuhuda wa kazi zitokanazo na Mungu, na sauti nzuri za watoto zisema Amina.

“Kampuni yetu isingeweza kukataa ombi hilo la kusaidia kanisa katika mradi ambao utatukuza kazi ya Mungu na maisha ya walio wengi katika jamii yetu yatabadilishwa kwa ujumla,” alisema Makandege. Aliliasa kanisa kutumia fedha hizo vizuri ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Naye, Mchungaji wa Kanisa hilo, Gallus Gido aliishukuru IPTL/PAP kwa mchango wao ambao alisema umewagusa watu wengi na utalisaidia kanisa kuweza kuwahudumia waumini wengi wanaomtukuza na kumuomba Mungu.

"Katika kitabu cha Matendo 10:1-4, kulikuwa na mtu aliyekuwa akitoa misaada/sadaka kwa jamii yake. Siku moja Mungu alimtokea na kumwambia kwamba sala na sadaka zake zimefika mbinguni. Nataka kuwaambia IPTL/PAP kwamba mchango wao wa kuendelea kusaidia taasisi mbalimbali ya kidini na jamii kwa ujumla, utawafungulia milango mbinguni kwa ajili ya baraka zaidi," alisema.

Mchungaji aliongeza kuwa mchango wa IPTL/PAP unadhihirisha upendo wa kampuni hiyo kwa Mungu na watu, na kuhaidi kuwa atafanyakazi kwa ukaribu na kamati ya ujenzi kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika vizuri kwa lengo lililokusudiwa.

TAHA WASHIRIKI MAONYESHO YA NANE NANE MBEYA

Afisa kilimo Mkoa wa Mbeya (Aliyevaa tai) akipokea maelezo ya kilimo cha mboga ndani ya hema maalumu ya kuoteshea nyanya iliyowekwa na Barton Tanzania kwa ushirikiano na TAHAAfisa kilimo Mkoa wa Mbeya (Aliyevaa tai) akipokea maelezo ya kilimo cha mboga ndani ya hema maalumu ya kuoteshea nyanya iliyowekwa na Barton Tanzania kwa ushirikiano na TAHA katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
Afisa Kilimo na Msimamizi wa ofisi ya TAHA ukanda wa Nyanda za Juu Kusini Bw. Ringo (Mwenye Jaketi jekundu) akifafanua juu ya matumizi bora ya teknoloji za kisasa kwenye kilimo cha mboga ili kuongeza tija kwa MkulimaAfisa Kilimo na Msimamizi wa ofisi ya TAHA ukanda wa Nyanda za Juu Kusini Bw. Ringo (Mwenye Jaketi jekundu) akifafanua juu ya matumizi bora ya teknoloji za kisasa kwenye kilimo cha mboga ili kuongeza tija kwa Mkulima katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
Mtaalamu wa Kilimo wa TAHA Bw. Anania Bansimbile akiwaonyesha wananchi namna bora ya kuotesha mimea ya mboga kabla ya kupandwa shambaniMtaalamu wa Kilimo wa TAHA Bw. Anania Bansimbile akiwaonyesha wananchi namna bora ya kuotesha mimea ya mboga kabla ya kupandwa shambani katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
Chainizi iliyopandwa kwa ustadi wa hali ya juuChainizi iliyopandwa kwa ustadi wa hali ya juu.
 
Hema maalumu(greenhouse) la kuoteshea mazao yanayohitaji joto ili yaweze kustawi vizuriHema maalumu(greenhouse) la kuoteshea mazao yanayohitaji joto ili yaweze kustawi vizuri
Plot ya TAHA na mshirika wake Barton kama inavyoonekana katika pichaPlot ya TAHA na mshirika wake Barton kama inavyoonekana katika picha
Mazao ya mboga yaliyopandwa kwa utaalamu wa hali ya juu kwenye vitalu vya mboga vya TAHAPlot ya TAHA na mshirika wake Barton kama inavyoonekana katika picha
Karoti iliyovunwa kutoka katika vitalu vya TAHA kwa ajili ya maonesho ya wakulima katika viwanja vya Nanenane MbeyaKaroti iliyovunwa kutoka katika vitalu vya TAHA kwa ajili ya maonesho ya wakulima katika viwanja vya Nanenane Mbeya
Wananchi wakipokea elimu kutoka kwa mtaalamu wa TAHA namna ya kuotesha nyanya kwenye hema maalumu ya kuoteshea mazao ya mbogaWananchi wakipewa elimu lishe kuhusu umuhimu wa matumizi ya mboga kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya lishe wa TAHA Bi. Lawrencia wakati wa maonyesho ya Nanenane Mbeya
Mtaalamu akimuelekeza jambo Mkulima aliyetembelea Banda la TAHAMtaalamu akimuelekeza jambo Mkulima aliyetembelea Banda la TAHA

Uhuru wanted to flee Kenya on Saba Saba day, Raila claims

Monday, August 4, 2014 - 00:00 -- BY JUSTUS OCHIENG
READY FOR TAKE-OFF: President Uhuru Kenyatta and his deputy William Ruto in the cockpit of the new Boeing 777-300ER Aircraft at JKIA. Photo/PSCU
READY FOR TAKE-OFF: President Uhuru Kenyatta and his deputy William Ruto in the cockpit of the new Boeing 777-300ER Aircraft at JKIA. Photo/PSCU
CORD leader Raila Odinga has slammed President Uhuru Kenyatta’s impromptu inspection of the new Terminal 1A at the Jomo Kenyatta International Airport during Saba Saba rally terming it “cowardly.”
Odinga said Uhuru made an unplanned visit at the JKIA in pretext that he was going to inspect the new Terminal 1A at the facility. Speaking in his mother tongue, Odinga said President Uhuru feared that Cord supporters would storm State House and moved to the JKIA airport “ready to flee.”
Raila added that the move to deploy several police officers to cordon off State House during their rally was cowardly. “He (President Kenyatta) thought that we would rally our supporters to storm State House. We were not stupid to make such a move,” said the former PM.
Raila criticized Jubilee leaders claiming that Saba Saba rally was an anticlimax. He was addressing mourners at Oindo village, Karachuonyo in Homabay County during the burial of former planning minister and area MP Adhu Awiti on Saturday.
- See more at: http://www.the-star.co.ke/news/article-182535/uhuru-wanted-flee-kenya-saba-saba-day-raila-claims#sthash.eEVUQp1S.dpuf

LAPF YATOA MIKOPO YA ELIMU KWA WANACHAMA WAKE

 Kaimu meneja Masoko wa LAPFBi Rehema Mkamba akitoa maelezo kwa wananchi na wanachama waliotembelea banda la lapf Nane Nane Mjini Dodoma.
 Afisa matekelezo wa LAPF  Bi Christina Mbaga akitoa maelezo juu ya Mkopo wa Elimu unaotolewa kwa wanachama wa LAPF. Mkopo huu umekuwa kivutio kikubwa kwa wanachama na wasio wanachama. 
 Afisa Mifumo ya Computer Bi. hilda Kato akifafanua jambo kwa wanachama waliotembelea bandani hapo. 
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF walioshiriki katika maonyesho ya Nane Nane Nzuguni Mjini Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja

MfukowaPensheniwa LAPF  umeanza kutoa Mikopo ya Elimu ya Juu kwa wanachama wake kwalengo la kuwasaidia wanachama wanaotaka kujiendeleza kielimu kwa kuwalipia ada ya masomo. LAPF inajua kuna baadhi ya wanachama walitamani kujiendeleza kielimu lakini kwa namna moja au nyingine wameshindwa kutokana na gharama za masomo hayo hivyo LAPF itawawezesha kutimiza malengo yao.  LAPF ndio Mfuko Pekee wa Pensheni nchini unaotoa mkopo wa Elimu kwa wanachama wake. 
LAPF, MCHANGO ULE ULE MAFAO ZAIDI.

WANAODAIWA KUMUUA AFISA USALAMA WA TAIFA WAFIKISHWA MAHAKAMANI WATAZAME HAPA

Watuhumiwa wakiwa wamembeba mtuhumiwa mwenzao ambaye inadaiwa kuwa ni afisa usalama wa taifa.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo imewapandisha kizimbani watu wanne wanaodaiwa kumuua kwa kumpiga risasi Ofisa Usalama wa Taifa, Sylvanus Mzeru maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Aprili 29, mwaka huu usiku.
Watuhumiwa hao ni Mohamed Othuman, Lucy Wiston,Omary Said , Kelvin Peter ambao walisomewa shitaka lao na wakili wa Serikali, Seina Kapenge.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 20, mwaka huu itakaposikilizwa tena katika mahakama hiyo.
 Mtuhumiwa Mohamed Othuman anayedaiwa kuwa ni afisa usalama akiwa amelala chini baada ya kushindwa kukaa.
 Mtuhuhiwa Lucy Wiston akiwa kwenye ulinzi mkali

SSRA YAZINDUA KANUNI MPYA ZA KUHUISHA MAFAO YA PENSHENI

Waziri wa Kazi na Ajira, Dk.Gaudensia Kabaka akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma juzi kuhusu mabadiliko ya Kanuni za Kuhuisha Mafao ya Pensheni kwa Mifuko ya  Hifadhi ya Jamii ya kuwa na aina moja kwa wastaafu.Katikati ni Mwenyekiti wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Juma Muhimbi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo, Irene Isaka.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Irene Isaka akifurahia jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Dodomajuzi.
 Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wakimsikiliza Waziri wa Kazi na Ajira Dk Gaudensia Kabaka,kuhusu mabadiliko ya Kanuni za Kuhuisha Mafao ya Pensheni kwa Mifuko ya  Hifadhi ya Jamii ya kuwa na aina moja kwa wastaafu kupitia Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wakiwa katika picha ya pamoja na  Waziri wa Kazi na Ajira Dk Gaudensia Kabaka na Naibu wake Makongoro Mahanga.

WEZI WA KAZI ZA WASANII KUKIONA,KAMATA KAMATA YAANZA RASMI

 Kampuni ya Msama Promotions Ltd,kwa kushirikiana na Wizara ya habari vijana,utamaduni na michezo  imetangaza neema kwa wasanii kuanza zoezi la kuwakamata watu wanaouza nakala feki  za wasanii hapa nchini.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Bwana  Alex Msama  amesema hayo jijini dar ,kuwa zoezi hilo limekwishaanza, na mpaka  sasa wamekamatwa vijana wane katika mkoa wa Dodoma na watatu jijini Mwanza.

‘’Kuna kazi mbalimbali ambazo zinaibiwa kila kukicha huku wamiliki wa kazi hizo wakiendelea  kushuka kiuchumi  na kutoona faida  yoyote ya kazi hizo,huu ni wakati kwa wasanii kuneemeka na kazi zao.Hivyo tutahakikisha tunafika kila mahali hata sehemu zisizofikika kirahisi na yote hii ni kuonyesha kuwa tunajali na tunathamini kazi za wasanii wetu’’,alisema Msama kwa msisitizo.

Alisema, nakala zote zitakuwa na stika za TRA  kuhakikisha hakuna wizi wowote unaofanyika  na unaotokea katika kazi mbalimbali za wasanii.Stika hizo zimewekwa ili kuwabaini wale wote wenye hulka hiyo ya kuiba kazi za wasanii .Operesheni  hiyo itafanyika  bila kujali wadhifa wake ama cheo chake,akaongeza kusema kuwa zoezi hilo ni salamu kwa wale wote wanoatumia kazi za wasanii bila kufuata  utaratibu wa sheria zilizopo.

Pia amelipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha katika changamoto,na pia wamekuwa wakishirikiana  nao kuhakikisha  zoezi hilo linakuwa endelevu na kuzunguka kila mkoa kuhakikisha  kazi za wasanii zinaheshimiwa na zinalindwa kwa kila namna.

TAARIFA RASMITOKA IKULU KUHUSU MCHAKATO WA KATIB

 Rais Jakaya Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameueleza mchakato wa kutafuta Katiba mpya nchini na changamoto zake kama barabara ndefu yenye kona.Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa mchakato huo, kimsingi, unatakiwa kuongozwa na ukweli kuwa Katiba ni kuhusu wananchi wenyewe na maisha yao na wala siyo tu mchakato huo kuongozwa na idadi ya Serikali – mbili ama tatu.Rais pia amesema kuwa ni dhahiri kuwa yapo mengi ambayo hayajakaa sawasawa katika mchakato mzima hasa kuhusu jinsi Katiba mpya itakavyolinda maisha ya wananchi na kusaidia kuboresha ustawi wao.Rais Kikwete ameyasema hayo usiku wa  Jumamosi, Agosti 2, 2014, kwenye Hoteli ya Marriot Washington, mjini Washington wakati alipokutana, akazungumza na kujadili na  Watanzania wanaoishi katika Marekani hasa kutoka maeneo ya jiji la Washington D.C., na majimbo ya Virginia, Maryland, California na New York.Akiwaeleza Watanzania kuhusu hali ilivyo nchini – kisiasa na kichumi – Rais Kikwete amesema kuwa ni kweli kuwa mchakato wa kutafuta Katiba mpya umekuwa unakabiliwa na changamoto kadhaa katika siku za karibuni.
Rais Kikwete amewaambia Watanzania hao: “Najua kuwa mchakato wa Katiba umekuwa na changamoto katika siku za karibuni lakini kwangu mimi mchakato huo ni sawa na barabara ndefu ambayo haikosi kona. Kona zitakuwepo lakini mimi ni mtu ambaye anaishi kwa matumaini na ni matumaini yangu kuwa mchakato huo utaendelea na hatimaye kufikia mwisho vizuri kama tunavyotarajia wote.”
Rais Kikwete ameongeza: “Aidha, naamini kuwa yapo mengi kuhusu Katiba ambayo hayajapata muda wa kutosha wa kuyajadili katika Bunge la Katiba. Kimsingi, Katiba ni Katiba ya wananchi, ni Katiba kuhusu maisha yao na ustawi wao. Hili jambo sijaona kama linaonekana sana katika mjadala wa Katiba.”
Ameongeza: “Mchakato wetu kwa muda mrefu umekuwa kuhusu idadi ya Serikali, ziwe mbili ama ziwe tatu. Kwangu mimi, idadi ya Serikali ni muhimu, lakini naamini kuwa Katiba iwe ni kuhusu maisha yenyewe ya wananchi na ustawi wao lakini mwelekeo mzima wa Mchakato huo usiwe kuhusu idadi ya Serikali tu.”
Rais Kikwete amesema kuwa anajua kuwa yamekuwepo maneno mengi kuhusu Katiba lakini akaongeza kuwa anaamini majawabu ya changamoto na matatizo ya sasa ya mchakato huo yatapatikana.
“Najua kuwa maneno yamekuwa mengi lakini siyo ndiyo demokrasia ya wazi inavyofanya kazi lakini sisi katika Serikali hatuna wasiwasi na hali hiyo. Ndiyo mambo yanavyotakiwa kuwa katika nchi ambako demokrasia inafanya kazi. Yale mambo yanayotusumbua kwa sasa yanazungumzwa na vyama vyetu na naamini majawabu yatapatikana.”
Wakati huo huo, Rais Kikwete amerudia kusema kuwa Serikali inaandaa utaratibu wa kisheria ambao utalinda mapato yatakayotokana na mauzo ya rasilimali ya gesi nchini kwa kizazi cha sasa cha Watanzania na vizazi vijavyo.
“Tutahakikisha kuwa tunaanzisha Mfuko Maalum kulinda fedha zitakazotokana na mauzo ya gesi. Raslimali hii pamoja na fedha ambazo zinatokana na rasilimali hiyo siyo mali ya kizazi chetu tu bali ni mali ya vizazi vijavyo vya Watanzania”.
Mwisho!
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
04 Agosti,2014