TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, September 17, 2014

Rais awasili Marekani kuhudhuria mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York. Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.
Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 15, 2014. Kushoto ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali
Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 15, 2014. Kulia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali
Rais Kikwete akisindikizwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakati alipokuwa anaondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuelekea Marekani Septemba 15, 2014. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili New York, Marekani. Kulia Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akifuatiwa na Mama  Upendo Manongi Septemba 16, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Tanzania  baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014.  PICHA NA IKULU

Tuesday, September 16, 2014

TISHIO LA EBOLA LAIKUMBA TANZANIA, NI NCHI 15 YENYE HATARI YA KUKUMBWA KUTOKANA NA MAELEZO YA WANASAYANSI.


Hata hivyo, kwa mujibu wa gazeti la Citizen toleo la jana, mamlaka zilizoko chini ya Wizara ya Afya zimeendelea kukabiliana na hofu ya kuibuka kwa ugonjwa huo hatari uliozikumba nchi nyingi za Afrika Magharibi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000.

Dar es Salaam. Tanzania ni miongoni mwa nchi 15 zilizoko katika hatari ya kupata mlipuko wa ugonjwa wa ebola kwa mujibu wa maelezo ya wanasayansi.
Wanasayansi hao wa Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza pia wameainisha kuwa zaidi ya watu milioni 22 barani Afrika wako katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo.

Hadhari hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Serikali ikiwahakikishia wananchi wake kwamba iko katika jitihada ya kuandaa mazingira ya kukabiliana na ugonjwa huo endapo utaingia nchini.

Wakati wanasayansi hao wakisema hayo, wiki iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alikagua maandalizi ya kituo cha kupokea wagonjwa wa ebola eneo la Temeke na mitambo iliyowekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) endapo watapatikana wasafiri wenye dalili za maradhi hayo.

Vilevile kuona jinsi wahusika walivyopewa mafunzo maalumu ya kuwahudumia wagonjwa hao.

Tayari mitambo hiyo imeshafungwa katika Viwanja vikubwa vya ndege vya Kilimanjaro (KIA), JNIA, Uwanja wa Ndege wa Zanzibar na Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Hata hivyo, kwa mujibu wa gazeti la Citizen toleo la jana, mamlaka zilizoko chini ya Wizara ya Afya zimeendelea kukabiliana na hofu ya kuibuka kwa ugonjwa huo hatari uliozikumba nchi nyingi za Afrika Magharibi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000.

Iwapo kutakuwa na taarifa zozote za kuibuka kwa ugonjwa huo, tayari kambi maalumu za kuwatambua wagonjwa wa ebola zimeshaanzishwa katika Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi cha Muhimbili ambako watafanyiwa uchunguzi na watakaobainika watapelekwa katika kituo maalumu cha kuwahifadhi kilichoko katika Hospitali ya Temeke.

Kengele ya hatari
Ugunduzi mpya uliofanywa katika eneo ambalo ebola imeonyesha athari kubwa Afrika Magharibi umezidi kutoa ishara ya hatari kwa Tanzania na nchi nyingine za Afrika ambazo mlipuko haukuwahi kuripotiwa.

Serikali za nchi hizo zimehadharushwa kuwa zinatakiwa zijipange kwa kujua njia na namna ya kukabiliana na tishio hilo badala ya kuelekeza nguvu katika kuwabaini waathiriwa kupitia viwanja vya ndege na bandari pekee.MWANANCHI

URAIS 2015 SINA MPANGO ASEMA WAZIRI NKAMIA

GEDSC DIGITAL CAMERANaibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ambaye pia ni   Mbunge wa Kondoa Kusini ,akiongea na waandishi wa habari leo  jijini Arusha katika studio za redio 5 zenye makao yake makuu njiro ambapo alisema kuwa hana mpango wowote wa kugombea nafasi ya Urais 2015
GEDSC DIGITAL CAMERABaadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa wanafanya mahojiano na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia leo jijini Arusha katika studio za redio 5 
GEDSC DIGITAL CAMERAMkurugenzi wa Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis akiwa anamsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia wakati akizungumza na waandishi wa habari kulia ni mwandishi wa chanel Ten Jamilah Omary 
GEDSC DIGITAL CAMERAMtangazaji wa redio 5 Mwangaza Jumanne akifanya mahojiano live na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia
GEDSC DIGITAL CAMERA 
Kulia Mwanaisha Suleiman akiwa anafanya yake ndani ya studio za redio 5 mara Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia alipofanya ziara kituoni hapo
GEDSC DIGITAL CAMERAMuonekano wa studio ya Redio 5 wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia akifanyiwa mahojiano hewani na mtangazaji wa kituo hicho Mwangaza Jumanne
GEDSC DIGITAL CAMERAMeneja masoko wa Tan Communication media Bi.Sarah Keiya akiwa anasalimiana na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia 
GEDSC DIGITAL CAMERAMkurugenzi  wa Radio 5  Bw Robert Francis akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ofisini kwake mda mfupi kabla ya kuingia studio za redio hiyo
GEDSC DIGITAL CAMERA
Waandishi wa habari pamoja na mkurugenzi wa kituo cha redio 5 Bw.Robert Francis  katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia,kulia ni mmiliki wa mtandao wa Jamiiblog Pamela Mollel
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ambaye pia ni , Mbunge wa Kondoa Kusini amesema kuwa hana mpango wowote wa kugombea nafasi ya urais 2015 kama viongozi wengine wanavyotangaza nia huku akidai kuwa kazi yake kubwa nikuhakikisha wananchi katika jimbo lake wanapata maendeleo kupitia nafasi yake ya  ubunge
Waziri Nkamia aliyasema hayo leo mara baada ya kufanya ziara fupi katika kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha,ambapo alisema kuwa bado hajawa na ndoto ya kuwa Rais 2015
Alisema kuwa kiongozi anayestahili kuwa rais ni lazima awe na uwezo wa kuongoza na anayekubalika na watanzania na vigezo isiwe umri wa mtu
”Pamoja na umri nilionao 42 sina mpango wowote wa kugombea nafasi ya Urais 2015 na umri usiwe kigezo cha kugombea uwezo wa kiongozi ni muhimu sana”alisema Nkamia
Pia Waziri huyo aliipongeza kituo hicho cha redio kwa kazi nzuri ya kuburudisha na kuelimisha jamii kupitianvipindi vyake mbalimbali huku akiwataka kuandaa vipindi ambavyo vitawashirikisha wachezaji wazamani hali itakayosaidia kukuza na kuibua changamoto katika michezo

Monday, September 15, 2014

JESHI LA POLISI LAAPA KULA SAHANI MOJA NA MBOWE,HAKUNA MAANDAMANO WALA MIGOMO

Na Karoli Vinsent
 
         SIKU  moja kupita baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe,kutangaza mgomo na Maandamano nchi nzima kwa ajili ya kushinikiza Bunge la Katiba lisitishwe mara moja kwa madai Bunge hilo limeshindwa kutengeneza katiba ya Nchi, badala yake linatunga Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM, Naye Mkuu wa jeshi la polisi Nchini IGP Ernest Mangu ameibuka na Kumvaa Mwenyekiti huyo wa Chadema Freeman Mbowe na kusema Jeshi hilo halitakubali kuona  amani ya nchi inavurugwa.
          
           Kwani  Maandamano hayo pamoja na Migomo ni kinyume Cha sheria na kanuni zinazosimamia  Jamii kutii sheria na utaratibu wake.
             Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam Kamishina wa polisi Oparesheni na Mafunzo Paul Chagonja -CP kwa Niaba ya Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Ernest Mangu wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari kuzungumzia kauli aliyoitoa Kiongozi huyo wa Chadema,ambapo Chagonja alisema Jeshi hilo halitakubali kushuhudia Migomo na Maandamo yenye kulenga kuvuruga Amani 
         “Jeshi la polisi tumepokea kwa masikitiko makubwa kauli aliyoitoa Freeman Mbowe kwamba yeye pamoja na wafuasi wake wa chama chake wanajipanga kufanya maandamano na migomo isiyokomo nchi nzima bila kufuata sheria,kanuni na taratibu za nchi ili kushinikiza Bunge la katiba kuhailishwa ,sisi jeshi la polisi tunaonya vikali kauli hiyo ambayo ni kinyume cha taratibu  za nchi na hatutakubali”alisema CP-Chagonja
   
          Chagonja alizidi kusema ieleweke wazi kwamba siasa zina mipaka  na zinapovuka mipaka hiyo na kuanza kwenda kinyume cha sheria,kanuni na taratibu za nchi  hiyo inageuka kuwa jinai na wala siyo siasa tena.
       Aidha Chagonja alisema Jeshi hilo la polisi aliweza kumvumilia mtu yeyote atakayetumia mwavuri wa siasa kutaka kuvuruga Amani na utulivu uliopo hapa nchini na Jeshi halitasita kumchukulia hatua kali kama mhalifu Mwengine yeyote.
                  Katika hatua nyingine Jeshi limewataka Wananchi wote kufuata sheria na taratibu za nchi na kuepuka kauli zenye kulenga kuvuruga Amani ya nchi.
           Kauli hiyo ya Jeshi la Polisi nchini limekuja siku moja baada ya Mwenyekiti waChama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe kutangaza kuwepo kwa maandamano bila kikomo nchi nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge la Katiba aliloliita la kifisadi linaloendelea mjini Dodoma.
        Pia, Chama chake kimeazimia kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais ifikapo mwakani, lengo likiwa kuung’oa utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), uliowafanya watanzania kuwa maskini wa kutupwa.
          Akihutubia mkutano mkuu wa uchaguzi, Mwenyekiti huyo wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, alisema umefika wakati sasa wa kuacha kukaa na kuzungumza na kwani kinachoendelea Dodoma ni wizi na ukatili wa hali ya juu kwa wananchi wanyonge ambao ndio walipa kodi.
         “Samahani maneno yangu ni makali na wala hapa sifanyi uchochezi…kinachoendelea Dodoma ni ufisadi na wizi, tumekaa Kinana, tumekaa na Mangula, tumekaa na Rais Kikwete tumekubaliana bunge lisitishwe lakini wanamwacha Sita afanye anachotaka kama utafikiri ndiye Rais…
          “Anachakachua rasimu, anabadili kanuni, anavunja sheria anakusanya maoni utafikiri yeye ni Warioba…hiki hakivumiliki, naomba mkutano huu utoke na tamko,” alisema Mbowe na kushangiliwa na wajumbe wakiafiki.
            Mbowe akipendekeza maadhimio, alisema kinachotakiwa ni kuungana na kufanya maamuzi ya kuandamana nchi nzima kushinikiza kusimamishwa kwa Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma ambalo linafuja fedha za wanyonge ili hali katiba haitapatikanani

KINANA AZINDUA MRADI WA MAJI MUYUYU NA KIKUNDI CHA UTENGENEZAJI BATIKI KIBITI RUFIJI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji mama mmoja  wa Kijiji cha Muyuyu, katika Jimbo la Kibiti, alipozindua mradi wa maji katika Kijiji cha Muyuyu, wakati wa ziara yake  ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya  maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Pwani.
 Katibu wa Ityikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika Kijiji cha Mchukwi ambapo Kinana alikwenda kuzindua kikundi cha Akina mama cha kutengeneza batiki.
Kinana akisaidia kutengeza batiki katika kijiji cha Mchukwi

NBC YAKUTANA NA WADAU WA PPF JIJINI ARUSHA

Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto) akizungumza huku Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa NBC, Mongateko Makongoro akimsikiliza katika Mkutano wa 24 wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa PPF uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha.
Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa NBC, Mongateko Makongoro akizungumza katika Mkutano huo.
Kaimu Mhazini Mkuu wa Benki ya NBC Tanzania, Ivan Tarimo, (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa tafrija ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wajumbe wa mkutano wa 24 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF jijini Arusha hivi karibuni. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Ramadhan Khija, na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (watatu kulia), akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Benki ya NBC Limited, kwa wajumbe wa mkutano wa 24 wa wanachama na wadau wa PPF jijini Arusha. Wengine pichani kutoka kushoto ni Kaimu Mhazini Mhuu Benki ya NBC, Ivan Tarimo, Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki, Mongateko Makongoro, mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Khija, na wafanyakazi wa NBC

WAJUMBE WA KAMATI UANDISHI BUNGE MAALUMU LA KATIBA WATAKA KULIPWA POSHO YA Sh500,000 KWA SIKU HUKO DODOMA.


“Unajua kuna ‘presha’ kubwa kwamba Rasimu ya Katiba inayopendekezwa iwe imetoka Septemba 21, sasa hiyo inaifanya kamati hiyo kufanya kazi hadi usiku,”.PICHA/MAKTABA.

Dodoma. Mzimu wa posho umeibuka upya katika Bunge la Katiba, safari hii wajumbe wake wa Kamati ya Uandishi wakiomba walipwe posho maalumu ya Sh500,000 kwa siku kutokana na kazi ya kuandika Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.
Habari zilizolifikia Mwananchi na kuthibitishwa na uongozi wa Bunge zinasema kuwa tayari maoni ya wajumbe yamewasilishwa kwa uongozi kwa ajili ya uamuzi.

Wajumbe wa kamati hiyo kwa sasa wanalipwa posho maalumu ya Sh210,000 zaidi kwa siku, nje ya ile ya Sh300,000 kwa siku wanayolipwa wajumbe wote wa Bunge hilo.

Kamati hiyo inayoongozwa na Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi-CCM inahusisha baadhi ya vigogo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Vigogo hao ni pamoja Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Asha-Rose Migiro, Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema, Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Othman Masoud Othman aliyejiuzulu ujumbe wa kamati hiyo hivi karibuni kwa sababu ambazo hazijaelezwa.

Katibu wa Bunge, Yahaya Khamis Hamad pamoja na kukiri kuwa kamati hiyo imeomba kuongezwa kiasi hicho cha posho, alisema Kamati ya Uongozi ambayo ndiyo huamua, haijayajadili maombi hayo na kuyatolea uamuzi.
Chenge hakupatikana jana kuzungumzia maombi hayo.

Gharama kuongezeka
Endapo Kamati ya Uongozi inayoongozwa na Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta itaridhia maombi hayo kwa wajumbe 24 wa kamati hiyo, Bunge hilo litatumia Sh12 milioni kwa siku.

Vyanzo vya habari vimedokeza kuwa iwapo nyongeza hiyo itaanza kulipwa, wajumbe wa kamati hiyo watakuwa wakizoa jumla ya Sh800,000 kwa siku.

“Msingi wa kuomba posho hiyo ya Sh500,000 kwa siku unatokana na wajumbe wa kamati kufanya kazi hadi usiku wa manane,” alidokeza mmoja wa wajumbe wa Bunge.

“Unajua kuna ‘presha’ kubwa kwamba Rasimu ya Katiba inayopendekezwa iwe imetoka Septemba 21, sasa hiyo inaifanya kamati hiyo kufanya kazi hadi usiku,” alifafanua mjumbe huyo.

Kwa sasa kamati hiyo imekuwa ikifanya kazi ya ziada kuingiza michango ya wajumbe wa Bunge hilo inayotokana na majadiliano baada ya kamati kumaliza kuwasilisha taarifa zake Septemba 8, mwaka huu.

Kamati hiyo inatarajiwa kuendelea na mchakamchaka huo hadi hatua ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa itakapopigiwa kura na wajumbe wa Bunge hilo kuanzia Septemba 26, mwaka huu.

Katibu aitetea
Katibu wa Bunge, Hamad aliitetea kamati hiyo akitaka Watanzania kufahamu kuwa wajumbe wake wamekuwa wakifanya kazi kubwa na wamekuwa wakitoka katika vikao saa 8.00 usiku.

“Hata jana (Jumamosi) mimi nilitoka pale saa 5.00 usiku niliwaacha ndiyo wanaletewa chakula cha usiku,” alisema Hamad.

Alisema hata baada ya wajumbe kukamilisha kazi yao, watendaji wamekuwa wakikesha ili kukamilisha kazi walizopewa na kamati hiyo.

Wakati Bunge hilo lilipoanza vikao Februari mwaka huu, baadhi ya wajumbe walitaka posho ya Sh300,000 wanayolipwa iongezwe wakisema ilikuwa haitoshelezi kuishi mjini hapa na kudai ifikie Sh500,000.MWANANCHI

ASKARI WA USALAMA BARABARANI AGONGWA NA DCM MBAGALA

Askari wa usalama barabarani, aliyejulikana kwa jina la Riziki, WP 2806 Cpl Riziki, akiwa hoi baada ya kugongwa na daladala aina ya DCM wakati akiwa katika harakati za kutimiza majukumu ya kazi eneo la Mbagala Rangi Tatu, leo asubuhi.

Habari zinasema kuwa baada ya ajali hiyo, askari huyo alikimbizwa katika hospitali ya Temeke na baadaye kuhamishiwa hospitali ya Muhimbili na hali yake inaendelea vizur

BAADA YA CHADEMA KUFANYA UCHAGUZI HATIMAYE -MRITHI WA ZITTO KABWE APATIKANA CHADEMA

DK SLAA,SALUM MWALIM PAMOJA NA JOHN MNYIKA Uchaguzi ndani ya chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA leo usiku huu umefikia tamati kwa kamati kuu ya chama hicho kupata viongozi wake wamwisho ambao ni KATIBU MKUU ,NAIBU KATIBU MKUU BARA pamoja na NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR
MATOKEO----

KATIBU MKUU --DK WILLBROD SLAA--
NAIBU KATIBU MKUU BARA---JOHN MNYIKA
NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR--SALUM MWALIM
viongozi awa waliteuliwa na mwenyekiti wa chama hicho kama katiba inavyosema na hatimaye baraza kuu likawapitisha wote bila kuwapinga
mh JOHN MNYIKA anateuliwa kushika nafasi ambayo ilikuwa inashikiliwa na mbunge wa jimbo la kigoma kaskazini mh ZITTO KABWE ambaye aliondolewa katika nafasi hiyo na kamati kuu ya chama kwa kile ambacho kilisemekana kuvunja katiba ya chama hicho
FAIDI PICHA ZA USHINDI HAPO CHINI

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WA SHIRIKA LA HEIFER INTERNATIONAL STEVE DENNE NCHINI

DSCN1621
Mfugaji wa Heifer International Tanzania Abel Mwakatumbula na mkewe wakiwa na Makamu wa Rais wa shirika hilo.
DSCN1660
Makamu wa Rais wa Heifer International Steve Denne, Mkurugenzi wa Heifer International Tanzania Dk. Henry Njakoi wakifurahia mafanikio ya miradi ya Heifer International.
DSCN1799
Makamu wa Rais wa Heifer International akigawa mtamba kwa mwana kikundi cha Faraja Wilayani Rungwe.
DSCN1908
Steve Denne akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Abbas Kandoro alipotembelea ofisi za Mkoa.

Steve Denne alitembelea Tanzania kwa mara kwanza wiki iliyopita kuona miradi inayoendeshwa na shirika hilo. Katika ziara hiyo, Steve Denne alitembelea ofisi za mkoa wa Mbeya akifuatana na Mkurugenzi wa Heifer International Tanzania Dk Henry Njakoi, Meneja Mradi wa EADD Tanzania Bwana Mark Tsoxo, ambapo walikutana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro. 

Katika Mazungumzo yake na Mheshimiwa Abbas Kandoro, Bw Denne aliishukuru sana serekali ya Tanzania kwa mahusiano mazuri na ushirikiano mkubwa kwenye kutekeleza miradi ya shirika hilo nchini na hasa katika kuanzisha Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD). 

Aliahidi kuwa shirika hilo kupitia mradi wa EADD na miradi mingine tarajiwa, litaendelea kuleta mabadiliko kwa kuwasaidia wafugaji wadogo kwenye mikoa wa Mbeya, Iringa na Njombe ili kuinua uchumi wao na kuwa na ufugaji wenye tija na endelevu.

Pamoja na miradi aliyoitembelea Steve Denne, mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD) unaoanza Mkoani Mbeya wilaya ya Rungwe kijiji cha Kyimo ambapo aligawa mtamba kwa mfugaji wa kikundi cha Faraja kama dira ya shirika hilo ya “Toa Zawadi Pia” – Pass On The Gift.
Akiwa nchini, Makamu wa Rais wa shirika la Heifer International alikutana na wadau mbalimbali wa sekta ya maziwa nchini wakiwemo wasindikaji, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar ambapo alikutana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr. Kassim Gharib Juma.
DSCN1909
Makamu wa Rais wa Shirika la Heifer International Steve Denne, Meneja Mradi wa EADD Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika picha ya pamoja.
DSCN2098
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana akiwakaribisha ofisini kwake, Makamu wa Rais wa Shirika la Heifer International Steve Denne na Mkurugenzi wa Shirika hilo Tanzania Dk. Henry Njakoi.
DSCN2100
Steve Denne alipomtembelea Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana.
DSCN2111
Steve Denne katika mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana.
DSCN2320
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar Dk. Kassim Gharib Juma (kushoto) akibadilishana mawazo na Makamu wa Rais wa Shirika la Heifer International Steve Denne na Dk. Henry Njakoi, Mkurugenzi wa Shirika hilo nchini.