TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, November 20, 2014

JESHI LA MAGEREZA LAPATA MAFANIKIO MAKUBWA UZALISHAJI WA MIFUGO KATIKA MASHAMBA HAPA NCHINI

 Sehemu ya Wanyama kazi katika Shamba Kubwa la Uzalishaji wa ngo'mbe wa nyama katika Gereza Ubena lililopo Mkoani Pwani. Shamba hilo lina takribani jumla ya ngo'mbe zaidi ya 1500. Uzalishaji wa ngo'mbe umekuwa ukiongezeka kwa mafanikio makubwa kila Mwaka hivi karibuni kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Uongozi wa Jeshi la Magereza katika kuyahudumia mashamba hayo Nchini.
 Lango Kuu la kuingilia Gereza la Mifugo Ubena lililopo Mkoani Pwani ambalo linashughulika zaidi  na Uzalishaji wa Mifugo. Wafungwa katika Gereza hilo wanapata elimu ya Ufugaji bora unaozingatia Kanuni za Ufugaji wa Kisasa ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa jukumu la Urekebishaji kwa Wafungwa.

 Kundi la ndama wakiwa zizini katika Shamba la Uzalishaji wa Mifugo Gereza la Mifugo Ubena, Mkoani Pwani.
Kundi la ngo'mbe wa maziwa katika Shamba la Mifugo la Mtego wa Simba lililopo Mkoani Morogoro. Shamba hili la Mifugo ni Maalum kwa Uzalishaji wa Ngo'mbe wa maziwa kama inavyoonekana katika picha na Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1944.
 Maziwa yakiwa tayari yamekamliwa na kuhifadhiwa kwenye majokovu kabla ya kwenda kwa walaji. Shamba hilo la Uzalishaji ngo'mbe wa maziwa la Gereza Mtego wa Simba limekuwa likipigiwa mfano hapa nchini(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
 

Wednesday, November 19, 2014

Doha kuandaa mashindano ya riadha 2019

Riadha Doha
Mji mkuu wa Qatar Doha, utakuwa mwenyeji wa mashindano ya dunia ya riadha mwaka 2019 baada ya kuzipiku Barcelona na mji wa Eugene nchini Marekani zilizotaka kuandaa mashindano hayo.
Imependekezwa kuwa mashindano hayo yafanyike kati ya tahere 28 Septemba hadi tarehe sita Oktoba mwaka huo ili kuondokana na msimu wa jua kali.
Maafisa wakuu nchini Qatar, wanadai kuwa nyuzi joto zitakuwa zimeshuka ikilinganishwa na mwezi Mei ambapo Doha itaandaa mashindano ya Diamond League.
Doha ilitaka kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya mwaka 2017 lakini London ikaipiku.
Mji huo pia unajiandaa kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022.
Mashindano ya riadha ya mwaka 2015, yatafanyika mjini Beijing kuanzia tarehe 22-30 Agosti wakati mashindano ya mwaka 2017 yatafanyika mwezi Agosti.
"tumekuwa na ndoto ya kuandaa mashindano haya kwa muda mrefu , '' alisema afisa mkuu wa Doha, Dahlan al Hamad.
Uwanja wa kimataifa wa Khalifa ambao utakuwa kitovu cha dimba la dunia mwaka 2022, ndiko mashindano hayo yatafanyika.

MISS TANZANIA IN LONDON FOR MISS WORLD

By  Ayoub  Mzee-London
Today    Miss Tanzania Happiness  Watimanywa  ,paid  a  courtesy  call to  the  Tanzania High  Commission  in  London. She was welcomed by the High Commissioner H.E Peter Kallaghe. During  their  meeting  Miss Happiness  was  able  to  update  the  high  commissioner  about  her   mission  to  represent  Tanzania  as  a  country  at  the  famous 64th  edition of Miss  world  beauty pageant  that  will  take  place  early  December. In  return  the  High  commissioner  promised  her  the  support   and  backing  of  the  Tanzania  mission  in  London  and  wished  her  all  the  best. There after a national flag was presented to her.
Tanzania may not win the Miss World crown this  year or ever or even surpass this year’s record in many years to come but we must learn to celebrate what we have achieved now as we prepare and plan for the future. Tanzanians must not wait for Tanzania to win the Miss World before celebrating, let’s celebrate now and leave the future to take care of itself.Lets  all  support Happiness Watimanywa
NOTES:
THE THEME AND ROLE OF MISS TANZANIA
THE THEME OF MISS TANZANIA BEAUTY PAGEANT IS BEAUTY WITH A PURPOSE. THIS THEME CLEARLY SPELLS OUT THE ULTIMATE GOAL OF THE PAGEANT. THE GOAL IS NOT PICK THE MOST BEAUTIFUL GIRL AS A WINNER JUST FOR THE SAKE OF IT BUT TO USE HER BEAUTY TO FURTHER MEANINGFUL COURSES.
 
ONCE MISS TANZANIA HAS BEEN SELECTED, SHE ASSUMES THE ROLE OF A GOODWILL AMBASSADOR. IT IS COMMON FOR FAMOUS PERSONS THE WORLD ALL OVER TO ACT AS GOODWILL AMBASSADOR S ON BEHALF OF VARIOUS ORGANIZATIONS IN FURTHERING THEIR COURSES. TO BE GOODWILL AMBASSADOR, ONE NEEDS TO COMMAND THE ADMIRATION OF EITHER LOCALLY OR INTERNATIONALLY.
Since the Beauty with a Purpose ethos was incorporated into Miss World, millions of pounds have been raised and countless hours of hard work have been carried out across the globe. As well as the official Beauty With A Purpose Charity, many other outlets of these selfless activities have been utilized through the years.
 
From the ground up thousands of contestants right from the regional heats to the global final have found countless ways to make a difference and bring about positive change to communities in need.
  
Below are the latest examples of Beauty with a Purpose in action. For more details visitwww.beautywithapurpose.com

KATAVI IMEFANIKIWA KUJENGA VYUMBA 17 VYA MAABARA KWA SHULE ZAKE SITA ZA SEKONDARI

Na Kibada Kibada –Mpanda Katavi
Katika kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Prof,Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu ujenzi wa vyumba vya Maabara kwa Shule za Sekondari nchini Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imefanikiwa kujenga vyumba 17 vya maabara kwa shule zake sita za Sekondari kwa gharama ya shilingi 568.6 milioni.
Akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa  ujenzi wa maabara kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima aliyekuwa Mwenyekiti wa  Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha wilaya , Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Estomihn Chang’ah   katika taarifa yake ilieleza kuwa ujenzi umekamilika kwa asilimia 90 na kazi zilizobakia ni kuweka miundo mbinu ya vifaa vya maabara tu, kazi ambayo inatarajia kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Novemba 2014, na kazi zinaendelea za ukamilishaji.
Chang’ah alieleza kuwa ujenzi wa Maabara hizo ulianza mwezi Januari 14 mwaka 2014  na ulitarajia kukamilika ifikapo Novemba 28 mwaka huu,ambapo kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huu ilikwa kiasi cha shilingi 686.3 milioni hadi  kutolewa kwa taarifa hiyo  kiasi cha shilingi 568.6 milioni zimetumika kwa ajili ya  ujenzi huo  ambao umekamilika sawa na asilimia 90.
Akifafanua zaidi alieleza kuwa baadaya kupewa maagizo ya ujenzi wa maabara kwa shule za Sekondari kama menejimenti walikaa na kujadili namna ya ukamilishaji wa ujenzi huu, ambapo walitenga kiasi cha shilingi milioni 686,310,179 kwa ajili ya kujenga vyumba 17,ambapo hadi kufikia walipofikia wametumia kiasi cha shilingi milioni 568,633,685 ndizo zimetumika.
Mkurugenzi huyo akaeleza kuwa  baada ya kukaa na kujadiliana na menejimenti walichakata na kuona namna ya kufanya ambapo waliomba kuhamisha fedha kutoka kwenye baadhi ya miradi ili kuipeleka kwenye Maabara ambapo Menejimenti ilipitisha fedha na kupeleka kwenye Kamati ya Fedha na Mipango ili kuweza kupewa ridhaa na Baraka.
  Kamati ya fedha ilipitisha na kupeleka kwenye Baraza la Madiwani na Madiwani wakatoa Baraka fedha hizo kutumika kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Maabara hivyo matumizi ya fedha hizo zilipata baraza za baraza la madiwani ambapo aliwashukuru madiwanikwa moyo wao wa uzalendo kuruhusu kutumiwa kwa fedha hizo vinginevyo wangekataa kupitia au kuridhia fedha hizo hali ingekuwa tete kupata  fedha za kujengea  hawajui ingetoka  wapi.
Mkurugenzi aliendalea kueleza kuwa  walipoanza ujenzi walitumia Wakandarasi ili waweze kujenga maabara,hivyo Halmashauri iliingia Mkataba naWakandarasi ili  kujenga Maabara lakini mwenendo wa Wakandarasi ulikuwa wa kusuasua,hivyo ikabidi Halmashauri ikaamua kuvunja Mkataba na kuwatumia Mafundi wa kienyeji ambao walisimamiwa na watalaam wa Halmashauri kupitia kitengo cha ujenzi.
 Kwa uwatumia Mafundi hao wa Kienyeji  ujenzi ulienda kwa kasi hadi hapo walipofikia,ambapo mafundi wa kienyeji wameonesha kuwa wakitumiwa vizuri wana uwezo mzuri  jambo la msingi ni usimamizi wa karibu na ufuatiliaji kisha kuelekezwa wama fanya Vizuri tofauti na wakandarasi ambao wanachelewesja kazi, na kama “tuendelea kuwategemea wakandarasi Maabara tusingefikia hapa tulipofikia’Alisema Mkurugenzi..
Aidha Mkurugenzi huyo alizitaja shule za Sekondari zilizojengwa Maabara kuwa ni Mwese,Karema,Ikola, Mpandandogo,Ilandamilumba na Kabungu ambazo zote zimejengwa vyumba vya maabara ya sayans na shule za Kata za Wananchii.
Pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba hivyo vya Maabara zipo changamoto kadhaa zilizojitokeza katika utekelezaji wa ujenzi huo ,baadhi ya changamoto hizo ni kukosekana kwa nguvu za wananchi katika kuchangia miradi hiyo ambapo katika maeneo mengi suala la kuchangia nguvu za wananchi  limekuwa ni changamoto kubwa.
Baadhi ya miradi mingi inayotekelezwa na Halmashauri ilibidi isimame kutokana na kuhamishwa kwa fedha kupelekwa kwa ajili ya  ujenzi wa maabara.
Changamoto nyingine ni kuwa pamoja na kukamilika kwa maboma bado kuna suala la miundombinu ya ndani na vifaa vya maabara  na bajeti bado inabana ,kubwa zaidi ni namna gani ya kuweza kukamilisha vifaa vilivyobakia.
Ambapo ukiwaambia wananchi kuchangia elimu katika mkoa huu bado ina kuwa suala ngumu tofauti na maeneo mengine hasa mikoa ya Kaskazini  wananchi wanamwamko kuchangia elimu huku nitofauti ,
Hata hivyo aliomba wadau mbalimbali wajitokeze kuchangia chochote walichonacho ili kufanikisha suala hilo la ukamilishaji wa miundo mbinu ya maabar kwa kuwatumia viongozi wa ngazi mbalimbali katika mkoa wajaribu kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali kujitokeza katika uchangiaji wa wa maabara.
Naye Mkurugenzi wa Mji wa Mpanda Seleman Lukanga  hadi kufikia Novemba 16 mwaka huu jumla ya maabara kumi zimikalika na nyingiene ziko katika hatu ya ukamilishaji.
Lukanga amezitaja shule za Sekondari za Kasimba kuwa maabara tau zimejenga mbili zimekamilika na moja imekamilika nyingine mbili zinaendelea kujengwa.
Shule ya Nsemlwa mabaara tatu ambazo ziko katika hatua ya kupauwa,,Kashaulili maabara tatu zinajengwa,Mwangaza moja iko katika hatua ya kupauwa na nyingine zinaendelea vizuri,Misunkumilo Sekondarizimejengwa mbili moja iko katika hatua ya ukamilishaji,Rungwa Sekondari mbili zimekamilika moja iko katika hatua ya ukamilishaji, Shanwe moja imekamilika na nyingine iko katika ya ukamilishaji.
Hata hivyo pamoja na ukamilishaji huo kwa baadhi ya maabara zipo changamoto kadhaa ambazo zinakabili ujenzi wa maabara hizo,ni wakandarasi kutokukamilisha kazi zao kwa wakati,mwamko mdogo kwa wananchi kuhusu uchangiaji wa shughuli za maendelo.
Changamoto nyingine ni upatikaji wa fedha,michango ya wananchi imekuwa ikisuasua,pamoja na usimamizi katika maeneo mbalimbali kwenye Halmashauri uko chini.
Akashauri  ushirikishwa wa wadau mbalimbali washirikishwe has kwa viongozi kwa nafasi walizonazo hasa wakuu wa Wilaya na Mikoa kwa kupata ushirikiano wa karibu ili wananchi washawishiwe kuchangia.

UZUNDUZI NA UHAMASISHAJI WA MFUKO WA AFYA YA JAMII(CHF) WILAYANI KILINDI MKOANI TANGA

unnamedMeneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya Mkoa wa Tanga(NHIF)Ally Mwakababu kulia akimuelezea mikakati ya mfuko wa Afya
ya Jamii (CHF) Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Suleimani Liwowa kulia kwake kabla ya kufanya uzinduzi wa Uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii wilayani humo (CHF) zoezi ambalo linaendeshwa na Meneja huyo na maafisa kutokana makao makuu na mkoani Tanga kwa muda wa siku kumi.
unnamed1Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Suleimani Liwowa akizungumza na viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF) na watumishi wa Halmashauri hiyo Idara ya Afya ofisini kwake kabla ya kuanza uzinduzi wa uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF).unnamed5Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilindi,Daudi Mayeji  akizungumza na viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF) hawapo pichani waliomtembelea ofisini kwake kabla
ya kuanza uzinduzi wa uhamasishaji wilayani humo kulia kwake ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoa wa Tanga(NHIF) Ally Mwakababu kushoto ni Ofisa wa Mfuko huo kutoka makao makuu Isaya Shekifu.
unnamed6Afisa Uanachama wa Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoa wa Tanga (NHIF) Miraji Swalehe akiwaelimisha waendesha pikipiki kwenye kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani Kilindi juu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kuweza kupata matibabu muda wote.unnamed7Meneja wa Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoa wa Tanga(NHIF) Ally Mwakababu akiwahimiza wananchi wa Kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani Kilindi umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wakati wa uzinduzi wake uliofanywa na Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Suleimani Liwowa.unnamed9Mwanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) tokea ulipoanzishwa wilayani humo akimuonyesha kadi zake Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF) Ally Mwakababu.unnamed10Mkuu wa wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga,Suleimani Liwowa akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa  Tanga(NHIF)Ally Mwakababu  na maafisa wengine wa mfuko huo na
madereva wa pikipiki “Bodaboda”mara baada ya kuwakabidhi kadi zao za
uachama wa Kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
unnamed12DC Liwowa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani humo wakati akiwahamasisha kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wakati wa uzinduzi wake.unnamed13Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya 
(NHIF)kutoka Makao Makuu ,Isaya Shekifu akiwahamisha wananchi wa Kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani Kilindi mkoani Tanga juu ya umuhimu wa Kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

UGANDA WAHITAJI HATA SARE UGENINI GHANA V TOGO, TUNISIA V MISIRI PATACHIMBIKA LEO KATIKA KUELEKEA SAFARI YA MOROCCO

AFRICA: Africa Cup of Nations – Qualification 
17:00 D.R. Congo-Sierra Leone   
17:00 Ivory Coast-Cameroon   
19:00 Ethiopia-Malawi   
19:00 Ghana-Togo   
19:00 Guinea-Uganda   
19:00 Mali-Algeria   
19:00 Niger-Mozambique   
19:00 Zambia-Cape Verde   
20:00 Nigeria-South Africa   
20:00 Sudan-Congo   
21:00 Burkina Faso-Angola   
21:00 Gabon-Lesotho   
22:00 Senegal-Botswana   
22:00 Tunisia-Egypt