TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, November 20, 2015

Picha na Matukio ya Mh. Majaliwa kassim Majaliwa baada ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu .

EAGT Dodoma walitaka Tamasha la Shukrani

TAASISI ZA ELIMU ZAHIMIZWA KUWATHAMINI WAHITIMU WANAOFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YAO.

Stanslaus Mabula alitaka Tamasha la Kushukuru


Na Mwandishi Wetu
MBUNGE  wa Nyamagana Stanslaus Mabula ameiomba Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kushukuru linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwewnye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, lihamie jijini Mwanza kwa lengo la kufikisha shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama wanayafanyia kazi mapendekezo ya Mabula ili kufanikisha tamasha hilo adhimu lenye nia ya kushukuru Mungu baada ya uchaguzi Mkuu.

Friday, November 13, 2015

WANACCM WALIOCHUKUA FOMU KUWANIA USPIKA WA BUNGE

Idadi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Uspika na Unaibu Spika katika Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) linalotarajiwa kuanza wiki ijayo, inazidi kuongezeka na hapa ni majina 21 ya ambao wameshachukua fomu hizo, kadiri ya taarifa ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib.

STARS KAMILI KUWAVAA MBWEHA WA JANGWANI

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Algeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari leo, Mkwasa amesema wamejiandaa kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo, wanajua Algeria ni miongoni mwa timu bora Afrika, lakini hilo halitawazuia kuibuka na ushindi.

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO AFANYA ZIARA BASATA,TBC NA TSN.


 Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(wa kwanza kushoto) akiangalia mitambo ya kurushia matangazo ya Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) wakati alipofanya ziara ya kikazi katika minara ya shirika hilo leo hii  Kisarawe.Profesa Elisante amefanya ziara katika Taasisi tatu zilizo chini ya Wizara hiyo ambazo ni Baraza la Sanaa Tanzabia (BASATA),Tanzania Standard Newspapers(TSN) na Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) lengo likiwa ni kufahamiana na wafanyakazi,kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii na kujua changamoto zinazowakabili ikiwa ni kutimiza kauli mbiu ya HAPA KAZI TU ya awamu ya Tano.Anaefuatia ni mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw.Clement Mshana.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiangalia tofauti ya santuri ya  zamani na flashi ya kisasa  zinavyozidiana ukubwa kwa umbo alipotembelea maktaba mojawapo katika ofisi za shirika la utangazaji Tanzania (TBC) alipofanya ziara kuongea na menejimenti ya shirika ilo leo jijini Dar es Salaam.Santuri zilitumika kipinda shirika hilo likiitwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD).
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (waliosimama watatu kulia) akiwa katika mojawapo ya studio za kurushia matangazo ya shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wwakati alipotembelea shirika ilo leo kuongea na menejimenti yake pamoja na kuona utendaji wake.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (aliyekaa mwenye miwani) akipata maelekezo jinsi gazeti linavyotengenezwa kutoka kwa mtumishi wa Standard News Papers(TSN) leo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi na kuangalia utendaji wa kazi.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(wa pili kulia) akiangalia moja ya kazi za vijana wanojifunza kutengeneza batiki na kuweka chapa alipotembelea ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) leo hii jijini Dar es Salaam.

Wednesday, November 11, 2015

LIGI KUU ZANZIBAR YAANZA ‘KICHAKANI’, MAFUNZO WACHEZEA KICHAPO CHA JKU

Na Salum Vuai, ZANZIBAR

KUFUATIA uwanja wa Amaan kuzuiwa kutumika kwa mechi za Ligi Kuu ya soka Zanzibar bila kuelezwa sababu za msingi, ligi hiyo iliyochelewa imelazimika kuanza jana katika uwanja wa kijiji cha Bweleo umbali wa takriban maili 15 kutoka mjini Zanzibar.
Kwa kuwa uwanja huo si rasmi na hauna uzio wala huduma muhimu ikiwemo vyoo, waandaaji wa ligi hiyo, kamati ya muda ya ZFA wamejikuta wakipata hasara kwani hakuna kiingilio cha fedha kilichowekwa kwa watazamaji.
Na katika mchezo wa ufunguzi jana, JKU makamu bingwa msimu uliopita, waliilaza Mafunzo mabao 2-1.
Kamisaa wa mchezo Ramadhani Ibada Kibo, akiwaongoza waamuzi wa mpambano huo kurudi uwanjani kuanza kipindi cha pili, baada ya kupumzika katika kichaka pembezoni mwa uwanja.  

Mafunzo ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo na wawakilishi wa Zanzibar kweli Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, wakati JKU watashiriki Kombe la Shirikisho.

TOTO AFRICANS WAAMUA ‘KUTEMBEZA BAKULI’ KWA WANACHAMA WAKE

Na Philipo Chimi, MWANZA
KLABU Toto Africans ya Mwanza imeandaa mkutano maalum kwa wanachama wake kwa ajili ya kufanya harambee kuchangia timu hiyo iweze kushiriki vyema Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
 Mwenyekiti wa klabu hiyo, Godwine Aiko amesema kwamba wameandaa mkutano huo kufuatia hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili timu.
Amesema timu inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji utatuzi wa haraka ili kunusuru mwendo wake mbovu katika Ligi Kuu.
“Tumeandaa mkutano huo ambao utafanyika siku ya Novemba 22 kwa ajili ya kufanya mipango kuona namna gani timu inapata fedha,” amesema na kuongeza. 

Ratiba ya Kombe la Challenge 2015 kama ilivyotolewa na CECAFA



MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Juma Ramadhani Mgunda ameteuliwa kuwa Msaidizi namba moja wa Alhaj Abdallah Athumani Seif 'King Kibaden' katika kikosi cha timu ya Tanzania Bara, 'Kilimanjaro Stars' kitakachoshiriki michuano ya CECAFA Chellenge baadaye mwezi huu mjini Addis Ababa, Ethiopia.

DK. KIMEI AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA SIHA SANGO

KAMERA YETU NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

VYOMBO HABARI VIMECHANGIA KUFANYA UCHAGUZI KUWA WAZI NA HAKI NA HURU –NEC

KIINGILIO CHA KUITIZAMA MECHI KATI YA STARS NA ALGERIA 5000

THANKSGIVING HOUSTON, TX PARTY - 2 More weeks

‘Marufuku kutumia ramani ya Tanzania isiyo sahihi’

Bunge jipya, mzigo zaidi

JESHI LA POLISI LAANZA KUTOA ELIMU KWA ABIRIA NA MADEREVA ILI KUKABILIANA NA AJALI KATIKA KIPINDI CHA MWISHO WA MWAKA