TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Friday, November 20, 2015
Picha na Matukio ya Mh. Majaliwa kassim Majaliwa baada ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu .
1.
Waziri Mkuu Mteule Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na moja ya watendaji wa Serikali
1.
Spika wa Bunge la Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwa kwenye picha ya pmaoja na Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu.
1.
Kabla ya uteuzi na kupigiwa kura kwa Waziri Mkuu na kuchaguliwa kwa Naibu Spika, Bunge lilianza kwa Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai kueleza utaratibu wa kumpata Kiongozi huyo Mkuu wa Serikali Bungeni.
1.
Wakati huo wabunge walikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua nani atateuliwa
1.
Punde si punde Msaidizi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (katikati) aliingia kwenye ukumbi wa Bunge akiwa na bahasha yenye jina la Waziri Mkuu Mteule huku akisindikizwa na wapambe wa Bunge.
1.
Msaidizi wa Rais akimkabidhi Spika habasha yenye jina la Waziri Mkuu Mteule.
1.
Spika akiwaonesha wabunge bahasha kutoka kwa Mhe. Rais yenye jina la Waziri Mkuu Mteule.
Baada ya kukabidhiwa bahasha, Mhe. Spika akamuita Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah wakiwa wameshafungua bahasha.
1.
Spika na Katibu wa Bunge akamuita Katibu wa Bunge ili kuifungua na kujua nini kilichomo ndani.
1.
Spika akiwasomea wabunge barua yenye jina la Waziri Mkuu Mteule.
1.
Baada ya jina kutangazwa wabunge walisimama kuashiria kuunga mkono uteuzi wa Mhe. Rais.
1.
Kisha Waziri Mkuu Mteule, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
1.
Kisha baadhi ya wabunge akiwemo mBunge wa Mwibara Kangi Lugola akapongeza uteuzi wa Waziri Mkuu.
1.
Baada ya michango ya wabunge, kazi ya kupiga kura kuthibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu ikaanza ambapo wahudumu wa Bunge walileta masanduku ya kura.
1.
Wahudumu wa Bunge wakigawa karatasi za kupigia kura za kumpitisha Waziri Mkuu Mteule.
1.
Mmoja wa wabunge akipiga kura yake kumthibitisha Waziri Mkuu Mteule.
1.
Baada ya upigaji kura kumalizika, kura zikakusanywa kwenye masanduku ya kura.
Wahudumu wa Bunge wakibeba masanduku ya kura kwenda kuhesabu kura za kumthibitisha Waziri Mkuu Mteule.
Maafisa wa Bunge (kulia) wakizipanga kura huku wawakilishi wa upande wa ndio (kutoka CCM) na hapana (kutoka Chadema na CUF) wakifuatilia kwa makini.
Baada ya kura kuhesabiwa, ujumlishaji wa kura ukafanyika
1.
Mmoja wa wabunge aliyewakilisha upande wa hapana akisaini fumo ya majibu ya upigaji kura kuashiria kukubali matokeo.
1.
Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah (kulia) akiwatangazia wawakilishi wa pande mbili matokeo ya upigaji kura.
1.
Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah akiwatangazia wabunge matokeo ya upigaji kura kumthibitisha Waziri Mkuu Mteule ambapo kura za Ndiyo zilikua 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote na kura za hapana zilikua 91 sawa na asilimia 25% ya kura zote wakati kura 2 sawa na asilimia 0.06% ya kura zote ziliharibika..
1.
Baada ya Waziri Mkuu Mteule kuthibitishwa na Bunge, wabunge wakaingia kwenye kazi ya kumchagua Naibu Spika wa Bunge ambapo wagombea Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu Mbunge wa Kuteuliwa na Rais (CCM) na Mbunge wa Kaliua Mhe. Magdalena Sakaya kutoka Chama cha Wananchi (CUF).
1.
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye (mwakilishi wa Dkt. Tulia) na mwenzake wa Chadema (waliovaa vitambulisho) wakifuatilia kwa makini kazi ya kuhesabu kura za Naibu Spika huku Msimamizi wa Uchaguzi Dkt. Thomas Kashilillah akifuatilia kazi hiyo.
1.
Baada ya kuhesabu kura, wawakilishi wa wagombea wakatia saini fomu ya matokeo na baadaye Msimamizi wa uchaguzi huo kuyatangaza matokeo kwa wabunge na Spika kumtangaza mshindi.
27
Spika Mtuele Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akila kiapo cha Unaibu Spika wa Bunge.
27
Spika Mtuele Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akila kiapo cha Unaibu Spika wa Bunge.
Spika wa Bunge akimkabidhi hati ya kiapo Naibu Spika Dkt. Tulia.
Baadhi ya wabunge wakimpongeza Naibu Spika baada ya kuapa.
Waziri Mkuu Mtuele Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na wandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Mwansasu akizungumza na wandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mtuele Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, akizungumza na mtangazaji wa Televisheni ya Azam Baruan Muhuza kwenye studio ya televisheni hiyo iliyoko kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mtuele Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa, akizungumza na mtangazaji wa Televisheni ya AzamBaruan Muhuza kwenye studio ya televisheni hiyo iliyoko kwenye ukumbi wa Bungemjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment