TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Saturday, November 21, 2015
NEC YATANGAZA VITI VYA MADIWANI WATEULE 1393
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani akizugumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya viti maalumu vya Udiwani ambavyo Madiwani wake wameteuliwa na Tume hiyo ni viti 1393, kutoka katika Vyama vya CCM,CHADEMA,NSSR-MAGEUZI pamoja na CUF.
Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam ,Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Huduma za Sheria wa NEC Emmanuel Kawishe.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani.
(Picha na Emmanuel Massaka )
TUME ya Taifa ya Uchaguzi( NEC) imesema hadi sasa viti maalumu vya Udiwani ambavyo Madiwani wake wameteuliwa na Tume hiyo ni viti 1393, kutoka katika Vyama vya CCM, CHADEMA, NSSR- MAGEUZI pamoja na CUF.
Hayo yalisemwa Jijijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka NEC Bw. Kailima Ramadhani wakati akitoa taarifa kwa Umma kuhusu uteuzi wa madiwani wanawake wa Viti Maalumu.
Aidha Bw.Ramadhani alisema kuwa idadi ya Viti maalumu Vya Udiwani ni 1,408 nakwamba kutokana na majimbo nane na kata thelathini na Nne ambapo Uchaguzi haujakamilika kwa Sababu mbalimbali, hatua hiyo itasababisha kubakia viti 15 ambavyo vitagawanywa mara baada ya Uchaguzi kukamilika ili kufikia idadi ya viti 1,408 kutoka viti 1393 vinavyo tambulika kwa sasa.
Aidha alifafanua kuwa kutokana na Viti hivyo Maalumu Vya Udiwani Vilivyoteuliwa na NEC, Chama Cha Mapinduzi CCM kimepata viti 1,022,Chama Cha Demokrasia na Mawendeleo CHADEMA 280,Chama Cha Wananchi CUF-79, ACT WAZALENDO viti 6 pamoja na NSSR MAGEUZI viti 6.
Alisema kuwa tume imeamua kutoa taarifa ya uteuzi wa viti maalumu Vya Udiwani Nchi nzima ya Madiwani waliyoteuliwa na Tume kutokana na Kanuni za Kudumu za Mikutano ya Halmashauri, Mabaraza ya Madiwani yanatakiwa kuitishwa siku thelathini tangu tarehe ya Uchaguzi ifanyike.
Katika hatua Nyingine Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi NEC alisema kuwa mwisho wa Uchaguzi katika Majimbo na Kata ambazo hazikufanya Uchaguzi ni Desemba 20 mwaka huu, ambapo katika jimbo la Uranga Mashariki pamoja na Lushoto uchaguzi utafanyika Novemba 22 mwaka huu,nakuwaomba Wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuchagua kiongozi wanaomtaka.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment