Shindano hilo la awamu ya nne linalosimamiwa na Mfuko wa Sekta binafsi (AECF) lina lengo la kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi katika kilimo cha biashara na huduma za kifedha vijijini na kuleta mabadiliko kwenye mfumo wa soko nchini.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugezi wa AECF Hugh Scott alisema mtazamo wake ni kuona ushiriki mpana wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Tanzania katika soko hilo kwa kuipa changamoto sekta binafsi.
“Natazamia kuona ushiriki mpana wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Tanzania katika shindano hili kwa kuipa changamoto sekta binafsi kuchangamkia fursa iliyotolewa na mfuko wa EACF na kuitika kwa kuwa na mawazo ya biashara yenye ubunifu ambayo yataleta manufaa kwa maisha ya watanzania waishio vijijini”, alisema Scott.
Scott aliendelea kusema shindano hilo lipo wazi kwa kampuni zinazotengeneza faida ya ndani na ya kigeni yenye lengo la kufanya kazi na kuimarisha sekta ya kilimo cha biashara pamoja na kupata ufumbuzi utakaoongeza huduma za kifedha vijijini na taarifa katika kusaidia uzalishaji katika kilimo cha biashara Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment