Na Woinde Shizza,Arusha
Bendi ya muziki wa taarabu ijulikanayo kwa jina la Jahazi modern taarab inayomilikiwa na mfalme mzee yusuphy inatarajia kutua rasmi jijini Arusha kwa ajili ya kuitambulisha album mpya inajulikana kwa jina la Mahaba niuee.
Akizungumza na waandishi wa habari muandaaji wa onyesho hilo ambaye ni mkurugenzi wa phide entertainment, Phidesia Mwakitalima alisema kuwa bendi hiii ya jahazi inatarajiwa kutua jijini Arusha na kufanya onyesho lao December 11 ambapo litafanyika ndani ya ukumbi wa Triple A com lex uliopo ndani ya jiji hili.
Alisema kuwa mpaka sasa utaratibu wote umekamilika na wanangoja tu siku ya onyesho ambapo alieleza kuwa onyesho hili litakuwa rasmi kwa ajili ya kutambulisha albamu mpya ya jahazi pamoja na kutambulisha nyimbo zilizopo katika alibamu hiyo.
Aidha alitaja baadhi ya nyimbo zilizopo katika albamu hiyo na ambazo zitatambulishwa kwa wapenzi wa jahazi modern taarabu kuwa ni pamoja na nyimbo iliyobeba albamu Mahaba niueee,alibainisha kuwa pamoja na uzinduzi huu hii pia itakuwa ni sehemu ya ziara yao kufunga mwaka Tanzania nzima kwa bendi hii ya muziki wa Taarabu.
Phidesia aliwasihi wakazi wa mji wa Arusha pamoja na vitongoji vyake wajitokeze kwa wingi kwani wasanii wote ,waimbaji wote wacheza show wote na wake wote wa mzee yusuphy watakuwepo katika onyesho hilo.
Aliwataja baadhi ya wadhamini wa onyesho hilo kuwa ni pamoja na Geo security, kwa udhamini mkubwa wa Geo Security Arusha kampuni bora ya ulinzi, security power fance na alarm ambapo alisema na katika siku hiyo ya onyesho watakuwepo pia kwa ajili ya usalama wa wapenzi wote kuhakikisha mnarudi salama majumbani salama .
No comments:
Post a Comment