TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, September 21, 2011

UBALOZI WA MAREKANI WADHAMINI WASANII WALIOSHIRIKI TAMASHA LA MTEMI MILAMBO TABORA.





Msanii wa Muziki wa Asili Ally Mango(kulia), akifafanua jambo kuhusiana na Tamasha hilo 

Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions, Amon Mkonga(Kushoto), akizungumzia Tamasha hilo.

Wasanii wa muziki wa asili walioshiriki Tamasha la tatu ta Mtemi Milambo mwaka huu lililofanyika Julai 8-10,201 katika viwanja vya Uyui sekondari Tabora na kufunguliwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mhe.Abeid Mwinyimussa wamepata udhamini wa kurekodi nyimbo za muziki wa asili za makabila ya Kisukuma na Kinyamwezi.

Wasanii waliofanya vizuri mwaka huu Ali Mango,Asha Kaombwe,Hamis Mpiga,Paulina Muhala,Paul Magadala wataungana na wasanii wengine wa miaka iliyopita na kuunda bendi ya muziki wa asili iitwayo Mwana Milambo ambayo itakuwa inapiga muziki huo katika mahoteli,maharusi na kumbi mbalimbali za burudani.

Nyimbo zitakazorekodiwa ni Kamnyagara kane, Usoga wi kuwa, Kushoke kukaya, kana nabuta, Sensema malunde, Ng,ombe yalala, Wela wa kulya, Nzagamba ya Sukuma na Miaka hamsini ya Uhuru

Lengo kuu ni kuzihifadhi nyimbo mbalimbali zilizotumiwa na wazee wetu wa kale katika vita, kilimo, harusi,na mazishi.

Nyimbo hizi nyingi huimbwa sehemu mbalimbali lakini ni muhimu kuzirekodi kwa ajiri ya faida ya vizazi vya baadae.

Nyimbo hizo zote zitarekodiwa katika studio ya Aegies chini ya muandaaji maarufu Peter John a.k.a Nice P.


Aksanteni kwa kunisikiliza.

Amon Mkoga
Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions.
www.chiefpromotions.or.tz
0755 638 004/0655 638 004
Baadhi ya Wajumbe wa Kampuni hiyo, Kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions, Amon Mkonga, Mwanamuziki wa Asili Ally Mango, na wajumbe.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakipiga Soga Muda mfupi Kabla ya Mkutano huo Kuanza

Hapa Wanahabari wakifuatlia kwa Makini Mazungumzo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions Amon Mkinga leo.

No comments:

Post a Comment