TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, September 24, 2011

Rais wa Zambia akubali kushindwa

Rais wa Zambia Rupiah Banda amekubali kushindwa kwake na kiongozi wa upinzani Michael Sata.
Bw Sata, aliyegombea urais mara nne, alitangazwa kuwa mshindi usiku baada ya kupata asilimia 43 ya kura zote.
"Watu wa Zambia wamezungumza na lazima sote tusikilize," Bw Banda aliwaambia waandishi wa habari, huku akifuta machozi baada ya kumaliza kutoa hotuba yake.
Chama chake cha Movement for Multiparty Democracy kimeongoza Zambia kwa miaka 20.
"Nikizungumza kwa nafsi yangu na chama changu, tunakubali matokeo. Sisi ni chama cha kidemokrasia na hakuna namna nyingine yeyote ile," Bw Banda alisema.
Siku ya Alhamis, kulikuwa na ghasia eneo la kaskazini lenye migodi zilizofanywa na wanaounga mkono upinzani wakiwa hawana subra na matokeo ya Jumanne.
Matokeo hayo yalitangazwa huku majimbo saba yakiwa bado kura zao kuhesabiwa, lakini maafisa wa uchaguzi wamesema Bw Banda hatoweza kumfikia Bw Sata.
Mwandishi wa BBC Louise Redvers kwenye mji mkuu, Lusaka, alisema kuhusu tangazo hilo, wasiwasi uliogubika matokeo hayo ulisababisha makelele huku wafuasi wa Patriotic Front wakishangilia ushindi wao.
Maelfu ya watu walifurika nje ya geti lenye ulinzi mkali wakipiga ngoma, wakipiga honi na kupeperusha bendera.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Rais Mstaafu wa Zambia,Mh. Ruphia Banda kwenye ofisi za Mahakama Kuu ya Zambia wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Michael Sata zilizofanyika jana mjini Lusaka Zambia.
(Picha na Amour Nassor VPO).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini,John Tendwa kwenye sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata mjini Lusaka jana
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia), Mama Asha Bilal (kulia) na Rais mstaafu wa Zambia Ruphia Banda, wakimsikiliza Rais mpya wa Zambia Michael Sata alipokuwa akijitambulisha kwa viongozi wakuu wa Nchi mbalimbali waliohudhuria kwenye sherehe ya kuapishwa kwake iliyofanyika jana katika Mahakama Kuu ya Nchi hiyo mjini Lusaka Zambia
katikati ni Mama Asha Bilal.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) na mkewe Mama Asha Bilal (wa pili kushoto), Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini John Tendwa (kushoto) na Rais wa kwanza wa Zambia,Dkt. Keneth Kaunda wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana kwenye sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata iliyofanyika jana katika Mahakama Kuu ya Nchi hiyo mjini Lusaka Zambia
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilala akisalimiana na Rais wa Malawi,Bingu wa Mutharika walipokutana kwenye Ofisi za Mahakama Kuu mjini Lusaka Zambia jana wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata

No comments:

Post a Comment