TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 26, 2014

KAULI MBIU YA SIKU YA WANAWAKE MWAKA 2014

 on FEBRUARY 26, 2014 in JAMII 

220px-Coat_of_arms_of_Tanzania.svgWizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto inawataarifu wanaanchi wote kuwa Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mwaka 2014 inasema ”Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa wa Kijinsia”. ujumbe huu unasisitiza na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia masuala ya jinsia katika kuandaa mipango, bajeti na programu za maendeleo katika jamii. Kwa mwaka 2014 maadhimisho yatafanyika katika ngazi ya mkoa. Wizara itatoa ‘Taarifa kwa Umma’ tarehe0 6/03/2014 ili kutoa ufafanuzi wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Aidha, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Sophia M. Simba (Mb) atapata fursa ya kuongea na Waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho na ujumbe wa kaulimbiu ya Siku ya Wanawake kwa mwaka 2014.
Tunawaomba Vyombo vya Habari kuendeleza ushirikiano na Serikali na wadau wengine katika kutangaza, kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu ujumbe maalum wa kaulimbiu ya Siku ya Wanawake kwa mwaka 2014 pamoja na kuratibu maadhimisho ili kufikia lengo la kuadhimisha siku hii katika nchi yetu.
Ni matumaini yangu kuwa kupitia taarifa hii jamii itahabarishwa ipasavyo na ujumbe maalum wa maadhimisho utasisitizwa kupitia mbinu na matukio mbalimbali kama yatakavyoibuliwa na kuratibiwa na wadao kataika ngazi zote.
Erasto T. Ching’oro
 Msemaji wa Wizara
Wizara ya Maendeleo ya Jmaii, Jinsia na Watoto
25/02/2014

No comments:

Post a Comment