TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 26, 2014

KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI MIKOA YA LINDI NA MTWARA

 on FEBRUARY 26, 2014 in BIASHARA 

01Mwenyekiti wa maandalizi ya Kongamano la Viongozi wa Dini mikoa ya Lindi na Mtwara MohamedSenani akiwakaribisha wajumbe katika kongamano la viongozi hao katika ukumbi wa VETA mjini Mtwara. Kongamano ambalo viongozi hao walijadiliana juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania.02Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akizungumza na viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wa kongamano la viongozi hao lililohusu rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madinikwa amani na maendeleo ya Tanzania.03Baadhi ya wajumbe wa kongamano la viongozi wa dini wakiwasili eneo la Mnazi Bay kujionea shughuli za namna visima vya gesi vinavyofanya kazi na kuzalisha gesi ambayo ni moja ya chanzo cha nishati ya umeme kwa maendeleo endelevu ya nchi yetu.04Hiki ni moja ya kisima cha gesi kilichopo Mnazi Bay eneo la nchi kavu kinachofikisha idadi ya visima vitatu ambapo kimoja kipo eneo la bahari kuu05Baadhi ya Viongozi wa Dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara wakitembelea na kujionea eneo ambapo kinajengwa kiwanda cha kuchakata gesi asili eneo la Madimba ikiwa ni moja ya ratiba yaokutembelea maeneo mbalimbali wakiwa Mtwara kwenye  kongamano lao kujadiliana na kuelimishana juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania.06Mgeni Rasmi katika kongamano la viongozi wa dini na Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Tanzania Dkt. Jacob Chimeledya akifungua kongamano ambapo viongozi hao walijadiliana na kuelimishana juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania.07Sheikh Abubakar Zuberi akitoa mada ya Mtazamo wa Kiteolojia/Kidini juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini wakati wa kongamano la viongozi hao mjini Mtwara.08Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akitoa  maelezo ya jumla ya Wizara kuhusu rasilimali zetu za gesiasilia, mafuta na madini wakati wa kongamano la viongozi hao mjini Mtwara.09Baadhi ya viongozi wa dini wakiwa katika ukumbi wa VETA Mtwara wakisikiliza mada mblimbali zilizotolewa kataka konganmano la vingozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara.10Baadhi ya viongozi wa dini wakiwa katika ukumbi wa VETA Mtwara wakisikiliza mada mblimbali zilizotolewa kataka konganmano la vingozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara.
…………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO Mtwara
RASILIMALI za gesi asilia, mafuta na madini zilizopo mikoa ya Lindi na Mtwara ni kwa neema, ukarimu, ufadhili na baraka za Mwenyezi Mungu alizoipatia Tanzania zitumike kwa manufaa ya wanachi wote.
Kauli hiyo ilitolewa na Mgeni rasmi Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikani Tanzania Dkt. Jacob Chimeledya alipokuwa akifungua kongamano la Viongozi wa Dini leo katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mjini Mtwara.
Kongamano hilo la viongozi wa dini liliongozwa na kauli mbiu iliyosema “Rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania”.
Lengo la kongamano la voingozi wa dini lilikuwa ni kupata elimu juu ya rasilimali hizo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi kwa minajili ya haki, upendo na amani kwa kuzingatia sera na taratibu za Serikali kwa maslahi ya wananchi wote.
“Pamoja na sheria na sera za rasilimali za gesi, mafuta na madini zilizopo nchini, ni lazima ziongozwe na misingi muhimu ya taifa letu” alisema Askofu Dkt.Chimeledya.
Dkt. Chimeledya aliitaja misingi hiyo kuwa ni pamoja na haki ya kila mtanzania, ukweli juu ya sera mipango na mikakati bora, mshikamano wa jamii, kujali maslahi ya wote na ushirikishwaji wa jamii zilizo katika maeneo yanayozunguka sehemu zilipo rasilimali mbalimbali nchini.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi alisema kuwa Serikali kupitia Wizara yake ipo tayari kuendelea kushirikiana na vingozi wa dini wa wanachi wote ili kuendelea kusukuma mbele maendeleo ya nchi kwa manufaa ya watu wake.
“Gesi ni ukombozi ni ukombozi na itatusogeza mbele ambapo italinufaisha taifa katika Nyanja mbalimbali, viwandani, majumbani na ndani ya nchi hata nje ya nchi” alisema Maswi
Kugunduliwa kwa gesi mikoa ya Lindi na Mtwara kumefungua milango ya kujengwa viwanda mabalimbali ambavyo vinatajiwa punguza tatizo la ajira katika mikoa hiyo na nchi nzima kwa ujumla.
Miongoni mwa viwanda vya saruji vinavyoendelea kujengwa ni Dangote kilichopo Mtwara na Meis kilichopo mkoani Lindi.
Katibu Mkuu Maswi ametoa rai kwa watanzania wenye uwezo wa kuwekeza kupitia viwanda wafikirie kuwekeza juu ya viwanda vinavyozalisha bidhaa zinazotumia malighafi zinazotokana na mabaki gesi baada ya kuchakatwana ikiwemo viwanda vya mbolea, plastiki, chupa na nguo.
Viongozi hao wa dini walipata fursa ya ziara ya kutembelea mitambo ya kusafisha gesi na visima vya gesi Mnazi Bay eneo la Msimbati na eneo la juenzi wa mitambo ya kusafisha na kuchakata gesi kilichopo eneo la Madimba mkoani Mtwara.
Kongamano kwa viongozi wa dini ni la siku mbili ambapo linawashirikisha viongozi wa dini mbalimbali za kikristo na kiislam kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na viongozi  na watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na madini na mashirika yaliyo chini yake ya TANESC, TPDC NA REA.
 Kongamano hilo ni muendelezo ulitokana na kongamano kama hilo lililofanyika Januari 2014 jijini Dar es salaam ambapo wajumbe kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara waliona kuna haja wao kama wadau wa gesi, mafuta na madini wapate elimu kama hiyo kwa manufaa ya wanachi wa mikoa yao na nchi nzima.

No comments:

Post a Comment