TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 26, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

 on FEBRUARY 25, 2014 

DSC00207WATU WASIOFAHAMIKA WAFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE NA KUPORA MALI ZA ABIRIA WILAYANI MBARALI.
WATU WASIOFAHAMIKA MAJINA, MAKAZI, WALA IDADI YAO WAKIWA NA SILAHA ZA JADI MAPANGA, MARUNGU, MAWE NA FIMBO WALIWEKA MAWE MAKUBWA NA MAGOGO KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE NA KUTEKA BAADHI YA MAGARI YALIYOKUWA YAKIPITA KATIKA BARABARA HIYO. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 24.02.2014 MAJIRA YA SAA 01:30HRS USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MACHIMBO, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI. KATIKA TUKIO HILO BAADHI YA ABIRIA WALIPORWA VITU MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA PESA TASLIMU, SIMU ZA MKONONI NA MIKOBA AMBAVYO THAMANI NA IDADI YAKE BADO KUFAHAMIKA. AIDHA WATU HAO WALIWASHAMBULIA BAADHI YA ABIRIA HAO KWA KUWAPIGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO KWA KUTUMIA SILAHA WALIZOKUWANAZO PIA WALIFANYA UHARIBIFU KATIKA BAADHI YA MAGARI KWA KUVUNJA VIOO IKIWA NI PAMOJA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.867 ARX AINA YA TOYOTA NOAH LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AHMED ABDALAH @ AMAN. KATIKA TUKIO HILO MASHAKA ABDALAH @ CHOMA ALIJERUHIWA NA KULAZWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI WILAYA YA MBARALI NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI, WATU WENGINE WAWILI WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. HATA HIVYO POLISI WALIOKUWA DORIA ENEO LA IGAWA MPAKA WA MBEYA NA NJOMBE WALIFIKA MARA MOJA ENEO HILO NA KUKUTA MAGARI YAKIWEMO YANAYOSAFIRISHWA KWENDA NJE YA NCHI IT YAKIWA YAMESIMAMISHWA, WATU HAO WALIPOONA GARI LA POLISI WALIKIMBILIA VICHAKANI NA MAGARI HAYO YALIONDOKA KATIKA ENEO KUENDELEA NA SAFARI. WATU KUMI [10] WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANO KUHUSIANA NA TUKIO HILI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILO AZITOE KWA JESHI LA POLISI/MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BARTON MWAKAPINDI [30] MKAZI WA ILEMI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 2. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOENDESHWA NA JESHI LA POLISI MNAMO TAREHE 24.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:00HRS MCHANA HUKO KATIKA MTAA WA ILEMI, KATA YA ILEMI, TARAFA YA  SISIMBA JIJI NA  MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA AMEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 17 KWA KOSA LA KUNYWA POMBE KABLA YA MUDA.
WATU 17 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA KWA KOSA LA KUNYWA POMBE KABLA YA MUDA. WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 24.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:00HRS MCHANA HUKO KATIKA MTAA WA MWAFUTE – ILEMI, KATA YA ILEMI, TARAFA YA  SISIMBA JIJI NA  MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUNYWA POMBE KABLA YA MUDA ULIOWEKWA NA SERIKALI  KWANI KUFANYA HIVYO NI KINYUME CHA SHERIA NA KAMWE JESHI LA POLISI HALITASITA KUMKAMATA/KUMCHUKULIA HATUA ZA KISHERIA YEYOTE ATAKAYE KWENDA KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTUMIA MUDA HUO KATIKA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO NA KUJITAFUTIA KIPATO KWA NJIA HALALI.
Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MISAADA KWA YATIMA NA MAPACHA WANNE YAFIKA SALAMA MBEYA

Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.
 
Misaada  toka kwa  Bi Gladness Sariah wa Uingereza,  Dar es salaam kwa Norah SilverBoutique 
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwakilisha msaada toka kwa familia ya mama Masawe wa DSM kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha NURU kilichopo Uyole, mkoani Mbeya.
———————–Kituo cha Mtandao wa kijamii cha Mbeya Yetu (www.mbeyayetu.blogspot.com) kimepokea Misaada mbalimbali kutoka kwa wasamaria wema kwa ajili ya Kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Nuru kilichopo Uyole Jijini Mbeya na  Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.
Msaada wa kwanza ulipokelewa hivi karibuni wenye thamani ya shilingi Laki Moja kutoka Familia ya Masawe wa Dar es salaam kwa ajili ya kituo cha Nuru ambapo Mbeya yetu iliuwasilisha kama ulivyo.
Mbali na msaada huo pia Mtandao huu ukishirikiana na mtandao wa kijamii wenye makao yake makuu Jijini Dar es salaam wa www.issamichuzi.blogspot.com ulipokea kutoka kwa Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ambaye alitoa maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto.
Aidha katika kuonesha wengi wameguswa na tukio la Mwanamke huyo kujifungua watoto wanne  ambao wanaendelea vizuri, pia Msamaria  mwema mwingine aliyejulikana kwa jina la  Dada Norah SilverBoutique toka Dar es salaam naye  ametoa Maziwa Lactogen makopo 24 pamoja na nguo ambavyo vimewasili salama katika ofisi ya Mbeya Yetu.
 Shukrani kwa Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza na ofisi za Michuzi Media Group (MMG) kuwezesha kufika kwa mizigo hii Mbeya.
Kutokana na kupokelewa kwa mizigo hiyo ambapo kituo cha Nuru kilikabidhiwa Katoni Mbili za Sukari, Sabuni na Biskuti pia Tunatarajia kuanza  safari ya kwenda huko Chiwanda Wilaya ya Momba Kilomita zaidi ya 260 toka Mbeya mjini kufikisha misaada ya Mama wa mapacha wanne. 
Hivyo ni wito wetu kwenu kuendelea kutuombea na kutuunga mkono katika safari hiyo ili tuweze kuifikisha salama mizigo hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia maendeleo ya Watoto hao ambapo watakuwa wameshatimiza mwezi mmoja na siku 24.
Tunawashukuru sana tena sana wote mliojitolea na Mungu awabariki sana. 
Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com 
Nasi tutafikisha ubani wako. 
Wazee wa Kazi Serengeti Freight wametoa ofa ya 
kusafirisha bure misaada ya aina hii toka Uingereza.
Mbarikiwe sana Wazee wa Kazi.

No comments:

Post a Comment