TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, July 19, 2014

HAKI NA MISINGI YA DEMOKRASIA IZINGATIWE KWA WOTE.: WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ILALA.

 
 
HII NDIYO SHULE YETU YA WIKI HII TAREHE 20/7/2014.
kama unavyofahamu tena sisi wajibu wetu ni kujaribu kufuatilia kwa makini maendeleo ya wanafunzi, juu ya haki zao za msingi kisheria na Demokrasia ya Kweli. Shule hii ipo eneo la Vingunguti / Kipawa ni kwa mwendo kama wa dakika 10 kwa miguu toka barabara kubwa liendalo gongolamboto buguruni, ambapo jicho na darubini yetu ilipiga kambi kwa siri. Kati ya Mambo mazuri katika Shule hii ni pamoja na Wanafunzi Kupenda Utulivu wakati wote, wanafunzi hawa wanakuwa kila mmoja bize na masomo pamoja na kwamba wapo wengine ambao muda mwingine pia wanapata fulsa ya kupenya penya hapa na pale kwa kuchengana na walimu wao kwa tofauti ambazo ni za kimasomo.
Aidha Darubini yetu ilifanikiwa pia kufanya mazungumzo na baadhi ya Wanafunzi na Walimu kuhusu Shule hiyo," Eh wewe kwani ni nani? Mpiga Picha au? aliuliza mwanafunzi mmoja aliyekuwa ameketi kwenye kundi la Wenziwe huku wakiendelea kupiga Stori, Wakati ilikuwa yapata majira ya saa sita, wakati huo njaa pia zilikuwa zinaonekana kuwakwaza maana vijembe navyo vilisikika vya uchokozi wao kwa wao, "wewe naye unataka kuwa mwandishi wa habari, au unatafuta habari? njaa tu inakuwasha tumboni muda huu, unamuuliza huyo mtu wa watu yeye nani kwani wewe unataka awe nani? je kama ni mwandishi wa habari anatafuta habari, unataka kumpa hizo habari? yaani watoto wale kiboko, mie " mi nataka nimpe habari akauze vizuri kama kweli yeye anatafuta habari, wewe mkaka uje unipige picha, kwani ni bure au na hela? na hela nikamjibu ili nisije nikaharibu kabisa dili lenyewe, " je ni shilingi ngapi? " ni mia tano ila nikikuletea utanipa sawa," oh kumbe Simple tu, aisee niphotoe haraka kabla Walimu hawajaleta zao, maana kuna mmoja huyo mnokon kweli utadhani nini, hataki hata sisi Wanafunzi tupige picha za kumbukumbu tunapokuwa kwenye pozi zetu, sijui yeye alipokuwa anasoma wakati wake hapakuwa na kamera? eti wewe mpiga picha ni Sahihi kupiga picha sisi tukitaka za kumbukumbu au ni makosa?
Swali lake ilikuwa mtego sana kwangu, lakini baada ya kutafakari nikampa " kwani Shule ni ya Nani? Shule ipo kwa ajili ya Walimu au Shule kwa ajili ya Wanafunzi? nikampa na hiyo" Lakini wakati zoezi linaendelea mara yule asiyependa wanafunzi wapige picha akatokea wakaanza kutoka mbio, nikajaribu kuwasihii wamsikilize mwalimu wao maana alikuwa sasa anawaita kwa asira, kama unavyofahamu tabia za wanafunzi, wakimuona mwalimu wanageuza mgongo ili wasionekane sura, kwa hiyo mimi nikawambia hapa msikimbie nyie msikilizeni tu na mimi hapa nitajaribu kuwatetea maana sidhani kama kuna kosa kwenu kupiga picha za ukumbusho baina yenu, isipokuwa kosa ni kujaribu/kupiga picha chafu.
basi baada ya kuitikia wito wa mwalimu wao, msamaha wa mwalimu huyo kwanza kabisa ilikuwa ni wote kupiga magoti kwenye eneo la jua kali,(Wakati wanapigishwa magoti tayari ailitwa asikari kuja kutazama kama wanatimiza adhabu, baada ya hapo huyo mwalimu akaniita na mimi na kutoa oda picha zote zilizoko ndani ya kamera zifutwe, " Askari ulikuwa wapi wakati hawa Vitoto wanapiga piga picha, ili lingine litazame hata akili hamnazo kabisa lakini kwa Picha, Hakikisha Picha zote zilizomo kwenye hiyo kamera zimefutwa. Inaendelea katika ukurasa wetu wa mtandao wa Blogs: www.missdemokrasia.blogspot.com/ www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com

No comments:

Post a Comment