Rais
 Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua Daraja la 
Ruhekei lililopo katika Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Rais
 Jakaya Mrisho Kikwete katikati akifurahia kikundi cha Ngoma cha mkoa wa
 Ruvuma katika sherehe ya uzinduzi wa Daraja la Ruhekei lililopo katika 
barabara Mbinga –Mbamba bay mkoani Ruvuma.
Rais
 Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe 
Magufuli, Mama Salma Kikwete pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali 
wakipita juu ya Daraja la Mto Ruhekei baada ya kulifungua mkoani Ruvuma.
 Daraja hilo ni kiungo muhimu kati ya Wilaya mpya ya Nyasa pamoja na 
Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Waziri
 wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) kushoto akizungumza na 
Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu Profesa Juma Athumani Kapuya (Mb) 
kabla ya uzinduzi wa Daraja la Ruhekei lililopo katika Barabara ya 
Mbinga-Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Waziri
 wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) katikati akizungumza na Waziri 
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe wakati 
wakisubiri kuwasili kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa 
Dkt.Jakaya Kikwete.
Rais
 Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli 
wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali mara 
baada ya ufunguzi wa Daraja la Mto Ruhekei mkoani Ruvuma.
No comments:
Post a Comment