TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, November 15, 2014

NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR MAHMOUD THABIT KOMBO AZUNGUMZA NA WANAHABARI JUU YA MADHIMISHO YA SIKU YA KISUKARI DUNIANI

2
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
…………………………………………………………………………..
NA RAMADHANI ALI
Wananchi wameshauriwa kujiepusha na vihatarishi vinavyoweza kupelekea kupata ugonjwa wa kisukari na kujenga tabia ya kupima afya zao ili kujuwa matatizo yanayowakabili.
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mnazimmoja katika kuadhimisha siku ya kisukari Duniani.
Alisema tatizo la ugonjwa wa kisukari na vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo limekuwa kubwa na inakisiwa zaidi ya watu milioni 346 duniani wanasumbuliwa na ugonjwa huo.
Alisema ongezeko   kisukari katika nchi nyingi linasababishwa  na  watu kubadili mfumo wao wa  maisha na mabadiliko ya kijamii na kiutamaduni.
Naibu Waziri ameongeza kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2011 hapa Zanzibar, unaonyesha kiwango cha ugonjwa wa kisukari ni asilimia 3.7 ambayo ni sawa na watu 50,000.
Alisema kwa mujibu wa takwimu zinazokusanywa  katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja pekee kunawastani wa wagonjwa wapya wa kisukari 300 kila mwaka na zaidi ya watu 180,000 wapo hatarini kupata maradhi hayo kutokana na uzito uliokithiri.
Amewakumbusha wananchi kuwa ugonjwa wa kisukari hauponi na mtu akishaupata hulazimika kutumia dawa katika uhai wake wote na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.
“Jambo la msingi ninalosisitiza ni kwamba ugonjwa wa kisukari hauponi, mtu anapothibitika kuwa nao inamaana ataendelea kuwa nao katika maisha yake yote na atalazimika kutumia dawa ama sindano katika uhai wake wote,” alieleza Naibu Waziri.
Katika kujikinga na ugonjwa huo Naibu Waziri amewasisitiza wananchi kufanya mazoezi, kujiepusha na matumizi ya pombe na matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku pamoja na kuzingatia umuhimu wa lishe bora.
Amewashauri wananchi kuweka umuhimu wa kuchunguza afya zao kama ni njia moja wapo ya kinga kwani inakadiriwa kuna zaidi ya asilimia 50 ya watu wenye ugonjwa wa kisukari ambao hawajijui.
Akizungumzia kadhia ya kisukari Mkuu wa Kitengo cha ugonjwa wa kisukari Dkt. Faiza Kassim Suleiman alisema tatizo kubwa linalowapata wenye maradhi hayo ni ganzi, kupoteza nuru ya macho na kupungua nguvu za kiume.
Hata hivyo amesema bado hakujawa na mikakati imara iliyoandaliwa kukabiliana na ongezeko kubwa la ugonjwa huo licha ya kuwepo dawa katika Hospitali na vituo vya Afya.
Mwenyekiti  wa Jumuiya ya watu wanaoishi na ugonjwa wa kisukari Zanzibar Waziri Said Othman amesema dawa za ugonjwa huo zinapatikana lakini tatizo linalowakabili ni  dawa  za maradhi mengine ambayo yanaenda sambamba na kisukari ikiwemo sinikizo la damu.
Amewashauri madaktari kuongeza juhudi katika kuwashughulikia wagonjwa wa kisukari wenye vidonda kwani tiba yake huchukua muda mrefu kabla mgonjwa  kupona.

No comments:

Post a Comment