TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, November 9, 2014

Sitti Mtemvu amejivua taji la Miss Tanzania 2014

Barua ya aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu aliyowaandikia Lino International Agency kuhusu uamuzi wake wa kujivua taji hilo.
Barua ya aliyekuwa 
Miss Tanzania 2014, 
Sitti 
Abbas Mtemvu, 

aliyowaandikia Lino International Agency
 kuhusu uamuzi wake 
wa
 kujivua taji hilo.
Hatimaye aliyekuwa mrembo wa Tanzania 2014 (Redd’s Miss Tanzania 2014), Sitti Abbas Mtemvu, ametangaza kujivua taji hilo. Taarifa News imebaini.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga, amesema Sitti amechukua hatua hiyo kutokana kuzongwa na madai ambayo amesema si ya kweli.
Lundenga amesema waandaaji wa Miss Tanzania wamekubaliana na uamuzi huo kumvua taji Sitti ambaye ni mtoto wa mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu.
Badala yake taji limeenda kwa Lilian Kamazima aliyekuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo yaliyozua tafran mbaya zaidi tangu kuanza kwa Miss Tanzania.
Taarifa zinaeleza kuwa mrembo huyo aliitumia barua kamati ya uandaaji wa Miss Tanzania iliyoeleza uamuzi wake wa kuvua taji hilo.
Baada ya kukabidhiwa taji la Redd’s Miss Tanzania 2014 Oktoba 11, siku chache baadaye Sitti alikumbwa na kashfa ya kudanganya umri baada ya kuonekana kuna utofauti wa umri kati ya leseni na pasipoti yake.

No comments:

Post a Comment