Posted: 13 Nov 2013 12:10 AM PST
- ALIKUWA KWENYE MATIBABU AFRIKA KUSINI
- NCCR- MAGEUZI KUZUNGUMZIA MSIBA
Aliyekuwa
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi, amefariki
dunia jana alasiri nchini Afrika Kusini, katika Hospitali ya Milpark,
Johannesburg.
Dkt.
Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha
NCCR-Mageuzi na Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria Chuo Kikuu cha Bagamoyo
(UB), alipelekwa nchini humo baada ya kuvamiwa na kujeruhiwa usiku wa
kuamkia Novemba 3 mwwaka huu akiwa nyumbani kwake, Kimbamba Msakuzi.
Chama
cha NCCR-Mageuzi, kimethibitisha juu ya kifo hicho na kuongeza kuwa,
taarifa kamili zitatolewa leo Makao Makuu ya chama yaliyopo Ilala,
kuanzia saa tatu asubuhi.
Mtoa
habari hizo ndani ya chama ambaye hakutaka jina lake liandikwe
gazetini, alisema marehemu Dkt. Mvungi alikuwa kiongozi mkubwa ndani ya
chama na ametumia fursa hiyo kukifanya chama hicho kiwe na wanachama
wengi.
Dkt.
Mvungi baada ya kujeruhiwa kwa mapanga, alikimbizwa katika Hospitali ya
Rufaa Tumbi, iliyopo Kibaha, mkoani Pwani na baadaye kuhamishiwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kitengo cha Wagonjwa Wanaohitaji
Uangalizi Maalumu (ICU).
Kutokana
na hali yake kutoimarika vizuri akiwa hospitalini hapo, Novemba 7 mwaka
huu, Dkt. Mvungi alisafirishwa kwa ndege ya kukodi ya Shirika la Ndege
la Flightlink, kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi hadi mauti
yalipomkuta wakati madaktari wakiendelea kuokoa maisha yake.
Msemaji
wa Kitengo cha Taasisi ya Mifupa (MOI), Bw. Jumaa Almas, alisema
walilazimika kumsafirisha Dkt. Mvungi kutokana na afya yake kutoimarika
vizuri.
Dkt.
Mvungi alipata majeraha makubwa kichwani ambapio katika msafara wake,
aliongozana na Daktari Bingwa wa Upasuaji Ubongo na Mishipa ya Fahamu
Dkt. Clement Mugisha na Muuguzi, Bi. Juliana Moshi.
Juzi
Jeshi la Polisi nchini kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.
Emmanuel Nchimbi, alisema watu tisa ambao walihusika kumpiga, kumjeruhi
na kuiba vitu mbalimbali vya marehemu Dkt. Mvungi, tayari wamekamatwa.
Dkt.
Nchimbi alisema watu hao walikamatwa katika maeneo mbalimbali ya Dar es
Salaam kwa nyakati tofauti ambapo awali walikamatwa sita na juzi
kufikia tisa.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova,
ambaye alikuwepo katika mkutano huo, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni
Msigwa Mpopela (30), Shabago Magozi na Hamadi Ally, jina maarufu
'Hatibu'.
Wengine
ni Zakaria Raphael (dereva wa bodaboda), Mmanda Saluwa, Juma Hamisi,
Longisho Semeriko (muuza ugolo), Paul Jeirosi na mwingine aliyemtaja kwa
jina moja la Kilimimazoka, ambao wote ni wakazi wa Dar es Salaam
"Watuhumiwa
hawa walikutwa na mapanga, kigoda ambavyo vimethibitika kuwa vilitumika
katika tukio hilo, pia walikutwa na simu ya mkononi mali ya Dkt.
Mvungi," alisema.
Kamishna
Kova alisema, katika mahojiano ya awali na watuhumiwa, walikiri
kuhusika na tukio hilo na ushahidi umekamilika kwa asilimia 80.
"Watuhumiwa wote wamekiri kosa hivyo tunakamilisha upelelezi ili wafikishwe mahakamani mara moja," alisema.
Marehemu Dkt. Mvungi, aliwahi kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi
|
Posted: 13 Nov 2013 12:16 AM PST
- ACHAFULIWA MTANDAONI, AITUHUMU UVCCM TAIFA
Queen Lema, Arusha na Mariam Mziwanda, Dar
Katika
hali isiyo ya kawaida, Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema,
ameutuhumu uongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),
Taifa kwa mada ya kusambaza picha zinazoonesha akiingiliwa kinyume na
maumbile katika mitandao ya kijamii.
Mbali
ya uongozi huo, Bw. Lema pia alimtuhumu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Bw.
Sadifa Juma Khamis, kwa kushiriki kumchafua hivyo amemtaka Spika wa
Bunge, Bi. Anne Makinda, achukue hatua na kudai ushahidi wa jambo hilo
upo hadharani.
Bw.
Lema aliyasema hayo Mjini Arusha jana alipokutana na waandishi wa
habari ili kuzungumzia jambo hilo na kusisitiza kuwa, suala hilo
limemsikitisha sana. “Ushahidi wa namba za simu zilizohusika kusambaza
picha hizo upo, Khamis (Mwakilishi Jimbo la Donge, Zanzibar), anahusika
na udhalilishaji uliofanywa na vijana wa UVCCM Taifa,” alisema Bw. Lema.
Alisema
picha hizo zimesambazwa katika mitandao ya kijamii na watumiaji wa simu
za mkononi zikiwa na ujumbe unaodai Lema akilawitiwa na wanaume
wenzake.Aliongeza kuwa, Oktoba 29 mwaka huu, mkewe aliyemtaja kwa jina
la Bi. Neema Lema, alipata picha hizo zilizotumwa moja kwa moja katika
simu yake zikiwa na ujumbe usemao “Hiyo ndiyo kazi anayoifanya mume
wako”.
Bw.
Lema alisema, suala hilo halikuishia hapo kwani picha hizo zilitumwa
kwa mama mkwe wake na kusababisha familia ya mke wake na wazazi wake
kukosa amani “Mke wangu alitumiwa picha hizi katika mtandao wa WhatsApp
na baadaye ilisambazwa zaidi hadi kwa wapigakura wangu jimboni na kudai
ndiyo kazi inayofanywa na Mbunge wao,” alisema.
Aliongeza
kuwa, uchafu huo ulikuwa ukifanyika wakati akiwa bungeni Dodoma ambapo
Bw. Khamis, alionekana akisambaza picha hizo kutoka kwenye kompyuta yake
(mpakato), kuwapa wabunge jambo ambalo lilichangia amani ya bunge
kuharibika siku hiyo.
“Wakati
picha hizi zikisambazwa, nilijulishwa suala hili na wabunge wanawake wa
CCM, ilibidi niende kwa Spika ambaye alikiri picha hizo zimesababisha
akose morali ya kuendesha vikao. “Pia nilizungumza na uongozi wa Bunge
nikilalamikia kudhalilishwa kwa kutengenezewa picha zinazoonesha
nikiingiliwa na wanaume wenzangu... Spika aliahidi kulishughulikia,”
alisema Bw. Lema.
Bw.
Lema alisema, kutokana na picha hizo, bado hazimnyimi kinga ya
kuendelea kusema ukweli juu ya jambo lolote badala yake ataendelea
kupambana ili kuwatetea wanyonge.“Kamwe siwezi kuwatafuta waliotengeneza
picha hizi na kuzisambaza kwenye mitandao na simu za watu bali
atawasaidia viongozi wa UVCCM kuzisambaza kwenye Makanisa, Misikiti,
mikutano ya hadhara ili kuwaonesha wananchi ukatili dhidi yake
unavyozidi kushika kasi asiwe na sauti ndani ya nchi,” alisema.
Wakati huo huo,
Mke wa Mbunge huyo, Bi. Neema, alisema hicho ni kitu kidogo sana dhidi
ya mumewe na waliofanya vitendo hivyo walilenga kuvunja ndo yake lakini
haitatokea. Sadifa azungumza
Akijibu
tuhuma hizo akiwa njiani kwenda nchini Ethiopia, Bw. Khamis alisema
jumuiya hiyo au yeye mwenyewe hawezi kutumia cheo chake kufanya vitendo
hivyo.
“Mimi
na Mheshimiwa Lema wote ni wabunge, tofauti yetu ipo katika vyama na
majimbo...tomefahamiana bungeni na wala simjui kwa undani, tuhuma dhidi
yangu si za kweli kwani siwezi kufanya kitendo hicho ambacho si cha
kibinadamu hata kama tuna tofauti za kisiasa.
“Mimi
ni Muislamu na dini yangu hairuhusu kufanya hivyo, binafsi sijui
kutumia kompyuta na Mheshimiwa Lema analijua hilo...hivi sasa Ofisi ya
Bunge imeanza kutoa mafunzo kwa wabunge wasiojua kutumia kompyuta, nami
najifunza,” alisema.
Alisema
simu anazomiliki ni mbili, moja ni Nokia ya tochi na nyingine ya
kichina yenye laini tatu na hajui kama simu hizo zina mitandao na
hajawahi kujaribu.Bw. Khamis aliongeza kuwa, hulka yake hayupo karibu na
makundi yanayoweza kumuingiza au kumshawishi afanye vitendo hivyo hivyo
yupo tayari kukutana na Bw. Lema kwa amani ili wazungumze na kuwasaka
waliofanya vitendo hivyo ambavyo si vya kistaarabu.
“Mheshimiwa
Lema akinitafuta nitampa ushirikiano, ninachokijua mimi, mwenzangu
ananitafutia umaarufu kwa sababu pamoja na vyeo nilivyonavyo bado
sifahamiki sana.
“Natumia
cheo changu ndani ya UVCCM kuijenga jumuiya na CCM... kwanza namuomba
radhi kwa sababu tayari ana imani potofu dhidi yangu, pili namshauri
afanye utafiti,” alisema.
Alisema
imani yake ni kwamba, tofauti zao kisiasa haziwezi kumshawishi afanye
vitendo hivyo kwani ipo siku Bw. Lema anaweza kurudi CCM na kufanya naye
kazi pamoja.
Aliongeza
kuwa, umefika wakati wa Bw. Lema kukumbuka kuwa, tofauti za kisiasa
zilizopo ndani ya chama chao pia zinaweza kutumika kumchafua katika
mitandao
|
Posted: 13 Nov 2013 12:25 AM PST
Rais Jakaya Kikwete, amerudisha zawadi ya dhahabu safi gramu 227 aliyopewa na Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings ya mkoani Geita na kutaka itumike kuwasaidia watoto yatima, anaripoti Mwandishi Wetu
. Zawadi
hiyo alikabidhiwa juzi katika sherehe ya uzinduzi wa Mgodi wa Uchenjuaj
iDhahabu wa kampuni hiyo uliopo nje kidogo ya Mji mdogo wa Kharuma
ambako ndiko Makao Makuu ya Wilaya Mpya ya Nyang’hwale,mkoani humo.
Dhahabu hiyo ina thamani ya sh. milioni 16 kwa bei ya sasa katika soko
la dhahabu duniani ambapo baada ya kukabidhiwa, Rais Kikwete aliuliza;
“Sasa nifanye nini na zawadi hii, naomba kuirudisha hii dhahabu muiuze
popote, fedha ambayo itapatikana tutawapa watoto yatima,” alisema.
Akizungumza na wananchi katika mgodi huo, Rais Kikwete aliupongeza
uongozi wa mgodi na kusema umeongeza thamani ya dhahabu na ya maisha ya
wananchi katika eneo hilo.Aliushauri
uongozi wa mgodi huo, kufanya jitihada za kuboresha teknolojia
inayotumika. “Mgodi huu ni mradi wa maana sana kwani umeongeza thamani
ya dhahabu na kuboresha maisha ya wananchi katika eneo hili, ubunifu huu
unastahili pongezi.
“Lazima tuboreshe teknolojia, ile inayotumika katika mgodi huu ni ya
zamani kidogo, hii ni sawa na hadithi ya mtu mwenye chongo katika jamii
ya vipofu watupu, yeye anaonekana kama mfalme,” alisema Rais Kikwete.
Mgodi wa Nyamigogo ni wa marudio kwa maana ya kuzalisha dhahabu
kutokana na mchanga ambao awali ulifukuliwa ili kutoa dhahabu na
ulianzishwa mwaka 2011 ambapo hadi sasa, sh. bilioni 1.6 zimewekezwa
katika uendelezaji wa mgodi huo.
Katika risala ya uongozi wa mgodi huo, ilisema mgodi huo unazalisha
kati ya gramu 500 na 600 kwa mwezi na umeajiri watu 45 wakiwemo wanawake
10.Tangu
kuanzishwa kwake, umekuwa unaunga mkono shughuli za jamii inayouzunguka
kwa kujenga zahanati na madarasa ya shule katika vijiji viwili.
Rais Kikwete amezindua mgodi huo kama sehemu ya kukagua na kuzindua
miradi ya maendeleo akiwa katika ziara yake rasmi ya kikazi mkoani humo
ambao ni miongoni mwa mikoa minne aliyoianzisha mwaka 2012.
Ziara hiyo imemalizika jana kwa kupokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya
ya Nyang’hwale na kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika Mji Mdogo wa Kharuma
|
Posted: 13 Nov 2013 12:29 AM PST
Frank Monyo na Daniel Samson
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Zuberi Samatabe, amewahimiza walimu wa shule za msingi
kuwajengea wanafunzi utamaduni wa kujisomea vitabu ili kuongeza uelewa
katika masomo yao.
Aliyasema
hayo katika uzinduzi wa tovuti ya kufuatilia mgawo wa vitabu vya chenji
ya Rada uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Lengo
la tovuti hiyo ya www. pesptz.org ni kutoa taarifa kwa wadau wa elimu
pamoja na wanafunzi juu ya vitabu vinavyosambazwa katika shule za msingi
kwa kutumia chenji hiyo.
Alisema,
Serikali ya Uingereza iliamuru fedha zilizotumika vibaya katika
manunuzi ya Rada zirudishwe kwa Watanzania na zitumike katika manunuzi
ya vitabu na madawati kwa shule za msingi.
"Fedha
za chenji ya Rada sh. bilioni 72 zilizorudishwa ziliingizwa katika
mpango wa manunuzi ya vitabu na madawati katika shule za msingi na
asilimia 75 zimetumika katika manunuzi ya vitabu vya wanafunzi na vya
mwongozo wa walimu kufundishia," alisema Samatabe.
Kwa
upande wake Meneja Takwimu wa Kampuni ya Data vision International,
William Kihula alisema Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kupitia Shirika la
Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) iliwapa jukumu la kutengeneza
tovuti kufuatilia mgao wa vitabu vya chenji ya Rada, ili kuwezesha
ushirikishwaji wa wadau wa elimu na wananchi katika kufuatilia
usambazaji wa vitabu shuleni.
Alisema
hatua hii itawezesha serikali kuendelea kutembelea katika maeneo yake
na kuwa na uendeshaji wa uwazi ndio maana wamejenga mfumo huu katika
namna ambayo itaweza kutumika na wizara hata baada ya mradi huo wa mgawo
wa vitabu vya chenji ya rada kuisha.
"Tovuti
hiyo ndio pekee inayoweka mtandaoni majina yote ya shule za hapa nchini
wilaya na mikoa iliyopo hii itatoa mwanga wa kuanzia katika ufuatiliaji
wa maendeleo ya mwanafunzi mmoja mmoja," alisema Kihula.
Aliongeza
kuwa, kuwepo kwa jitihada za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
kuanza kutumia mfumo mpya wa kupima ufaulu wa wanafunzi kwa kuhusisha
"Continous Assessment" kwa kuanza na shule za sekondari.
"Katika
hili Datavision tupo kwenye hatua za mwisho za kutengeneza mfumo wa
teknolojia itakayowezesha kupatikana na kutunza taarifa za maendeleo ya
mwanafunzi shuleni kwa wakati," alisema Kihula.
|
Posted: 13 Nov 2013 12:32 AM PST
Penina Malundo na Maua Mashu
Wafanyakazi
wakiwemo vibarua zaidi ya 200 wa Kampuni ya STRABAG inayojenga barabara
ya mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam wamegoma.
Mgomo
huo ulianza jana jijini humo kwa madai ya kutaka kulipwa stahiki zao za
zamani kabla ya kampuni hiyo kuingia mkataba na kampuni nyingine.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti jana na waandishi wa habari, wafanyakazi wa kampuni
hiyo walisema kuwa, wameingia katika kampuni hiyo kwa sheria zote na
wengi wao wameweza kufanya kazi zaidi ya mwaka mmoja, hivyo wanapaswa
kulipwa madai yao kabla ya kuvunja mkataba na Kampuni ya STRABAG.
Walisema
kuwa, mgogoro mkubwa uliibuka kati ya vibarua hao na kampuni iliyoingia
mkataba na Strabag ijulikanayo kama Laba Constractors juu ya malipo
watakayolipwa kuwa madogo tofauti na malipo ya Kampuni ya Strabag.
"Jumamosi
tulikaa kikao na viongozi wa Laba Constractors wakatueleza kuwa kuanzia
siku ya Jumatatu (juzi), malipo yetu yatakuwa chini yao, kwani
wameingia mkataba na Kampuni ya Strabag kwa ajili ya kulipa wafanyakazi
wake na vibarua, jambo la kushangaza sisi hatujapata taarifa yoyote
kutoka kwa Strabag juu ya mkataba huo walioingia na Kampuni ya Laba
Constractors," alisema mmoja wa vibarua hao ambaye hakutaka kutaja jina
lake.
Alisema
kuwa, Kampuni ya Strabag ingefanya utaratibu maalumu wa kumaliza madai
yote ya msingi kwa vibarua wake na hapo ndipo wangeweza kuanza kuingia
mkataba na kampuni nyingine.
"Mpaka
sasa hatujui hatma yetu, sisi tumekaa hapa toka saa 12 asubuhi na
tutaendelea kukaa mpaka kieleweke hadi tupatiwe haki yetu, malipo yetu
tupewe ndiyo kampuni nyingine ianze upya na sisi, kwani tumeshakaa zaidi
ya mwaka mmoja, kisheria sisi tayari ni wafanyakazi halali," alisema.
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi katika Kampuni ya STRABAG (TAMICO),
Abdullah Rukusa alisema kuwa, Kampuni ya Strabag ilikuwa inawalipa
vibarua hao malipo ya sh. 12,500 kwa siku huku malipo ya posho yakiwa
sh. 4,800 kwa saa za ziada.
Alisema
kuwa, Kampuni ya Laba Contractors inataka kuwalipa vibarua hao kiasi
cha sh.10,000 kwa siku hali itakayofanya kampuni hiyo kuwanyonya
wafanyakazi hao pindi wanapoanza kazi saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Laba Contractors, Emanuel
Mshana alisema kuwa, mkataba kati yao na Kampuni ya Strabag ulisainiwa
Jumamosi iliyopita na kazi rasmi ilianza kufanyika juzi huku tayari
akidai wamekutana na wafanyakazi hao kwa mazungumzo.
Alisema
kuwa, vibarua 95 waliopewa na Kampuni ya Strabag kati yao 45 ndio
walioanza kufanya kazi nao juzi na kampuni yao kuongeza vibarua 28 kwa
siku, kwa ajili ya kufanya kazi.
Juhudi
za kumtafuta Mkurugenzi wa Kampuni ya Strabag ziligonga mwamba baada ya
kugoma kuzungumza na waandishi wa habari huku geti likizuiliwa na mawe
makubwa ya barabaran
|
Posted: 13 Nov 2013 12:39 AM PST
Na Grace Ndossa
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba (NHC), Nehemia Mchechu ametunukiwa tuzo ya
uongozi bora pamoja na cheti kwa kutambua mchango wake mkubwa katika
jamii na ndani ya shirika hilo.
Tuzo
hiyo ilikabidhiwa jana jijini Dar es Salaam na Rais wa Rotary Klabu ya
Mzizima, Ambrose Nshala ambapo alieleza kuwa Mkurugenzi huyo amekuwa
kiongozi bora na amethubutu kufanya kazi kwa ujasiri na kuonesha ndoto
za kufika mbali.
Alisema
kuwa, Mkurugenzi huyo ni kijana mdogo, lakini ameonesha uthubutu wake
katika kufanya kazi na mageuzi ndani ya shirika, hali ambayo imeonesha
hatua kubwa kiuchumi na kazi anazofanya zitalifikisha mbali shirika.
Alisema
kuwa, Rotary klabu inathamini mchango wake na kutambua kazi aliyofanya
kwa jamii kwani ni kubwa hivyo wametoa tuzo hiyo na cheti kwa ajili ya
kuongeza hamasa kwa viongozi wengine kuiga mfano wa mkurugenzi huyo ili
nchi iweze kupata maendeleo.
Kwa
upande wake, Mchechu alisema kuwa, tuzo hiyo itasaidia kuongeza hamasa
zaidi katika kufanya kazi ili nchi iweze kupata maendeleo.
Alisema
kuwa, sera za Tanzania ni nzuri ila tatizo liko kwenye utekelezaji
kwani viongozi wengi wanathamini maneno kuliko vitendo, hivyo ndiyo
vinavyofanya mambo mengi kukwama.
Pia
alisema, sera nyingi hapa nchini nyingi huishia kwenye karatasi na nchi
nyingi huiga sera za Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali
ndiyo maana zimepiga hatua
|
Posted: 13 Nov 2013 12:36 AM PST
Na Mwandishi Wetu
Imeelezwa
kuwa kuanzishwa kwa kampuni huru za minara ya mawasiliano ya simu,
kunaweza kupunguza gharama za uendeshaji kwa kampuni za simu za mkononi
nchini, hivyo kuweza kusaidia kuleta ahueni kwa watumiaji wa simu hizo.
Kabla
ya hapo kampuni zote za simu za mkononi nchini kila moja ililazimika
kujenga mnara wake ambao unahitaji kiasi kikubwa cha uwekezaji ikiwa ni
pamoja na matumizi ya jenereta, ulinzi na gharama nyingine za
uendeshaji.
Hayo
yalibainishwa jana na Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya
Helios Towers, Michael Magambo wakati akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam.
"Hapo
ndipo kampuni huru za minara zinapoingia. Humiliki, husimamia na
huendesha minara, inayoweza kutumiwa na kampuni nyingi za simu kwa
wakati mmoja na pia hata matangazo ya Tv, redio na mawakala wa hali ya
hewa," alisema.
Alisema,
matumizi ya mnara mmoja huondoa mzigo wa gharama za uwekezaji wa
miondominu pamoja na shughuli nyingine kwenye eneo la mnara.
Pia
alisema, kampuni za simu zinapata nafasi ya kuelekeza nguvu zaidi
katika eneo wanaloliweza zaidi kutoa huduma za sauti na 'data' kwa
Watanzania.
"Wengi
hawaufahamu mchango wetu katika kupanua huduma za simu Tanzania na
Afrika kwa ujumla. Helios Towers ni kampuni kubwa ya minara huru nchini,
ikiwa imejenga zaidi ya minara 1,000 ya Tigo Tanzania mwaka 2010, kisha
ikajenga minara mingine 250 na inatarajia kuongeza mingine 150 ifikapo
Desemba mwaka huu," alisema Magambo.
Aidha,
alisema kwa miaka miwili iliyopita, maeneo ya Helios yanayotumiwa kwa
pamoja na kampuni za simu ni asilimia 53 kwa sasa na ni asilimia 60 ya
maeneo mapya kwa nchi nzima huku ikisubiri uthibitisho wa serikali wa
kuchukua minara ya Vodacom Tanzania.
"Tumekuwa tukisikia wakosoaji wakidai kwamba, kampuni kama Helios hayana ushindani kwa kuwa yamekamata soko kubwa.
"Hii
si kweli. Uhakika ni kwamba Helios imekuwa chachu ya kuwapo kwa
ushindani kwenye soko la huduma za simu, ikiruhusu wageni kuingia kwenye
soko na kuwapa nafasi watoa huduma kupeleka vijijini bila wasiwasi.
"Mwishowe
ni walaji ndio hufaidika zaidi kwa kupunguziwa bei za simu na kuchagua
mtandao wanaoutaka. Ukweli ni kwamba tunafungua zaidi soko," aliongeza
Magambo.
Hata
hivyo, katika kupunguza changamoto za kupeleka huduma maeneo ya
vijijini yasiyo na huduma za simu, awali Serikali ilitoa gari
lijulikanalo kama Universal Communication Action Fund (UCAF)
linalosaidia kupunguza gharama na kuwahamasisha watoa huduma kwenda
kwenye soko la vijijini.
Hatua
hiyo ilitokana na Sheria ya Upatikanaji wa Mawasiliano ya mwaka 2006
yenye lengo la kukuza maendeleo ya kijamii na uchumi mijini na vijijini
kupitia TEKNOHAMA.Mbali na hayo Kampuni ya Helios iko mbioni kuweka
mitambo 27 chini ya UCAF
|
Posted: 13 Nov 2013 12:42 AM PST
Na Mwandishi Wetu
Kampuni
ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania imeamua kupambana na changamoto
zinazoikabili sekta ya elimu nchini kwa kuzisaidia shule mbalimbali za
sekondari kupata miundombinu ya kufundishia na vifaa vya kujifunzia.
Pia
kampuni hiyo kupitia mradi wake wa Shule Yetu imewanufaisha wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Chalinze iliyopo mkoani Pwani baada ya kukabidhi
vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya sh. milioni tano kwa
shule hiyo.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vitabu hivyo, Meneja Masoko wa Airtel Kanda ya
Kusini na Mkoa wa Morogoro, Aminata Keita alisema vitabu hivyo
vitatumika katika kuongeza kiwango cha uelewa na kukuza ufaulu kwa
wanafunzi wa shule hiyo ambao walikuwa na tatizo la uhaba wa vitabu.
"Vitabu
hivi...vitatumika kukuza ufaulu kwa wanafunzi maana wanafunzi wataweza
kujisomea kwa urahisi na kufuatilia masomo kwa ukaribu zaidi," alisema
Aminata.
Aliongeza
kuwa, msaada huo wa vitabu ni sehemu ya mpango mkakati wa kuzisaidia
shule za kata zinazolalamikiwa kufanya vibaya katika mitihani yao ya
kitaifa.
"Tumetoa
vitabu vya masomo ya sayansi tukijua kabisa wanafunzi wengi hushindwa
masomo hayo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo upungufu wa zana za
kujifunzia ila nina imani mradi huu wa Shule Yetu utaziwezesha shule za
kata kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa," alisema Aminata.
Kwa
upande wake mkuu wa shule hiyo, Emmanuel Kahabi alisema, upatikanaji wa
vitabu utarahisisha kazi ya ufundishaji kwa wanafunzi na pia wanafunzi
wataweza kuelewa kiurahisi maana zana za kufundishia zinapatikana
|
Posted: 13 Nov 2013 12:49 AM PST
Neema Ndugulile
Timu
ya Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 na Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania (TPL Board) na kupewa onyo kali kwa timu yake ya U20 kutocheza
mechi ya utangulizi walipocheza na Yanga.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Ofisa Habari wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu wa
shirikisho hilo, Boniface Wambura alisema pia Mbeya City wanatakiwa
kulipa gharama za uharibifu, baada ya mashabiki wao kuvunja kioo cha
basi la Yanga, baada ya gharama hizo kuthibitishwa na bodi hiyo.
"Pia
Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mashabiki wake kushambulia
basi la wachezaji wa Tanzania Prisons, baada ya mechi dhidi yao na
kulipa gharama za uharibifu baada ya kuthibitishwa na Bodi ya Ligi,"
alisema Wambura.
Alisema
Coastal Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za
mashabiki wake ilipocheza na Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambapo
mwamuzi msaidizi, Hassan Zani alishambuliwa kwa mawe na kujeruhiwa
mkononi na kichwani, tukio lililosababisha mchezo kusimama kwa dakika
tatu.
Wambura
alisema beki wa Coastal Union, Hamad Khamis amepigwa faini ya sh.
500,000 kwa kumpiga kichwa kwa makusudi Kipre Tchetche wa Azam. "Kitendo
hicho kilisababisha refa amtoe nje kwa kadi nyekundu, hivyo atakosa
mechi tatu zinazofuata za timu yake.
"Nayo
Simba wamepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za mashabiki
wake wakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar," alisema Wambura.
Alisema
adhabu zote zimetolewa kwa mujibu wa kanuni. Pia Bodi ya Ligi
imeahirisha kufanya uamuzi wa mechi kati ya Stand United na Kanembwa JKT
iliyochezwa Uwanja wa Kambarage, ili kukusanya taarifa zaidi. Mechi
hiyo haikumalizika. Bodi ya Ligi itakutana tena Jumapili.
|
Posted: 13 Nov 2013 12:46 AM PST
Na Fatuma Rashid
Bodi ya
Ligi Kuu Tanzania (TPL Board), imefungia viwanja saba vilivyokuwa
vikitumiwa na timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza
(FDL), hadi vitakapofanyiwa marekebisho ili kukidhi mahitaji ya mechi
za mpira wa miguu.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Ofisa Habari wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema uamuzi huo
umefikiwa na TPL Board katika kikao chake cha kwanza kilichofanyika juzi
ambapo pamoja na mambo mengine, kilipitia ripoti za mechi za VPL na FDL
katika mzunguko wa kwanza.
Alisema
viwanja vilivyofungiwa na marekebisho yanayotakiwa kufanyika kwanza,
ili viruhusiwe kutumika tena ni Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba (majukwaa
yake yamechakaa, hivyo kuhatarisha usalama wa watazamaji) na Uwanja wa
CCM Mkwakwani jijini Tanga (vyumba vya wachezaji kubadilishia nguo
(dressing rooms) havina hadhi.
Wambura
alisema Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya (sehemu ya kuchezea-pitch ni
mbovu), Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha (sehemu ya kuchezea ni
mbovu), Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi (vyumba vya kubadilishia kutumika
kwa ajili ya shule ya awali), Uwanja wa Majimaji mjini Songea (pitch ni
mbovu) na Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro (pitch ni mbovu).
Wambura
ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, alisema klabu ambazo timu zake
zinatumia viwanja hivyo zimeshataarifiwa rasmi juu ya uamuzi huo, ambapo
ama vinatakiwa kuwasiliana na wamiliki wa viwanja hivyo, ili wafanye
marekebisho au kutafuta viwanja vingine vya kuchezea mechi zao.
Wakati huo huo, timu
za Taifa za Future Taifa Stars na Taifa Stars zinacheza leo. Mechi hiyo
ya kirafiki itafanyika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kuanzia
saa 10 kamili jioni.
Mechi
hiyo ni maalumu kwa Benchi la Ufundi la Taifa Stars linaloongozwa na
Kim Poulsen, kuangalia wachezaji kumi kutoka Future Taifa Stars
watakaoongezwa katika Taifa Stars, tayari kwa mechi ya kirafiki ya
kimataifa itakayochezwa Novemba 19, mwaka huu jijini Arusha.
Watazamaji
300 tu wataruhusiwa kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 5,000.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini
jana. Miongoni mwa wachezaji wanaotarajia kuripoti ni kipa Ivo Mapunda
wa Gor Mahia.
|
Posted: 13 Nov 2013 12:57 AM PST
Na Fatuma Rashid
Kocha mpya wa timu ya Azam Fc anatarajiwa kutua katika kikosi hicho mapema, kabla ya wachezaji wa timu hiyo kurudi kambini.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Msemaji wa timu hiyo, Jaffer
Iddi alisema wachezaji wote wamepewa likizo ya wiki mbili, hivyo uongozi
upo katika mchakato wa kutafuta kocha atakayerithi mikoba ya aliyekuwa
kocha wa timu hiyo, Mwingereza Stewart John Hall.
Msemaji
huyo alisema kocha mpya atakapowasili, ndipo atakapojua ni mchezaji
gani atataka aanze naye na yupi amalize naye, kwani yeye ndiye atakuwa
akiufahamu uwezo wa wachezaji kuanzia mazoezini hadi katika mechi.
Akizungumzia
katika mechi ya mwisho ya mzunguko wa kwanza ya michuano ya Ligi Kuu
Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City, Iddi alisema ilikuwa nzuri kuliko
nyingine kwani wote walikuwa wazuri na walipigana kutafuta nafasi nzuri
katika kumalizia mzunguko huo.
Alisema
timu yake kwa sasa ipo mapumziko na itarudi kambini baada ya wiki
mbili, ili kujipanga zaidi kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo na michuano
ya kimataifa.
Aliongeza
kuwa, katika mzunguko wa pili anaimani timu yake itakuwa vizuri zaidi
kutokana na kuona pamoja na kupima uwezo wa kila timu shiriki za Ligi
Kuu, ambazo uwezo wake wameshauona, hivyo anaona timu itajifunza
kutokana na walichokiona katika mzunguko wa kwanza.
Kocha
Hall aliwaaga wachezaji na benchi la ufundi, mara tu baada ya mchezo wa
mwisho wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Mbeya City uliomalizika kwa sare
ya mabao 3-3 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.
|
No comments:
Post a Comment