TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, November 15, 2013

NITAMNG’OA SPIKA MAKINDA-MBUNGE, CHADEMA: HATUHUSIKI MADAI YA ZITTO,

Posted: 12 Nov 2013 12:15 AM PST

  •  ASEMA CCM HAIWEZI KUONDOA HOJA YAKE BUNGENI
  • ASISITIZA MSIMAMO WAKE KWA WAPIGA KURA JIMBONI

Na Suleiman Abeid, Nzega
   Mbunge wa Nzega mkoani Tabora ,Dkt.Hamisi Kig wangalla,amesema bado ana dhamira ya kuwasilisha hoja ya kumng’ oa madarakani Spika  wa B unge, Bi.Anne Makinda .Alisema uvumi ulioenea kuwa hoja yake imeondolewa kwa agizo la Chama Cha Mapinduzi (CCM), hauna ukweli
.  Dkt. Kigwangalla aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara ulioshirikisha wakazi wa jimbo hilo na vitongoji vyake uliofanyika katika Uwanja wa Parking.Katika mkutano huo, Dkt. Kigwangalla aliulizwa swali na mkazi wa jimbo hilo kama kweli ana ubavu wa kumng’oa Bi.Makinda, anayetokana na chama chake.
“Mheshimiwa mbunge,naomba utu thibitishie kama una uwezo wa kumng’oa Spika wa Bunge (Makinda), kama ulivyotangaza dhamira ya kuwasilisha hoja binafsi bungeni ili bunge liweze kumng’oa.
“Kwa jinsit unavyofahamu utaratibu ndani ya CCM, huna ubavu wa kufanya hivyo , inaonesha ulikuwa ukijifurahisha tu,”alihoji mwananchi huyo.
Mwananchi huyo aliongeza kuwa, kwa kawaida CCM ina utaratibu wa kuzuia hatua mbalimbali zinazotaka kuchukuliwa na wanachama wake hivyo alimshauri Dkt.Kigwangalla, aacha ne na hoja hiyo kwani hana ubavu wa kumng’oa Bi.Makinda.
Akijibu swali hilo,Dkt. Kigwangalla alisema,si kweli kwamba CCM ina utaratibu wa kuondoa kinyemela hoja ambazo haikubaliani nazo ambapo suala la kutaka kumng’oa Bi. Makinda lipo ndani ya uwezo wake na kufafanua kuwa, hoja hiyo haijaondo lewa na hivi sasa ipo katika hatua za mwisho ili iweze kufikish wa bungeni.
“Kwa hili la kumng’oa Spika wa Bunge,niwaeleze wazi kuwa si kweli linawezaku nishinda... hoja imewasilishwa na Bi.Makin da atang’oka kama nikiamua kuendelea nayo kwa sababu tayari hoja nimeiwasilisha na nimekidhi mashart iyote.
“Hivi tunavyoongea, hoja yangu tayari imetoka hatua ya kwanz a na kukidhi vigezo vyote sasa inaenda hatua y a pili ambayo Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge,itaamua ho ja yangu iingizwe bungeni au isiingizwe,”alisema .
Aliongeza kuwa, baada ya hapo utafuata mcha kato wa mwisho ambao ni hoja hiyo kufikishwa bungeni na yeye kuiwasilisha rasmi mbele ya Bunge ili kufanyiwa uamuzi na wabunge wote kwa kupiga kura na kama atashinda au kushindwa,hilo ni jambo lingine.
Dkt.Kigwangalla alisema uamuzi wa kuondoka au kutoondoka kwa Spika, kutategemea uamuzi wa wabunge wenzake na kusisitiza kuwa , CCM haiwezi kuzuia hoja hiyo bila ya kupatiwa uamuzi na wabunge wote.
Akijibu swali ambalo lilihusiana na fedha za ushuru wa huduma zilizotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Resolute, ulioko wilayani humo, Dkt. Kigwangalla alisema fedha hizo sh. Bilioni 2.340,zililipwa na mgodi huo na sasa zimehifadhiwa katika ak aunti maalumu ili baadaye zitumike kama mtaji wa kuanzishia Ben ki ya Maendeleo ya Wananchi wa Nzega .
“Fedha hizi tulizipigania kwa kiasi kikubwa hadi kuandam ana lakini tulifanikiwa kuzipata, niwathibitishie zipo sa lama katika akaunti maalumu tuliyoianzisha ili baadaye ziweze kuanzisha Benki yetu ya Maendeleo ambayo itaweza kutupa mikopo ya kuendesha shughuli zetu,”a lisema .
Alisema lengo lake ni kuhakikisha fedha hizo zinatumika vizuri ili kuwasaidia wananchi wa Nzega kubadilisha maisha yao ambapo watu watahamasishwa kujiunga katika ushirikaau SACCOS ili waweze kupewa mikopo pia zitatumika kununulia mitambo ya kutengeneza barabara na uchimbaji visima vya maji.
Gazeti moja linalotoka kila siku (si Majira), liliandika habari inayosema Dkt. Kigwangalla anadai Bi. Makinda amekiuka kanuni kwa kuidhinisha malipo ya sh. 430,000 kama posho kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, tofauti na wajumbe wa kamati nyingine ambao malipo yao ni sh. 180,000 kwa siku.
Hoja hiyo ilipingwa vikali na baadhi ya wabunge akiwemo Mbunge wa Tabora Mjini, Bw. Ismail Aden Rage (CCM) na Mbunge wa Kigoma Kusini, Bw. David Kafulila (NCCR-Mageuzi) ambao walidai hawaoni sababu ya kumuondoa Bi. Makinda madarakani.
Bw. Kafulila alisema hilo ni suala la wana-CCM, kwani Bi. Makinda aking’olewa madarakani, mtu ambaye ataziba pengo lake hawezi kutoka upinzani. Hoja hiyo ya Dkt. Kigwangalla iliibua mjadala kwa baadhi ya wabunge na wengine kukataa kusaini karatasi ambayo walipelekewa ili kuunga mkono.
Mbunge wa Ludewa, mkoani Njombe, Bw. Deo Filikunjombe, alisema hoja ya Dkt. Kigwangalla imejengwa katika msingi hafifu isiyozingatia masilahi mapana ya nchi na mtazamo finyu
Posted: 12 Nov 2013 12:36 AM PST
  • SASA WAFIKIA TISA, WAKUTWA NA MAPANGA,SIMU YAKE
 Rehema Maigala na Isaya Ng wijo
Jeshi la Polisi nchini, linawashikilia watuhumiwa tisa wanaosh ukiwa kumvamia, kumjeruhi na kuiba vitu mbalimbali vya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu yaC hama cha NCCR-Mageuzi, Dkt.Sengondo Mvungi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Sa laam jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi,alis ema kukamatwa kwa watuhumiwa hao, kumechangiwa na ushirikiano uliotolewa na familia ya Dkt. Mvungi.
Alisema watuhumiwa hao wamekamatwa jijini Dar es Sa laam kwa nyakati tofauti ambapo awali walikamatwa sita lakini majina yao yalifichwa ili kutovuruga upelelezi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova,ambaye alikuwepo katika mkutano huo, waliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Msigwa Mpopela (30) ,Shabago Magozi na Hamadi Ally, jina maarufu‘Hatibu’.
Wengine ni Zakaria Raphael (dereva wa bodaboda), Mmanda Saluwa,Juma Hamisi,Longisho Semeriko(muuza ugolo), Paul Jeirosina mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Kilimimazoka,am bao wote ni wakazi wa Dar es Salaam.
“Watuhumiwa hawa walikutwa na mapanga, kigoda ambavyo vim ethibitika kuwa vilitumika katika tukio hilo, pia wa likutwa na simu ya m kononi mali ya Dkt. Mvungi,”alisema.
Kamishna Kova alisema, katika mahojiano ya awali na watuhumiwa, walikiri kuhusika na tukio hilo na ushahidi umekamilika kwa asilimia 80.
“Watuhumiwa wote wamekiri kosa hivyo tunakamilisha upelelezi ili wafi kishwe mahakamani mara moja,”alisema .
Dkt. Mvungi alivamiwa, kujeruhiwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi usiku wa kuamkia Novemba 3 mwaka huu , nyumbani kwake Kibamba, Dar es Salaam.
Hivi sasa,Dkt. Mvungi anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Milpark, nchini Afrika Kusini na hali yake inaendelea kuimarika .
Akizungumzia suala la kuwakamata wahamiaji haramu, Dkt.Nchimbi alisema mpango walionao ni kuweka Ofisa mmoja wa Polisi kila Tarafa nchini aweze kusaidiana na Polisi Jamii pa moja na wananchi kuwabaini watu hao.
Posted: 12 Nov 2013 12:52 AM PST
 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Ofisi ya Katibu Mkuu wa chama hicho imepokea barua iliyoandikwa na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Zitto Kabwe, anaripoti Rose Itono.

Barua hiyo, inamtaka Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt
 Wilbrod Slaa athibitishe madai ya ripoti inayosema“Taarifa ya Siri ya CHADEMA”iliyosamba zwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Taarifa hiyo inadai kuchunguza mwenendo wa Bw.Kabwe tangu mwaka2008-2010 na kubaini amepokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuivuruga CHADEMA.
Akizungumza na Majira jana, Ofisa Habari wa CHADE MA,Tumaini Makene,alisema barua aliyoiandika Bw. Ka bwe itafanyiwa kazi kwa mujibu wa taratibu, kanuni za katiba ya chama.
“Chama chetu kinaongozwa na vikao hivyo barua yake itafanyiwa kazi...CHADEMA haiendeshwi na taarifa za magazetini au mitandaoni,”alisema Bw. Makene.
Aliongeza kuwa,si mara ya kwanza makundi yasiyojulikana kusambaza taarifa za kutaka kumchafua Bw. Kabwe kupitia mitandao hiyo ambapo Ofisi ya Habari,ilishughulikia suala hilo na kuhakikisha taarifa hizo zinaondolewa .
“Hivi sasa ni mara ya pili, Bw. Kabwe anali fahamu hilo hivyo CHADEMA hakihusiki, lakini kitashughulikia s uala hili kupitia vikao ili kupata majibu sahihi,” alisisitiza Bw.Makene.
Katika taarifa yake aliyoitoa juzi kwa vyombo vya habari, Bw.Kabwe alisema taarifa hizo zimesambazwa katika mitandao ya kijamii hivyo alimtaka Dkt.Slaa, athibitishe ki nachoitwa“Taarifa ya Siri ya CHADEMA”,kama ni taa rifa ya chama au kuikanusha ili kumpa fursa ya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa taarifa hiyo.
Hata hivyo, Bw. Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kig oma Kaskazini,aliziita taarifa hizo za kutunga zilizojaa uongo wa kiwango cha kutisha hali ambayo imemfedhehesha, kumsikitisha na kumkasirisha.
Alisema taarifa hizo ziliibuliwa katika kipindi ambach o alikuwa safarini kutetea haki zaWatanzania na Afrika amb ao utajiri wao wa rasilimali unafaidiwa na watu wachache waliohifadhi fedha katika akaunti nje ya nchi.

Posted: 12 Nov 2013 02:46 AM PST

   Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, amestaafu rasmi kazi kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha umriwamiaka 60.Katika utumishi wake ndani ya Jeshi la Polisi, amefanya kazi katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo chumba cha kupokea mashtaka kuanzia mwaka (1976-1977).

  Nafasi nyingine ni Mwendesha Mashtaka Wilaya ya Kibondo na Kasulu, mkoani Kigoma (1977- 1984), Mkufunzi wa Chuo cha Polisi Dar es Salaam, (1984-1987), Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Magomeni, Kinondoni na Naibu Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (1987-1993),
  Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Msemaji wa jeshi hilo, SSP Advera Senso, ilisema Manumba pia aliwahi kuwa Mkuu wa Upelelezi mkoani Arusha (1993- 1995), Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi (1995-1996) na Mkuu wa Kitengo cha Fraud Makao Makuu ya Upelelezi (1996-1997).
  Nafasi nyingine Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Nchi, Intelijensia na Dawa ya Kulevya Makao Makuu ya Upelelezi (1997- 2001) na Msaidizi wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (2001-2006).
 Alisema kuanzia 2006 hadi anastaafu, alikuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI).Mkuu wa jeshi hilo nchini, IGP Said Mwema, amemshukuru Manumba kwa kulitumikia Taifa katika nyadhifa mbalimbali ndani ya jeshi hilo kwa weledi na uaminifu mkubwa wakati wote wa utumishi wake.
  Alimtaka aendelee kuwa msaada kwa jeshi hilo, kutoa ushirikiano wa namna yoyote unaoweza kupunguza uhalifu nchini kwa sababu suala la usalama ni taaluma kama zilivyo taaluma zingine na taaluma hiyo wanayo watu wachache.
  SSP Senso alisema, wakati taratibu za uteuzi wa DCI mpya zikiendelea, Mkuu wa Ufuatiliaji na Tathmini CID Makao Makuu, Kamishna Isaya Mungulu, atakua akikaimu nafasi hiyo.
Posted: 12 Nov 2013 03:00 AM PST


Na Elizabeth Joseph, Dodoma
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepanga kuiburuza mahakamani Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kwa kosa la kubomoa nyumba za wananchi bila fidia.

Uamuzi huo ulitolewa juzi na Mkurugenzi wa Organizesheni na Mafunzo Taifa (CHADEMA), Benson Kigaila wakati akihutubia wananchi katika mikutano wa hadhara uliyofanywa katika Kata ya Mkonze na Kikuyu Kusini mkoani humo ambapo alisema kuwa hivi karibuni wakazi wa maeneo hayo walitangaziwa kubomolewa nyumba zao na CDA kwa madai kuwa wameyavamia.
Kigaila aliwataka wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kujiorodhesha majina yao ili kupitia chama hicho waweze kutafuta wakili kwa ajili ya kuweka pingamizi la kusitisha ubomoaji huo.
Kigaila alisema kuwa CDA ilitakiwa kufanya kazi ya kustawisha mji na kuondoka lakini cha kushangaza hadi leo bado iko Dodoma na kuwanyanyasa wananchi kwa kuwauzia viwanja kwa bei ya kiasi kisichopungua milioni 5 pindi wanapohitaji viwanja na wakati mwingine kufukuzwa katika ardhi ambazo wamezikuta toka enzi za mababu zao jambo ambalo ni kuwanyima haki ya kumiliki ardhi yao.
  Hivyo ili kutetea haki ya wananchi chama hicho kimeona ni vyema kuungana na wananchi katika kuishtaki Mamlaka hiyo ili kujua suluhu ya wakazi wa mkoa huu .
  Aliongeza kuwa hata chama kilichopo madarakani (CCM) kimekuwa kikifumbia macho kero za wananchi wa mkoa huu kuhusiana na Mamlaka hiyo kwani taarifa juu ya CDA inajulikana lakini kimekuwa kikipiga danadana katika kutoa uamuzi wa kuiondoa mamlaka hiyo ili wazawa waweze kujua suluhisho la maisha yao katika kumiliki ardhi ambayo walifukuzwa bila kulipwa fidia.
  Aidha, aliwataka wananchi kwa pamoja kupinga suala la CDA kuvunja maeneo yao bila fidia na kuungana na chama hicho katika kutetea haki yao ili waweze kuishi kwa amani katika ardhi ya nchi yao pamoja na kuwataka wananchi kuondoa ukereketwa wa vyama ili kufanikisha suala hilo.
  Mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mussa Ndalu katika Kata ya Mkonze alisema kuwa Chama kilichopo madarakani ndio kinaoongoza kwa kuwagawanya Watanzania kwa kuyafumbia macho malalamiko ya wananchi juu ya umiliki wa ardhi ya nchi yao huku wageni wakipewa kipaumbele katika suala hilo.
Posted: 12 Nov 2013 03:05 AM PST


  •   AL AHLY BINGWA AFRIKA
MANCHESTER, Uingereza
  Mholanzi Robin van Persie juzi aliizamisha klabu yake ya zamani, Arsenal akiifungia bao pekee la ushindi Manchester United na kuirejeshea matumaini ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England.

 Van Persie alifunga bao tamu kwa kichwa akiunganisha kona iliyochongwa kitaalamu na Wayne Rooney dakika ya 27 Uwanja wa Old Trafford.
Kikosi cha Man United kilikuwa; De Gea, Smalling, Vidic/Cleverley dk45, Evans, Evra, Valencia, Jones, Carrick, Kagawa/Giggs dk78, Rooney na Van Persie/ Fellaini dk85.
Arsenal; Szczesny, Sagna, Koscielny, Vermaelen, Gibbs, Arteta/Gnabry dk82, Flamini/Wilshere dk61, Ramsey, Ozil, Cazorla/Bendtner dk78 na Giroud.
CAIRO, Misri
TIMU ya Al Ahly ya Misri, imenyakua taji la Klabu bingwa Afrika baada ya kuicharaza Orlando Pirates ya Afrika Kusini mabao 2-0 katika mechi ya fainali ya pili iliyopigwa juzi katika Uwanja wa Arab Contractors jijini Cairo. Al Ahly, wamejinyakulia kombe hilo kwa mara ya saba.
Hata hivyo, kulikuwa na ripoti za vurugu kuzuka kati ya mamia ya wafuasi wa Al Ahly na polisi nchini Misri, kabla ya mechi kuanza.
Baada ya vurugu kusitishwa mchezaji mkongwe, Mohamed Aboutrika ndiye aliyefunga bao la kwanza dakika ya 54. Dakika ya 78, Ahmed Abdul Zaher aliipatia Al Ahly bao la pili.
Hata hivyo, mabingwa hao wa Misri walipata pigo baada ya beki wake, Sherif Abdel Fadil kutolewa na mwamuzi kwa kadi nyekundu kutokana na kumfanyia dhihaki mchezaji wa Orlando Pirates, Daine Klate.
Pirates, ambao ni mabingwa wa mwaka 1995, walicheza kwa nguvu zote, lakini walikosa nguvu baada ya Al Ahly kupata bao la pili katika mechi hiyo iliyokuwa na mashabiki lukuki.
Hata hivyo, mabingwa hao wa Afrika Kusini walikosa nafasi nyingi za kufunga katika mechi hiyo.
Baada Al Ahly kunyakua kombe hilo walizawadiwa kitita cha dola milioni 1.5 za Marekani, Pia watawakilisha Afrika katika Kombe la Dunia la Klabu Bingwa Duniani litakalofanyika nchini Morocco mwezi ujao.
Kabla ya mechi hiyo mamia ya mashabiki wa Ahly walikabiliana na polisi ambao walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya mashabiki waliokuwa wakitupa mawe huku wakilazimisha kuingia uwanjani kwa nguvu.
Ni mechi ya kwanza kubwa, ambako mashabiki waliruhusiwa kuingia uwanjani tangu mashabiki wa Al Ahly, walipouawa katika mechi iliyokumbwa na vurugu mwaka jana.

No comments:

Post a Comment