Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka
jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga – Uyovu
yenye urefu wakilometa 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
(aliyeshika mkasi) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga
– Uyovu yenye urefu wa kilometa 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Geita.
Kulia kwa Rais ni Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto kwa
Rais ni Mbunge wa Bukombe Mhe. Kulikoyela Kahigi kutoka CHADEMA. Wengine ni baadhi
ya Mawaziri na Viongozi wa Kitaifa na kutoka mkoa wa Geita waliokuwepo katika sherehe
hizo.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (aliyeshika kipazasauti) akitoa
taarifa kwa wananchi wa Iboya waliousimamisha msafara wa Rais Kikwete alipokuwa
kwenye ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
na Kiongozi wa Kikundi cha Mchelemchele kilichotumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi
wa ujenzi wa barabara ya Bwanga – Uyovu inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani
Geita.
Kikundi cha Mchelemchele kutoka Mwanza kikitumbuiza wakati wa sherehe za
uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga – Uyovu inayojengwa kwa kiwango cha
lami mkoani Geita.
===============================================================
“Hii imekuwa ni faraja kubwa kwa wana Mbogwe kwani suala la usafiri limekuwa ni kero ya muda mrefu, tunashukuru sana kwa kutembelewa na ugeni huu wa Kitaifa hapa mkoa ni kwetu” alisisitiza Mheshimiwa Masele.
===============================================================
ZIARA YA RAIS KIKWETE WILAYANI MBOGWE,
BARABARA YAPANDISHWA DARAJA
Wananchi wa
wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wamenufaika kwa ziara ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kusikilizwa ombi
lao ambapo barabara inayounganisha maeneo ya Masumbwe na Makao Makuu ya wilaya
hiyo imepandishwa daraja na kuwa barabara ya mkoa. Awali barabara hiyo ilikuwa
ikihudumuwa na wilaya lakini ikipatiwa matengenezo ambayo hayakidhi ongezeko la
magari yanayotumia barabara hiyo kwa sasa.
Mheshimiwa Rais
akiwa njiani kutokea mji wa Masumbwe kupitia makao makuu ya wilaya mpya ya
Mbogwe kabla ya kuingia Geita alisimamishwa mara kadhaa na wananchi wanaoishi
katika vijiji inakopita barabara hiyo ambao walitumia fursa hiyo kuwasilisha
kero zao na hususan suala la barabara ambayo ilielezewa kutokidhi mahitaji
halisi kwa wakazi hao na maeneo jirani.
Akijibu maombi
ya wananchi hao, Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alielezea
kuwa barabara hiyo inayolalamikiwa kwa hivi sasa iko chini ya usimamizi wa
wilaya husika. Hata hivyo, kwa kuzingatia umuhimu wa barabara husika na uchanga
wa wilaya hiyo mpya, alikipokea kilio cha wananchi hao na kukubali barabara
hiyo ipandishwe daraja na kuwa ya mkoa.
“Nitatumia
mamlaka niliyopewa chini ya Sheriaya Mfuko wa Barabara Namba 13 ya mwaka
2007 kuipandisha barabara hii ambayo inaanzia Masumbwe kupitia
Mbogwe, Nyikanga hadi Butengo Lumasa yenye urefu wa kilometa 81 kwamba
itakuwa ya mkoa na hivyo kuwa chini ya usimamizi wa Tanroads” alisemaWaziri
Magufuli.
Aidha,
katika hatua nyingine Mheshimiwa Magufuli alibainisha kuwa katika mipango
ya mwaka ujao wa fedha wa 2014/2015, wizara yake itaanza kufanya upembuzi
yakinifu na usanifu wa kina wa barabara inayotokea mji wa Katoro hadi Ushirombo
yenye urefu wa kilometa 56 ili kuijenga kwa kiwango cha lami.
Naye Mbunge wa
Mbogwe Mheshimiwa Augusto Manyanda Masele kwa upande wake alielezea
kufurahishwa kwake na hatua hiyo na hasa katika kipindi hiki ambacho wilaya
hiyo mpya inahitaji kuimarisha miundombinu mbalimbali kwa lengo la kuharakisha
maendeleo katika eneo hilo.
“Hii imekuwa ni faraja kubwa kwa wana Mbogwe kwani suala la usafiri limekuwa ni kero ya muda mrefu, tunashukuru sana kwa kutembelewa na ugeni huu wa Kitaifa hapa mkoa ni kwetu” alisisitiza Mheshimiwa Masele.
No comments:
Post a Comment