Madiwani na watalaam wa Halmashauri ya Nsimbo wakijadili
mstakabali wa maendeleo ya Halmashauri yao Nsimbo,pamoja na kujadili
masuala ya elimu, Afya, Miundo mbinu ya barabara,utawala,na maengineyo
lakini suala la maji lilichukua nafasi ya kipekee katika kikao hicho cha
baraza la madiwani kilichomalizika mwishoni mwa wiki iiliyo
(Picha zote Kibada Kibada -Nsimbo Mlele Katavi).
Mama akisukuma maji kwenye
kisima kifupi kilichopo hapo huku akina mama wengine na watoto
wakisubiri zamu yao ifike ili waweze kuchota maji ambayo yanatoka
kidogokidogo kwenye kisima hicho hapo madumu yanaonekana hayana maji,
dumu moja kujaa inawachukua zaidi ya saa, hivyo kuwafanya watumie muda
mwingi kutafuta maji badala ya kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
……………………………………………….
Na Kibada Kibada –Nsimbo Mlele
Wakazi wa Songambele Halmashauri
ya Nsimbo Wilayani Mlele wanakabiliwa na Changamoto ya uhaba wa maji
kufuatia visima vifupi vilivyopo kutokuwa maji ya kutosha.
Hali hiyo ya uhaba wa maji kwa
baadhi ya Vijiji vya Kata ya Nsimbo na maeneo mengine ya Halmashauri
hiyo inayowafanya akina mama na watoto kuamka kila siku alfajiri
majira saa kumi usiku kwenda kutafuta maji kwa au kusubiria maji
kwenye visim vifupi vilivyopo ambavyo navyo havitoi maji ya kutosha
hivyo kutumia muda mrefu kutafuta na kukosa muda wa kufanya shughuli
nyingine za maendeleo.
Akizungumzia hali ilivyotete
kuhusu upatikanaji wa maji katika Kijiji cha Songambele na Kata ya
Nsimbo kwa ujumla Afisa Mtendaji wa Kata ya Nsimbo Wilbroad Milala
anasema kwa kweli hapo maji ni shida kubwa kwa wakazi wa hapo.
Milala anasema hata visima
vilivyopo havitoi maji ya kutosha wakati mwingine kama msimu huu wa
kiangazi maji hukata hata miezi miwili bila kutoa maji hali inayofanya
wakazi hao hasa akina mama na watoto kufuata maji kwenye mbuga umbali wa
takribani kilometa tatu hadi nne maji amabyo siyo safi wala salama.
Kufuatia kuwepo kwa changamoto
hiyo ya Maji wawakilishi wa wananchi ambao ni madiwani kupitia kwenye
vikao vya baraza la madiwani suala la maji lilionekana kuchukua nafasi
ya kipekee kuzungumzia ikiwa ni pamoja na kutafuta mbinu za kulipatia
ufumbuzi.
Akiongea katika kikao cha Baraza
la madiwani kwa nyakati tofauti Mjini Nsimbo Diwani wa Kata ya
NsimboMichael Kasanga, Diwani wa Kata ya Mtapenda Eliezer
Fyula,walieleza kuwa lazima hatua zichukuliwe kwa haraka ili kulipatia
ufumbuzi suala la upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Halamshauri hiyo
hasa maeneo yale yenye visima vifupi vichimbwe visima virefu.
Wakaeleza kuwa pia visima
vinapoharibika taarifa iwe inatolewa mapema kwenye Idara ya Maji ili
kuona namna ya kuweza kulipatia ufumbuzi pale panapo wezeakana kama
kununua vifaa vya ukarabati wa pump.
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya
Elimu na Maji Raphael Kalinga akiwasilisha taarifa ya Kamati yake
alieleza mikakati inayochukuliwa na halmashauri ili kukabiliana na
changamoto ya uhaba wa maji ikiwa ni pamoja na kutenga fedha kupitia
bajeti zake na fedha kutoka kwenye mifuko ya maji ili kusaidia
upatikanaji wa maji ikiwa pia na kuomba ufadhili kutoka kwa wahisani
mbalimbali kusaidia suala la maji.
Aidha aliwashauri madiwani
kuwahamasisha wananchi kuanzisha kamati za mifuko ya maji ili fedha
inayopatikana iwe inasaidia katika matengenezo madogo madogo pindi pump
za visima vya maji vinapo haribika fedha hizo zitasaidia ukarabati mdogo
mdogo.
Katika hatua nyingine Baraza la
Madiwani la Halmashauri ya Nsimbo limemwagiza Kaimu Mhandisi wa Mji
katika Halmashauri Enock Msengi kuhakikisha anapoondoka awe anakaimisha
ofisi kwa mwenzake anayekuwa ofisini kuliko kuacha amefunga ofisi na
pia mali za ofisi inatakiwa awe anacha ofisi ikiwa wazi na awe
anaandika barua ya kukabidhi ofisi kuliko kijiondokea kama anavyofanya
kwa kuwa ofisi siyo mali yake bali ni mali ya Serikalai.
No comments:
Post a Comment