Makamu
mkuu wa shule ya sekondari Mukulati ya mkoani arusha mwalimu Vitalisi
Martine akiwakabidhi baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo vitabu vya
sayansi vilivyo tolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakati wa
mahafali ya 17 ya kidato cha nne katika shule hiyo. Meneja
Mauzo wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mkoa wa kilimanjaro
Paschal Bikomagu kushoto akimkabidhi baadhi ya vitabu vya sayansi
kwa Diwani wa kata ya Olkokola Joseph laizer kwa niaba ya shule ya
sekondari Mukulati mkoani arusha wakati wa mahafali ya 17 ya kidato
cha nne ya shule hiyo.
……………………………………………………………….
Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel imeedelea kuungana na serikali katika kusaidia kuboresha
maendeleo ya sekta ya elimu nchini ambapo imetoa vitabu vya ziada na
kiada katika masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari mukulati wilayani
Arumeru mkoani Arusha
Licha ya Kada ya sayansi kuwa ndio
chimbuko kubwa la wataalamu wengi katika fani mbalimbali bado
inatajwa kutofanya vizuri kutokana na uhaba wa miundombinu na vifaa
stahiki ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya kada hiyo.
Meneja wa Airtel mkoa wa
Kilimanjaro Paschal Mikomagu akizungumzia mchango wa kampuni hiyo
wakati wa mahafali ya 17 ya shule ya sekondari mukulati amesema Airtel
kwa kutambua changamoto mbalimbali ndani ya kada ya sayansi nchini
ikiwemo uhaba wa vitabu vya kujifunzia imeamua kuwa na utaratibu wa
kugawa vitabu hivyo. Leo tumehudhuria mahafali na kuchangia kutatua
moja ya kero zinazokumba sekta ya elimu na tuaamini kwa msaada huu wa
vitabu vitaongeza ufaulu wa wanafunzi na kusaidia shule kufanya vizuri
kitaaluma
Tutaendelea kutimiza dhamira yetu
kwa vitengo ya kusaidia kutatua changamoto mbalimbali mashuleni na
kuhakikisha tunaboresha uwiano wa vitabu kwa wanafunzi hadi kitabu
kimoja kwa mtoto moja au wawili.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya
Olkokola Joseph laizer leo ni sisi Airtel imetoa msaada huu wa vitabu
ambavyo vitasaidia shule hapa , lakini zaidi tunawaomba Airtel waendelee
kujitolea kushirikiana nasi na kutufadhili katika ujenzi wa maabara
katika shule hii ili kuweza kufikia malengo tuliyowekewa ya kuhakikisha
kila shule ya sekondari inajenga maabara kwa ajili ya mafunzo ya ziada
Akiongea mara baada ya kupokea
vitabu hivyo MkeeVitalisi Martine mkuu wa shule kwa msaada huu
umeongeza uwiano wa vitabu shule hapa ambapo kwa sasa kitabu kimoja
kitatatumika na wanafunzi wawili, napenda kuwhakikishia vitabu hivi
havitakaa kwenye kabati bali vitatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa ili
atimaye watoto waweze kupata ujuzi kupitia vitabu hivi
Nao baadhi ya wanafunzi walito
maoni yao kuhusu mchango huu shule ni hapo ambapo Happy Lyimo alisema
natoa shukurani za dhati kwa niaba ya wanafunzi wenzangu kwa Airtel kwa
kutupatia mchango wa vitabu vingi vya sayansi. Nimatumaini yangu kuwa
vitabu hivi vitasaidia kuinua taaluma kwa wanafunzi na shule kwa
ujumla.
No comments:
Post a Comment