DEREVA MMOJA KATI YA WAWILI AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA
JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 25 – 30
AMEFARIKI DUNIA BAADA YA MAGARI YA ABIRIA WALIYOKUWA WAKIENDESHA YENYE
NAMBA ZA USAJILI T.473 CNT AINA YA TOYOTA HIACE NA GARI T.135 AJF AINA
YA TOYOTA HIACE KUGONGANA USO KWA USO ENEO LA MWISHO WA WAYA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE
22.10.2014 MAJIRA YA SAA 22:20 USIKU HUKO MAENEO YA MWISHO WA WAYA, KATA
YA IYUNGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA
MBEYA/TUNDUMA.
AIDHA, WATU WATATU WALIJERUHIWA
KATIKA AJALI HIYO AMBAO NI 1. LAMECK LIMO 2. ANGOLISYE MWAKALOBO NA 3.
JOYCE ASAJILE AMBAO WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA
MATIBABU.
CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA
MKAZI WA MKWAJUNI WILAYA YA CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PRISCA
SINKALA (31) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA
POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 05.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
22.10.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAJENGO,
KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA
MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AITWAYE ISAYA DARON (27)
MKAZI WA SOWETO AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU AINA
YA BOSS PAKETI 30.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
22.10.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO SOWETO, KATA YA RUANDA,
TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE
HIZO.
KATIKA MSAKO WA TATU, MTU MMOJA MKAZI WA AIRPORT JIJINI MBEYA
AITWAYE SALEHE SEKILE (32) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
AKIWA NA KETE 12 ZA BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAMU 60.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO
ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 22.10.2014 MAJIRA YA SAA 17:30 JIONI HUKO
MAENEO YA FOREST MPYA, KATA YA FOREST, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA
MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUTWA NA KETE HIZO BAADA YA KUPEKULIWA KWENYE
MIFUKO YAKE YA SURUALI. AIDHA, MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA
BHANGI HIYO.
KATIKA MSAKO WA NNE, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKAZI WA MANGA JIJINI MBEYA AMBAO NI 1. TERESIA MWAISAKILE (31) NA 2. ELIZABETH LONDELE (29) WAKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 01.
WATUHUMIWA KWA PAMOJA WALIKAMATWA
KATIKA MSAKO ULIENDESHWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA MNAMO TAREHE
22.10.2014 MAJIRA YA SAA 13:30 MCHANA HUKO MAENEO YA MANGA, KATA YA
MANGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI WA
POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA/POMBE YA MOSHI PAMOJA NA POMBE KALI
ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA, ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA
MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UINGIZAJI/USAMBAZAJI NA UUZAJI WA POMBE KALI
NA POMBE YA MOSHI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI
YAO.
Imesainiwa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment