TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, June 22, 2016

KAMISHNA MSTAAFU SULEIMAN KOVA AAGWA RASMI KIJESHI BAADA YA KUSTAAFU



Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akipunga mkono kwa Maofisa, wakaguzi, Askari na wageni mbalimbali waliohudhururia sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi .


Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi.
Maofisa wa Polisi wakisukuma gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova kutoka katika viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi wakati wa sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki.

Gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova likipita katika ya gwaride ikiwa ni ishara ya kumuaga zilizofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi nakuongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki .
Gwaride Maalumu la Kumuaga Kamishna Mstaafu Suleiman Kova likipita mbele yake kwa mwendo wa haraka wakati wa Sherehe za kumuaga rasmi baada ya kustaafu utumishi.Sherehe hizo zilifanyika katika chuo cha Polisi Moshi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Gwaride Maalumu la Kumuaga Kamishna Mstaafu Suleiman Kova likipita mbele yake kwa mwendo wa haraka wakati wa Sherehe za kumuaga rasmi baada ya kustaafu utumishi.Sherehe hizo zilifanyika katika chuo cha Polisi Moshi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
======================================


PROF. MAKAME MBARAWA AZINDUA BODI YA TPA






TPA5

TPA6
===============================================


Mkurugenzi Muhimbili Akutana na Madaktari, Aongeza Posho


MSE1

Dk Saidia Primos wa hospitali hiyo akiuliza swali kwenye mkutano huo. MSE4Mkurugenzi wa Fedha, Gerald Kimambo (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario kwenye mkutano huo LEO.










=================================================



Magari yanayoingizwa kwa msamaha wa kodi kuwa na namba na rangi maalum


Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

22/06/2016

Katika kuthibiti matumizi ya magari yanayoingia Nchini kwa msamaha wa kodi Serikali imesema kuanzia Julai Mosi magari hayo sasa yatakuwa na namba na rangi maalum.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu tamko la kuondoa misamaha ya kodi kwenye taasisi za dini kwa kuwa zinatoa huduma za kijamii kama shule na hospitali.

“Kwa kutambuua mchango mkubwa wa Taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu na afya, napendekeza kufuta utaratibu niliotangaza katika hotuba ya bajeti na badala yake Serikali itaimarisha zaidi hatua mbalimbali za uthibiti misamaha ya kodi ikiwemo magari yaliyoingia kwa msamaha wa kodi kuwa na namba na rangi maalum,” alifafanua Mhe.Dkt. Mpango.

Aliendelea kutaja hatua nyingine kuwa ni taasisi za kidini kuwasilisha vifaa vinavyotarajiwa kununuliwa kutoka nje ya nchi kila mwazo mwa mwaka wa kalenda na kuthibitisha kama vifaa vilivyopewa msamaha mwaka uliopita vilitumika kama sheria inavyotaka.

Pia, kuwasilisha majina ya watu walioidhinishwa na Shirika au Taasisi kuandika barua ya kuomba msamaha wa kodi, wakiainisha cheo, saini, picha, anwani na namba zao za simu ili kuiwezesha Mamlaka ya Mapato Tanzania kufuatilia bidhaa zilizoombewa na kupewa msamaha kama zimepata kibali cha taasisi hizo.

Vile vile taasisi hizo zinatakiwa kupata barua kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Serikali ya Mtaa na Mkuu wa Wilaya mahali Taasisi au Mradi unaotekelezwa ulipo. Mhe. Mpango amesema kuwa hatua hizo zimekuja kutokana na bidhaa zinazoombewa msamaha wa kodi kutumika tofauti na kusudi la msamaha huo.

Aidha ametoa tahadhari kwa mashirika ya kidini kuanzia sasa, kuhakikisha kuwa yanafuata taratibu zote na Kuzingatia masharti ya msamaha unaotolewa ili kuepuka kufutiwa leseni zao pale zitakapokwenda kinyume na sheria na kanuni zilizowekwa.
=================================================




Wakala ya serikali mtandao kufanya ziara ya kutembelea taasisi za serikali.


Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano toka Wakala wa Serikali Mtandao Bi Suzan Mshakangoto akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa taasisi yake kutembelea wateja wake ambao ni taasisi za Umma ikiwa ni sehemu ya maadhimishi ya wiki ya Utumishi wa Umma.
Na Eliphace Marwa - Maelezo

Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) imeandaa utaratibu wa kutembelea wateja wake ambao ni taasisi za umma ili kusikiliza na kutatua changamoto zinazo tokana na huduma wanazotoa,huduma hizo ni pamoja na mfumo wa barua pepe unaorahisisha mawasiliano serikalini.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wataasisi hiyo Bi Suzan Mshakangoto, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mapema hii leo jijini Dar es Salam na kutaja baadhi ya taasisi 34 zitakazoanza kutembelewa kuanzia tarehe 22 Juni hadi Juni 23.

Alizitaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni pamoja na Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, vijana, Ajira na Walemavu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi, Wizara ya Habari,utamaduni Sanaa na Michezo, Wizara ya kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.

Aidha aliongeza kuwa huduma nyingine zinazotolewa na wakala wa serikali ni pamoja na uhifadhi wa mifumo ya tovuti za serikalini, utoaji huduma za simu za mikononi, Uratibu wa mitandao serikalini, Ugawaji wa masafa ya internet, huduma za ujumbe mfupi wa maandishi (sms) pamoja na utengenezaji wa mifumo ya tovuti na usajili anuani za tovuti.

Hiyo ni kutimiza Agizo la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Angela Kairuki la kutaka kila Wizara, wakala na Taasisi za Serikali katika kipindi cha Wiki ya Utumishi wa Umma kukutana na wateja wao na kusikiliza kero walizonazo ili kuweza kuzipatia ufumbuzi, aidha kauli mbiu ya mwaka huu ni, “Uongozi wa Umma kwa Ukuaji jumuishi kuelekea katika Afrika tunayoitaka”.

Kila taasisi itatembelewa na wataalam wawili wa wakala wa serikali watakao sikiliza maoni na kutoa msaada wa kiufundi na ushauri wa kitaalamu katika kutatua changamoto mbali mbali zinazojitokeza juu ya huduma mbali mbali zinazotolewa na wakala. 
==========================================


Wizara ya Ardhi kubaini taasisi zinazodaiwa fidia na wananchi

Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 itabaini taasisi zote na watu binafsi wanaodaiwa fidia na wananchi ili waweze kulipa fidia hizo.

Akiongea leo Bungeni, mjini Dodoma Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Angelina Mabula amesema kuwa ni kweli tatizo hilo lipo na tayari Serikali imechukua hatua kwa kuzielekeza Halmashauri zote na taasisi nyingine kulipa fidia stahiki kwa wananchi pale wanapotaka kutwaa maeneo yao.

Mhe. Mabula amesema kuwa taasisi nyingi zimekuwa zikichukua mashamba ya wananchi na kushindwa kuwalipa fidia hivyo kulimbikiza madeni hayo kwa muda mrefu hali inayokwamisha shughuli za maendeleo.

“Halmashauri za Wilaya, Taasisi na Maafisa Ardhi hawaruhusiwi kuchukua mashamba ya wananchi kabla hawajakamilisha utaratibu wa malipo ya fidia kwa wananchi hao, ili kuondokana na malimbikizo ya madeni ya fidia ambayo malipo yake huchukua muda mrefu na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi,” alisema Mhe. Mabula.

Aidha Mhe. Mabula amewataka wananchi wanaodai fidia kuwa wavumilivu wakati Wizara yake inaendelea kufanya upembuzi wa taasisi hizo ili ziweze kulipa fidia zote zinazodaiwa na wananchi.

Vilevile Wizara hiyo imetoa ramani za mitaa kwa wenyeviti wa mitaa wa Jiji la Dar es Salaam ili wenyeviti hao waweze kutambua matumizi ya maeneo yao, kwa mfano maeneo ya wazi, na nini kijengwe katika maeneo yao kama vile nyumba fupi au ndefu, hoteli au chuo ili kuondokana na migogoro ya kubolewa nyumba kwa kujenga eneo lisiloruhusiwa.

“Tumeanza kwa mkoa wa Dar es Salaam lakini zoezi litaendelea kila Mkoa na kila Wilaya Nchi nzima, ili Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji waweze kutambua matumizi ya maeneo yao, hivyo kuchukua hatua kwa haraka pindi ambapo maeneo hayo yanatumika tofauti na matumizi yaliyoko” alifafanua Mhe. Mabula.

Aidha Mhe. Mabula amezitaka Halmashauri kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba, na Maendeleo ya Makazi kuwapa uwezo wenyeviti hao ili waweze kufanya kazi hiyo kiufanisi.
==============================================



Serikali yapokea msaada wa madawati 300 toka Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania.



Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) akikabidhi msaada wa madawati kwa Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima mapemahii leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) pamoja na Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (kulia) wakiwa wamekalia madawati ambayo yametolewa msaada kwa serikali ya Tanzania, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (Katikati aliyekaa) kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem na kulia ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi na Wakurugenzi toka wizara hiyo mara baada ya kupokea msaada wa madawati toka ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam. 


Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akikabdhi msaada wa madawati kwa Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga akitoa neno la shukrani kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem wakati akipokea msaada wa madawati toka kwa balozi huyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo

———————————————————————–

Na Eliphace Marwa- Maelezo

Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa madawati 300 toka Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya kutatua tatizo la uhaba wa madawati katika shule za msingi hapa nchini.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga kwa niaba ya serikali alisema kuwa amesema kuwa kupokea madawati hayo ni sehemu ya kutekeleza wito wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

“Waziri Mkuu alitutaka sisi katika nafasi zetu tuwashirikishe wadau mbalimbali ili kuweza kutekeleza adhma ya serikali ya kutatua tatizo la wanafunzi kukaa chini ili waweze kupata mazingira bora ya kupata elimu, alisema Balozi Maige.

Balozi Maigaaliongeza kuwa Kuwait iko tayari kuisaidia nchi ya Tanzania kwa kuwajengea uwezo wataalam toka Tanzania kwa kuwapa elimu ya mafuta na gesi kwani Kuwait ina uzoefu mkubwa katika sekta ya mafuta na gesi.

Naye Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem alisema kuwa Serikali ya Kuwait itaendelea kutoa misaada kwa serikali ya Tanzania kadri itakavyowezekana pindi pale itakapohitajika.

Aidha Balozi Maiga alitumia muda huo kutoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu ujio wa Rais wa Rwanda Paul Kagame hapa nchini siku ya Julai Mosi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi.

“Rais wa Rwanda atawasili hapa nchini Julai Mosi na ataweka saini makubaliano mbalimbali waliyofikia kati ya Tanzania na Rwanda baada ya hapo Rais Kagame ataambatana na mwenyeji wake Rais Magufuli mpaka katika viwanja vya maonesho vya Sabasaba ambapo Rais Kagame atayazindua rasmi maonesho hayo ya arobaini”, alisema Balozi Maiga.

Aidha Balozi Maiga aliongeza kuwa Rais Kagame jioni atakaribishwa Ikulu na mwenyeji wake Rais Magufuli kwa ajili ya dhifa ya kitaifa.
================================================





WAZIRI WA AFYA , MAENDELEO YA JAMII , JINSIA, WAZEE NA WATOTO ATEMBELEA VIJIJI VILIVYOKUMBWA NA MLIPUKO WA UGONJWA USIOJULIKANA WILAYANI KONDOA.








====================================

WLAC WAENDELEA KULILIA SHERIA KANDAMIZI KWA WANAWAKE NA WAJANE


Mkurugenzi mtendaji wa WKAC Tanzania Bi THEODOSIA NUHULO akiizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu maswala mbalimbali yanayohusu ukandamizwaji wa wanawake hususani wajane nchini Tanzania ikiwemo sheria kandamizi ya mirati ya kimila nchini sheria ambayo imetajwa kuwaumiza wajane wengi .PICHA ZOTE NA EXAUD MTEI MSAKA HABARI

Na Exaud Mtei

Serikali ya Tanzania imetakiwa kufanya marekebisho makubwa ya sheria ya mirathi ya kimila sheria ambayo imetajwa kuwa ni kandamizi na inawanyima haki wanawake na wasichana ikiwa ni utekelezaji wa mkataba wa CEDAW ambao nchi imesaini mwaka 1986 ambapo ulikuwa unawaelekeza wanachama kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake katika ngazi za kisiasa,kiuchumi,na kijamii ili kuletwa usawa.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na kikosi kazi cha kamati ya mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake CEDAW ambacho kinaundwa na mashirika tisa yanayotetea haki za wanawake Tanzania kwa namna mbalimbali.

Akizungumza kwa niaba ya mashirika hayo yote mkurugenzi mtendaji wa kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake WLAC ambao wameyaongoza mashirika hayo katika tamko hilo Bi Theodosia Nuhulo ameeleza kuwa mnamo mwaka 2005 WLAC kwa kushirikana na wadau wengine watetezi wa haki za wanawake walifungua kesi mkakati katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam kupinga vipengele kandamizi katika sheria hiyo ya mirathi (Tamko la Mirathi la kimila) la mwaka 1963 lakini mnamo mwaka 2006 ilitupilia mbali kesi hiyo huku ikitamka wazi kuwa vifungu vilivyolalamikiwa ni vya kibaguzi kweli lakini haiwezi kufanya mabadiliko ya kimila katika tamko la kisheria.
Mkurugenzi wa umOja wa wajane nchi i Tanzania ROSE SARWAT akizngumza na wanahabari wakati Tanzania ikiingia kuadhimisha siku ya wajene nchini ambapo amewataka wajene na watanzania kujitokeza kwa wiingi kesho katika viwanja vya mnazi mmoja kuadhimisha siku hiyo ili kupata Fursa ya kujadili kwa pamoja kuhusu haki zao hususani sjheria hiyo kandamizi kwa wajane.

Ameeleza kuwa WLAC kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walifanya jitihada zote za kukata Rufaa dhidi ya uamuzi huo lakini mnamo 2010 rufaa hiyo ilitupiliwa mbali tena kwa kigezo kwamba uamuzi na amri iliyotolewa na mahakama kuu ilikuwa na tarehe mbili Tofauti yani tarehe 8/9/2006 na tarehe 7/12/2006.

Amesema kuwa baada ya jitihada zote hizo kugonga mwamba juu ya sheria hiyo kandamizi ameeleza kuwa serikali ya Tanzania kuzingatia ukubwa wa swala hilo kufanya marekebisho ya haraka kwani ndio chanzo kikubwa cha wanawake wajane nchini Tanzania kushindwa kupata haki zao za msingi zikiwemo za mirathi baada ya vifo vya wenzi wao.
Mkutano huo ukiendelea

Bi Theodosia ameendelea kusema kuwa pamoja na jitihada nyingi mbalimbali zinazofanywa na WLAC na wadau mbalimbali watetezi wa haki za wanawake bado serikali haijaonyesha jitihada za maksudi za kutekeleza Taarifa /maamuzi ya kamati ya mkataba wa CEDAW kuhusu sheria ya miradhi ya kimila na hali ya wajane Tanzania ili kuhakikisha kwamba wajane wanapata haki zao.

Aidha WLAC wameitaka serikali ya Tanzania kuwajengea uwezo majaji na waendesha mastaka na watumishi wa mahakama na wanasheria kuhusu mkataba wa CEDAW na umuhimu kwa kuzingatia haki za binadamu katika maamuzi yao.

No comments:

Post a Comment