TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, June 20, 2016

WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI LEO.

Mkutano wa Magavana unaosimamiwa na Taasisi ya Usimamizi wa Fedha na Uchumi kutoka (MEFMI).

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Serikali imesema itaendelea kufanya biashara na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia fursa zilizopo nchini ikiwemo uwekezaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Beno Ndulu alipokuwa akifungua mkutano wa Magavana na Manaibu Gavana kutoka nchi 14 za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaosimamiwa na Taasisi ya Usimamizi wa Fedha na Uchumi kutoka (MEFMI).

“Tanzania imeanza miaka 2 hadi 3 kujiwekea akiba ya sarafu ya Yuan ya nchini China kutokana biashara mbalimbali ambapo hadi sasa nchi ina akiba ya asilimia 5 za fedha ya China Yuan” alisema Profesa Ndulu.

Hatua hiyo ya Tanzania inafuatia Sarafu ya China ijulikanayo kama Yuan kuingizwa kuwa miongoni mwa sarafu sita zinazotumika Duniani.

Mkutano huo unafuatia majumu ya Benki Kuu hizo za nchi wanachama kuwa na jukumu la kuwa walinzi wa akiba ya fedha za kigeni na wawezeshaji wa masuala ya biashara za kimataifa.

Maweneo ambayo Tanzania inayatumia kama njia moja wapo ya kujiongezea sarafu ya China ni pamoja na uwekezaji katika hati fungani inafaida zaidi ikilinganishwa na nchi za Ulaya na nchi nyingine duniani.

Profesa Ndulu alizitaja sarafu nyingine ambazo zinatumika duniani zinazotambuliwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ni pamoja na Dola ya Marekani, Euro inayotumiwa na nchi za Ulaya, Swiss Frank ya Uswiss, Paund ya Uingereza, Yen ya Japani pamoja na Yuan ambayo itaanza kutumika kimataifa kuanzia mwezi Septemba 2016.

Mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na China ni ya kihistoria yanayohusisha Serikali za nchi hizo mbili ambao ulijengwa kwa msingi imara wa Waasisi wa mataifa hayo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Muasisi wa Taifa la China Mwenyekiti Mao Tse Tung.

Mkutano wa huo wa MEFMI unatoa fursa ya kipekee kubadilishana mawazo kwa viongozi hao juu ya ushirikishwaji wa Yuan Kichina ndani ya kikapu cha hifadhi ya sarafu ya IMF / Benki ya Dunia katika nchi wanachama wa MEFMI.

Kufanyika kwa mkutano huo ni moja matukio ya kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yanayotarajiwa kutahudhuriwa na Wachumi waliobobea wa ndani na nje ya nchi, wakiwemo magavana 20 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). 
==============================================

Bilioni 2.5 kuanza kujenga hospitali ya Wilaya ya Morogoro








=====================================================

Milioni 200 kupanua mfumo wa maji safi Kasulu

Na: Lilian Lundo – Maelezo – Dodoma


Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imetenga jumla ya shilingi milioni 200 katika bajeti ya Mwaka 2016/2017 ili kupanua mfumo wa maji safi katika Mji wa Kasulu.

Hayo yamesemwa leo, Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kasulu Mhe. Daniel Nswanzugwako juu ya ukabarati wa vyanzo vya maji vilivyopo Mjini Kasulu ili maji yafike katika mitaa ya kata za Mrusi, Mwilavya na Kidyama.

“Serikali inatambua changamoto ya mtandao wa maji inayoukabili Mji wa Kasulu, katika mwaka wa fedha 2016/17 imetenga Milioni 200 kwa ajili ya kupanua mfumo wa maji safi katika mji huo,” alisema Mhe. Kamwelwe

Aidha, Mhe. Kamwelwe aliendelea kwa kusema kuwa, fedha hizo zitatumika katika kuboresha hali ya huduma ya maji ikiwemo kuongeza mtandao wa maji Mjini Kasulu ambapo pia kata za Mrusi, Mwilavya na Kidyama zitapata huduma ya maji safi na salama.
=============================================

SERIKALI YAASWA KUPIGA VITA DHIDI YA UKATILI NA UNYANYAPAA DHIDI YA WATU WENYE UALBINO.

 Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za watu wenye ualbino, Ikpowose Ero, akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana juu ya maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa watu wenye ualbino Afrika uliofanyika nchini hivi karibuni, Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa UN, Alvaro Rodrigers na Mkurugenzi mkazi wa Under the same  Sun.







========================================

Mangula azindua Kitabu cha “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es salaam


Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akizindua Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Bi. Deborah Charles, Agusto Matefu, Mwenyekiti wa Kamati ya Mijadala na Kongamano ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na wa mwisho kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Kampeni hiyo inalengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akionyesha Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua mara baada ya kukizindua leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Amosi Siyantemi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Majipu ya Nchi yetu “ Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na kushoto Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi wa Kitabu cha Majipu ya Nchi Yetu “Tushirikiane kuyatumbua” leo jijini jijini Dar es Salaam. Kitabu hiko kimezinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula (hayupo pichani).Uzinduzi wa Kitabu hicho umeenda sambamba na utambulisho wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM). Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.

Picha zote na: Frank Shija, MAELEZO
==================================================

SERIKALI YAONYA MATUMIZI MABAYA YA VYANDARUA.


Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akionyesha kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 kwa wadau wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es salaam.

Wadau mbalimbali wa takwimu wakifauatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya hayupo pichani wakati wa kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akikata utepe kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na wadau mbalimbali wa takwimu hawapo pichani wakati wa kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam. Picha zote na Ally Daud-maelezo.
Na Ally Daud-Maelezo

SERIKALI imetoa wito kwa wananchi kuacha matumizi mabaya ya vyandarua ili kusaidia jitihada za Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini.Akizungumza leo Jijini Dar es salaam katika Uzinduzi wa Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya wananchi kutumia vyandarua wanavyopewa na Serikali kwa matumizi yasiyo sahihi kama kuvulia samaki, kuwekea wigo mifugo na kuzungushia wigo bustani.

‘‘Watu wengi wamekuwa wakitumia vyandarua vinavyotolewa na Serikali kwa matumizi yasiyo sahihi badala ya kujikinga na Mbu waenezao malaria. Hii ni kutokana na utafiti huu kuonyesha kuwa asilimia 14 ya watoto wa chini ya miaka 5 ambao walipimwa Malaria kwa kutumia kipimo cha kutoa matokeo kwa haraka yaani Rapid Diagnostic Tests (RDT) walikuwa na Malaria,” amesema Dkt. Ulisubisya.

Aidha amesema kuwa kiwango cha maambukizi ya Malaria bado ni kikubwa ikilinganishwa na kiwango kilichopatikana wakati wa Utafiti wa UKIMWI na Malaria wa Mwaka 2011-12 hivyo ni vyema jamii ikaendelea kupambana na ugonjwa huu kwani bado ni tishio kwa watoto na Wananchi kwa ujumla.Dkt.

Ulisubisya amesema kuzinduliwa kwa Matokeo haya kutasaidia Serikali kuboresha huduma za afya kwa kuyafanyia marekebisho mapungufu yaliyopo katika utoaji wa huduma za malaria nchini.Akizungmzia huduma za afya kwa akinamama wajawazito, Dkt. Ulisubisya amesema utafiti umeonyesha kuwa kiwango cha akina mama wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya, kutoka asilimia 51 mwaka 2010 kufikia asilimia 60 mwaka 2015 na kuongezeka kwa kiwango cha akina mama wanaosaidiwa na wataalam waliosomea wakati wa kujifungua kutoka asilimia 50 kufikia asilimia 60 mwaka 20015/16.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Kitakwimu, Mr. Irenius Ruyobya amesema kuwa utafiti huu ni wa muhimu sana katika kuboresha huduma za afya hasa katika kupambana na Malaria.

Amesema ili Serikali iweze kuboresha huduma za afya na kupambana na Malaria, takwimu hizi ambazo zimezinduliwa leo zitasaidia Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa afya katika kupanga, kutekeleza na kupima utekelezaji wa miradi mbalimbali ya afya nchini.Mr. Ruyobya amesema utafiti huu ni wa sita kufanyika nchini ambapo kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka 1991 na kufuatiwa na utafiti wa mwaka 1996, 1999, 2004/5 na 2010. 
===================================================

TUSKER FANYA KWELI UWINI YATOA MILLION 20 KWA WASHINDI 20 WIKI HII









=========================================
===================================================

Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino


Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino Pamoja na juhudi ambazo serikali imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha Watanzania wenye ualbino wanakuwa salama na amani lakini bado Tanzania inaendelea kuwa nchi ya hatari kwa watu hao kwa kuwa katika orodha ya nchi ambazo zina kiwango kikubwa cha unyanyasaji.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha kongamano la kikanda kwa ajili ya hatua kuhusu ulemavu wa ngozi Afrika lililofanyika Dar es Salaam, Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero alisema kuwa kwa ripoti ambazo wamekuwa wakizipokea inaonyesha Tanzania ni moja ya nchi ambazo zina unyanyasaji kwa watu wenye ualbino.

"Tangu nimeingia sijawahi kufanya uchunguzi hata katika matokeo ya uchunguzi wa nchi 29 sijaujua sana lakini kwa taarifa ambazo nimekuwa nikipata kutoka kwa taasisi mbalimbali inaonyesha Tanzania ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa watu walio na uablino," alisema Ero.
==================================================

WABUNGE WAJADILI MAREKEBISHO YA SHERIA MPYA YA UNUNUZI WA UMMA, DODOMA

lik11
==============================================

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA KITUO CHA UHAMIAJI HOLILI


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), akikagua mzigo wa John Evarist ambaye ni mfanyabiashara aliyekua akipita kutoka nchini Kenya kupitia mpaka uliopo katika kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yuko mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Mfanyabiashara John Evarist aliyekua akipita kutoka nchini Kenya kupitia mpaka uliopo katika kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro, akijibu maswali aliyoulizwa na Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea(wa kwanza kushoto).Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira aliyepo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea ( aliyenyoosha mkono), akimuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), mwisho wa mpaka unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya wakati wa ziara ya Katibu Mkuu kukagua njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.Wa pili kushoto ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, RPC Wilbrod Mutafungwa
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), akipanda Mlima kwenda kukagua jiwe linalotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya katika Mpaka uliopo eneo la Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
====================================================

MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILEMELA MKOANI MWANZA AKABIDHI MADAWATI KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI.


Madawati hayo ambayo yametengenezwa kwenye karakana ya shule ya sekondari ya wavulana ya Bwiru, ni sehemu ya mpango wa kutengeneza madawati 9,080 na hivyo kumaliza kabisa tatizo la uhaba wa madawati katika manispaa hiyo.

Akikabidhi madawati hayo hii leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga, amesema madawati hayo yametengenezwa kutokana na fedha zitokanazo na makusanyo ya ndani pamoja na michango ya wadau wengine ambapo katika mgawo wa awali, kata zote 19 za manispaa hiyo zimepewa madawati 139 kila moja.

Wanga amesema kila dawati moja lenye uwezo wa kukaliwa na wanafunzi watatu, limegharimu shilingi 98,000 ambapo manispaa ilinunua vifaa ikiwemo mbao, misumari na vyuma na kulipa gharama za ufundi zinazofikia shilingi 15,000 kwa kila dawati na kwamba madawati mengine yaliyobakia kukidhi mahitaji yanaendelea kutengenezwa kwenye karakana hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Manju Msambya, amepiga marufuku matumizi ya madawati hayo kwenye shughuli nyingine ikiwemo mikutano ya kisiasa huku akiwataka wazazi,walezi na jamii nzima kwa ujumla kutambua umuhimu wa kuchangia juhudi za kuboresha elimu.

Renatus Mulunga ambae ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela amesema halmashauri hiyo inafanya kila jitihada kuhakikisha kwamba inatatua tatizo la upungufu wa madawati kwa shule za msingi katika manispaa hiyo, hatua ambayo itasaidia kuboresha ari ya wanafunzi kujisomea.
Utengenezaji wa Madawati ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, ukiendelea katika karakana ya Shule ya Sekondari ya wavulana Bwiru.

==============================================

Airtel na VETA yapeleka VSOMO DODOMA.








No comments:

Post a Comment