Kituo hicho cha kwanza kuanzishwa na Jeshi la Polisi hapa nchini kipo
katika kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam na kinafanya
kazi kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya simu na mfumo wa utambuzi
wa eneo (GPS) ambapo askari polisi waliopo katika kituo cha mawasiliano
watakuwa wakipokea simu kutoka kwa wananchi wanaotoa taarifa za matukio
ya uhalifu na kisha kuwaelekeza askari walio jirani ili wafike eneo la
tukio na kukabiliana na wahalifu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali (IGP) Ernest Mangu
amemueleza Rais Magufuli kuwa kituo hicho kina uwezo wa kupokea simu 18
kwa mpigo kutoka kwa watu wanaopiga simu ya bure namba 111 au 112 kwa
ajili ya kutoa taarifa za uhalifu na kwamba lengo la jeshi hilo ni
kuhakikisha askari wanafika eneo la tukio ndani ya dakika 15.
IGP Mangu ameongeza kuwa kituo hicho kimeanzishwa kwa msaada kutoka
benki ya CRDB iliyotoa shilingi milioni 320, kitaanza kutoa huduma
tarehe 01 Julai, 2016 kikianzia katika mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni
Kanda maalum ya Dar es salaam na polisi imejiwekea malengo ya kuwa na
vituo kama hivyo nchi nzima ifikapo mwaka 2019.
Akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho, Rais Magufuli amelipongeza
Jeshi la Polisi kwa kuanzisha mradi huo na ameahidi kuwa serikali
itahakikisha inaunga mkono mpango huo ikiwa ni pamoja na kulifanyia kazi
ombi la kununuliwa helkopta itakayorahisisha zaidi ufikaji eneo la
tukio.
Aidha, Rais Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kuwanyang’anya silaha
wahalifu kabla hawajawadhuru raia na kupora mali zao ama kusababisha
mauaji, na amewataka viongozi wa jeshi hilo kuwazawadia askari
wanaofanya kazi nzuri ya kupambana na wahalifu.
Dkt. Magufuli pia ametaka jeshi la polisi lisimame imara kuhakikisha
serikali inatekeleza ahadi zake kwa wananchi zikiwemo upatikanaji wa
maji na huduma nyingine za kijamii na kwamba hatarajii kuona mtu yeyote
anafanya vitendo vitakavyosababisha ahadi hizo kutotekelezwa.
Katika hatua nyingine, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir
Ali amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kuiongoza nchi.
Mufti Mkuu Sheikh Aboubakar Zubeir Ali ametoa pongezi hizo jana jioni
tarehe 24 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam katika futari
iliyoandaliwa na Rais Magufuli na akatumia nafasi hiyo kuwasihi Waislamu
na watanzania wote kwa ujumla kukataa vitendo vinavyoashiria uvunjifu
wa amani.
“Niwahusie ndugu zangu watanzania wote, kwamba amani ni kitu muhimu
tuitunze amani tuliyokuwa nayo, tuienzi amani tuliyonayo, na hapo
tutakuwa tunaisadia serikali na tutakuwa tunamsadia Mhe. Rais katika
kuilinda amani” Amesema Mufti Mkuu.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
25 Juni, 2016.
===================================================
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ashiriki kampeni ya Media Car Wash mjini Dodoma leo
Naibu
Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameshiriki harambee ya kuchangia waandishi
wa habari kwa ajili ya kuwakatia Bima ya Afya “Media Car Wash For
Health” iliyofanyika leo katika viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma ambapo
amechangia jumla ya shilingi milioni 5 ili kuokoa maisha ya waandishi wa
habari.
“Kuna
umuhimu mkubwa wa kuwachangia waandishi wa habari kwani wamekuwa na
mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya nchi na kuhamasisha amani ya
nchi, kwa kutambua umuhimu wao nitachangia shilingi 5,000,000 ili iweze
kuwakatia Bima ya Afya,” alisema Mhe.Dkt. Tulia.
Licha ya kuchangia fedha hizo Mhe. Tulia aliosha baadhi ya magari ya waheshimiwa wabunge kwa ajili ya kuchangia harambee hiyo ambapo kila mbunge aliyeoshewa gari yake alichangia shilingi 100,000 ambazo moja kwa moja ziliingia katika mfuko wa kuokoa maisha ya waandishi wa habari kwa kuwakatia Bima ya Afya.

Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendelea ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla amechangia shilingi 1,000,000/= ambayo
nayo inaenda kusaidia waandishi wa habari ili waweze kukatiwa Bima ya
Afya.
Mwenyekiti
wa Bunge Sports, William Ngeleja (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza
kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari
‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF), Athuman Rehani.
Msanii
wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel na Mkongwe wa Bongo Fleva Inspector Haroun
wakiosha moja ya magari yaliofika kuoshwa kwa ajili ya harambee ya
kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari
‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili
ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini.
====================================
====================================
TRA yazidi kuboresha timu ya kutoa elimu ya kodi, yazindua Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi IFM
================================================
MGAHAWA WA KIPEKEE WA PWEZA WAZINDULIWA JIJINI DAR
Akiongea
na mwanidishi wetu, mmoja wa wamiliki wa mgahawa huo bwana Alfred
Kiwuyo alisema, "Sisi wenyewe ni wapenzi wa supu na nyama ya pweza,
kamba (prawns) na ngisi lakini mazingira ya awali ya kuuza vyakula hivi
kwenye vituo vya daladala na makutano ya barabara kadhaa hapa jijini
yalikuwa yanatukatisha tamaa hasa ukizingatia usafi na mapishi yenyewe
haukuwa wa kuridhisha sana.
Sasa tukajiuliza swali je, haiwezekani kuwa na sehemu ya kisasa zaidi ya kuuza pweza, ngisi na kamba (prawns) na kukawa na mapishi zaidi ya haya. Ndipo tukaamua kuanzisha mgahawa huu ambapo tunapika mpaka makange ya pweza, prawns (kamba) na ngisi."

=====================================================
RIDHIWANI AKABIDHI MAGARI YA WAGONJWA KITUO CHA AFYA CHALINZE NA MIONO
================================================
Serikali yasitisha tamko la utoaji wa Chakula Muhimbili.
Na Ally Daud-Maelezo
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , imesitisha tamko la utoaji wa vyakula kwa wagonjwa watakaolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kupisha utafiti wa kina kuhusu huduma hiyo ili kuweza kutoa kilicho bora kwa watanzania.
Akizungumza hayo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu amesema kwamba wameamua kusitisha mpango mpaka watapotangaza tena ili kufanya utafiti kujua kama kuna faida au hasara kwa wananchi.
“Natoa tamko kwamba huduma hii iliyotarajiwa kuanza hivi karibuni isitishwe mara moja ili kupisha watafiti waweze kufanya uchunguzi kujua inawasaidia kwa kiasi gani wananchi” alisisitiza Bi. Mwalimu.
Aidha Bi. Mwalimu amesema kwamba huduma hiyo itatolewa kwa wagonjwa watakaolazwa hapo kwa kulipia shilingi elfu 50 ikiwemo shilingi elfu kumi ya kumuona daktari , elfu kumi ya kitanda na elfu 30 iliyobaki ni kwa malipo ya chakula kwa wiki.
“Huduma hii inalenga kuwasaidia wananchi katika kuwaandalia chakula stahiki kwa wagonjwa na kupunguza usumbufu kwa waangalizi wa wagonjwa wao kuleta vyakula hospitalini ili kuimalisha afya zao kwa ujumla” aliongeza Bi.Mwalimu.

=================================================
No comments:
Post a Comment