TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, January 26, 2014

Benki ya Kilimo Tanzania kuanzishwa

IMG_8863 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Profesa Jeffrey Sachs usiku wa juzi, Jumatano, Januari 22, 2014, wakati wa mjadala kuhusu jinsi ya kuongeza kasi ya mafanikio katika kilimo cha Afrika kwenye Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na Taasisi ya Kilimo ya Grow Africa mjini Davos, Uswisi, ikiwa ni moja ya shughuli za Mkutano wa Mwaka 2014 wa Taasisi ya Uchumi Duniani (WEF). Katikati ni Waziri wa Kilimo wa Nigeria Mhe Dr. Akinwumi Adesina
Picha na IKULU

Ziara ya Waziri Mkuu Lindi na Mtwara

04
Bi  Asha Ismail mkazi wa Kitomanga mkoani Lindi akitwishwa ndoo ya maji na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mizengo Pinda baada ya kuzindua kisima cha maji kilichojengwa na kampuni ya CCP inayojenga bomba la mafuta kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam. 05
Mhandisi Baltazari Mrosso akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa bomba la gesi linalotoka Mtwara mpaka Dar es salaam kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mizengo Pinda wakati anakagua maendeleo ya ujenzi wa bomba hilo.
01
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mizengo Pinda akizindua na kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha saruji cha MEIS eneo la Machole mkoani. 02
Sehemu iliyoandaliwa kitakapojengwa kiwanda cha saruji cha MEIS eneo la Machole mkoani. 03
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mizengo Pinda akitembelea baadhi ya maeneo ya kiwanda cha saruji cha MEIS  baada ya kikizindua.

ASKARI POLISI, VIONGOZI WA TARAFA WATAKIWA KUSHIRIKIANA

GEDSC DIGITAL CAMERA 
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi ambaye ni Polisi Tarafa wa Muklati Elibariki Kileo akitoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas wakati wa makabidhiano ya kikosi kazi cha askari 15 watakaofanya kazi pamoja na wananchi wa Tarafa ya Muklati wilayani Arumeru. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha) GEDSC DIGITAL CAMERA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akitoa elimu ya Polisi Jamii kwa viongozi, vikundi vya ulinzi shirikishi na wananchi wa Tarafa za Muklati na Enaboishu wilayani Arumeru. Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Askari wa Jeshi la Polisi pamoja na viongozi wa Tarafa za Muklati, Enaboishu, Poli, Mbuguni  Moshono na King’ori zilizopo katika wilaya ya Arumeru wametakiwa kuungana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuweza kufanikisha dhana nzima ya Ulinzi Shirikishi.
Akiongea katika vikao tofauti vilivyofanyika mwishoni mwa wiki hii wakati wa kusambaza askari 15 kwa kila Tarafa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema ushirikiano huo utafanikiwa endapo tu askari Polisi watakuwa wanatumia lugha nzuri na kufanya kazi kwa maadili huku viongozi wa Tarafa, Kata, Mitaa au vijiji watakuwa tayari kuwapa ushirikiano.
“Kama kutakuwa na ushirikiano wa dhati ambao utawezesha kufanya kazi kama timu moja basi kutakuwa na kuelezana ukweli na hivyo kuondoa majungu badala ya kila kundi kufanya kazi kwa kujitenga”. Alisema Kamanda Sabas.
Kamanda Sabas alisema serikali wanayoitumikia ni moja hivyo ili kukidhi malengo ya kuimarisha Ulinzi na Usalama katika maeneo yao makundi hayo yanatakiwa kuungana na kufanya kazi kama familia moja hali ambayo itasaidia kuongeza vikundi vya ulinzi shirikishi, kupata taarifa za uhalifu na wahalifu na hatimaye kupunguza vitendo vya uhalifu kama si kuutokomeza kabisa.
Alisema siku zote wahalifu wanafanikiwa sehemu ambazo ni dhaifu na zile sehemu ambazo zimeungana wanashindwa kupenya kwani uhalifu wowote ambao unahusisha watu wa mbali unaanzia toka kwa mwenyeji hivyo kama kila mwenyeji ataungana na wenzake kwa kuukataa uhalifu basi daima maeneo yao yatakuwa salama.
Kamishna huyo Msaidizi Mwandamizi wa Polisi pia aliwaomba wananchi hao kujitokeza mahakamani pindi wanapotakiwa kutoa ushahidi hali ambayo itasaidia kuwatia hatiani watuhumiwa watakaowakamata kinyume cha hapo jamii itaendelea kuvivyooshea vidole jeshi la Polisi pamoja na Mahakama.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ngaramtoni iliyopo katika Tarafa ya Muklati Bw. David Kimisi (CCM) alimpongeza Kamanda Sabas kwa hatua yake ya kuamua kutembelea Tarafa zote za Mkoa huu kwa nia ya kutoa elimu ya Polisi Jamii kwa viongozi, vikundi vya Ulinzi Shirikishi pamoja na wananchi na pia hatua yake ya kusambaza askari hao 15 kila tarafa ili waweze kutoa huduma karibu na jamii.
Diwani huyo alisema katika Tarafa yake kuna ushirikiano mkubwa kati ya Viongozi, wananchi ambao wanashirikiana vema na Mkaguzi wa Polisi wa Tarafa hiyo Elibariki Kileo pamoja na askari wa Tarafa hiyo hali ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa vitendo vya uhalifu na wahalifu.
Alimalizia kwa kusema maneno ya Kamanda Sabas yameongeza chachu ya kuimarisha ulinzi katika eneo hilo huku viongozi na wananchi wa eneo hilo wakiwa na mipango dhabiti ya kukikarabati kama si kujenga kituo cha Polisi  kingine ili kiweze kuhudumia idadi kubwa ya watu wa eneo hilo kwa wakati mmoja.

SITASITA KUWAONDOA WATUMISHI / WAKUU WA IDARA WANAOWACHONGANISHA MADIWANI NA MKURUGENZI WAO – ASEMA INJINIA MANYANYA MKUU WA MKOA WA RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kilichofanyika jana tarehe 25 Januari 2014 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo Sumbawanga Mjini. 
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akizungumza katika kikao hicho ambapo alitilia mkazo juu kuboresha elimu na ufaulu katika halmashauri hiyo ambayo haijafanya vizuri katika siku za karibuni. Alisisitiza pia umuhimu wa upandaji miti hususani katika msimu huu wa masika.
Mbunge wa Jimbo la Kwela (CCM) Ignas Malocha akishukuru ujio wa Mkuu huyo wa Mkoa katika kikao hicho na maelekezo aliyoyatoa ambayo alisema ni muongozo mzuri na wa kuzingatiwa katika maendeleo ya halmshauri hiyo.
Mkuu huyo wa Mkoa akizungumza na wajumbe wa kikao hicho kushoto wakiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na kulia wakiwa ni wakuu wa idara katika halmashauri hiyo.
Madiwani wa halmashauiri ya wailaya ya Sumbwanga.
Wakuu wa Idara Halmashauri ya Wilaya ya Sumbwanga.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Madiwani na Viongozi wa Chama tawala (CCM) walioalikwa katika kikao hicho.

NA HAMZA TEMBA – OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA
………………………………………………..
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya amewaonya watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wakiwemo wakuu wa idara wenye tabia ya kuwachonganisha madiwani na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndugu Adam Misana, “watumishi mnaofanya mchezo huo nitawaondoeni” Alisema Manyanya. 
Manyanya aliyasema hayo jana katika kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga alipotembelea kutoa salam zake za mwaka mpya kwenye baraza hilo. Alisema kuwa tangu Mkurugenzi huyo ateuliwe kuiongoza Halmashauri hiyo amekuwa akifanya vizuri katika udhibiti wa mapato jambo ambalo limekuwa kero kubwa wakuu wa idara na watumishi wa ofisi hiyo.
Alieleza kuwa Mkurugenzi aliyekuwepo kabla ya Misana alikua akikaimisha ofisi mara kwa mara kwa watu tofauti jambo ambalo lilizorotesha utendaji na kupelekea mambo kufanyika kienyeji na kwa mazoea bila kujali matumizi sahihi ya mapato ya Halmashauri. Ujio wa Mkurugenzi huyu mpya umerekebisha hali hiyo kwa kiwango kikubwa hususani katika matumizi ya fedha za halmashauri, aliongeza Mkuu huyo wa Mkoa.
Katika salam zake alilieleza baraza hilo kuwa mpaka sasa toka ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ameshatembelea kata 51 sawa na asilimia 80% ya kata zote Mkoani Rukwa. Alisema baadhi ya kata hizo ameshazitembelea zaidi ya mara tano kutokana na umuhimu na matukio yaliyojitokeza.
Aliwata madiwani, viongozi wa chama na halmashauri pamoja watumishi kwa ujumla kutoa uongozi uliotukuka katika maeneo yao kwa kushirikiana katika kutoa huduma bora kwa wanachi na kuwafikia mara kwa mara pale inapowezekana na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Katika hali nyingine Mkuu huyo wa Mkoa alishangazwa kwa Wilaya ya Sumbwanga kutokuwa na Hospitali yake ya Wilaya na badala yake kutegemea huduma katika Hospitali  Kuu ya Mkoa. Alisema mwaka huu 2014 ni mwaka wa afya na kwamba Halmashauri za Wilaya ya Sumbwanga zijipange kuhakikisha zinakuwa na hospitali yao ya Wilaya ili kuweza  kutoa nafasi kwa hospitali kuu ya Mkoa kuhudumia wagonjwa wa rufaa kuliko ilivyo hivi sasa ambapo ambapo inabebeshwa mzigo mkubwa na Wilaya hiyo.
Katika salam zake Injinia Manyanya aliwashauri madiwani na viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kujipanga kuhakikisha wanahamia katika Mji mdogo wa Laela uliopo takribani kilomita 100 kutoka mjini Sumbawanga. Alisema zipo faida kubwa za kufanya hivyo ikiwemo ya halmasahuri kuwa na mji wake watakaouendeleza kisasa na kujiwekea mikakati mbalimbali ya kimaendeleo. Aliongeza pia kuwa itakuwa fursa ya kuwasogezea wananchi huduma.
 Akielezea kuhusu jengo kubwa la kisasa la Halmashauri hiyo linaloendelea kujengwa mjini Sumabwanga alisema linaweza kutumika kama kitega uchumi cha Halmashauri ambapo litawapatia fedha nyingi za kujiendesha na kwamba wataomba fedha nyingine TAMISEMI ya kujenga ofisi kubwa kama hiyo Laela kwa lengo la kuwasogezea wananchi huduma.
Akizungumzia kilimo na ufugaji aliwataka viongozi wa halmashauri wakishirikiana na madiwani kuhakikisha wanajiwekea utaratibu maalumu wa maeneo ya wakulima na wafugaji na kuhakikisha kunakuwepo na idadi maalum ya mifugo inayotakiwa kufugwa katika maeneo yaliyotengwa na kuwekewa alama maalum za utambuzi.
Kwa upande wa ONYARU – Ondoa Nyasi Rukwa alisema kuwa mpango huu umekuwa na mafanikio makubwa kwani maeneo mengi wananchi wamehamasika kwa kuondoa nyasi na kuezeka kwa bati nyumba zao. Aliwataka viongozi na wasimamizi wa halmashauri kuendelea na uhamasihaji huo kuhakikisha nyumba za nyasi zinauhama Mkoa wa Rukwa. 

VIWANDA VYA NGOZI, MAFUTA VYAKAMILIKA SHINYANGA

viwandani 159
Mkuu wa Mkoa Mhe. Ally N.Rufunga akipata maelezo ya maendeleo ya kiwanda hicho mapema leo alipotembelea ili kuona shughuli zinazoendelea viwandani 163
Mashine za kuosha na kulainisha ngozi zikijaribiwa, chini ni ngozi zinazosubiri kuwekwa kwenye mashine hizo viwandani 165
Mkuu wa Mkoa akioneshwa baada ya kazi ngozi laini inavyokuwa na tayari kwa matumizi mbalimbali kama kutengeneza viatu,mabegi,pochi,n.k viwandani 171
Hizi ni mashine za kutengeneza yuzi katika kiwanda cha nyuzi na nguo kilichopo manispaa ya Shinyanga
  viwandani 180
Mkuu wa Mkoa Mhe. Ally N. Rufunga akiona shughuli ya kujaribu mitambo katika kiwanda cha kukamua mafuta cha Jielong leo alipotembelea kiwanda hicho viwandani 156
Kiwanda cha ngozi kilichopo manispaa ya Shinyanga ambacho kimekamilika na kazi ya kujaribisha mitambo inaendelea
…………………………………………………………………….
Kiwanda cha kutengeneza Ngozi kwa ajili ya matumizi mbalimbali cha kampuni ya Kichina “Xiu hua”  kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga kimekamilika ambapo mhandisi na msimamizi wa kiwanda hicho “Mr.Way” amesema kwa sasa majaribio yanafanyika kabla ya kuanza uzalishaji wakati wowote.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga ametembelea kiwanda hicho mapema jana na kujionea majaribio ya mitambo ya kutengeneza ngozi za mbuzi,kondoo na ng’ombe.
Kiwanda hicho kinachotarajiwa kutengeneza jumla ya ngozi za kondoo na mbuzi Elfu kumi hadi 12 kwa siku na ngozi za ng’ombe 2500, kitaajiri zaidi ya Watanzania 500 ambapo Mr.Way amesema kipaumbele zaidi ni kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa pia ametembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya pamba cha Jielong Holdings, ameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Mr. Jerry Q kuwa wanaendelea kuzifanyia majaribio mashine na wakati wowote kitaanza kazi ya uzalishaji.
Mr.Jerry amesema kitaajiri zaidi ya wananchi 180 kitakapoanza uzalishaji na tayari kimeanza kuajiri.
Aidha,kiwanda cha kutengeneza nyuzi za nguo cha Dahong ambacho  kinatarajiwa kuanza kazi mapema mwezi Machi baada ya kukamilisha kazi ya kufunga mashine mwishoni mwa mwezi Februari.
Msimamizi wa kiwanda hicho Mr.Saimon amesema kiwanda hicho kitaajiri wananchi zaidi ya 80.
Mhe.Rufunga amefanya ziara hiyo ili kujua maendeleo ya viwanda hivyo ambavyo vinatarajiwa vitakapokamilika pamoja na viwanda vingine, vitabadili sura ya mkoa wa Shinyanga kimaendeleo kwa kukuza uchumi wa mkoa,kwani amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha maisha ya wananchi wa Shinyanga yanabadilika kwa kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vitakavyozalisha ajira nyingi zitakazonufaisha wananchi.

Waziri Mkuu awaasa wanachi kutunza miundo mbinu ya mradi wa gesi nchini.

2 
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akieleza hatua iliyofikiwa katika ujennzi wa bomba la gasi linalojengwa kutoka Mtwara hadi Dar es salaam kwa Waziri Mkuu na msafara wake. Kushoto ni Balozi wa China nchini, Lu Younqing. 3 
Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akimsikiliza Waziri wa Nishati na Prof. Madini Sospeter Muhongo akizungumzia ujenzi wa bomba la gasi eneo la Bungu mkoa wa Pwani. 4 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na msafara wake wakiangalia eneo utakapochimbwa mtaro wa kupitishia bomba la gesi. 5 
Mafundi wakiendelea na kazi ya kuunganisha mabomba kabla ya kuyalaza na kuyafukia chini kwenye mitaro 6 
Mkuu wa mkoa wa Lindi akiwa na Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili mkoani humo na kuendelea na ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha saruji cha MEIS Merea Barabuu akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo eneo la Machole Mkoani Lindi. 8 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia wananchi na wafanyakazi wa ujenzi kiwanda cha MEIS faida zitzkazotokana na kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa gasi kijijini hapo kwa njia rahisi baada ya kuunganishwa kutoka bomba kuu la gasi ikiwemo ajira kwa wanachi na upatikanaji wa saruji kwa bei nafuu ili kuboresha makazi yao. 9 
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha MEIS kilichopo eneo la Machole Mkoani Lindi. 10 
Picha ya sura na muonekano wa kiwanda cha MEIS kitakapokamilioka
……………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-Maelezo Mtwara
SERIKALI imewapa jukumu wananchi wanaoishi maeneo linapopita  bomba la kusafirishia gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam la kulitunza na kulilinda  kwa manufaa yao na taifa zima.
Wito huo ulitolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda  leo alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa bomba hilo.
Waziri Mkuu Pinda alisema Serikali inavihakikishia vijiji lilipopita bomba hilo kuwa watapatiwa umeme unaotokana na uzalishaji wa gasi na utakuwa wa gharama nafuu.
Zaidi ya hayo, gasi itatumika kwa matumizi ya nyumbani kwa kuunganishiwa bomba la gasi na ambao hawatafanikiwa watakuwa na fursa ya kupata mitungi ya gesi ambayo itakuwa ya bei nafuu.
Waziri Mkuu ameagiza mashirika ya Shirika la gasi na Petroli Tanzania (TPDC) na Mradi wa Nishati Vijijini (REA) wachukue jukumu la kuboresha maisha ya wananchi wa maeneo lilipopita bomba hilo katika maeneo ya barabara, shule, kuwapatia maji safi na salama,kuwaboreshea utoaji wa huduma za afya kwa kuboresha zahanati na vituo vya afya kama mchango wao kwa jamii.
Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alisema kuwa serikali kupitia shirika la TPDC na REA itahakikisha wanachi waishio vjijini wanapata umeme mapema iwezekanavyo.
Kwa kuthibitisha kauli hiyo Prof. Muhongo alisema serikali kupitia TPDC na REA imetenga sh. Bilioni 20 kwa awamu ya kwanza ambayo itasimamiwa na REA wakati awamu ya pili nayo itatumia bilioni 20 iotkaysimamiwa na TPDC.
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu aliambatana na mke wake bi Tunu Pinda, Balozi wa China nchini, Lu Younqing, Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, mbunge wa Mchinga Said Matanda na Fatma Mikidadi mbunge wa viti maalum.
Maeneo aliyotembelea Waziri Mkuu ni pamoja na Vikindu, Jopika, Bungu, Ikwiriri, Somanga, Somanga Fungu, Kitomanga na Lindi.

WASANII WA FILAMU WAASWA KUACHA KUTUMIA MAJANGA HALISI KUTENGENEZA FILAMU

IMG_9886
Katibu Mtendaji wa  Bodi ya Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk Suleiman (kushoto) . akifafanua jambo  kuhusu  filamu  ya  MV spice  Islander. Kulia ni Katibu  Mtendaji  wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce  Fissoo. IMG_9914
Katibu  Mtendaji  wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce  Fissoo(kulia) akifafanua jambo  kuhusu  filamu  ya  MV spice  Islander . Kushoto ni Katibu Mtendaji wa  Bodi ya Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk Suleiman  . IMG_9950 
Katibu  Mtendaji  wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce  Fissoo(kushoto) akipeana mkono na Mwakilishi wa kampuni ya kutengeneza filamu  ya  Steps,  Moses  Mwanyilo (kulia).Katibu Mtendaji wa  Bodi ya Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk Suleiman (kushoto) akipeana mkono  kulia Mwakilishi wa kampuni ya kutengeneza filamu  ya  Steps,  Moses  Mwanyilo.
(Picha na Magreth Kinabo)
………………………………………………………………………………
Na Magreth  Kinabo – Maelezo
 Viongozi  wa Bodi za Filamu  wa Tanzania Bara na Zanzibar wametoa ushauri  kwa wasanii nchini  kuacha kutumia majanga halisi kwa ajili ya kutengenezea filamu Kibiashara.
Kauli hiyo imetolewa jana na viongozi  hao , wakati wa kikao cha  kati ya  Katibu  Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce  Fissoo  na  Bodi ya Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk Suleiman  na Mwakilishi wa kampuni ya kutengeneza filamu ya Steps,  Moses  Mwanyilo  kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 Akizungumza katika kikao hicho, Bi.Fissoo   alisema  kampuni hiyo imetengeneza  filamu  ya  MV Spice  Islander kwa  kuchukua picha halisi za ajali ya  MV spice,ambayo iliwasilishwa katika ofisi yake Novemba 2013 kitendo ambacho ni kinyume na sheria , taratibu na kanuni  za utengenezaji wa filamu.
Alisema filamu hiyo ilichukua picha halisi ya ajali hiyo, hivyo ofisi yake ilimwandikia barua mtengenezaji huyo kuwa ibadilishwe, lakini aliomba ashiriki kikao na bodi. Hata hivyo aliitwa mara nne kwa ajili ya kikao na bodi hiyo  lakini hakushiriki  badala yake alileta marekebisho ya  filamu hiyo mara tano ambayo bado yalikuwa na kasoro hizo.
 Naye Bw. Suleiman    alisema filamu hiyo ni muhimu . Hivyo alimtaka mtengenezaji huyo kutoingilia uhuru wa mtu, jamii na Serikali na kutaka filamu hiyo ifanyiwe marekebisho, hivyo ni vema wasanii wakawa wabunifu kutengeneza  filamu zinazogusa  bila kutumia  uhalisia wa janga na majina halisi.   
Aliipongeza bodi ya filamu  ya Bara kwa ushirikiano waliouonesha kwa kuwa filamu ikataliwa Zanzibar na Bara inakataliwa kwani  kazi kama hiyo iliwasilishwa Zanzibar na ilikataliwa kwa kuwa ajali iliyotokea si sherehe, bali itatonesha  vidonda vya watu walioathirika.
Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni hiyo alikiri kosa hilo na aliahidi kufanya marekebisho katika filamu hiyo.

DK KAMANI: AFUNGUKA, AWATAKA WAFANYAKAZI WASIOENDANA NA KASI YAKE WAJIONDOE MAPEMA!

IMG-20140124-WA0007
Na Mukhsin Mambo
………………………………………………………………
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Titus Kamani, amesema ili kwenda na kasi ya maboresho ya wizara hiyo, inahitajika dhana ya uwajibikaji na uwazi sambamba na kujitolea kwa nguvu zote katika kufanya kazi.
Waziri Kamani, ameyasema hayo leo katika mkutano wa kwanza uliowakutanisha wafanyakazi wote wa wizara hiyo, wakiwemo wastaafu wa mwaka jana katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Amesema kama kuna mtu ambaye ni kikwazo katika kukwamisha shughuli za wizara, ni bora akawapisha mapema na kwamba kila mtumishi kwa nafasi yake, anatakiwa kuifanya kazi kwa uwazi na akaitaka wizara kufanya kazi na vyombo vya habari kwani ndio njia pekee ya kuwafanya watanzania wajue wizara inafanya nini.
“Wewe upo ofisini, halafu unaogopa ogopa vyombo vya habari, kwani unatatizo gani, kuweni wazi mambo yenu yawe hadharani, watanzania wa Mbeya wayajue, Rufiji mpaka Pemba, hakuna kufichaficha jambo katika wizara yangu.” Alisistiza Dk Kamani.
Amesema wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi ndio moyo wa taifa kwani huwajumuisha watanzania wengi wenye maisha ya kawaida, lakini amesikitishwa kwa jinsi ambavyo wizara hiyo imekuwa ikichukuliwa na baadhi ya watu kama ni wizara ya yenye migogoro na kuleta hasara maeneo mengine.
“N’gombe hawa wamekua wakiingia kwenye hifadhi, wanapigwa risasi, wanaaribu mashamba ya watu na kuleta njaa kwa wananchi, ngombe hawa wamekuwa wakiambiwa wanaleta uharibifu wa mazingira kwa wananchi kwa sababu ya kuhamahama, kama ngombe hawa ungepatikana utaratibu mzuri wa kuwatunza, kuwahifadhi basi, taifa hili lingeingiza kipato kikubwa ikiwemo kuuza nyama hadi nje ya nchi, maziwa na kuboresha afya za watanzania” alisema Dk Kamani.
Dk. Kamani, amesema anafahamu Wizara yake ina changamoto nyingi katika kutekeleza majukumu yake, ikiwemo bajeti kuwa ndogo, lakini kwa kutumia taaluma yake pamoja na ushirikiano wa wafanyakazi wote wa wizara hiyo, anaamini wizara hiyo badala ya kuonekana ni laana kwa watanzania, itakuwa ni wizara yenye neema kwa watanzania, yenye kueneza ajira na kipato kwa sababu hakuna jambo lisilowezekana kama kila mmoja atafanya kazi kwa dhamira moja.
Akizungumzia juu ya ranchi za taifa, waziri Kamani amesema ana nia ya dhati ya kuona ranchi za taifa zinafufuka na kutengeneza uchumi imara wa taifa, kuzalisha Ngombe wenye ubora ambao watatoa mazao ya mifugo yatakayoliingizia taifa hili kipato kikubwa.
Akizungumzia sekta ya uvuvi, Waziri Kamani, amesema sekta hiyo ni tabu tupu, amesema leo tunaambiwa kuna uvuvi haramu, nyavu zisizokidhi viwango, huku wavuvi wakiendelea kuwa masikini, katika nchi yenye bahari, maziwa na mito mikubwa kila kona, ameuliza ni kweli wanahitaji bajeti kubwa ya kushughulika na mambo hayo?.
“Tunahitaji utashi wa kuwasadia wavuvi wetu, kwa kutoa elimu na kufanya mazungumzo nao ya mara kwa mara, kuwatembelea maeneo yao ya kazi na kubaini matatizo yao kisha kuyafanyia kazi” Alibainisha Dk Kamani.
Kuhusu zao la kuku, Waziri Kamani amesema sasa hivi kuna tatizo la mayai feki na chanjo feki, alihoji ni kweli kwamba wafanyakazi wa wizara hiyo haiwajui wahusika au kuna baadhi ya watumishi ndio miradi yao? ambapo aliagiza wizara kubaini wanaofanya biashara hiyo feki ambayo inaleta madhara hasa wakazi wa mjini ambao ni watumiaji wakubwa wa bidhaa hizo.
Awali, kaimu katibu mkuu wa wizara hiyo Dk Yohana Budeba alipongeza uteuzi wa Dk Kamani, kuingia katika wizara hiyo kwakuwa ajira yake ya kwanza mwaka 1982  alikuwa chini ya wizara hiyo kama afisa Mifugo wa kata ya Kisongo wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha, hivyo changamoto nyingi anazifahamu, ni mwenzao na anaamini watashirikiana vyema katika kukabiliana nazo.

Rais Kikwete ateta na Mbowe wakati wa Mazishi

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe (CHADEMA) wakati wa mazishi ya mbunge wa Chalinze Marehemu Said Bwanamdogo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika huko Miono Wilayani Bagamoyo jana (picha na Freddy Maro)
  D92A4088

PATO LA TAIFA LIMEONGEZEKA KWA KASI YA ASILIMIA 6.5 KWA KIPINDI CHA JULAI – SEPTEMBA, 2013 IKILINGANISHWA NA ASILIMIA 7.2 KWA KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2012

PICTURE NO 01Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Bw. Morice Oyuke kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo mwaka ya tatu ya mwaka 2013 ambapo katika kipindi cha Julai – Septemba, 2013 Pato la Taifa kwa bei za soko liliongezeka kwa kasi ya asilimia 6.5 ikilinganishwa na asilimia 7.2 kwa kipindi kama hicho mwaka 2012. Kulia kwake ni Bw. Juma Omary, Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Mipango na kushoto ni Bw. Daniel Masolwa Meneja Takwimu za Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
 (Picha na Veronica Kazimoto)
PICHA NAMBA 02
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Bw. Morice Oyuke kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (katikati) akizungumza kuhusu ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo mwaka ya tatu ya mwaka 2013 katika ukumbi uliopo Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Dar es Salaam. (Picha na Veronica Kazimoto).

RAIS KIKWETE AONGOZA WANANCHI WA MIONO KATIKA MAZIKO YA ALIYEKUWA MBUNGE WA CHALINZE, RAMADHAN BWANAMDOGO.


 1 
Rais Jakaya Kikwete  akiteta jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiteta jambo na Waziri Mkuu mstaafu  Edward Lowasa. 
 02
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo. Picha na OMR 2
Rais Jakaya Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo. Picha na OMR 03
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwaongoza waombolezaji kuswalia mwili wa marehemu Ramadhan Bwanamdogo, aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, aliyefariki juzi. Mazishi ya mbunge huyo yamefanyika leo kijijini kwao Miono. Picha na OMR
  04
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Ramadhan Bwanamdogo, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Miono leo wakati wa shughuli za maziko. Picha na OMR 4
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiweka udongo kaburini 05
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo. Picha na OMR 5
Waombolezaji wakibeba jeneza la Marehemu Ramadhan Bwabamdogo 6
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto) na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati wakiwa katika maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Picha na OMR 7
Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi katika mazishi hayo 
 8Waombolezaji mbalimbali wakiswali 9

Rais Kikwete aalikwa Nigeria na Rais Jonathan

j1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo  na Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria wakati viongozi hao wawili walipokutana na kufanya mazungumzo Alhamisi, Januari 23, 2014, kwenye Hoteli ya Intercontinental, Davos, Uswisi, ambako  walikuwa wakihudhuria  Mkutano wa Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi Duniani –WEF. 

PICHA NA IKULU
…………………………………………………………………………
Rais wa Nigeria Mheshimiwa Goodluck Jonathan amemwalika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria Mkutano wa Taasisi ya Uchumi Duniani Afrika (WEF-Africa) unaofanyika katika mji mkuu wa Nigeria wa Abuja mwezi Mei mwaka huu.
Rais Jonathan ametoa mwaliko huo kwa Rais Kikwete wakati viongozi hao wawili walipokutana na kufanya mazungumzo leo, Alhamisi, Januari 23, 2014, kwenye Hoteli ya Intercontinental, Davos, Uswisi, ambako viongozi hao wanahudhuria wa Mkutano wa Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi Duniani –WEF.
Rais Kikwete amekubali mwaliko huo wa kuhudhuria Mkutano huo uliopangwa kufanyika Mei 7-9 mwaka huu mjini Abuja, Nigeria.
Mkutano huo kati ya viongozi hao wawili umehudhuriwa na Mawaziri wa Nigeria wa Mambo ya Nje na Fedha na Uchumi. 
Nigeria inakuwa nchi ya nne katika Afrika kuandaa mkutano huo. Kwa miaka mingi, mkutano huo wa WEF-Africa ulikuwa unafanyika Cape Town, Afrika Kusini mpaka Tanzania ilipofanikiwa kuwa nchi ya kwanza ya Afrika nje ya Afrika Kusini kuandaa Mkutano huo mwaka 2010.
Tokea wakati huo, Ethiopia imeandaa mkutano huo na sasa Nigeria.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.