TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, August 18, 2014

Atlanta Falcons Edition

Boxing Edition

KAAT WAJITAMBULISHA KWA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR

*Yadhamiria kuwasaidia wazee wasiojiweza

Na Saidi Mkabakuli

Uongozi mpya wa Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea (KAAT) wamekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Zanzibar na kutoa ombi rasmi la kuharakishwa kwa kufunguliwa kwa Ofisi za Kibalozi nchini Korea Kusini.
Wakizungumza mara baada ya kukaribishwa na Mhe. Balozi Iddi, Rais wa KAAT, Bw. Stephen Katemba alitoa wito kwa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kufikiria kufungua ubalozi nchi Korea Kusini kwa kuzingatia umuhimu wa nchi hiyo katika uchumi wa Tanzania.
Bw. Katemba alisema kuwa kufunguliwa kwa ubalozi huo kutaongeza chachu ya mahusiano ya kibiashara na kindugu baina ya nchi hizi mbili zenye urafiki wa hali ya juu.
“Tunakosa fursa nyingi za kufanya biashara na Korea Kusini kwani wengi wa wafanyabiashara wa Korea Kusini tuliokutana nao nchini humo wanaona usumbufu kufuata huduma za kibalozi nje ya nchi yao,” alisema Bw. Katemba.
Kwa mujibu wa Bw. Katemba, Korea Kusini ina soko kubwa kwa bidhaa za Tanzania ikiwemo bidhaa za vyakula na matunda, pia Tanzania ina fursa kubwa ya kupata ujuzi hasa kwenye eneo la kiteknolojia na ujenzi.
Kwa upande wake Balozi Iddi, alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu na fursa zilizopo nchini Korea, na kuahidi kulifanyia kazi ombi hilo.
Wakati huo huo, katika kutimiza wajibu wa kusaidia wazee na watu wasiojiweza, uongozi mpya wa Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea (KAAT) upo mbioni kufanyia matengenezo nyumba za kukaa wazee za Sebuleni, mjini Zanzibar.
Akizungumzia mpango huo, Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar), Bw. Bukheti Juma amesema “KAAT inatambua mchango mkubwa wa wazee nchini Tanzania, hivyo katika kuhakikisha wanaishi katika mazingira safi na salama, KAAT tutafanyia matengenezo baadhi ya majengo yaliyo kwenye hali mbaya kituoni hapo,” alisema.
Kwa mujibu wa Bw. Juma zoezi hilo linatarajiwa kufanywa katikati ya mwezi ujao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akiwakaribisha viongozi wa KAAT walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake. Katikati ni Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba na Kulia ni Bw. Bukheti Juma ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar).
Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) akiongea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) wakati walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar. Kulia ni Bw. Bukheti Juma ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar).
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akifurahia jambo na viongozi wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Bukheti Juma (Kulia). Viongozi hao walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar.
Bw. Bukheti Juma (Kulia) ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar) akiongea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) wakati walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar. Katikati ni Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba akiwasikiliza.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akitilia mkazo umuhimu wa jamii kusaidia wazee wasiojiweza, wakati alipofanya mazungumzo na viongozi wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Bukheti Juma (Kulia). Viongozi hao walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar.
Baadhi ya wanachama wa KAAT wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Katikati).

Sunday, August 17, 2014

NEWS ALERT: MOTO WATEKETEZA KITUO CHA KUPOZEA UMEME CHA MJINI MOSHI ASUBUHI HII

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au  namba +255767869133.

Askari wa kikosi cha Zimamoto wakifika eneo la tukio asubuhi hii
Wananchi wakishuhudia juhudi za kuzima moto huo
Moto ukiendelea 
Juhudi zikiendelea. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 
Transforma zinazosambaza umeme katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro zilizoko eneo la Bomambuzi zimewaka moto asubuhi hii muda mfupi baada ya kutokea shoti ambayo haijafahamika chanzo chake ni nini.
 Moto huo umetokea majira ya saa 1:10 na kusababisha maeneo kadhaa ya mji wa Moshi kukosa umeme hadi sasa.
 Globu ya jamii imeshuhudia kikosi cha zimamoto kutoka manispaa ya moshi kikijaribu kuzima moto huo ambao hata hivyo ulikwisha teketeza sehemu kubwa ya  kituo hicho cha kupozea umeme.

DEREVA WA DALADALA NI JEURI? SHUHUDIA TRAFIKI WAKIMUONESHA KUWA WAO NI ZAIDI

DEREVA wa Basi la Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, amejikuta akipewa kibano hevi na askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ baada ya kuleta ubabe wakati alipotakiwa kutii sheria bila shuruti.
Askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ wakimdhibiti dereva wa basi la Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) aliyevunja sheria ya usalama barabarani. 

Tukio hilo la aina yake lililosababisha usumbufu kwa abiria wa basi hilo, lilitokea juzi Bamaga-Mwenge jijini Dar kufuatia dereva huyo kukataa kuegesha pembeni basi hilo lenye namba za usajili T 619 CVP lililokuwa limevunja sheria ya usalama barabarani.
Dereva huyo akionyesha ubishi wa kutotii maagizo ya 'trafiki'.

Imedaiwa kuwa, basi hilo lilishusha abiria kinyume na sheria kwenye kituo kisicho rasmi maeneo ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Barabara ya Shekilango.
Chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo kimedai kuwa, kufuatia hali hiyo ndipo trafiki hao watatu walio makini na kazi yao, walilisimamisha basi hilo ili kumsomea mashitaka dereva huyo sambamba na kondakta wake lakini wakaleta ubishi na kutoa lugha chafu kitendo ambacho trafiki hao walishindwa kukivumilia.
Askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ wakimtoa nje dereva jeuri wa UDA.
“Waliendelea kutoa lugha chafu, hawakuonesha kutii amri ili waambiwe walichokosea ndipo trafiki wakalazimika kuwadhibiti kwa kuwafunga pingu baada ya kukataa kutii sheria bila shuruti, tunawapongeza trafiki hawa kwa kuwataiti,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya trafiki kuwadhibiti wawili hao,  mmoja wao alishika usukani, wenzake wakakaa kwenye viti na kuliendesha basi hilo hadi  Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Wananchi wakishuhudia mkasa huo.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kwamba, madereva wa mabasi ya Uda wamekuwa wakivunja sana sheria kama wao wako juu ya sheria kuliko madereva wengine.

MWANASHERIA NA WAKILI MAARUFU MBEYA APANDISHWA KIZIMBANI.

 Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au  namba +255767869133.

 Na  Mbeya yetu

Picha na Rashid Mkwinda Blog
WAKILI wa kujitegemea mkoani Mbeya na mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa(MNEC) Sambwee Sitambala (42)amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu mkazi Mfawidhi wilaya ya Mbeya akituhumiwa kwa makosa mawili.
Shitambala amepandishwa leo akituhumiwa kwa makosa ya kuingia kwa jinai na kujenga nyumba katika viwanja viwili namba 27 na 28 Block BB lililopo eneo la Gombe Uyole Jijini Mbeya.
Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi, Gilbert Ndeuruo, wakili wa serikali, Ahmed Stambuli, alisema kuwa Shitambala anashitakiwa kwa kosa la kuingia kwa jinai kinyume cha kifungu  namba 79 ya mwaka 2014 cha kanuni ya adhabu sura ya 16.
Alisema kuwa mshitakiwa kwa nyakati tofauti kati ya Juni 18, 2012 na Novemba 28, 2013 aliingia na kujenga katika viwanja namba 27 na 28 ambavyo vinadaiwa kuwa ni mali ya raia wa Tanzania mwenye asili ya kiasia aliyefahamika kwa jina la Jaswinder Palsingh.
Alisema kulingana na mazingira hayo, mshitakiwa amesababisha maudhi kwa mmiliki wa kiwanja hicho Palsingh na hivyo kushitakiwa kwa kosa la jinai.
Shitambala ambaye alikuwa akitetewa na Wakili wa kujitegemea Tasco Luambano alikana shitaka hilo ambapo Hakimu Ndeuruo alisema kuwa dhamana ya Mshitakiwa iko wazi ikiwa atatimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja na ahadi ya fedha kiasi cha sh. milioni 1.
Kwa upande wake wakili wa serikali Stambuli alisema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kwamba iko tayari kuanza kusikilizwa na kuiomba mahakama ipange tarehe ya kuanza kuisikiliza kesi hiyo.
Hakimu Ndeuruo aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 10 ambapo itaanza kusikilizwa rasmi.
Akizungumza nje ya mahakama mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo Wakili anayemtetea Shitambala,Luambano alisema kuwa kesi hiyo imefika hapo kutokana na maslahi ya baadhi ya watu na kuwa kisheria kesi za aina hiyo zinapaswa kusomwa katika mahakama ya Ardhi.

Alisema kuwa mteja amejenga katika eneo ambalo wamejenga watu wengine wapatao 400 na kuwa hata hivyo kesi hiyo imemhusu mteja wake pekee hali ambayo inaonesha nia mbaya iliyofanywa na mlalamikaji dhidi ya mteja wake.


WANAOTUMIA MIZANI `FEKI` UNUNUZI WA PAMBA WAONYWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au  namba +255767869133.
Waziri wa Chakula, Ushirika na Masoko, Christopher Chiza
 
Wafanyabiashara ‘wanaochakachua’ mizani wakati wa ununuzi wa zao la pamba toka kwa wakulima katika mikoa ya kanda ya ziwa, wameonywa huku Wakala wa vipimo wakitakiwa kuwachukulia hatua wanunuzi hao.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 11 wa wadau wa sekta ndogo ya pamba jijini Mwanza jana, Waziri wa Chakula, Ushirika na Masoko, Christopher Chiza, alisema kutokana na malalamiko ya mara kwa mara ya wakulima wa zao hilo, mamlaka ya vipimo isikwepe jukumu lake.

Aidha, Chiza alisema changamoto zinazowakabili wakulima zisiwe zile zile kila mwaka, bali lazima wajadili utatuzi wake badala ya kulalamikia matatizo.

Hata hivyo, alisema serikali inaendelea na juhudi za kuboresha chuo cha utafiti cha Ukirigulu ili kiweze kuwasaidia wadau wengi wa kilimo hicho.

Akizungumzia kampuni ya Quton inayodaiwa kutoa mbegu Uk 91 zenye manyoya na kuwapa hasara wakulima, Chiza alisema kampuni hiyo lazima ikae na wakulima ili kuwapa elimu kuhusiana na mbegu hizo.

Alisema kutokana na wakulima kupata hasara kupitia mbegu hizo, serikali imeamua kuwalipa fidia wakulima wa zao hilo katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Awali mkuu wa mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikillo, aliwahimiza wakulima wa pamba kuendelea kutumia kilimo cha mkataba kutokana na kuwa na faida.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba, Festus Limbu, alisema wakulima wa zao hilo wanakabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo za mabadiliko ya mara kwa mara ya bei katika soko la dunia, pembejeo kutopatikana kwa wakati, wakulima kutegemea mvua, usimamizi hafifu na mfuko kuwa na madeni makubwa.
SOURCE: NIPASHE

MARIA SHILA NDIYE REDD'S MISS KINONDONI 2014

Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila akipunga mkono baada ya kutawazwa kuwa malkia wa Kanda ya Kinondoni katika shindano lililoshirikisha wanyange 16 waliokuwa wakiwania tiketi ya  kushiriki shindano la Miss Tanzania 2014. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamkia. 

Shila ameungana na warembo wengine Camila Cindy John aliyeshika nafasi ya pili na Queenlatifa Hashim aliyeshika nafasi ya tatu ambao kwa pamoja wamepata tiketi ya kuiwakilisha Kanda ya Kinondoni katika mashindano ya taifa ya Miss Tanzania 2014 yanayotaraji kufanyika mapema mwezi Oktoba.
  Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila (klatikati) akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi wa taji hilo na kuwaongoza warembo wengine 15 waliokuwa wakiwania taji hilo. Wengine mshindi wa pili Camila Cindy John (kulia) na
Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila akipunga mkono baada ya kutawazwa kuwa malkia wa Kanda ya Kinondoni katika shindano lililoshirikisha wanyange 16 waliokuwa wakiwania tiketi ya  kushiriki shindano la Miss Tanzania 2014. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamkia. 

Shila ameungana na warembo wengine Camila Cindy John aliyeshika nafasi ya pili na Queenlatifa Hashim aliyeshika nafasi ya tatu ambao kwa pamoja wamepata tiketi ya kuiwakilisha Kanda ya Kinondoni katika mashindano ya taifa ya Miss Tanzania 2014 yanayotaraji kufanyika mapema mwezi Oktoba.
  Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila (klatikati) akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi wa taji hilo na kuwaongoza warembo wengine 15 waliokuwa wakiwania taji hilo. Wengine mshindi wa pili Camila Cindy John (kulia) na mshindi wa tatu Queenlatifa Hasim. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamia leo. PICHA ZAIDI: FATHER KIDEVU BLOGwa tatu Queenlatifa Hasim. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamia leo. PICHA ZAIDI: FATHER KIDEVU BLOG